Mashabiki wa Tanzania wabezwa kukaa vitini kwenye show za muziki

March 31, 2013

[image]

Pichani juu na chini ni mashabiki wakifuatilia show ya Koffi Olomide aliyetumbuiza katika viwanja vya Leaders.

[image]

Picha za Mashabiki wa Tanzania wakifuatilia Show ya mwanamuziki Koffi Olomide ambazo kwa nyakati tofauti zimeleta mijadala kwenye ulimwengu wa muziki wa Congo huku wachangiaji na mashabiki wakitubeza watanzania kuwa hatujui starehe.

Wakiongea mashabiki hao wamesema kuwa ni jambo la kushangaza mwanamuziki kama Koffi au JB Mpiana anapiga kwenye show tena ya wazi kunapangwa vitu akina dada wanakuja na poda zao mpaka wanaondoka wanazo usoni. “…angalia show za JB, Wera au Koffi huko Matadi, Kinshasa na hata za Ufaransa kama utaona viti vimepangwa hivyo kama watu wako Concert ya dini, hii ni Tanzania tuu …” alisema Julie Weston Ilunga, Mzaire anayeishi na kufanya shughuli zake za kibiashara hapa Dar Esalaam, naye Sisco Kapinga aliunga mkono na kusema haelewi kabisa ama mashabiki hawajui kucheza au hawauelewi muziki.

“…Kuna haja ya waaandaaji kuwahamasisha mashabiki na kuwaandaa kisaikolojia ni nini wanaenda kukiona pale” alisema Sisco.

Hali hiyo haikuishia hapo hata kwenye mtandao maarufu wa Vibe Afrika jambo hili lilizungumziwa huku wengi wakionyesha kushangaa sana na utaratibu huu.


Process Mambika toka Titanic ya Wenge BCBG

March 31, 2013

Ukiniuliza binafsi yangu tangu Wenge iparanganyike Titanic ilikuwa ni moja ya Albamu bora kabisa kuwahi kutengenezwa na Wenge BCBG, tangu bendi ianze kuparanganyika hakuna mtu aliwahi kuniuma kama alivyoniuma Allain Mpella, kwa ujumla jamaa nilikuwa namkubali sana nafasi yake ndani ya BCBG.

katika albamu hii kila mtu alionyesha kipaji kikweli kweli, wimbo huu unaitwa Process Mambika ambao aliutunga Afande Allain Mpela kaka wa Bouro Mpela na mgombea ubunge kwenye uchaguzi wa 2011 huko Congo bahati mbaya hakupata.

Usikilize hasa walipokuwa wakijibizana na sauti mwanana ya Aimelia Lyase Doming’ong’o na kunakshiwa kwa ghani/Atalaku ya Tutuu Kaluji.


Likambo; Wimbo wa Werasson unaoelezea mateso baina ya wanandoa.

March 31, 2013

LIKAMBO maana yake : NENO,SHIDA,SHARI,Jambo

image

Wengi wetu tungekuwa tunaelewa maana ya nyimbo hizi za Congo ni wazi mapenzi yangekuwa makubwa zaidi na watu wangezipenda zaidi na zaidi kwani nyingi zinaongelea maisha ya kila siku ya wanadamu na nyingi zinaongelea mapenzi na ndio maana zikapewa jina la Bolingo ambalo linamaanisha mapenzi.

Katika utohoaji wa nyimbo za ki Congo leo nawaletea wimbo Likambo wake Werrason na Wenge Musica Maison Merre (WMMM). kama ulivyotoholewa kwa hisani kubwa ya mwenzetu Lubonji wa Lubonji, Merci mingi Papaa Lubonji.

Mama likambo ; likambo ; likambo té
Mama neno,maneno ila hamna neo
to vandi na ndaku yo kangueli ngai elongui
tupo nyumbani unanikunjia uso
esali nga m’passi nde essengueli na yeba oh na bengui na chambre po to solola na memi nde nguambo eh eh
Napatwa na hudhuni,napendelea kujua nini chakusibu,tafadhali njoo chumbani tupate kuzungumza, mambo ndo mambo eh
Oh fingui fingui ngai eh pé o beti ngai
Oh wanitukana na kunichafua pia wanipiga
na butu bana ba lamuki ba tuni ngai mama nini na zangui ndé maloba ya ko loba na bango m’passi eh
Usiku watoto wanaamka na kuanza kuniuliza mama nikitu gani kinaendelea, nakosa nini cha kuwajibu.taabu eh
Oh bwaki biloko na ngai na libanda na bala bala batu ba yé ko tuna ngai mama nini na zangui nde maloba ya ko loba na bango soni éh
Wanitolea mizigo yangu inje na kutupa barabarani watu wananiuliza mama kunanini nashindwa chakuwajibu aibu jamani eh
Oh parvenir ko belela ngai na balabala moyibi oh parvenir lisusu ko sambwisa ngai epayi ya bato et ngai ndumba eh
Unafikia kunitolea maneno machafu barabarani na kuniita mwizi, unafikia kunipakazia mbele ya umati eti mimi malaya
ndumba ya liboso et zalaka yo o yebaka té oh koma ko lala na ndaku na ba delestage
Malaya mkubwa ni wewe kamahujuagi hilo,unaanza kulala kwenye nyumba za mgao wa umeme
mbongo ya bileyi okoma ko tika epayi ya bana biloko na lambi a lingui lisusu ko lia té
Hela ya matumizi badala ya kuniachie mimi unawagea watoto chakula ninachopika hutaki hata kukiona
Libala ya ngai na yo é tikali sé ya bana ah na sali nyoso essengueli muasi ya libala a salaka na ndaku na ye kasi o lingui ngai té éh mobali ndoki éh
Ndoa yetu kwa sasa ipo kwa ajili ya watoto najitahidi niwezavyo kama mwanamke yeyote anaweza jitolea ili alinde ndoa yake ila naona hunipendi wewe mwanaume mchawi
nani a lessi mobali na ngai mbuma mabé a lingui ko yokela lisusu ngai té soki na meki ko loba a ko tuta ngai a ko tuta tuta tuta tuta ngai a ko tuta ngai lokola pondu
Nani kamlisha mume wangu limbwata!!! leo hii hataki kunisikia nikithubutu kumuuliza jambo ndo ntabondwa,kupigwa na kutwangwatwangwa kama kisanvu.
Na eboka mutu té yo mbanda bika pender bika pender awa yo kangui ya ngai molongani na kati ya kusu okomisa yé lokola mwana mosala kitunga na wenzi
Sijamkosea mtu mie, wewe mkemwenza umejiona umefika,umefika unanichukulia mume wangu na kumfunga kiuchawi kawa kama mfanyakazi wako kapu lakuendea nalo gengeni.
il faut kaka a memela yo mbetu o lalaka yendé a tanda yango ba sani nyoso yé mutu a sokolela yo eko yebana eh ko yebana eh ko yebana eh ko yebana oh mama !
yeye ndie kakununulia kitanda na ndie pia anayo kazi ya kutandika,tutayajua tutayajua itajulikana tuu oh mama!
ASANTENI


Dominguez huyo na Untouchable yake sokoni

March 31, 2013

[image]

Adolph Dominguez “Tata Domy” ni mmoja wa wanamuziki wa Wenge Music BCBG ambaye alitamba sana akiwa na kundi hili kabla ya kujiengua mwishoni mwa miaka ya 90 na kuondoka yeye na Werasson na kuanzisha kundi la WMMM. lakini hakudumu sana kwani aliamua kwenda kipekee baada ya kutokea sintofahamu na kaunzisha kundi lake la Wenge Tonya tonya.

Alitoa albamu ya kwanza amabayo haikupata promo ya kutosha na kutofanya vyema sana sokoni ingawa amekuwa akipata show za hapa na pale ndani na nje ya nchi.

Kwa sasa Dominguez anakuja na albamu yake mpya ya Untouchable ambayo aliitangaza tangu mwakajana.

Sijui hii itafanyaje sokoni ngoja tuone.


Werasson na WMMM kukinukisha Zambia Pasaka hii

March 31, 2013

De La Forret Werrason Ngiama Makanda na kundi lake la Wenge Musica Maison Merre wanatazamiwa kukinukisha Nchini Zambia katika jiji la Lusaka na Ndola wakati wa Pasaka hii.

Werrason ambaye amerejea Kinshasa akitoke Tshengeni alipokuwa kwa takribani miezi miweili alihitimisha recording ya albamu yake ya Flèche Ingeta Ezwi Ezwi ambayo imesemwa kuchukua muda mrefu huku akikabiliwa na wimbi la sintofahamu kwenye kundi lake baada ya wanamuziki wake kutangaza kutoa kazi zao binafsi huku kukiwa na migogoro ya hapa na pale, Werrason anataraji kujikamilisha na kuwatumbuiza vyema mashabiki wake huko Zambia ambako kuna mashabiki wengi wa muziki wa Congo.

Werasson na kundi zima la Maison Merre leo jumamosi 30/3/2013 atatumbuiza mji wa Masina kabla ya kuanza safari ya huko Zambia.

Werrason kwa sasa anakazi kubwa ya kurekebisha nidhamu katika kundi lake huku watu wakilaumu wanamuziki hao kila mmoja kujiona ni mkubwa na kuleta hali ya sintofahamu kwenye kundi hilo ambalo lina mashabiki wengi vijana nchini Congo.


Kura uako utaipeleka kwa nani hapa?

March 31, 2013

Msikilize Mtaalamu Heritier Watanabe, Mzee wa masauti hapa…

Hapa kuna nyimbo mbili ambazo zinafanana kimiondoko kwa maana zote zimepigwa taratibu, ni nyimbo ambazo kiukweli ndio zinapendwa zaidi katika ulimwengu wa wazungumza lingala, nyimbo hizi ni 3éme doigt ya FERRE GOLA ambae nadhani kila mtu anafahamu kwamba hizi ndio njia zake ukitaka kumjua sawasawa basi ni kwenye hizi Rhumba za kicongo, lakini pia tuna wimbo Remise et Reprise wakwake Heritier Wata Plus akimshirikisha De La Forret Werrason…… zitazame na kuzisikiliza vizuri then kama unachochote kiseme, la huna cha kusema basi pata burudani kimya kimya tu.


Je Ungependa kuandika habari za Burudani hapa?

March 2, 2013

Je wewe unapenda muziki wa Kiafrika? Unaufatilia muziki wa Kiafrika, Unaujua Muziki wa Kiafrika? Na ungependa kuwajuza wengine unachokijua? Kama ndivyo tafadhali wasiliana nasi tunakuhitaji.

Kwa yeyote anayeweza kuandika kuhusu Muziki wa Dansi na habari za Burudani anakaribishwa kujiunga na Blog hii.

Tafadhali tuwasiliane ama kwa email: piusmicky@yahoo.co.uk au Simu: 0713 666616


%d bloggers like this: