Kaka achomoa ofa ya Manchester City

January 21, 2009

Mchezaji wa AC Milan toka Brazil KAKA amechomoa mpango wa kumsajili na kumfanya kuwa mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi na pia mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa wa Pound 500,000 kwa wiki. Kaka amesema kuwa hatoweza kuhama klabu yake ya AC Milan, aidha akiunga mkono uamuzi wa Kaka mchezaji mwenzie David Bekham amesema kuwa kama Kaka anataka kucheza ligi ya Uingereza basi ni klabu moja tuu ambayo inamfaa na ni Manchester United.


Chelsea kumchukua Kaka kwa dau la kuvunja rekodi ya mwaka!

July 20, 2008
Kaka huenda akaenda Chelsea

Kaka huenda akaenda Chelsea

LONDON: Mchezaji wa AC Milan nyota Mbrazili Kaka anakaribia kutua kucheza English Premier League kwa klabu ya Chelsea kwa kile kinachosemwa rekodi ya dunia ya uhamisho ya Paund £80milioni (sawa na 100mil euros), alisema mshauri wa Kaka jana.

Kama kaka ataondoka itakuwa pigo kwa mshambuliaji Ronaldinho ambaye alisema amefurahi sana kucheza timu moja na Kaka na ni katika vito vilivyomfanya asisite kuhamia timu hiyo ni kuwepo kwa Kaka. na msemaji wa Kaka ambaye ni Meneja wake binafsi Diogo Kotscho aliongeza kuwa pande zote mbili ziko tayari kumaliza deal hiyo na kuifanikisha.

“Real Madrid walitaka kutoa euro 90milioni msimu uliopita kwa mchezaji Kaka lakini Milan hawakuwa tayari kumuachia kwa wakati huo, alisema” Kotscho akiongea na gazeti la The Guardian.

“Wakati huu ni tofauti na nafikiri huu ni muda muafaka wa kufanya hii deal, ni wakati pekee tunafikiri huu mpango twaweza ufanikisha na hii ni kwa sababu ya hali ya kifedha iliyopo klabuni hivyo ni muda muafaka kumalizana na jambo hili”.

Kama Kaka atakwenda Chelsea basi mashabiki wanaipa nafasi kubwa kwa kampeni yake ya kuchukua vikombe vyote viwili ambao ndio mission ya mmiliki wa klabu hiyo alipomkabidhi jahazi Philipe Scollari.

Wakati huo huo Chelsea imekataa mpango wa Real Madrid wa kubadilishana Samuel E’too na wao wamtoe Didie Drogba. HAbari kamili inakuja.


%d bloggers like this: