Mwana wa Mohammed Ali alipozuru Kinshasa

November 30, 2009

Lilikuwa pambano la kipekee, ambalo bara la Afrika halijabahatika kushuhudia tena kwa miaka 35.

Tarehe 30 mwezi Oktoba, 1974, mabondia maarufu Mohammed Ali na George Foreman walitandikana jijini Kinshasa, katika nchi ambayo wakati huko ilikuwa ikijulikana kama Zaire – sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Khaliah Ali akiwa na Katibu mkuu wa wizara ya michezo, Barthelemy Okito, wakati alipozuru Kinshasa.

Mwaka huu Kongo imepata ugeni unaokumbushia mpambano huo, Khaliah Ali, binti na mtoto wa mwisho wa Mohammed Ali, alizuru Kinshasa na kujiunga na wanandondi kusherekea kumbukumbu la pigano hilo la kihistoria.

Khaliah Ali, alishangiliwa na wanandondi wengi katika uwanja wa Tata Rafael kwa jina maarufu “Rumble in the Jungle” kwenye sherehe ya kumbukumbu ya pigano baba yake Mohammed Ali alimtandika George Foreman kwenye uwanja huo miaka 35 iliyopita.

Bi Khaliah Ali, ambaye alikuwa bado mchanga wakati baba yake akitoana jasho na George Foreman, alizuru vyumba na sehemu mbali mbali za uwanja huo. Na alipofika katika chumba kilichotengwa kwa ajili ya baba yake, alibubujikwa na machozi.

“Ni hali yenye harara kuzuru mahali ambapo baba yangu aliwahi kupigina hapa Congo. Singeliweza kuzuia machozi yangu nilipo ona picha za baba na mababu zangu hapa. Nakukutana na Waziri wa michezo na wanandondi hapa ilitugusa sana. Ni muhimu kwangu kuwapatia yale mliyompatia baba yangu wakati alipopigana hapa,” alisema Khaliah.

Hata hivyo, ziara yake iliambatana na madai kuwa wakati Mohammed Ali alipokuwa Kinshasa aliwaahidi wanandondi kuwa atawasaidia kuchangia kuendeleza ndondi za DRC wakati huo ikijulikana kama Zaire.

Wanandondi hao wanadai mpaka sasa Mohammed Ali hajatekeleza ahadi hiyo. Lakini katibu mkuu wa wizara ya michezo, Barthelemy Okito, ndiye alichukua fursa ya ziara ya Khaliah Ali kuomba amkumbushe baba yake kuhusu ahadi hiyo.

“Mohammed Ali, baba yake Khaliah alikuwa akisema kuwa ana mizizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na barani Afrika. Nilikutana na wanandondi hapa ambao walisema kuwa Mohammed Ali, aliwaahidi kusaidia maendeleo ya ndondi hapa nchini. Na tutatumia ziara ya mtoto wake kumkumbusha kuhusu ahadi hiyo.”

 Uwanja wa Tata Rafael

Hapa ndipo "Rumble in the Jungle" ilipofanyika, uwanja wa Tata Rafael mjini Kinshasa.

Si wanandondi peke yao waliokuwa wakitegema kutumia ziara hiyo kuomba usaidizi. Meneja mkuu wa uwanja wa Tata Rafael, anategemea kuwa ziara ya mtoto wa Mohammed Ali inaweza kuwasaidia kupata msaada ya kukarabati uwanja wao.

Uwanja huo umekuwa katika hali duni sababu umeachwa baada ya uwanja mwingine mkubwa wa Kinshasa, “Stade des Martyrs”, kujengwa kutokana na uhusiano kati ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na China.

Kabla ya kuwasili Kinshasa na kuzuru uwanja wa “Rumble in the Jungle” ambapo baba yake alimdunda George Foreman katika raundi ya nane kwa knockout, Khaliah, alizuru Lubumbashi ambako anafadhili kituo kimoja cha kusaidia kinadada na wanawake wasiojiweza.

Habari hii ni kwa mujibu wa BBC


Chokoraa, Kalala Jr, Chaz Baba na Jose Mara waja kama Mapacha wanne! na kuwasha moto LEO!!

November 30, 2009

image

Wanamuziki wanne wenye kipaji cha Muziki hasa Khalid Chokoraa, Kalala Jr, Chaz Baba na Josee Mara, kwa pamoja usiku wa leo watatoa burudani katika ukumbi wa Java Stereo Kinondoni katika kutambulisha Albamu yao na nyimbo zao mpya.

Katika usiku huu wa aina yake wanamuziki hawa watasindikizwa na TID akiongoza bendi yake ya Top Band na kiingilio kimetajwa kuwa ni Tsh. 5000 tuu.


Drogba awekeza katika huduma za afya

November 30, 2009

image

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba ambaye jana aliikabili Arsenal na kuifungia timu yake bao mbili kati ya tatu  katika mchezo wa Ligi Kuu England, lakini akiwa ameelekeza akili zake nyumbani kwao.

Kupitia wakfu wake, Drogba Foundation, mshambuliaji huyo aliyekuwa ziarani hapa wiki moja iliyopita na kutembelea makazi ya watu maskini ameamua kuweka nguvu zake katika kuwasaidia.

Alianzia ziara yake katika viunga vya jiji la Abidjan vyenye vumbi jingi na kujionea hali mbaya ya afya inayowakabili ndugu zake.

"Nilikulia mahali hapa, mahali hapa ninapenda kujenga hospitali kwa ajili ya watu wangu wakatibiwe," alieleza.

Read the rest of this entry »


Maximo inatosha tuachie timu yetu!!

November 30, 2009

image

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara – Kilimanjaro Stars jana imebugizwa na Uganda mabao 2-0 Katika mchezo ulichezwa upande mmoja zaidi kwenye michezo ya Chalenji mjini Mumais.

kila msiba una mwenyewe na sie wengine tunasaidia kulia tuu, lakini Mnapokuwa kwenye familia ndugu kumi haina maana akifa baba kaka mkubwa ndio mfiwa, wote ndio wafiwa. kwa msiba wa Taifa Stars, wafiwa sio TFF wao wanasimamia shughuli za Msiba kwa niaba yetu

Tanzania ambayo haikuonyesha mchezo mzuri imeendeleza wimbi la kushindwa jambo ambalo linampa wakati mhumu Kocha wa Timu hiyo Mbrazir Marcio Maximo.

Mashabiki ambao wameonyesha kuchoshwa na matokeo mabaya ya timu hiyo wanashangazwa na ujasiri na kiburi ambacho Marcio Maximo anacho kwenye timu hiyo. Aidha mashabiki wake wamesema kuwa inatosha MAximo alipoifikisha timu kwa sasa inafaa mtu apewe mtu mwingine aiendeleze, “ Maximo amefikia kikomo cha uwezo wake ni wazi alipoifikisha klabu ni pazuri aiache apewe mtu mwingine, kwa mshahara anaopewa tunaweza kupata Kocha mzuri tuu tukiamua” Alisema mshabiki mmoja kwa jina la Jibaba.

“ si suala la uraia, hatutaki hata kama ni Mbraziri kama hatuoni mafanikio ni bora aondoke tumpate mtu mwingine ambaye tutamuajiri kwa malengo kwa mkataba wa miaka angalao mitatu tumuangalie” aliongeza mshabiki mwingine.

Kwa kawaida Maximo hawezi kuondoka pale kwa mshahara anaopata hawezi kupata timu inamlipa vile kwa kiwango chake cha ufundishaji, TFF kwa kushirikiana na asasi husika wanaweza kuendesha mchakato mzuri tuu wa kutangaza ajira ya Kocha na kumpata mtu ambaye ana vigezo na viwango.

Leo hii timu ina kila aina ya msaada na wadhamini lukuki lakini bado haina mafanikio yoyote. Kwa nini watu washabikie ligi ya uingereza kwa kasi zote inaonyesha kuchoshwa na matokeo mabaya ya timu yao kila uchao. Taifa Stars imekuwa na sababu za kushinda na sababu za kushindwa. Watanzania tumechoka!!! Maximo tuachie timu yetu!.

Rais alisema wakati wa kupokea ujio wa Kombe la Dunia kwamba kila msiba una mwenyewe na sie wengine tunasaidia kulia tuu, mi nasena Mnapokuwa kwenye familia ndugu kumi haina maana akifa baba kaka mkubwa ndio mfiwa, wote ndio wafiwa. kwa msiba wa Taifa Stars, wafiwa sio TFF wao wanasimamia shughuli za Msiba kwa niaba yetu ila wote sisi ni familia moja pia tuna machungu ya msiba huu na sauti kwenye mipango ya Mazishi.


Maximo inatosha tuachie timu yetu!!

November 30, 2009

image

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara – Kilimanjaro Stars jana imebugizwa na Uganda mabao 2-0 Katika mchezo ulichezwa upande mmoja zaidi kwenye michezo ya Chalenji mjini Mumais.

kila msiba una mwenyewe na sie wengine tunasaidia kulia tuu, lakini Mnapokuwa kwenye familia ndugu kumi haina maana akifa baba kaka mkubwa ndio mfiwa, wote ndio wafiwa. kwa msiba wa Taifa Stars, wafiwa sio TFF wao wanasimamia shughuli za Msiba kwa niaba yetu

Tanzania ambayo haikuonyesha mchezo mzuri imeendeleza wimbi la kushindwa jambo ambalo linampa wakati mhumu Kocha wa Timu hiyo Mbrazir Marcio Maximo.

Mashabiki ambao wameonyesha kuchoshwa na matokeo mabaya ya timu hiyo wanashangazwa na ujasiri na kiburi ambacho Marcio Maximo anacho kwenye timu hiyo. Aidha mashabiki wake wamesema kuwa inatosha MAximo alipoifikisha timu kwa sasa inafaa mtu apewe mtu mwingine aiendeleze, “ Maximo amefikia kikomo cha uwezo wake ni wazi alipoifikisha klabu ni pazuri aiache apewe mtu mwingine, kwa mshahara anaopewa tunaweza kupata Kocha mzuri tuu tukiamua” Alisema mshabiki mmoja kwa jina la Jibaba.

“ si suala la uraia, hatutaki hata kama ni Mbraziri kama hatuoni mafanikio ni bora aondoke tumpate mtu mwingine ambaye tutamuajiri kwa malengo kwa mkataba wa miaka angalao mitatu tumuangalie” aliongeza mshabiki mwingine.

Kwa kawaida Maximo hawezi kuondoka pale kwa mshahara anaopata hawezi kupata timu inamlipa vile kwa kiwango chake cha ufundishaji, TFF kwa kushirikiana na asasi husika wanaweza kuendesha mchakato mzuri tuu wa kutangaza ajira ya Kocha na kumpata mtu ambaye ana vigezo na viwango.

Leo hii timu ina kila aina ya msaada na wadhamini lukuki lakini bado haina mafanikio yoyote. Kwa nini watu washabikie ligi ya uingereza kwa kasi zote inaonyesha kuchoshwa na matokeo mabaya ya timu yao kila uchao. Taifa Stars imekuwa na sababu za kushinda na sababu za kushindwa. Watanzania tumechoka!!! Maximo tuachie timu yetu!.

Rais alisema wakati wa kupokea ujio wa Kombe la Dunia kwamba kila msiba una mwenyewe na sie wengine tunasaidia kulia tuu, mi nasena Mnapokuwa kwenye familia ndugu kumi haina maana akifa baba kaka mkubwa ndio mfiwa, wote ndio wafiwa. kwa msiba wa Taifa Stars, wafiwa sio TFF wao wanasimamia shughuli za Msiba kwa niaba yetu ila wote sisi ni familia moja pia tuna machungu ya msiba huu na sauti kwenye mipango ya Mazishi.


Maisha Music Newsletter November 2009 – Kiswahili

November 30, 2009

Maisha Music ndani ya Womex 2009

091128 Ashimba email

Ikihudhuriwa na zaidi ya wadau 3000, Womex 2009 ilifanyika katika ukumbi wa Bella Center (Mikutano na vibanda vya maonyesho) pamoja na ukumbi mpya unaomilikiwa na Taasisi ya habari Denmark, ujulikanao kama Koncerthuset. Na kama ilivyo ada, tukio hili ni moja ya matukio muhimu sana na huwakusanya wadau wa muziki kutoka karibu kila nchi duniani. Kwa miaka 14 Womex imeweza kutngeneza mazingira madhubuti na ambayo huwawezesha waandaaji matamasha, makampuni ya muziki, wasanii, mameneja na mapromota kukutana na kubadilishana uzoefu kuhusu mambo mbalimbali yanayoigusa sekta ya muziki wa kidunia. Maisha Music Tanzania iliwakilishwa na Kwame Mchauru na jakob Poll. Kwa muda wa siku nne madhari ilikuwa ni ya pilikapilika, huku wadau wakikwaruzana mabega kutembelea banda moja hadi lingine pamoja na kuhudhuria mihadhara na mikutano. Wakati wa usiku wengi wetu tulikusanyika katika ukumbi wa Koncerthuset kwa ajili ya kuangalia na kusikiliza burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali ambao walifanya maonyesho katika kumbi tano tofauti.

Maisha Music tunayo imani kubwa kuwa mahusiano ya ushirikiano yaliyojengwa katika tukio hili, siku za baadaye yatasaidia katika kuchochea juhudi za kuupandisha muziki wetu ili uweze kufahamika na kukubalika kimataifa zaidi. Makampuni mbalimbali ya usambazaji, matamasha pamoja na wasanii wameonyesha nia thabiti ya kufanya kazi pamoja nasi baada ya muda si mrefu.

Mwaka huu tuzo ya Womex (Womex award) imekwenda kwa Staff Benda Bilili, Kundi la wanamuziki walemavu na wasio na makaazi maaluma lakini wapigao muziki wenye mvuto wa kipekee kutoka katika viunga vya mji wa Kinshasa.

Maisha Compilation 2009 ipo mtaani tayari…

Huu ni mwendelezo wa matoleo ya kila mwaka na hili likiwa ni la pili baada ya lile la mwaka 2008. Albamu hii inakuonjesha ladha ya nyingine (Maisha Lounge Vol 1) inayotarajiwa kutolewa hivi karibuni . Toleo hili ni mchanganyiko wa wasanii maarufu hapa Tanzania kama vile Carola Kinasha, Ray C, Ashimba, K-Lyinn, Hardmad wakishirikiana na wasanii wa kimataifa Karen Mukupa na Phantom kutoka Denmark. Ladha ya mchanganyiko huu inaanza kwa muziki taratibu kabisa katika nyimbo 5 za kwanza. Zilizobaki ni zile zenye mahadhi ya kuchezeka ambazo ni mchanganyiko wa afro pop, reggae, dancehall na R&B.

Albamu hii itauzwa kwenye mtandao kuanzia katikati ya mwezi Desemba, lakini kwa sasa hivi nakala za CD zinapatikana bila ya malipo kwa ma-DJ, maduka mbalimbali, migahawa, Mabaa, taxi, Mabasi, Daladala, radio nk…. TAFADHALI TUANDIKIE IWAPO UTAHITAJI NAKALA YA BURE KATIKA ENEO LAKO NA TUTAKULETEA, hapa Tanzania na kwa upande wa radio popote duniani…

Maisha Music, Ashimba & Karen Mukupa watoa wimbo unaotumika kwenye mchezo wa Kompyuta "Kiberas Stjerne"

Kama kawaida shirikika la utangazaji la Denmark, huwa linasaidia katika miradi mbalimbali ya maendeleo Duniani kote, na hii ni kutokana na fedha zinazopatikana kutokana na mauzo ya kalenda ya kila mwaka ya Krismasi. Mwaka huu fedha hizo zitatumika katika mradi wa kusaidia watu waishio makaazi yasiyo rasmi ya Kibera huko Nairobi Kenya. Na kutokana na mauzo ya kalenda ya hiyo mchezo maarufu wa kompyuta umebuniwa na kutayarishwa, mchezo huo unamwelezea kijana mdogo kutoka maeneo ya Kibera ambaye anajaribu kupata ala kwa ajili ya shindano la kutafuta vipaji. Muziki uliotumika katika mchezo huu wa Kiberas Stjerne (Nyota wa Kibera) umetolewa na Maisha Music na unahusisha wimbo mkali wa Ashimba “Yaya”. Lakini katika toleo hili wimbo huu umeimbwa na msanii maarufu mwenye asili ya Denmark na Zambia Karen Mukupa. Karen amekulia Tanzania na ni mwenye ufahamu mzuri kabisa wa lugha ya Kiswahili. Kiberas Stjerne imetengezwa na Congin, Danida og OVE.

Angalia mchezo huu katika www.kiberasstjerne.dk

41 Boom Shack – Jumamosi tarehe 28 Novemba

41 Records na Maisha Music kwa mara nyingine wanaandaa tukio la muziki wa reggae, dancehall na Hip Hop night la kila mwezi ambalo hufanyika katika ukumbi wa Alliance Francaise. Mwezi huu kutakuwa na onyesho kali kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Nako 2 Nako Soldiers.. Wasanii hao watakuwa ni sehemu ya wale watakaoonyesha umahiri wao wa kufokafoka juu ya midundo ya Rap za zamani hususan ile ya De La Soul na kuingiza Kiswahili ndani yake. Wasanii wengine watakaoshiriki ni pamoja na Mr Mbeya na Lufu. Muongozaji wa midundo (DJ) atakuwa si mwingine bali ni Jakob Poll kutoka Maisha Music. Burudani nyingine kwa siku hiyo itaporomoshwa na wasanii mahiri katika upigaji wa ngoma, Afriye (Band With no Name) na Twaba (Wahapahapa band)….

Nini: 41 Boom Shack – Nako 2 Nako Soldiers, Old School De La Soul Jam, katika Percussion Crash watakuwepo Afriye na Twaba lakini pia na wengine wengi watakaribishwa …

Wapi: Alliance Francaise

Lini: Jumamosi tarehe 28 Novemba, Saa 3:00 Usiku

Kiingilio: Shilingi 5000 tu …

Maisha Music Kutayarisha sauti kwa ajili y maonyesho ya "The Roof of Africa"

Hili ni onyesho la sanaa mchanganyiko ambalo limeandaliwa na mchoraji maarufu L.M. Johannessen, mpiga picha Sasja van Vechgel, mshairi Langa na sauti imetayarishwa na produza Jakob Poll wa maisha Music.

Onyesho hili la “The Roof Of Africa”   Litafanyika katika ukumbi wa maonyesho uliopo Alliance Francaise kuanzia tarehe 4 Desemba hadi tarehe 16 Januari 2010, na ni kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi 12:00 jioni (AF itafungwa kuanzia tarehe 13 Desemba hadi 3 Januari).

Nini: michoro, picha, ushairi, sauti na taa  – ni sanaa mchanganyiko…

Lini: Alhamisi tarehe 3 Desemba saa 1:00 usiku

Wapi: Alliance Francaise – Ukumbi wa maonyesho

Kiingilio ni bure…

Maisha Events/Booking

Maisha Music vile vile inafanya kazi ya kupeleka wasanii katika maonyesho mbalimbali na kuandaa shughuli. Hadi sasa tunayo orodha ya wasanii wengi na baadhi yao ni bendi za muziki, wasanii wa muziki wa kizazi kipya, sarakasi, ngoma za utamaduni, ma-DJ nk. Uhusiano wetu wa karibu na Our 41 Records umetuhakikishia kupata vifaa vya muziki vyenye uhakika pamoja na fundi mitambo bora hapa mjini.

Baadhi ya wasanii ni hawa wafutao:

Ashimba

– Hardmad

– Jagwa Music

– Splendid Theatre

– Carola Kinasha

– Wahapahapa Band

– DJ Mukada

– DJ Mateo

Iwapo utahitaji taarifa zaidi, tafadhali wasiliana nasi katika info@maishamusic.com.

Kalenda ya burudani

Sasa Maisha Music tumeanzisha utaratibu mpya wa kuwa na kalenda ya matukio ya sanaa na utamaduni. Kalenda hii itajumisha matukio binafsi pamoja na yale ya kila wiki. Tunafahamu kuwa siyo rahisi kutoa taarifa za kila kinachojiri, lakini tutajitahidi kwa kadri invyowezekana. Hivyo iwapo unayo taarifa ya tukio lolote tafadhali tutumie taarifa kwa barua pepe.

Jumatano Jioni/Usiku

Out of Afrika, Twanga Pepeta

Club Bilicanas, City Centre

Alhamisi saa 4:00 usiku

Inafrika Band

Sweet Easy, Oysterbay

Ijumaa Saa  3:00 hadi-7:00 Usiku

Carola Kinasha

Kempinski, Level 8

Jumapili saa 10:00 hadi 2:00 usiku

Splendid Theatre

Daralive, Mikocheni B

Jumapili saa 11:00 hadi 5:00 usiku

Akudo Impact

Msasani Beach Club, Kawe

Jumapili saa 6:30-9:30 usiku

Carola Kinasha

Kempinski "Brunch"

Jumapili Usiku

Lady Jay Dee

Thai Village, Masaki

Jumapili saa 12:00 Jioni

FM Academia

New Msasani Club

Novemba:

Tarehe 24 hadi 28 Kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Maonyesho ya mavazi kutoka kwa Mustafa Hassanali

Alliance Francaise, Upanga

Tarehe 27 hadi 28 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Makutano Fair

Diamond Jubilee Hall, Upanga

Tarehe 27 kuanzia saa 3:00 usiku

Usiku wa HIP HOP – Massive Töne (Germany) + Fid Q na Mzungu Kichaa

Russian Cultural Center, Sea View Road

Tarehe 27 kuanzia saa 3:00 usiku

Urban Motion – Ashimba, Malfred & Abby Sykes

Hugo Bar, Kinondoni Road

Tarehe 27 kuanzia saa 9 alasiri hadi 3 usiku

WaPi Zanzibar -Jukwaa la kuonyesha vipaji mbalimbali-   Swahili vibe, Cheka nao, Chabi six na wengine wengi. Pia kutakuwa na shindano la uchoraji.

Ngome Kongwe, Zanzibar

Tarehe 27 kuanzia saa 3 usiku

Urban motion ikimshirikisha Ashimba

Hugo Bar, Kinondoni makaburini

Tarehe 28 kuanzia saa 3:00 usiku

41 Boom Shack – Reggae, Dancehall na Hip Hop (Percussion splash na Nako 2 Nako Soldiers)

Alliance Francaise, Upanga

Tarehe 28 kuanzia saa 2 usiku

Ashimba kufanya onyesho – Kamambe nights

Tasuba theatre, Bagamoyo

Desemba:

Tarehe 2 kuanzia saa 1:00 usiku

Barazani – muziki kutoka kwa (Jhikoman & John Sombi Band) simulizi kutoka kwiz dance

Simulizio kutoka Alliance Francaise, Upanga

Tarehe3 kuanzia saa 1:00 usiklu

Roof Of Africa – Ufunguzi wa maonyesho ya picha, sauti na ushairi

Alliance Francaise, Upanga

Tarehe 12 kuanzia saa 3:00 usiku

41 Boom Shack – Reggae, Dancehall na Hip Hop

Alliance Francaise, Upanga

Subscription to newsletter
If you want to subscribe to Maisha Music’s Newsletters you can send an email to info@maishamusic.com and write "subscribe" in the subject box. If you have recieved this newsletter from info@maishamusic.com, your email are for some reason subscribed to Maisha Music’s newsletter. If you don’t wish to receive more newsletters from Maisha Music, please send us a email saying "unsubscribe newsletter" and your email address will be deleted from the list. Sorry for any inconvenience..


www.maishamusic.com
www.myspace.com/maishamusictz
www.youtube.com/maishamusictz
www.twitter.com/maishamusictz
www.facebook.com/group.php?gid=74932459086


Mat-Rapisti

November 30, 2009

image

Mat Rapisti ni neno linalotumika kwa Wamalay kuelezea utundu wa barabarani wa madereva wa pikipiki ambao mara nyingi hupelekea ajali ambazo zinapoteza maisha na mali zao.

Mat likiimaanisha Motor, na Rapisti likimaanisha chizi. MAlaysia ni moja ya nchi ambazo zina pikipiki nyingi mnoo jambo ambalo linapelekea serikali kupata taabu kupambana na wakorofi hawa.

Hivi karibuni serikali iliwakilisha bungeni mswada wa kuomba hawa watu watambuliwe kwa kuwepo mchezo rasmi na hivyo kuwafanya wawe na sehemu maalumu ya kuonyesha uhodari wao, mjadala huo haukupita kwa vile ulikuwa na na mapungufu kadhaa.


%d bloggers like this: