Kwa Taabu sana ila ndo Ubingwa tayari! Viva Liverpool fc

February 26, 2012

image


Makampuni ya Bia Tanzania igeni mfano huu kuinua muziki wa Tanzania.

February 26, 2012

Hivi ndivyo Bendi za Congo Zinavyojipatia pesa nyingi ndani ya Congo Kuliko nje ya Congo,hapa nyumbani bendi zetu vipi zinashindwa kuyatumia makampuni ya pombe kutengeneza pesa zaidi ya vijisenti wanavyopata sasa hivi????

Huu ni generique (wimbo wa vyombo na atalaku) ambayo ni maalum kwa ajili ya kuitangaza product ya kampuni ya bia ya PRIMUS ambao ndio wadhamini wakuu wa wenge bcbg ya Mpiana.

Kampuni hii pia ni mdhamini wa Werrason na kampuni nyingine inayotengeneza bia nyingine ya SKOL yenyewe inawadhamini Koffi na Ferre. Mbali ya udhamini wa kawaida wanamuziki hawa wamefaidika kwa kujengewa majumba, kununuliwa magari ya kifahari na kuwakatia Bima wanamuziki wote wa Bendi, mathalani inasemekana kuwa wanamuziki wa BCBG pamoja na kuwa wote ni wanahisa kwenye kampuni ya BCBG vile vile wote wanalipwa mshahara na PRIMUS kwa miaka mitatu.


Jb Mpiana na Werrason walipokutanishwa na kukumbushia enzi zao wenge musica stejini kwa pamoja..

February 26, 2012

Na The Romantic

Katika vitu ambavyo wenyewe wanasisitiza ni kwamba hawana tofauti zaidi ya kukuzwa na mashabiki wao, wanasema tofauti zao ni kujenga muziki wa Kongo lakini kwenye masuala ya kimaisha bado ni marafiki na wanaheshimiana na hili lilidhihirika hivi majuzi baada  ya Werasson kupata ajali na JB kuwa miongoni ya watu wa mwanzo kufika.

Angalia Video hii pale JB na Wera walipokutanishwa na kutoa vipande vya wimbo ambao waliimba wakiwa bado pamoja kiukweli inatia raha sana.


Ezau wimbo uliomaliza ubishi wa umiliki wa wimbo wa Mulolo na Kin Ebouge

February 24, 2012

Kwa wafuatiliaji wa Muziki wa Kongo wanajua utata uliokuwepo kati ya umiliki wa nyimbo mbili za Mulolo na Kin ebougee ambazo zilibeba majina ya albamu huku wengine wakimtaja Ngiama Makanda kama mtunzi wa na mmiliki wa nyimbo hizo.

JB Mpiana alikuja na wimbo wa Ezzau ambao ulikuwa kwenye albamu ya Anti Terro ambayo kwa kiasi fulani haikutamba hapa nyumbani kwa kutokupata si tu promo bali hata airtime ya kutosha haikupata. Katika wimbo huu JB Mpiana anajifanananisha story yake sawa na story ya  Esau wa kwenye Biblia ambaye alikosa baraka za baba yake ambaye alikuwa kipofu na na alikuwa na manyoya mengi siku Baba aliomba aletewe mwanaye Ezzau ili ampe baraka kwa vile Esau alikuwa hapendwi na mama yake basi mama alimtuma porini na kumpaka manyoya kaka yake ambaye ni Yakobo na Baba alipomshika akajua ni Ezzau na akambariki.

JB Mpiana kwenye wimbo huu anasema histoir eshanjaka te zembo  nanga ya mulolo ebimisa wenge zembo nanga ya kin ebouge ekofirma wenge bolinga bolinga te yango wana akiimaanisha Story haitobadilika wimbo wangu wa Mulolo ndio ulioitoa Wenge, kisha wimbo wangu wa Kin Ebouge ndio ukai komfemu Wenge mtake msitake Stori haitobadilika, na kabla ya hapo JB Mpiana aliwataja mashahidi ambao anasema wanaujua ukweli huku akimtaja Papa Wemba, Presidaa Nyoshi aka Nyoka Longa na Josiki ya Mbukuta kuwa wanaujua ukweli huo.

Hivyo Wimbo huo unamaliza ubishi huo, Maneno yaliyokwenye Wimbo huu ni kama mahubiri ambayo kiukweli kila mtu na muumini anapaswa kuyasikiliza. Kwani anasema kuwa baraka zake zimetoka kwa Mungu ana kusisitiza Binadamu wapendane hakuna sababu ya kuchukiana.

JB anasema ukila pamoja na watu wanakuita ndugu mshkaji lakini siku ya siku unabaki kama Yesu Masia peke yako.

JB anasema Yesu alimfufua Razaro na watu hawakuamini, Mapenzi ni ya Mungu ingawa Mwili unarudi udongoni, mtafanya kila mfanyavyo akisema Mungu yatakuwa. Sichekagi matatizo ya mutu wala kutangaza ubaya kwa sababu nayajua yapo, mlitangaza kwamba nilikuwa Kichaa ili mniharibie kwa watu.

Anaongeza hata leo nikifa mtanikumbuka kwa kitu kimoja yule mwenye deni lake kwangu aseme hapa nimlipe… Kiukweli maneno ya Wimbo huu ni mazito sana. nitamtafuta Papaa Julie we Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama ili niwaletee wimbo huu mwanzo mwisho.

Anasema ukiwa na pesa wanakuja kwako wanajaa mnakula na kunywa zikiisha nyumba inakuwa kama iko Jangwani hakuna anayekuja, ukiwa unamatatizo na kuumwa hakuna anayekuja kukusalimia au kukusaidia wakisikia umekufa wanakuja na magari ya kifahari na michango wanatoa kukusindikiza kaburini, Kisha anaongeza kuwa yeye si kama Ezzau yeye ni kama Noah aliyeokoa viumbe vya dunia hivyo atawaokoa wote.

Merci Mingi Papaa Julie Weston Ilunga ntakutafuta tumalizie hii kazi.


Ruge na Sugu mmemaliza tofauti vipi Wafuasi wenu?

February 22, 2012

image

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.

Niliwahi kuandika makala yangu juu ya umuhimu wa Ruge Mutahaba na Joseph Mbilinyi aka Mr II aka Sugu kumaliza tofauti zao na mstakabali mzima wa muziki huu wa kizazi kipya. Kama hukuwahi kusoma gonga hapa usome zaidi.

Katika makala yangu ile wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa juu ya makundi ama wafuasi ambao wako nyuma ya makundi haya. Nawaongelea Mabagafresh, Mkoloni, Dannymcmamo, Sumag, DWA Gheto, Mapacha, Hardmad, Soggy Doggy, Peenlawyer, Rama D, Adil, Sister P na Zay B, Mr Simple, nk watakuwa ktk hali gan? nauliza hivi kwa sababu hawa wote ni Antivirus ambao walikuwa ama kwa kujua ama kwa kutokujua wakiwa upande wa Sugu ambao walikuwa wanagombea haki ambazo Sugu alikuwa muwakilishi wao.

Leo hii wao wamepatana nani atawatetea hawa? Kimsingi unatakiwa kuwepo mkakati wa pamoja wa kuangalia ni jinsi gani kundi hili limewakilishwa kwenye mgogoro huu nia iwe si tu kumaliza mgogoro wa wakubwa wao bali makubaliano yao yawanufaishe na hawa ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza kuwa waathirika wa uliokuwa mgogoro.

Hivyo basi wakati bado habari hizi ni breaking news kwa wapenda burudani ingekuwa vizuri tungeelewa hawa mabwana wako kwennye kundi gani.

Vinginevyo napenda kuchukua nafasi hii kama mpenda burudani na mwana starehe kuwapongeza Mheshimiwa Nchimbi na Mheshimiwa Tindu Lissu kwa jitihada zenu kuwapatanisha hawa mabwana ambao kwa kiasi fulani wana ushawishi mkubwa kwenye sekta nzima ya burudani hasa kwa vijana.


Zawadi ya Nono Fuji toka Soyons Serieuxe ya Wenge BCBG

February 17, 2012

Kwa wanaomjua Nono Fuji ni kijana chale sana anapenda sana vituko jukwaani na anacheza sana huwa wakiachiwa mmoja mmoja, kijana anaomba na anatunga pia.

Wimbo huu ni utunzi wake Nono Fuji kiukweli dogo anajitahidi sana kuimba kwa hisia na ni kati ya vijana ambao JB Mpiana anawapenda sana ingawa mwenyewe awali alitamani sana kughani akiwa anamzimia sana Tutu Caludji ambaye awali alikuwa na Wenge BCBG kabla ya kukimbia mwaka juzi.

Wimbo huu umerekodiwa Video mara mbili na Video hii ni Version ya Kinshasa. enjoy mdau.


Tour Eiffel ya Wenge BCBG na Weekend njema

February 17, 2012

Moja kati y wanamuziki wa Wenge ya JB Mpiana ambao waliondoka na bado nawalilia Allain Mpela, Huyu bwana alikuwa anauwezo mkubwa si tu wa kutunga bali alikuwa anakarabati Verse, yaani wimbo ukitungwa wakisikilizishana yeye huwa anazirekebisha na akirekebisha na kuzitengenezea mtiririko wa sauti hakuna anayepinga na moja ya albamu ambazo alishiriki kwa kiasi kikubwa kuiratibu ni hii ya Titanic (Titanike) ambayo waliitoa baada ya kuparaganyika na akina Werason na wao kuunda WMMM.

Japokuwa wimbo huuu ulitungwa na mpiga drums maarufu Titina Alcapone ukisikiliza beti ya Allain Mpella Afande utakubaliana na mimi kuwa alikuwa jembe, msikilize kuanzia 3:20 kisha unipe maoni yako.

Mwingine ambaye kwa sasa mepotezwa kabisa na hajawahi kuwika tangu atoke kundini ni Aimelia Lyase Doming’ong’o ambaye kwa kiasi kikubwa JB Mwenyewe ameweza kuziba pengo lake kwa kuimba sauti yake ingawa ya Aimelia ni kali na nyembamba zaidi lakini pengo lake haijaonekana sana.

Wimbo huu ni kwenu Jay Single Suvereigh Mukullu, Papaa Mabamba Maregesi pamoko sana mkuu (Full Mzaire), Papaa Julie We Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama, Papaa Sultan ndani ya jiji la Dar, Engineer Mboneka Mwana BCBG, Juma Mukulu nakati ya Airport, Hadji Le BeeCeeBeeGeeque Nambari wani, Mapenzi Club tuko pamoja, Muzee ya Tunduma sina haja ya kukutaja, Papaa na kati ya Muscat unajijua, Wenge BCBG Arusha Club pamoja sana.

Weekend njema.


%d bloggers like this: