Collabo kwa inanogesha muziki zaidi.

October 25, 2011

Sikiliza Huu wimbo wa Mzee wa Busara toka kwa Nature na Inspekta enzi hizo (Si video Rasmi)

Kuna vitu ambavyo huwa kila siku naombea kitokee tena kwenye burudani ya muziki wa Bongo Flava:-

1. Kuwaona Hard Blasters wanafanya kazi pamoja tena.

2. Kuwaona Nature na Inspector wakifanya kazi pamoja tena

3. Kuendelea kumsikia Mr. Paul akizirudia nyimbo za zamani

4. Niwasikie Mandojo na Domokaya

5. Kuwasikia GWM wakiimba tena

Oamoja na wengineo lakini ningependa kuwatolea mfano Nature na Inspekta au Hard Blasterz (Terry, Jay na Willy).

Kwa kiasi kikubwa collabo ya hawa watu wawili ilileta muamko kwenye sekta nzima ya burudani ya Bongo Flava kwani ilikuwa inatoa hadhi hasa ya Flava za Bongo, Namkumbuka mmoja wa watangazaji wa wakati huo Mike Mhagama akiwa Radio One aliitaja hii Collable kama hazina ambayo wangeendelea basi wangeleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta nzima ya Muziki wa kizazi kipya.

Wakati huo haikuwa rahisi kupenya kwenye uzio wa nyimbo kama Bongo Dance ambapo Bendi za Dance nazo zilikuwa zimeleta mageuzi kwa kutumia Mirindimo ya Ki Congo na Muziki wa Dance ndipo zikazaliwa Bendi kama African Revolution, Twanga Pepepta, TOT, Diamond sound na muendelezo wa bendi jizo.

Hivyo basi vijana wakawa wameachwa nyumba na kujiliwaza kwa muziki toka Magharibi na ndipo huu muziki wa kizazi kipya ulipoaanza na kupitia mageuzi na vikwazo kadha wa kadha kwani wakati huo ulikuwa ukijulikana kama mziki wa kihuni.

Picha ya Maktaba ikiwaonyesha The Hard Blasters, Terry kushoto,   Prof Jay (kati) na Biggie Willy (Kulia)

Nakubaliana na kila  mmoja wao kwenda solo kwani inampa uwanja mpana zaidi lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye makundi siku zote kila mmoja ana nafasi yake, kuna wengine wanajua sana kupanga sauti wengine kupanga vina na wengine kupanga mpokezano. Mfano kwenye bendi ya Wenge Muzika wakati huo kulikuwa na mtu anaitwa Blaise Bulla kwenye wimbo utamsikia Verse moja tuu ila kazi yake kubwa alikuwa kupanga sauti na wakati mwingine hata kushauri kuwa beti hii haifai kuimbwa na wewe ikiimbwa na fulani italeta mguso zaidi.

Muziki wa Bongo Flava unatofautiana na Genge (wa KEnya) kwani wao ni Commercial zaidi wakilenga kuchezesha watu na wakati mwingine hupati maana kwenye wimbo mzima hata wakihojiwa wanashindwa kusema mziki ulilenga nini. Tofauti na muziki wetu ambao unalenga kutoa ujumbe na kuburudisha na ndio maana utaona kila mtu anajitahidi kumshirikisha mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti ambayo pia inapatikana kwenye makundi, na utao nyimbo nyingi ambazo mtu ameshirikisha mwingine zimewatoa sana.

Hivyo basi ni muhimu kwa makundi ya muziki kuthamini mchango wa kila mmoja tumeshuhudia makundi kama HArd Blasters baada ya kupanguka mmoja tuu amefanikiwa kutoka na wengine wamebaki waki piga kwata kwenye sekta ya burudani. Kuna ladha ambayo tunaikosa kama wapenzi napenda kumsikia Pro. Jay lakini naikosa ladha ya Loon T (Terry), naikosa ladha ya Biggie Willy (Baba Walter).  Hivyo usia wangu ni kwamba mnatutia kilema mashabiki wenu ambacho mkipanguka mnatupa kazi kuikubali hali halisi.


Awali ni awali na hakuna awali mbovu

September 8, 2011

289245_10150368921001495_762011494_9893583_969178972_o

330026_10150368923766495_762011494_9893609_677086014_o

Pichani ni Prof. Jay akiwa na Bi Kidude wakiburudika kwa “gahawa”, Inapendeza vijana wakichota hekima kwa wakongwe.


Afande Sele na Prof Jay ndani ya “Tunawajali”

September 9, 2008

 

.

.

Pichani ni wasani nyota wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva Afande Sele a.k.a Simba Mzee pamoja na Prof Jay a.k.a Dady na mengineyo wakiacha ujumbe leo jioni ndani ya viwanja vya mnazi mmoja kwenye Kongamano lililoitwa Tuwajali wenzetu,lililoandaliwa na kituo cha redio ya Times Fm ya jijini Dar.Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa kamanda wa jiji la Dar Kamanda Suleiman Kova, Picha kwa hisani ya Michiuzi Jr


Prof Jay naye alalamikia Kili Award

July 15, 2008

Mkali wa miondoko ya muziki wa Bongofleva Mc Shupavu a.k.a Pro Jay akijimiminia kinywaji taraatiibu hivi karibuni ndani ya tuzo za Kill music awards huku akiwa amevalia kimasai.Pro Jay nae ameonekana kuzikandia tuzo hizo za 2007 kwa kudai kuwa maandalizi yake hayakuwa ya umakini wa kutosha,kwani aliyestahili kupewa tuzo hakupewa,asiyestaili ndiye aliyepewa tuzo,hali hiyo imekuwa ikiwavunja nguvu baadhi ya wadau na wasanii wenyewe.Kulalamika huko si kwa msanii huyo tu hata Bushoke pia amezilalamikia tuzo hizo kwa kuwa zilikosa umakini, kwani yeye alipewa tuzo ambayo haikuwa sahihii yeye kupewa,kutokana na uugwana alionao, Bushoke akaamaua kuirudisha tuzo hiyo kwa waandaji kwani tuzo hiyo ilipaswa kwenda kwa msanii wa kike nchini Kenya habari hii kwa msaada wa MichuziJr


%d bloggers like this: