PAPY KAKOL wa WMMM achezea kichapo toka kwa Les Combattant

February 22, 2013

 

image

Pichani mwanamuziki Papy Kakol akiwa anavuja damu baada ya kupata kipigo kutoka kwa vijana wanaojiita “Wapiganaji” wa Congo wanaoupinga utawala wa Rais Kabila

Mwanamuziki Mpiga tumba machachari wa WMMM Papy Kakol amesurika kifo baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa vijana wanamageuzi wanajulikana kama Les Combattants ambao wameapa kuwakomesha wanamuziki wote waliompigia kampeni Rais Kabila uchaguzi uliopita.

Tangu ufanyike uchaguzi mkuu wa DRC na kumrejesha madarakani Rais Kanila, imekuwa sio Neema kabisa kwa wanamuziki wa Congo ambao walikuwa wakitegemea show za nje hasa Belgium na Ufaransa ambako walikuwa wakipata show nyingi.

Kilichowaponza wanamuziki wa Congo ni kitendo chao cha kumpigia kampeni Rais Kabila jambo ambalo limeaudhi sana vijana wa Congo walioko nje hasa wa Ufaransa na Belgium wanaopendelea mageuzi nchini Congo na kutofurahishwa na uongozi wa Rais Kabila wanaojiita  LES COMBATTANTS yaani wapiganaji.

image

Pichani Kakol akisindikizwa na Polisi wa Ufaransa chini ya Ulinzi mkali

 

Kakol alikuwa nchini Ufaransa alipokwenda kwa shughuli zake na kutaka kumuombea msamaha Boss wake Werasson jambo lililowaudhi mnoo hawa wapiganaji, wapo wanaohusisha na sababu binafsi huku wakisema kuwa Werasson hapendwi sana na Le Combattant wa Ufaransa ambao inasemekana wanamchukia, “Kupigwa kwa Kakol si kwa sababu ya WMMM kumsupport Kabila ila ni kwa sababu binafsi, Ni sababu za kushtua ambapo Gola Ferre aliruhusiwa kufanya Show katika Paris kwa sababu yeye ni kuonekana kama kupambana na Werrason. Bet yangu ni kwamba watu bana chuki na Werrason wanaweza kuruhusiwa kufanya lakini kama ni pro-Werrason, basi itakuwa combattants wanawakataa  Hiyo ni nini mimi naona…” alisema Franko Pepe wa Vibes De Africa  kwa kiswahili cha kubabaisha nilipochat naye jana.

Habari zinasema kuwa hata Felix Wazekwa ambaye ni Shemeji ya Kabila naye yumo matatani, na maa ya mwisho alikuwa nchini Ufaransa kumalizia Albamu yake na hakuna aliyejua isipokuwa familia yake na marafiki wa karibu. Wapo wanaowahusisha Les Combatant na JB Mpiana kuwa wao wanamkataa zaidi Wera na kumkubali JB angawa Wenge BCBG nao walishiriki lakini kwa BCBG Belgium ndio kuna walakini zaidi ukilinganisha na Ufaransa.

Kwa wanaojua Kifaransa haya ni Majibu ya Kakol kwa kilichotokea bado nimeomba mtu anisaidie kutohoa ili niwajuze hapa.


MSIKILIZE JDL LOKO TRABENDO NA KITU DJIKIDJIKI

February 22, 2013

Siku kama ya leo Rafiki zangu Musa na Husna wa 87.8 Pride Fm ni siku wanagonga Rhumba tuu zilizotukuka, nawakubali sana hawa jamaa na kutamani km ungewaaikiliza wiki nzima kiukweli wamekiweza kipindi chao cha African Vibes ambacho wanapiga muziki wa Kiafrika tuu, nikuache na wimbo toka kwake JDL Loko wa kundi la Wenge BCBG akikwambia Djiki Djiki.


Gari inauzwa 8m

February 21, 2013

image

image

image

image

image

image

Gari Suzuki Swift iko kwenye haki nzuri sana, Clean Interior Condition, No dents, Alloy Rims, Beand New Tyres, Good Sound System with Original Subwoofer, Inaanzia 8M maongezi yapo. Dalali hatakiwi. Maongezi na Kuiona 0713 666616


La Protection des femmes

February 20, 2013

 Mwenyewe anawaita la protection des femmes kwa kiswahili unaweza sema Walinzi wa Kike, Ni Wanadada warembo wachezaji wa kundi la Quartier Latin la Koffi Olomide.

Koffi huwalinda na kuwachunga sana hawa akina dada akiwa kwenye ziara yeyote ndani ama nje ya Kongo, angalia wimbo huuu unaopatikana kwenye albamu ya Abracadabra utawaona uzuri.


Sara Fiona akimshirikisha Koffi Olomide

February 19, 2013

Ni mara chache kusikia Koffi ameshirikishwa kwenye wimbo wa mtu, tena hasa ikiwa mwanamuziki mwenyewe ni mchanga au asiyejulikana kama alivyo Sarah Fiona ambaye wengi wetu hatumjui, anaitwa Mopao Mokonzi Koffi Olomide Papaa na Didi Stone,Papaa na Sean James hapa yuko kivingine akiwa mwanadada mrembo Sarah Fiona wanakwambia J’ai tout Quit akimaanisha nimeacha Yoote.

Ndani ya wimbo huu Mopao analalamikia mapenzi jinsi alivyojitoa kwa mpenzi lakini mpenzi mwisho wa siku kambwaga, anasema “J’ai tout quittée pour lui et il m’a quitté”….tafsiri ya haraka haraka “Nimeacha kila kitu kwa ajili yake lakini mwisho wa siku kaniacha”, Ukiangalia Video hii utakubaliana na mimi kuwa Koffi anajipanga sana kwenye utengenezaji wa Video na inasemwa kuwa anaongoza kwa kutumia pesa nyingi kwenye uzalishaji wa Video zake.


Djino atangaza Albamu yake iko jikoni

February 19, 2013

Wiki mbili baada ya kutangaza kuachana na bendi ya Wenge BCBG mwanamuziki Djino hatimaye ametangaza kuwa Albamu yake ya Commandant de bord iko njiani kutoka.

Djino alithibitisha kuondoka BCBG baada ya kutokea sintofahamu kati yake na kiongozi wa bendi hiyo JB Mpiana. Djino ambaye amefanya kazi na BCBG zaidi ya muongo mmoja na kusikika kwenye albamu karibu zote za Wenge BCBG alitamba na Kibao cha Zadio Kongolo ZK ambcho kiko kwenye mahadhi ya taratibu na hivi majuzi kwenye albamu ya Soyons Serieux alitunga na kuimba kibao kingine humo kibao ambacho kilirudiwa na dada yake.

Wapo wanaosema kuwa kitendo chake cha kutaka kutoa Albamu yake ndio kilicho anza kumchefua boss wake huyo na ilipopatikana sababu aliamua kumsimamisha kabla ya yeye mwenyewe kutangaza kujitoa.

Albamu ya Djino yenye nyimbo nane inatazamiwa kutoka baada ya kumalizaka kazi ya uchanganyaji inayofanyika nchini ufaransa. Akiongea Djino amesema sasa ananafasi ya kufanya kazi vizuri Albamu yake ambayo awali alibanwa na muda kwa vile Wenge kama kampuni ilimhitaji pia, vile vile Djino alimuasa kiongozi wao JB Mpiana kuwa makini na kuwa na tabia ya kusikiliza wanamuziki wa chini kwani wale walio karibu naye wanachukua faida ya ukaribu wao na kuwaharibia wengine.

Djino alikorofishana na mwanamuziki Sunda Bass kabla ya kusimamishwa


JB Mpiana inaendelea…

February 5, 2013

182368

JEAN BEDEL MPIANA WA TSHIKUTA (JB MPIANA) akiwa Swaiba wake WERASSON NGIAMA MAKANDA wakati wa msiba wa mcheza show wa BCBG mwaka jana.

Mwaka 2001, JB MPIANA katoa ALBUM ya INTERNET ikiwa na Volume 2 :

Volume 1

No Titre Auteur(s)

1. Internet JB Mpiana

2. Kap Kapita Alain Mpela

3. Beazodeguem JB Mpiana

4. Espoir de Chicago Ficarre Mwamba

5. Jeannette JB Mpiana

6. Love airlines Jules Kibens

7. Tshico Londonien Tutu Callugi

8. Pacte Divin Seguin Mignion

9. Le duo de Paries Chay Ngenge

10. Sans te toucher JB Mpiana

Volume 2

No Titre Auteur(s)

1. Le tenant du titre Titina Mbwinga

2. Sens Unique Theo Bidens

3. Feux D’artifice JB Mpiana

4. Persecution JB Mpiana

5. Fleur d’amour Rio

6. Consolation JB Mpiana

Sifa nyingi zilimjia na kapata mualiko uliomwezesha kufanya SHOO kwenye Ukumbi wa SPECTRUM (Montréal CANADA) , Tarehe 22/09/2001 akadumwiza kwenye ukumba wa BERCY Mjini PARIS.

Kurundi kwake KINSHASA akafanya SHOO kabambe mnoo iliyo chaguliwa SHOO bora mwaka huo kwenye uwanja wa STADE DES MARTYRS. Yasemekana zaidi ya watu 250.000 walikuwepo.

Mwaka 2002, Kapewa Tuzo nyingi kutokana na kazi aliofanya Mwaka 2001,zikiwemo Tuzo la Mwanamuziki Bora,Mwimbaji Bora,Mtunzi Bora wa wimbo “SANS TOUCHER” na pia tuzo la Wimbo Bora (JEANNETTE).

Kutokana na CAREER (Quarry) nzuri aliekua akijijengea JB MPIANA,hali ya wivu na chuki ikaanza kujitokeza kwa wale ambao ni wapinzani wake.

wakaanza kumtupia Kashfa mbaya kutokana na kabila lake; (JB MPIANA katoka kwenye kabila la WALUBA au LUBA,inasemekana huko CONGO kabila hilo hua linachukiliwa na makabila mengine).

Wakaanza kumchimbia chini kwa chini ili wamuangushe kimziki wengine wakishirikiana na baadhi ya watu maarufu walioko serekalini na kumuwekea mikwala mbalimbali kwenye shughuli zake.

Imetokea siku nyingine, Serekali ikaamua kumkatalia asifanye SHOO bila sababu yeyote. Wakati mwengine akiwa tayari kwenye SHOO umeme unakatika, baada ya masaa kadha hurudishwa.

katukanywa mara kwa mara, kazuliwa mambo ya uongo iliyo sababisha Ndoa yake kuvunjika kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2003, Palitokea na KESI ya VISA Mjini PARIS,iliyomkumba MwanaMUZIKI Mkongwe PAPA WEMBA, Kwa tuhuma za kuwaongeza kwenye List ya wanamuziki wake watu ambao sio wanamuziki na kuwaleta Ulaya, na hapo baadae wakazamia.

Yasemekana PAPA WEMBA kawaleta zaidi ya watu 50 kwa pamoja, na kila mmoja alikua akimpa pesa zinazo fikia kiwango cha Euros 5000. Mkasa huo ukafanya Inchi za Ulaya kuwanyima Visa wanamuziki woote wa CONGO,akiwemo JB MPIANA na kusababisha kazi aliyekua akiaandaa Album yake ya ANTI-TERRO kuchelewa.

Mwaka 2004, JB MPIANA kafanikiwa kutoa ALBUM ya ANTI-TERRO huko Saouth Africa. ikiwa na CD 2 :

CD1

Anti Terro

Nungu Nungu

Lekasopo

Plainte A

J’ Suis La

Decision

Vicky Nsongi

Amour Sans Tache

Clin d’œil

Guy Mbuala

CD2

Doleance

BK Le Senateur

Le Baron

Ezau

Temperature

Kolo Martyrs

Somewhere

Album hii ilimwezesha JB MPIANA apewe kwa mara ya tano tuzo la Mwimbaji Bora na kufikia Rekodi aliyekua nayo kipenzi chake Mkongwe PAPA WEMBA.na kumzidi alipopewa tuzo hilo kwa mara ya Sita mwaka 2008 na kushikilia Rekodi hiyo hadi leo.

JB MPIANA Keshapewa tuzo ya GOLD PALM zaidi ya mara 25 :

-Mwimbaji Bora, kapewa GOLDEN PALM 6,( 1991,1997,2000,2001,2004,2008 ).

-Wimbo Bora, kapewa GOLDEN PALM 5 ( Mulolo 1988 )

( Feux de L’amour 1997 )

( Omba 1998 )

( 48 Heures Gecoco 2000 )

( Jeannette 2001 )

-Palm ( Flipper ) of Money Silver kwa wimbo ( Zadio 2008 )

-Palm ( Flipper ) Tans ( Sunbathes ) Wimbo ( Ezau 2004 )

ALBUM BORA, kapewa GOLDEN PALM 2 :

– Feux de L’amour 1997

– TH 2000

-Palm ( Flipper) of Money Silver Album Anti-Terro 2004

-Palm ( Flipper ) Tans ( Sumbathes ) Album Internet INTERENT

BETTER AUTHOR COMPOSER kapewa GOLDEN PALM 3 :

– FEUX DE L’AMOUR ( 1997 )

– TH ( 2000 )

– INTERNET ( 2001 )

BETTER COMPOSITION, kapewa GOLDEN PALM 3 :

– FEUX DE L’AMOUR ( 1997 )

– GRACE À TOI GERMAIN ( 2000 )

– SANS TOUCHER ( 2001 )

MWANAMUZIKI BORA kapewa GOLDEN PALM 4: 1997,2000,2001,2010

GROUP BORA YA MUZIKI KAPEWA GOLDEN PALM 3 : 2004,2008,2010

PALM ( FLIPPER ) OF MONEY SILVER 2 : 2000,2001

PALM ( FLIPPER ) TANS ( SUNBATHES ) 1 : 2002

Kapewa pia tuzo ya SHOO bora aliyo ifanya mwaka 2001 kwenye Uwanja wa STADE DES MARTYRS, na SHOO yake ya mwaka 2003 kwenye Viwanja vya FIKIN Mjini KINSHASA Mwaka 2003.

Mwaka 2005, JB MPIANA katoa wimbo wa BONGOLOWAYI, ambao ni matangazo ya biashara ya kampuni inayo tengeneza Bia ya PRIMUS,Akapata sifa nyingi hadi kuchanganya Album zilizo tolewa na wanamuziki wengine.

2006 – 2007, JB MPIANA akachezesha ulimwengu mzima na miondoko ya LOPELE Kwenye Album yake ya KIPE YAYO (JIHUSISHE NA NANAYO KUHUSU) Ikiwa na nyimbo 9 :

1. Kipe yayo – JB Mpiana

2. Identité d’amour – Chai Ngenge Ibuba

3. Mal au cœur – Rio Kazadi

4. Alino Kizaza – JB Mpiana

5. Sans permission – Seguin Maniata

6. Voiture – Jules Kibens

7. Guantanamo – Tutu Kaludji

8. Francis Solution – JB Mpiana

9. Elégie – Boguys Bopema

Utawasikia wakitupa maneno haya :

LE POISSON A COMBIEN DES PARTIES ? (SAMAKI ANAGAWANYWA MARA NGAPI?) AU ANA VIPANDE VINGAPI?

WANAITIKA : 3 PARTIES (VIPANDE VITATU)

ALLEZ !!! CITEZ – LES !!! ( HAYA!!! VITAJE!!!) :

MUTU ( KICHWA ), LIBUMU ( TUMBO ) NA LOPELE ( NA MKIA)…

PELE PELE YA LOPELE PELE!!! PELE YA LOPELE!!!!! HMMM!!!

Mwaka 2008,Mwishoni, JB MPIANA katoa Album ya QUEL EST TON PROBLÈME (SHIDA YAKO NINI) ikiwa na nyimbo 5 :

1. Quel est ton problème? – (JB Mpiana)

2. Zadio Kongoklo (ZK)- (JB Mpiana)

3. Claude Itoma (Seguim Mignion Maniata)

4. Libérez – (Sunda Bass)

5. Excès d’amour – (Gentamycine Lisimo)

Album hii alimwezesha JB MPIANA apewe tuzo kwa mara ya sita ya Mwimbaji Bora.

Mwaka 2009, JB MPIANA kawa Mwanamuziki pekee wa KICONGO aliye shiriki Mjini WASHINGTON alipo apishwa RAISI BARAK OBAMA, na akiwa huko, akatoa wimbo mwengine wa matangazo ya Bia PRIMUS (KIYUNGUZUNA).

Mwaka 2011, akatoa Album SOYONS SERIEUX (TUJIHESHEMU):

CD 1

1 Mpunda “La Danse du Cheval” (JB Mpiana)

2 Etoile du Berger (JB Mpiana)

3 Engobo “le Gros Bebe” (JB Mpiana)

4 Bolonia “8eme merveille” (JB Mpiana)

5 Loniatara (cedric Guez)

6 Cherie Enlever (Djino Kezipame)

7 Mombamba (Nono Fuji)

8 My Love (Eric Menthe)

9 Mbua (Chai Ngenge)

CD 2

1 Telecommande (JB Mpiana)

2 Code Moral (Abraham Mignon)

3 Amour Infini (Gessan Sakoko)

4 Ezala Zala (Gentamicine Lisimo)

5 Mbeto (Jules Kibens)

6 Boulowook (Sunda Basse)

7 Eloko ya Pema (seguin Manita)

8 Sanguluma (Rio Kazadi)

9 Djiki Djiki (JDL)

10 Loboko (JB Mpiana)

Bonus:

1. Bolingo ya Charlot (Roger Ngandu)-interpret: Athsuda et JB Mpiana

2. Homme d’affaires

WATU WANANENGUA NA MIONDOKO YA PUNDA!!! AMATAKA NA PUNDA AYOKAKA BILENGI (AKIPANDA KWENYE FARASI HUA ANAJISIKIA RAHA!!!)

JB MPIANA kapachikwa majina Mengi saaana :

BIN ADAM,SOUVERAIN PREMIER,PAPA CHERI,LE MARÉCHAL MUKULU,LA STAR DU RÉEL,HÉEO NATIONAL,SALVADORA DE LA PATRIA,L’HOMME QUI A MIS DE L’EAU DANS LE COCO,L’EAU QUI A SUCRÉ LA BANANE,MOTO PAMBA,MWANA CONGO,L’ENFANT DU PAYS,L’ÉTOILE DE DIEU,MOKONZI YA BA WENGÉ,LEADER CHARISMATIQUE,LEADER YA BA OEUVRES, MOKONZI YA FIKIN…


Djino athibitisha kuondoka rasmi Wenge BCBG

February 5, 2013

Lile sakata la mwanamuziki Djino wa Wenge BCBG hatimaye amethibitisha kuondoka katika kundi la Wenge BCBG.

akinukuliwa na Gazeti la  Journal Visa Mwanamuziki huyo amesema kuwa ameamua kuondoka Wenge BCBG kwa sababu hajui hatimaye yake baada ya kusimamishwa katika kundi hilo. Hata hivyo Djino amesema kuwa bado ataendelea kumheshimu Papaa Mpiana kwa kuwa bila yeye ulimwengu usingemjua, “…ndio baba wa muziki wangu, yeye ndio amenitoa na kunitambulisha kwa dunia namuheshimu na siwezi kubadilishana maneno na yeye ni utovu wa nidhamu…”.

Hata hivyo mwanamuziki huyo amesema kuwa chanzo cha yeye kufarakana na boss wake ni mwanamuziki mwenzie Sunda Bass ambaye anatumia ukaribu wake na JB Mpiana kuwaumiza wengine, hivyo amemuomba boss wake huyo wa zamani kutengeneza utaratibu wa kuwasikiliza wanamuziki wengine kabla ya kutoa maamuzi.


Balle de Match kutambulisha mpya ya JB Mpiana na Wenge BCBG

February 3, 2013

clip_image001

Sikiliza balaa la Genta Lisimo humu!!

Mwanamuziki JB Mpiana ambaye alifunga mwaka kama wenzie kwa kuzindua Single yake mpya ijulikanayo kama Balle de Match ambayo aliizindua huko Equatorial Guinea

Hii ilikuwa ni baada ya show ndefu ambazo alizifanya hapa nchini na huko Zambia ambako aliangusha show ya nguvu. Inasemekana kuwa hii ndio itafungulia ujio wa albamu yao mpya ambayo wanamuziki wengine nao wametunga nyimbo kadhaa ndani yake kama Zoule Atshuda alias na Diego Milito. Wimbo Balle de Match ni moto wa kuotea mbali kwani Genta Lisimo amefanya kufuru humo na kwa mara ya kwanza JB ameamua kutumia electric drums kit kwenye Sebene.

Ukisikia Solo lililopigwa humu ni lile Solo kali la Metre Ficare Mwamba akishirikiana na kijana mdogo anayekuja kwa kasi Djany Solo, baada ya Rotarota utamsikia kijana anaingia hapo anagonga mpaka mwisho tofauti na ulilozoea humu Solo limesikika barabara. Hii inaashiria moto uliopo kwenye albamu ya Mpiana ijayo.

Aidha Mpiana amesema kuwa ameichelewesha albamu yake ili kuzipisha albamu za wanamuziki wenzake ambazo nazo zimeingia sokoni kwa sasa, anasema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwani mwisho wa siku mashabiki wanaonunua CD na DVD zao ni hao hao na wanahitaji muda kusikiliza nyimbo za mwanamuziki mmoja mmoja alisema Mpiana.


Kimenuka Wenge BCBG; Djino atimuliwa kundini

February 3, 2013

image

Djino wa BCBG

Habari zilizothibitishwa na JB Mpiana mwenyewe zinasema kuwa uongozi wa BCBG umemtimua mwanamuziki Djino ambaye alikuwa na kundi hilo kwa miaka kadhaa, Djino ambaye amesikika vyema kwenye wimbo wa ZK au Zadio Kongolo, inasemekekana Djino aligombana na mwanamuziki mwenzake Tshai Ngenge na amekuwa na tabia zisizo njema ndani ya kundi zima.

Hata hivyo habari ambazo Spoti na Starehe imezipata zinasema kuwa Djino amesimamishwa jukwaani na hafanyi mazoezi kwa kile kilichoelezwa kuwa alionekana na mwanamuziki Koffi Olomide, Ikumbukwe kuwa mpiga chants na ngoma wa Wenge BCBG wakati huo Titina Acapolne aliingia matatizoni alipoonekana kuwa karibu sana na mwanamuziki Koffi Olomide kiasi cha kumuomba kumsimamia harusi yake, jambo hilo lilipelekea kutokuwa na mahusiano mazuri na hatimaye Alcapolne alijiondoa BCBG na kwa sasa yuko Dubai akifanya shughuli zake huko.

Hata walivyokuwa nchini kariibuni baadhi ya wanamuziki wa BCBG hawakuwa wazi sana kwa nini Djino hakuja nchini, vile vile nikukumbushe pia Mwanamuziki mwingine Sunda Bass naye aliwahi kusimamamishwa kwa takribani miezi nane kundini na aliporejea alikuja na kibao Liberez ambacho kinashika mpaka wa sasa.

Binafsi nilikuwa nampenda sana Djino ambaye alitunga wimbo wa CHERIE ENVELEE ambao uko kwenye albamu ya SOYONS SERIEUX. Wimbo huu mara ya kwanza Djino aliurekodi na bcbg ukiwa ni moja ya nyimbo zilizomo kwenye album lao jipya la Sayons Serieux,dada yake Djino anaekwenda kwa jina la Claudia Bakisa amekuja kuurekodi upya Kama remix,je upi umetoka bomba?

Hii sasa ndio original version iliyoimbwa na Djino mwenyewe,mwana kisangani,huyu ndio anaongea kiswahili kwenye ile video ya jb tolingana kisangani kama mlisikia akisema sema pole pole ndio mwendo na watu wakalipuka, watu wa kisangani wanaongea zaidi kiswahili.

Na huu ni wa Dada mtu Claudia Bakisa

Sikiliza hizi sauti kisha uniambie version ipi ni bomba kwako, The Romantic wa Mapenzi Club mercy mingi papaa kwa hii, Papaa Julie Elystone Le Charismatique Leader, Presidaa wa Congolee ya Darisalama, Uko juu Papaa Salute!!! , hebu sema kidogo hapa.


Lobeso, Atalaku wa WMMM anayeng’ara kwenye Albamu mpya.

February 3, 2013

Kundi la Wenge Musica Maison Merre linaloongozwa na Werasson Ngiama Makanda “Roi de la Foret” nguli mwenyewe liliangusha albamu yake mupya sokoni ikiwa ni siku moja baada ya kusherehekea siku ya Kuzaliwa kwa mwanamuziki huyo na siku ya ufunguzi wa zawadi yaani Boxing day.

Albamu hiyo tangu imeingia sokoni takribani mwezi mmoja sasa inasemwa imefanya vizuri na watu wameanza kuimba ghani za atalaku Lobeso huku ikiendelea kupendwa zaidi, Albamu hiyo ambayo inajulikana kama Satellite +2.

Lobeso amekuwa kinara kwenye albamu hii inasemwa kwa sababu ya kutokuwepo atalaku namba moja jambo lililopelekea Lobeso kushika hatamu wakati wa mazoezi ya nyimbo za albamu hii na sasa iko sokoni.

Naomba nikuwekee moja ya kibao cha Werasson kipya ujionee mwenyewe.


Meneja akanusha Ferre kushikiliwa na Polisi huko Paris

February 3, 2013

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Jet Set Vasco Mabiala amekanusha habari zilizozagaa kuwa Boss wake Ferre Gola amekamatwa huko Paris Ufaransa.

Akiongea na wanahabari jijini Kinshasa Vasco Mabiala amesema kuwa si kweli Ferre Gola amekamatwa na wala hajawekwa ndani kama ilivyoripotiwa awali na kuwa Ferre Gola yuko huko kukamilisha albamu yake ambayo imechelewa kidogo kutoka kutokana na sababu za Kiufundi.

Awali iliripotiwa Kuwa Mwanamuziki Ferre Gola alikuwa ameshikiliwa na Polisi wa Ufaransa kwa kile kilichooelezwa kuwa taratibu za kiuhamiaji. Meneja huyo amesema kuwa Ferre yuko bussy katika Studio za Zet akikamilisha albamu yake hiyo inayokuja kwa jina la Black Box. Aidha meneja huyo alisema kuwa Ferre akimaliza hapo anakwenda Hollywood kufanya shooting ya nyimbo zake sita zilizomo kwenye albamu hiyo, Mabiala amesema kuwa habari hizo zimevumishwa na kundi la vijana walioanzisha vita na wanamuziki wa Congo kwa sababu za Kisiasa bila kufafanua zaidi.


JEAN BEDEL MPIANA WA TSHIKUTA (JB MPIANA)

February 3, 2013

Na Lubonji wa Lubonji

Muite vyovyote BIN ADAM,SOUVERAIN PREMIER,PAPA CHERI,LE MARÉCHAL MUKULU,LA STAR DU RÉEL,HÉEO NATIONAL,SALVADORA DE LA PATRIA,L’HOMME QUI A MIS DE L’EAU DANS LE COCO,L’EAU QUI A SUCRÉ LA BANANE,MOTO PAMBA,MWANA CONGO,L’ENFANT DU PAYS,L’ÉTOILE DE DIEU,MOKONZI YA BA WENGÉ,LEADER CHARISMATIQUE,LEADER YA BA OEUVRES, MOKONZI YA FIKIN…

Leo nitawaletea Historia fupi ya Mwanamuziki JB Mpiana kama ilivyoandika na Shabiki Lubonji wa Lubonji, Kuna mengi sana yameshasemwa kuhusu JB Mpiana lakini hii ni moja ya historia zake ambazo zimewekwa kwenye kumbukumbu na mashabiki wake kwa ushirikiana na vyanzo mbalimbali.

Pichani ni JB Mpiana akiwa na mwanaye Kipenzi Daida Mpiana.

JB MPIANA kazaliwa tarehe 2/06/1967 mjini KANANGA mkoa wa KASAI (katikati mwa Inchi ya CONGO.

Mtoto wa Mzee Mpiana na Mama LUSAMBO Agnès,

Siku mbili baada ya kuzaliwa kwake, wazazi wake wakaamua kuhamia kwenye Mji Mkuu wa KINSHASA.

Mwaka 1981 kama tulivyo fahamishwa kwenye sehemu zilizo pita, JB MPIANA akiungana na wenzake WERRASON na kadhalika, waliunda Group WENGE MUSICA 4×4.

JB MPIANA katokea kuwa mwanamuziki nyota kwenye Group WENGE MUSICA,na hapo baadae kateuliwa kama Raisi wa Group. hadi sasa yeye na WERRASON ndo wanaonekana kama ma Iconic figure wa Group WENGE MUSICA.

Ni mmoja katiyao aliewezesha WENGE MUSICA kuingia katika Historia ya Muziki huko ZAÏRE (CONGO) kwa sababu :

1.Ni wa kwanza katika Generation yake kupewa tuzo binafsi la Dhahabu kutokana na wimbo wake wa MULOLO Mwaka 1988.

2.Kateuliwa mwimbaji bora Inchini ZAÏRE Mwaka 1991

3.Ni wakwanza kati ya wanamuziki wa kizazi kipya huko CONGO kufanya SHOO kwenye Kumbi za kifahari Mjini PARIS (OLYMPIA na ZÉNITH).

4.Ni kijana wa kwanza kwa wale wa umri wake ambae kapewa tuzo la GOLDEN RECORD (DISK)

JB MPIANA ni mmoja kati ya wanamuziki wa huko CONGO amabae kapewa tuzo nyingi huku bado akiwa na Umri mdogo :

-Mwaka 1988 akiwa bado na miaka 21 kapewa tuzo la mtunzi wa wimbo bora (MULOLO)

-Mwaka 1991 akiwa na miaka 24 kateuliwa mwimbaji bora

-Mwaka 1999 akiwa na miaka 32 kapewa tuzo la Golden Record (DISK) kutokana na Album yake ya LES FEUX DE L’AMOUR iliyotolewa mwaka 1997.

JB MPIANA kashika record ya kuwa kijana mwana muziki mwenye kua na Umri mdogo (CONGO) kufanya SHOO kabambe kwenye kumbi za ZÉNITH,OLYMPIA,PALAIS OMNISPORTS DE BERCY,Mjini PARIS.

JB MPIANA kafanya SHOO kabambe pia kwenye kumbi za ELYSÉE MONTMARTRE,BATACLAN,DOCK EIFFEL hapohapo PARIS,

Kwenye PALAIS DE CONGRÈS Mjini LIÈGE (BELGIUM)

Na kwenye ukumbi wa MEDLEY Mjini MONTRÉAL huko CANADA.

Baada ya mgawanyiko wa WENGE MUSICA 4×4,mwaka 1997, JB MPIANA kawa na kundi lake la WENGE MUSICA “LES ANGES ADORABLES”akiwa pamoja na ALAIN MAKABA,BLAISE BULA,ALAIN MPELA,TUTU KALUDJI,ROBERTO EKOKOTA,AIMELIA yaani baadhi ya wanamuziki wote wa WENGE MUSICA asilia.

Papo hapo JB MPIANA na kundi lake wakaenda Ulaya ku rekodi ALBUM ya TITANIC amabayo inadhihirisha mgawanyiko wa kundi la WENGE MUSICA 4×4.

Utamsikia JB MPIANA akisema “IL N’Y A RIEN C’EST L’HOMME QUI A PEUR” HAMNA LOLOTE NIWOGA TUU UNAO WASHIKA.

ALBUM TITANIC ina nyimbo 10 :

1. Titanic Tutu Callugi/Wenge BCBG

2. RDC JB Mpiana

3. Barakuda Alain Makaba

4. Omba JB Mpiana

5. Proces Mambika Alain Mpela

6. Likala Moto Blaise Bula

7. Tour Eiffel Titina Mbwinga Alcapone

8. Champion Kapangala JB Mpiana

9. Liberation Aimelia Lias

10. Serge Palmier Burkina Fasso

Mwaka 1999 kamayalivyo andikwa hapo juu,JB MPIANA kafanya SHOO kabambe Mjini PARIS kwenye Kumbi za ZÉNITH na OLYMPIA.

Baadae kasema hataki tena kudumbwiza kwenye ukumbi bali kwenye viwanja,ndipo mwaka huohuo kashuka Mjini COTONOU huko BENIN na kafanya Shoo kabambe.

Baada ya hapo kaja dumbwiza Mjini KINSHASA kwenye STADE DE MARTYRS watu zaidi ya 85000 waliudhuria…

Mwaka huo 1999 JB MPIANA katoa Album SINGLE yake akaipa jina

Y’A PAS MATCH Y’A PAS PHOTO ikiwa na nyimbo 2 :

1. Y’a pas match, Y’a pas photo JB Mpiana

2. Papito Mbala (Version 2) JB Mpiana

Mwaka 2000 JB MPIANA katoa ALBUM yake ya pili ya SOLO

Pichani JB Mpiana akiwa na Mke wa Debs Demukalinga jijini Dar Es Salaam Hivi Karibuni.

T H ( TOUJOURS HUMBLE) ikiwa na Volume 2 na nyimbo 16 :

Volume 1

No Titre Auteur(s) Durée

1. TH (Toujours Humble) JB Mpiana

2. Walay Danico JB Mpiana

3. Education JB Mpiana

4. Sultan de Bruneil Kaskinto JB Mpiana

5. Dis-moi Amour JB Mpiana

6. Rose verte JB Mpiana

7. Grâce à toi Germain JB Mpiana

8. Jeanpy Pipina JB Mpiana

9. 48 Heures Gecoco JB Mpiana

10. Bye Bye Julie JB Mpiana

Volume 2

No Titre Auteur(s) Durée

1. Mohamed Kaniansy JB Mpiana

2. Aminata Sylla JB Mpiana

3. Kinshasa JB Mpiana

4. Bye Bye Julie (version disco) JB Mpiana

5. Lauréat’s 2000 JB Mpiana

6. Acappella

Sifa nyingi zilimwendea JB MPIANA kutokana na ALBUM hii na ikamwezesha kupata kwa mara ya pili tuzo la GOLDEN RECORD (DISK) pia na tuzo nyingine nyingi :

-Mwimbaji bora,-Album bora,-Wimbo bora “48 Heures GECOCO”

-Mtunzi Bora “wimbo Grace à toi Germain”

-Mwanamuziki Bora.

Masterpiece hii ilifanya JB MPIANA aweke Mguu wake kwenye World Music, na pia kajifungua kwenye aina mbalimbali ya Muziki kama vile : RAP,SALSA,

Hebu pata uondo kwa kusikiliza nyimbo zifwatazo (WALAY DANICO,EDUCATION,SULTAN DE BRUNEI,DIS MOI AMOUR,LA ROSE VERTE,BYE BYE JULIE,AMINATA SYLLA.

Mwaka 2000 mwezi wa nane hadi kufikia mwaka 2001 mwezi wa Inne,

JB MPIANA na kundi lake wakaanza kufanya SHOO mbalimbali mjini KINSHASA,mwishowe wakafaanikiwa kusafiri na kwenda Nchi mbalimbali duniani ambako walifanya zaidi ya SHOO 30. walienda FRANCE,BELGIUM,HOLLAND,GERMANY,SWISS,IRELAND,UK, na CANADA.Wakamalizia dhiara yao Nchini CHAD amabapo walifanya SHOO kabambe 3.

Itaendelea Jumatano…


%d bloggers like this: