Wamtambua nani hapa?

July 28, 2013

image


Tutu Kaludji aokoka, ageukia Muziki wa Injili

July 26, 2013

Mwanamuziki Nguli aliyewahi kutamba na bendi ya Wenge BCBG Tutu Kaludji ameokoka na sasa ameamua kumuimbia Mungu. Kaludji ambaye mbali ya kuwa atalaku namba moja wa Wenge BCBG alikuwa mtunzi pia na aliwahi kutamba na kibao kama Tchico Londonien.

Kaludji alipanda mdhabahuni kanisani huko Paris na kuungama dhambi akiongozwa na mchungaji mbele ya waumini na kutangazwa kaokoka rasmi. Nimeamua kuwa balozi wa Yesu alisema Kaludji huku akibubujikwa na machozi.

Kaludji ambaye mbali ya kuwa mwanamuziki wa Wenge BCBG pia alikuwa mmoja wa Share holder, Habari zaidi zinasema baada ya ungamo la toba Kaludji alisimama mbele na kutoa ushuhuda jinsi alivyoishi maisha yake ya kipagani na kusema sasa maisha ya kumtumikia shetani sasa basi ameamua kumrudia na kumtumiakia Mungu ambapo waumini walimshangilia kwa neremo na vifijo.

Katika historia ya muziki wa Kongo Kaludji anachukuliwa kama ni mmoja ya watu walioleta mageuzi kwa kuingiza ghani huku akiwa amempokea Robert Wunda Ikokota kwenye atalaku na wanamuziki wengine kuiga style hiyo ambayo mwenyewe aliwaita “Wana Kaludjist”. alijitambulisha kwenye ulimwengu wa muziki kama atalaku mwaka 1995 kwenye albamu ya JB Mpiana ya Feux de l’amour. Huyu ni mmoja wa wanamuziki wa kizazi cha nne cha muziki wa Congo ambaye ana nafsasi (Share) kwenye mageuzi ya muziki wa Congo na hatosahaulika haraka.

mwaka 1997 kundi la Wenge Musica liliposambaratika Kaludji aliamua kubaki kambi ya JB Mpiana ambapo waliendeleza mapambano na mwaka 2001 baadaye walipiga show kubwa sana yenye mafanikio Zenith Ufaransa. miaka 12 baadaye Kaludji aliamua kujitoa kwenye kundi la Wenge BCBG na kuanza kivyake ambapo alitoa albamu moja iliyojulikana kama “Paris Match” ambayo haikufanya vizuri kutokana na Promotion ndogo na hatimaye mwaka huu kuamua kuokoka.”


Koffi aingia Studio kuipika albamu yake mpya itakayoitwa "13th Apostle"

July 26, 2013

Koffi Olomide Pichani akifurahia jambo na shabiki wake katika kushereheka siku yake ya kuzaliwa karibuni.

Mwanamuziki Koffi Olomide anazidi kusherehekea mnafanikio yake kimuziki baada ya kuingia Studio hivi karibuni akiwa anapika albamu yake mpya huku akisherehekea mafanikio ya albamu yake ambayo bado iko sokoni na inafanya vizuri.

Kwa mujibu wa Meneja wa Koffi albamu hiyo mpya inatengenezwa Studio Ndiaye ambapo inatazamiwa kutoka kwenye sherehe za mwaka mpya 2014.

Koffi anakubukwa kwa uwezo mkubwa wa kuunda timu ya wanamuziki hatari ambapo bendi yake imeshavunjika zaidi ya mara mbili na kila mara amekuwa na uwezo mkubwa wa kuunda kikosi ambacho kinakuja na uwezo wa kuwasahaulisha mashabiki kama kuna mabadiliko yaliwahi kutokea.

“Koffi Olomide ni kama Morinho na timu yake, Qurtier Latin ni kama Dream Team ya Marekani, anatoka mzuri anakuja mzuri zaidi” alisema Julie Weston Ilunga aka Baba Bee, Mtanzania mwenye asili ya Congo anayeishi nchini na Mtu pekee toka hapa anayeimbwa kwenye Albamu zote mpya ya Koffi, JB Mpiana, Fally Ipupa na Werasson, usiniulize amekata bei gani kwani hilo nitakuja nalo kwenye story inayomhusu Julie Weston Ilunga hivi karibuni.

Hii itakuwa ni albamu ya 20 ya Koffi tangu aanze kujishughulisa na muziki, na mpaka sasa anasherehekea akiwa na mafanikio makubwa sana, Katika kizazi chake ambacho kilikuwa na wanamuziki kama Pascal Tabu Ley, Franco Luambo Makiadi et Lutumba Simaro Masiya. Koffi ana Albamu nyingi ambazo zimefanya vizuri sokoni  Attentat, Monde arabe, Koweit rive gauche, Abracadabra, Album du patron, kati ya hizo albamu kama Haut de Gamme: Koweït, Rive Gauche zimo ndani ya Albamu 1001 ambazo unapaswa kuzisikia kabla hujafa (1001 Albums You Must Hear Before You Die). Hiki ni kitabu akinachohusu mambo ya muziki gonga link usome zaidi.

Mbali na hiyo Koffi ameshawafunda wanamuziki wengi ambao ama walipita ama kufanya kazi katika bendi yake mfano Fele Mudogo, Sam Tshintu, Suzuki 4×4,Soleil Wanga, Fally Ipupa, Montana Kamenga, Ferre Gola na wengineo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kurejea kutoka ziarani Angola ambako alikuwa na VIP Show kadhaa Koffi amesema kuwa mashabiki wategemee makubwa kwenye albamu yake inayokuja ambayo anatazamiwa kuwa na nyimbo 12. Ziara hiyo ya Koffi ilimaliza uvumi kuwa mwanamuziki huyo alinyimwa Romeo Golf huko Gombe majuzi na kufanya wanausalama kuingilia kati na kuongeza nguvu kuwababili mashabiki ambao walikuwa na shauku ya kumuona.


%d bloggers like this: