Tamasha la Pasaka lafana

April 8, 2012

image

Mgeni Rasmi Waziri wa Mambo ya nje Mheshimiwa Bernald Membe (White) akifatilia na kupata upako kupitia Nyimbo toa kwa wanamuziki tofauti waliokuwa wakitumbuza kwenye Tamasha la Pasaka ambalo kwa kiasi kikubwa limekusanya mamia ya wanachi.

image

image

Mfalme wa Amani song all vitambaa up kila mmmoja amesimama this is great Solomo Mkubwa rocks

image

Toka shoto ni Davis Mosha na anayefata ni Mafuru wa Vodacom wakifatilia, Davis Mosha ni muumini mzuri na amekuwa akienda Hija kule Israel zaidi ya mara mbili.

image

Chini hapakaliki. Picha zote kwa hisani kubwa kabisa ya Mkurumba Richard Kasesela.


Mh. Rais Kikwete ahani msiba wa Kanumba

April 8, 2012

image

Rais Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha Maombolezo cha Msanii Marehemu Kanumba nyumbani kwa marehemu Sinza baada ya kufika huko mchana wa leo.

image

Rais Kikwete akibadilishana mawazo na mmoja wa waratibu wa shughuli ya Msiba wa Marehemu Kanumba mara baada ya kutia saini kitabu cha Rambirambi nyumbani kwa marehemu. Rais Kikwete ni Rais pekee ambaye amekuwa karibu sana na wasanii ukilinganisha na wengine waliotangulia. 

Baadhi ya wananchi wametoa maoni yao na kukipongeza kitendo cha Mheshimiwa Rais kuhani msiba na kuonyesha kuwa yupo karibu na watu wake. Mpaka sasa viongozi kadhaa wameshahani msiba huo akiwemo Waziri Mkuu Mheshimiwa Pinda, Mawaziri na wabunge kadhaa.


Tweet tatu za mwisho za Marehemu Kanumba

April 8, 2012

image


Salamu za Rambirambi za Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa watanzania kupitia Twitter na Facebook.

April 8, 2012
image
Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika.
Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu. Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu wadau wote wa tasnia ya filamu nchini za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Aidha, naungana na wanafamilia na wasanii wote kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.

%d bloggers like this: