Brazil yaitungua Chile 3-0

September 8, 2008
Robinho

Robinho

Mchezaji wa Brazil Robinho akishangilia bao lake kwenye mchezo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2o1o dhidi ya Chile. Kwenye mchezo huo Brazil ilishinda 3-0. Robinho amesajiliwa na Man City ambao kwa sasa wanataka kumsajili Ronaldino pia.


Brazil yamtema Robinho kikosi cha Olympic

July 22, 2008
Robinho

Robinho

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brasil na Real Madrid ya Hispania Robinho jana ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kitakachokwenda kwenye ngija ngija za kuwania medali ya dhahabuu kwenye michezo ya Olympic huko China imefahamika leo.

Sababu za kumtema Robinho zimesemwa kuwa ni kutokana na machezaji huyo kuwa majeruhi kwa mujibu wa daktari wa timu ya Real Madrid.

Hata hivyo Shirikisho la soka la nchini Brazili limelaani uamuzi wa Real Madrid na kuuita wa dharau kwa nchi yao na wabrazili kwa ujumla kwa kusema hizi ni njama za kutaka kumtumia mchezaji huyo. akizungumzia sakata hilo, daktari wa timu ya Brazili Luiz Alberto Rosan alisema kuwa alijua kuwa Robinho ni majeruhi lakini bado alikuwa na nafasi ya kupona kwani aliumia kidogo sio vya kumfanya ashindwe kucheza kwa muda mrefu. Aidha akiongea juu ya sakata hilo Robinho mwenye miaka 24 anayecheza nafasi ya forward alisema kuwa amesikitishwa na kuikosa nafasi ya kuichezea timu yake kwenye mashindano muhimu ya Olympic huko Beijing.

Akizungumzia suala hili agent wa Robinho Wagner Ribeiro alisema sijawahi kumuona Robinho aliwa na huzuni kiasi a hiki, mara ya mwisho ni kipindi mama yake mzazi alipotekwa nyara na maharamia mwaka 2004. ingawa baadaye aliachiwa bila kudhuriwa.


%d bloggers like this: