Mpoto kuiwakilisha tanzania Ufaransa

May 7, 2009

MSANII Mrisho Mpoto ataliwakilisha bara la afrika katika mashindano ya Ushairi yatakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao.

Akizungumza na Mwananchi, Mpoto alisema amepata bahati ya kushiriki katika mashindano hayo yajulikanayo kama World Slum Championship yatakayofanyika katika jiji la Ufaransa.

"Nathubutu kusema kuwa naiwakilisha Afrika katika mashindano hayo kwa kuwa mimi ni mtu pekee niliyepata bahati ya kushiriki katika mashindano hayo kutoka bara la Afrika" alisema.

Alisema mashindano hayo yatafunguliwa June 16 katika jiji la Ufaransa na kuendelea kwa wiki nzima ambapo washairi mbalimbali watakuwa wakichuana katika mashindano hayo.

Habari na Mwananchi Isome zaidi kwa kugonga hapa


Salamu zangu kwako Mjomba

July 25, 2008

Irene Sanga(kushoto) akiwa jukwaani na Elidadi Msangi. (Picha na Bob Sankofa)

Blog ya Bongo Celebrity kama kawaida ijumaa hukupatia wimbo mmoja kwa ajili ya kukupoza na mchakamchaka wa wiki nzima, weekend hii wamekuja na kibao Salamu Zangu tokakwake Irene Sanga akimshirikisha Mrisho mpoto na Elidadi Msangi ikiwa ni ombi langu rasmi, Bofya hapa ukakisikilize kibao hiki mwanana chenye mahadhi ya mashairi ya kimapokezo.

Aidha mashairi ya wimbo huo kama ulivyoandikwa na Irene Sanga ni haya hapa:-

Kiitikio
Taifa liwapo na huzuni lazima wote tufunge mikanda kiunoni ili matanga yaishe upesi, majanga yanapozidi kimo mioyo ya wanadamu huota kutu hizo ni salam zangu…
Pepo hazina sifa ila pawapo Jehanamu, uzuri ni kipimo cha ubaya, kwani kiumbe chenye uhai na mauti huongozwa na tamaa salam zangu kwako eeehh! Bonyeza hapa kusoma zaidi Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: