Kwenye Maisha Plus wiki hii!!

March 31, 2009

Kissa out!!

Mwanamke pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Mbeya, Kissa Kiposa ameaga mashindano haya Jumapili ya wiki hii.
Kisa ambaye alikuwa kikaangoni na washiriki kutoka Mwanza na Dar es Salaam, Maulidi Wadi na Upendo Peneza aliaaga baada ya kukosa kura nyingi za kumwezesha kuendelea kubaki ndani ya shindano hilo.
Kissa alilazimika kurejea nyumbani akiwa peke yake tofauti na ilivyozoeleka baada ya mshiriki mmoja kuondoka wiki iliyopita, Juma Madaraka.

Machalii wa Arusha kikaangoni

Machalii wawili wanaowakilisha pande za A Town, Charles Ngaja na Steve Sandhu wamewekwa kikaangoni lakini kama watapa kura nyingi hawatarudi makwao na badala yake watapelekwa kula bata katika hoteli ya Grand Villa iliyopo maeneo ya Kijitonyama.
Kama kawaida washiriki hao hawajui kama wamependekezwa na pia siku ya Jumapili kama wakitolewa hawata aambiwa kama kutolewa kwao ni FAKE.
Wasichana wawili kutoka Dar na Zanzibar, Asha na Modesta nao wanaiwania nafasi hiyo ya kwenda kula bata kwa siku mbili.
Washiriki watakao tolewa watakaa kwa siku mbili katika hoteli hiyo bila kuambiwa kinachoendelea na usiku wa siku ya Jumanne watarudishwa kijijini ambako pia wanakijiji wenzao watakuwa hawaufahamu mpango mzima.

King Kong atimba kijijini

Chidi Benzino akiwa na chama zima la Familia aliibukia kijijini usiku wa ‘Live’ ya mtoano na kufanya shoo ya ‘Surprise’ kwa washiriki wa shindano hilo.
Pamoja na kuburudisha Chid pia alizungumza na washiriki huku akipigwa maswali ya hapa na pale ambayo yalimlazimu pia kukanusha tuhuma za kuwa na Bif na Profesa Jay.
Washiriki walimuuliza kama kweli ana ugomvi na msanii huyo  naye kwa kifupi alikanusha kwa kusema kuwa hana bifu na msanii yeyote Bongo.

Namba za kupigiwa kura za washirki walioko kikaangoni

Charles 11,  Steve 14, Asha 31 na Modesta 36

Unaandika MP then namba ya mshiriki na unatuma kwenda 155222


Wamkumbuka Bebe Chery wa JB Mpiana?

March 30, 2009

Katika wanadada wa JB Mpiana bwana huyu dada anaitwa Bebe Cherie si mchezo!!


MAshabiki wafariki baada ya Ukuta wa uwanja kubomoka huko Ivory Coast

March 30, 2009

 

Hali ya huzuni imetanda nchini Ivory Coast baada ya mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kukumbwa na mkasa ambapo zaidi ya watu 20 walifariki dunia kutokana na msongamano.

Ukuta wa uwanja wa Houphouet-Boigny uliporomoka kufuatia msongamano uliosababishwa na mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia mechi ya kati ya Ivory Coast na Malawi.

Mkasa huo ulitokea wakati mechi hiyo ilipokuwa ikianza.

Maelfu ya mashabiki walijitokeza kushangilia timu ya nyumbani na wale ambao hawakuwa na tiketi walighadhabika baada ya kufungiwa nje.

Zaidi ya 100 wajeruhiwa

Maafisa wa Polisi walijaribu kutawanya umati mkubwa wa mashabiki hao kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Mmoja wa mashabiki walijipata katikati ya msongamano huo anasema ulisababishwa na maafisa wa polisi.

Serikali ya Ivory Coast imethibitisha kuwa watu 22 wameuawa huku wengine zaidi ya 100 wakinusurika na majeraha.

Waziri wa michezo Dagobert Banzio ameelezea masikitiko yake kufuatia tukio hilo.

Didier Drogba

Hii siyo mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea barani Afrika lakini hili limetajwa kama moja wapo ya matukio mabaya zaidi kuwahi kutokea.

Shirikisho la soka nchini Ivory coast lilikuwa limeamrisha mashabiki ambao hawakuwa na tiketi kutofika uwanjani.

Didier Drogba

Wengi walikuwa na hamu ya kumuona Drogba

Hata hivyo walikaidi amri hiyo na kumiminika kwa wingi wakitarajia kuona wachezaji wa Ivory Coast wanaochezea vilabu vya uingereza.

Mmoja wao ni nyota Didier Drogba ambaye aliifungia timu yake mabao mawili kati ya matano dhidi ya Malawi ambao walirudi nyumbani mkono mtupu.

Sherehe za kushangilia ushindi huo zilikatizwa na mkasa huo.


Usiku wa Mchinga usipime!!

March 30, 2009

hapa alikuwa hakamatiki mtu kwa shangwe mdau kila mtu alijipa raha vyakutosha wakati Wanamuziki wa iliyokuwa bendi ya Mchinga Sound walipoamua kufanya kweli na kujikumbusha mambo yalivyokuwa.

Kwa mujibu wa mdau wa Full Shangwe usiku huu ulifana vilivyo na mashabiki walitamani bendi hii iendelee kutumbuiza tena na tena.

Habari zaidi na matukio ya usiku huu pata kumtembelea mzee wa Full Shangwe


Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA

March 30, 2009

 

Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA
Msanii Mike Mwakatundu a.k.a Mike T au Mnyalu ambaye hivi karibuni aliachana na ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ameibuka na kuendeleza malumbano yaliyoanzishwa na Inspector Haroun aliyejibu wimbo wa Mwana FA, ‘Bado nipo nipo’.
Mike T alisema kwamba, wimbo wake mpya wenye jina la ‘Wala wasielewe’ aliomshirikisha Mwana FA aliyeimba wimbo wa ‘Bado nipo nipo’ unawazungumzia wana ndoa ambao huzisaliti ndoa zao na kutafuta wapenzi wengine wa pembeni.
“Kwa kifupi nataka kuleta changamoto kwa wasanii wengine waliowahi kufanya nyimbo za aina hiyo wakiwemo Mwana FA na Inspector Haroun, sipendi watu wanifikirie vibaya kwa kuwa yote ni sanaa tu na si vinginevyo,” alisema Mnyalu.

Habari hii na Abdallah Mrisho (Gonga hapo umtembelee kujua mengi zaidi)


Ukimwi unavyoenea kwa wenye ndoa…

March 30, 2009

hiv

Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwepo na ongezeko la maambukizi mapya kwa walioko kwenye ndoa inayosababishwa na kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja. Tubadilike ukimwi upo!!


Libeneke liko kwenye damu wallah

March 29, 2009

IMAGE_045

Libeneke linaendelea ukiwa mpiganaji haijalishi ulipo wiki ilopita hali haikuwa njema kiasi nilikuwa Hospital lakini nilipopata afueni haikunizuia kuendeleza libeneke. Shukrani kwa dua na sala zenu niko kitaani sasa.


%d bloggers like this: