Ally Mayai Tembele

July 31, 2012

Niko na Ally Mayai Tembele aliyekuwa mchezaji wa Yanga kwa takribani miaka Saba (Kiboko ya Azam) Kwa sasa ni Afisa Masoko Wizara ya Viwanda na Biashara, tuko Dodoma kwa sherehe za Nanenane zitakazoanza rasmi kesho.

Mayai ana mengi ya kuongea kuhusu soka la bongo nitakuletea kwa kina hapa hapa stay tuned humu ni Spoti na Starehe


Natamani Bongo Star Search ifikie huku siku moja…

July 31, 2012

Chezea Balotel wewe, ni Spoti na Starehe

July 27, 2012

Wataalamu wa michezo wanasema Pombe, Sigara na mazao yake ikiwemo shisha na mademu haviendani kabisa kwa wanamichezo, na huu ndio ugomvi mkibwa wa makocha na wachezaji wao, mpoo hapo?


Risasi kidole ya Mashujaa Band.

July 27, 2012

 

Mashujaa Band ni Bendi inayokuja kwa kasi sana kwenye muziki wa Dansi huku ikiundwa na wanamuziki mahiri kutoka bendi kongwe ya Twanga Pepeta, hii imefanya hata muziki wao kutotofautiana ladha na ule wa Twanga Pepeta, hi ni kibao chao kipya hebu na we kisikilize kisha uniambie kuna tofauti na Twanga unayoisikia?


Dessert ingeta (Malewa 2) ya WMMM iko jikoni

July 26, 2012

Na Hadj Le Jbnique,Boston,Massachussets,USA.

Hayawi hayawi sasa  yanaelekea kuwa,baada ya zile danadana nyingi kwa takriban miaka miwili za kukamilika kwa sehemu ya pili ya album ya malewa ya kwao wenge maison mere wakiwa pamoja na mzee mzima Le Roi De La Forret WERRASON sasas kwa uhakika mzigo uko mbioni kuwa realeased ambapo mashabiki wa WERRA na wa muziki wa lingala kiujumla watapata nafasi ya kuisikiliza na hatimae kuicheza album hiyo ambayo itakwenda kwa jina la “DESSERT INGETA” sasa itakua na nyimbo 14 badala ya 10 zilizopangwa kuwemo awali.

Album hii ingeweza kuwa sokoni mapema zaidi kabla ya mwezi huu wa july 2012 lakini kukatokea matatizo ya kiufundi ambayo yalisababisha kufutika kwa kazi kubwa ambayo tayari ilikua imesharekodiwa kitu kilichowalazimu Bana Maison Mere kurejea tena studio kuweka sawa mambo kazi ambayo wanaendelea nayo mpaka muda huu naandika hapa ambapo kwa sasa  Heritier Wata ya Ngiama a.k.a. Heritier Watanabe pamoja na kina Eboa Lotin, Capuccino, Papy Kakol, Olivier na Japonais ndio wanaingiza sauti zao ndani ya  “DESSERT INGETA” na baadae kundi lote lwa waimbaji watafuatia kutia vocals zao humo,je album hiyo itamaliza ubabe wa album ya SAYONS SERIEUX “mpunda” ya wenge bcbg uliodumu sokoni kwa takriban 2 years now?ama kwa hakika hilo ni suala la kusubiri na kuona

Pata kitu “likambo” hapa kama utangulizi tu wa raha zitakazokuwemo ndani ya DESSERT INGETA”,Sikiliza Congo Rhumba hilo,kamata mamaa cheza  malinga nayee Taratibu eeeeh…ha ha haaaa!


Mr Paul na The Okapi Guitar band ya Australia

July 26, 2012

 

Sundeck Paul

Kama kawaida Spoti Starehe inapenda kukukumbusha wanamuziki ambao walivuma na pengine hawajulikani wako wapi wanafanya nini, tuliwahi kufanya mahojiano na Mr Paul, Mr.Paul ambaye jina lake kamili ni Paul Mbena hivi sasa anaishi nchini Australia akiwa ameoa na ana mtoto mmoja, pia ni muajiriwa anafanya kazi kama Case Manager katika Brain Injury Rehabilitatioun Unit, Liverpool hospital huko huko Australia na bado anaendeleza muziki akiwa na kundi la Okapi Guitars, safari hii tulitaka kujua mengi kuhusu kundi hili ndipo nilipomuuliza Okapi Guitars na akina nani na wameanza lini kazi ya muziki?

Okapi Guitars imeanza lini?

Mr Paul: The Okapi Guitars ni Afropop bendi ya muda mrefu (since 1990s)  hapa Sydney. Mimi nilijiunga nayo mwishoni mwa mwaka jana November 2011 nikiwa mwaka wa mwisho Melborune University. Okapi Guitars wana historia ya muda mrefu katika medani ya muziki wa Kiafrika. Wamekuwa wakipiga  Zimbabwean chimurenga to Kenyan classics, to West African hi-life and afrobeat. The Okapi Guitars, kabla ya mimi kujiunga nao, wame-share stage na bands kama the  Mahotella Queens (South Africa), Tchico Tchicaya (Congo), na Oliver Mtukudzi na Thomas Mafumo (Zimbabwe)

Hivyo kujiunga kwangu na the Okapi Guitras ni nafasi kwangu kutangaza muziki wa Kiswahili toka Tanzania. 

IMG_1251

Kuna wananmuziki wangapi?

Mr Paul: The Okapi Guitars ina jumla ya manamuziki watano, pamoja na mimi kama lead singer. Wengine ni:

· John-Rhythm guitar

· Bernhard – Lead guitar

· Sigi- Bass guitar

· Chris- Drummer 

 

Paul_Mbenna_and_the_Okapi_Guitar_Band_compressed

Mr Paul akiwa na The Okapi Guitars

Je Kuna mkataba wowote kati yako na kundi hili? 

Mr Paul: Hakuna mkataba wowote kati yangu na the Okapi Guitars. Pia hakuna mkataba kati ya the Okapi Guitars na any of its members. Hii ni kwa sababu, wanamuziki wote wa the Okapi Guitars band wanachukulia musiki kama hobbie, usually tunapiga muziki weekends. Fortunately, kila member wa bendi ana kazi nyingine nje ya muziki. For instance, mimi (Paul) ni Case Manager katika Brain Injury Rehabilitatioun Unit, Liverpool hospital, John (Rhythm Guitar) ni Researcher, Bernard (Lead Guitar) ni High School Teacher, Sigi (Bass Guitar) ni Disability Worker, na Chris (Drummer) yupo katika field ya logistics.

Pia nilitaka kujua kama kwa sasa yuko chini ya Label yeyote yeye ama hilo kundi la Okapi Guitar

Mr Paul: Kwa sasa the Okapi Guitar band inarekodi kazi zake chini ya the Cut Snake records, ambayo inamilikiwa na John (rhythm guitarist). Pia, John ni founder member wa the Bembeya Association, ambayo mara nyingi huusika na kuandaa gigs kwa ajili ya the Okapi guitars. Mapato toka katika records na gigs hutumika kusaidia gharama za usafiri wa vyombo to/from festivals etc.

IMG_1252

Unawezaje ku balance muda wa kazi na shughuli za muziki ukizingatia maisha ya huko nje ni mchakamchaka?

Mr Paul: Kazi yangu ni 9 AM to 5PM on Mon- Friday. Hivyo, muziki siku za Jomamosi na Jumapili ni nafasi nzuri ya kukutana na ndugu, jamaa na marafiki maeneo ya starehe na kupumzisha akili. Kujibu swali lako, ni kwamba, muziki haujaanza kula muda wa kazi so far. Rather, muziki unasaidia kuondoa stress nilizozichanga siku za kazi.

Mr Paul alikuwa mmoja wa wanamuziki waliounda kundi la Four Crewz Flavour ambalo lilikuwa na wanamuziki wanne na baadaye walitawanyika na kila mmoja akatoka kivyake, Mr Paul alitamba sana miaka ya 90 na miaka ya 2000 kabla ya kwenda nje kwa masomo na kuendeleza maisha huko, tunamtakia maisha mema na ametoa wito kuwa atasambaza kazi zake na watu wataweza kumsikiliza redioni hivi karibuni.

10062012370 small

DSCN8125

Mr Paul akiimba kwa hisia akiwa na kundi la Okapi Guitar


Maisha Plus kurejea kwa kishindo

July 22, 2012

Kile Kipindi cha Reality Show cha Maisha Plus kinaendelea na safari hii kikiwa kimenogeshwa zaidi.

Akizungumza nami mtaarishaji na muanzilishi wa kipindi hicho Masud Kipanya amesema kuwa watu wengi walidhani maisha Plus imekufa lakini ilisimama kwa vile ilibidi mabadiliko makubwa yafanyike ili kuboresha “maisha Plus haikufa wala kuondoka isipokuwa tulisimamamisha mwaka jana ili tufanye maboresho ikiwa ni pamoja na kufunga Camera na mic za kisasa pale kijijini na kuboresha miundo mbinu zaidi” alisema Masoud.

Audition itaanza mwezi ujao na itaanzia Arusha na kuzunguka mikoa tofauti na hatimaye mwezi wa kumi washiriki wataingia kijijini rasmi. Aidha Masoud aliongeza kuwa umri ni kati ya miaka 21 na 26 huku akisema kigezo cha elimu ni kidato cha nne “age 21-26, elimu O’level, na ujue jinsi ya kuishi, Ukiwa na ujuzi wa ziada ni faida zaidi” alisema Kipanya.  Aidha Masoud ameongeza kuwa kipindi cha Maisha Plus kitarushwa na Television ya TBC ambapo kila kitu kimekamilika na atawajulisha mashabiki muda na wakati ambapo kipindi hiki kitakuwa hewani.

Kipindi cha Maisha Plus kimejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na mguso wa maisha halisi na tamaduni sio tu za Kitanzania bali za kiafrika zaidi.

Usikose kupitia Spoti na Starehe mara kwa mara ili upate updates za kuhusu kipindi hiki ambacho binafsi nakifagilia sana.


%d bloggers like this: