Nzembo Mabele, Simaro Lutumba na TP Ok Jazz wakituasa kuhusu Kifo

April 18, 2012

 

Kunapotokea misiba watu huwa wanasikitika sana na kwa vile Mungu ametuumba na kusahau huwa tunasahau mara moja, Basi leo nakuletea hiyo ikiwa Poete Lutumba akiwaasa walimwengu Juu ya Maisha ya bindamu na Kifo na udongo unavyomeza watu ni maneno mazito ya Mafundisho kwetu sote wlimwengu wape wadau katika hizi aroba za Kanumba.

Nsoso eleli, nsoso ekolela ngoya nsoso ekolela bandoki bazongi ndako, Sima ya mwa ngonga tongo ekotana ndeko ya makambo, Basusu na bisengo Basusu na mawa wapi yoo Mboleo.

Jogoo anawika, Jogoo anawika, Jogoo anawika wachawi wanarudi nyumbani baada ya muda asubuhi kutakucha ndugu wana mambo wengine wana furaha wengine wana huzuni/matatizo uko wapi Mboleo.

Kadi opesi nkanda esika na motema bougie ekotangisaka pinzoli mpo na mpasi eleli mpasi ya moto ngai naleli ya lolango okotiaka kobanza soki moto akobela oo mpo nayo bolingo eleki metele mama a mabele o dis Zwani mabele.

Kadi umeipa hasira nafasi moyoni Mshumaa unadondosha machozi kwa maumivu unalia maumivu ya moto mimi nalia ya mapenzi utafikiri kama mtu anaumwa oo kwa ajili yako mpenzi yamezidi mita mama rafiki Zwani udongo.

Mokolo nakokoma mobange ma Asimie nayeba nakotambola na nzete na balabala mpo nasengaka likuta ngai nabikela Basusu batunako soki ngai nabotaki te ba oyo nakabelaka bakomi nde koseka ngai nakipa teo nzambe nasakala la vie ya sans soucis mabele, mabele mabele

Siku nitakapokuwa mzee ma Asimie najua nitatembea kwa fimbo/mkongojo barabarani ili niombe pesa niponee wengine watauliza kama sikuoa wengine watauliza kama sikuzaa hawa niliwagawia watanza kunicheka sitojali Mungu naishi maisha bila kusononeka udongo, udongo, udongo

Mokolo nakokufa nkake ekobeta dis Tati olobelaka batu maloba na ngai ya nsuka moto na ngai bakamata basala monument soki mopaya aye balobela ye nsango bambanda bakosepela basi ngai natiki ba familles bakoepela biloko ngai natiki baenemi bakoloba apusaka lofundu ebembe ya nsoso matangate alanga nzémbo nalanga makambo mabele

Siku nitakufa radi itapiga rafiki Tati uwambie watu maneno yangu ya mwisho, kichwa changu watengeneze sanamu kama mgeni akija wamwambie Habari wanaume wenza watafurahi wake nilioacha wanafamilia watafurahi vitu nilivyoacha maadui watasema alizidi maringo maiti ya kuku haina matanga nimenzisha Wimbo nimeanzisha mambo, udongo

La vie na ngai oyo ya sans soucis e mwasi na ngai nzinzi famille na ngai mabele nautaka na mabele, na kozonga na mabele mokolo nakokufa nayeba nakopola e baliaka na ngai bakokanga nzolo na nsolo bamelaka na ngai bakokima nde kosokola ngai ebembe ya Masia e atabokimie ba nzinzi bakolela ngai nazali na confiance mabele.

Maisha yangu haya yasiyo ya huzuni mke wangu nzi familia yangu udongo nimetoka kwenye udongo nitarudi kwenye udongo Siku nitakufa najua nitaoza waliokula na mimi wataziba pua kwa harufu waliokunywa na mimi watakimbia kuniosha maiti ya Masia hata mkiikimbia nzi watanililia nina imani udongo.

La vie na ngai oyo ya bayanke falanga nasalaka ya mboto na lituma mwasi aboya ngai kasi nkopo ya masanga ve etoko na ngai nasombo mpo ngiliba tokoluka tozipa miso tongo etanela namesana kolata kaki na lipapa, oo mpo nayebi mokolo tokokufaka tokendeke na drap ya pembe ata ozali riche Joe mabele ngai nalela ye.

Maisha yangu ya ujana pesa ninayopata ya kambale na ndizi Mwanamke anikatae lakini Kilauri/Kopo la pombe hapana mkeka wangu nimenunua kwa kujisitiri tunatafuta tufunge macho asubuhi kuche nimezoea kuvaa kaki na kandambili oo sababu najua siku tunakufa tunakwenda na sanda hata kama uku tajiri Joe udongo nakulilia.

Ye yeyeye mama pokwa ekomi moi mokokota e butu ekoinda mokolo mwa bandoki banganga libala oyo ya mwana na kati Masua ekokufaka Libongo ekotikalaka mama na Lola tangelaka mwana nkombo ya tata Masia, Mokili ekokufa masumu maleki kasi nkombo ya Nzambe ekotikala seko Mundele asala manduki ya koboma batu kasi ya koboma verite Mundele akoki te Mabele, mabele, mabele.

Ye yeyeye mama jioni imefika jua linazama usiku unaingia giza siku ya wachawi waganga ndoa ya mtoto katikati Mashua inakufa (haribika) Bandari itabaki mama yake Lola mtajie mtoto jina la baba, Masia dunia itakufa dhambi zimezidi lakini jina la Mungu litabaki milele Mzungu ametengeneza silaha za kuua watu lakini ya kuua ukweli hakuweza udongo, udongo, udongo

Melesi mingi Shaibu Mwambungu Mbinga


Unaikumbuka Loketo Group?

April 18, 2012

 Wakati huo Loketo Group ikiwa na mkali wa kupiga solo barani Afrika Diblo Dibala na wakongwe wengine kama Aurlus Mabere, Jean Baron, Lucien Bokilo, Mack Mackaire ambaye alikuwa anapiga Drums huyu jamaa alikuwa balaa na wengineo waling’ara sana na kufanikiwa kuziteka nyoyo za wapenda midundo ya Afrika si tu kwa Congo bali kwa Bara zima la Afrika.

Namkumbuka Ronald Rubinel ambaye alikuwa anapiga kinanda enzi hizo wapiga vinanda mashuhuri walikuwa yeye na Jamaa wa Pepe Kalle kama sikosei anaitwa Butamu. Huku wakiwa na wacheza show wao wawili “Wana Wandere” wazungu ambao walikuwa wakicheza vilivyo.

Kwa kilingala Loketo inamaana chezeza hips zako “move your hips” na ndivyo Aurlus Mabere ilikuwa style yake ya kuchezesha.

Mwaka 1987 wakiwa wametiamia Loketo waliwasha moto kwenye klabu moja ijulikanayo kama Kennel Club huko San Francisco Amerika na inasemekana ile ilikuwa ni Concert kubwa na iliyobamba sana. Baadaye walianza kutoa kila mmoja na solo albam yake. Jamaa walitisha sana.

Kaka yangu Mungu Marehemu Nhangale Nkandi Mungu amlaze peponi alikuwa analipenda sana hili kundi enzi hizo tunakunywa Texco Club pale Sea View Upanga kabla ya kuingia Pink Coconut nilikuwa mdogo lakini burudani nilikuwa naipenda sana.

Wimbo nimeweka Malou kwa heshima ya mdau Le Grand Paa Sentuke, Sikiliza huu wimbo pale Lucien Bokilo alipompa nafasi Diblo Dibala ambaye kwa kiasi kikubwa aliutendea haki.

Nimefarijika kupata simu kutoka kwa mdau na shabiki mwenzetu Neema Jua akiwa Dodoma Mwangaza Fm anasema anapenda sana tunavyowachambua na kuuchambua huu muziki wa Africa Congo. Na kwa leo alitaka kujua kuhusu Aurlus Mabere na loketo Group yake.


KITABU CHA HISTORIA(BIOGRAPHY) YA WERRASON CHATOKA!

April 18, 2012

Na Hadji Le JBeeneque

Nadhani Werrason ni mmoja wa wanamuziki wa Congo wenye washabiki wengi sana hapa nchini na Africa kama sio duniani kiujumla. Lakini kwa muda mrefu mashabiki na wapenzi wake hao wamekua wakimfahamu Le Roi De La Forret Papaa na Exocee Mobali ya Mama Pastor Sylvie Mampata kijuu juu tu. Lakini safari hii mashabiki wake na wa muziki kiujumla hususan wanafamilia wa wenge wamepewa fursa maalum ya kumjua nguli huyu wa muziki wa congo kupitia kitabu maalau ambacho kimeshachapishwa kikielezea historia ya mwanamuziki huyo binafsi na katika harakati zake za kujiingiza kwenye muziki, kuwa star na mpaka sasa kumiliki bendi kubwa na yenye mafanikio makubwa pia.

Dondoo za yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kwamba ndani ya kitabu hicho werrason anaelezea kwa mfano wenge musica ilivyozaliwa. Katika hilo Werrason anasema mwanzoni kabisa walikua yeye Werra, Aime Buanga, Jean Belix Luvutula, Didier Masela na Christian Zitu, ambapo Aime Buanga alichukuliwa kama muanzilishi wa kundi kutoka na yeye kujitolea nyumba ya wazazi wake alimokua akiishi itumike kama sehemu ya kufanyia mazoezi ya kundi lao hilo na pia Didier Masela nae kwa upande mwingine akichuliwa kama muanzilishi pia kutokana na kwamba wazo la kuanzisha bendi lilitoka kwake.Lakini wakati fulani kwenye siku hizo hizo za mwanzo mwanzo za kundi lao Aime Buanga alitaka kuachana na kundi hilo changa ili aendeleze kipaji chake kwenye sanaa za mapigano (martial arts) huku akimpa masharti rafiki yake werrason kwamba kama unataka nirudi kundini na wewe jiunge na mimi kwenye sanaa za mapigano (martial arts) sharti ambalo kwenye kitabu hiki werra anadai alilitekeleza kwa kujumuika na swahiba wake kwenye martial arts.

Wakati ya Werrason na Aime Buanga yakiendelea hivyo kwa upande mwingine Didier Masela alikua shule nje ya Kinshasa katika mji mdogo uitwao Mbanza Boma pamoja na Alain Makaba.Baadae huku nyuma Jb Mpiana akafika kuja kujiunga na bendi ambapo werra anasema katika kitabu hiki akamueleza “rafiki yangu nimesikia wewe ni muimbaji mzuri sana kama hitajali naomba uniimbie wimbo kidogo nikusikie na mimi” baada ya kauli hiyo ya werra jb inaelezwa akaimba wimbo uitwao “Abidjan” wa Viva la Musica uliotungwa na Debaba,ambapo Werrason mwenyewe na kila aliekuwepo pale wakavutiwa nae sana kiasi cha kumpigia makofi kwa wingi na watu wote, baada ya hapo werra akapendekeza Jb ajiunge na bendi ambapo Jb alikubali bila kusita.

Siku hiyo miongoni mwa waliomshuhudia Jb akiimba pamoja na werrason ni Didier Masela na Jean Belix.Na aliyemleta na kumtambulisha Jb hapo kundini alikua ni Jean Belix Luvutula ambae walikua wakiishi jirani na alikua akimuona Jb akiimba mtaani.

Baadae Blaize Bula akaletwa na Makaba kujiunga na bendi kama mpiga drums kutokana na kwamba alikua mpiga drum wa bendi ya shule waliyokuwa wakisoma lengo likiwa aje achukue nafasi ya binamu yake werrason  aliyekwenda kwa jina la Ladins Montana ambae ndio alikua mpiga drums, lakini Sele Bula akaonekana hana muonekano wa bcbg lakini Makaba kwa kujua kipaji cha Sele kwenye uimbaji pia akasisitiza aingizwe kundini. Hivyo wakawa wamempata Blaize(sele)Bula kama muimbaji,na kwa upande mwingine Jb ambae alikua tayari kundini alikutana na Tata Mobitch Adolphe Dominguez ambae alikua ni mtoto wa tajiri mkubwa sana Congo lakini pia akiwa na dancer mzuri akicheza sana nyimbo za DEFAO.

Jb na Adolphe baada ya kujuana kutokana na Jb kuvutiwa na uvaaji wa Adolphe wakatokea kuwa marafiki wakubwa huku Adolphe akimpigisha Jb pamba za ukweli kiasi cha kung’aa mbaya miongoni mwa wanabendi,ndipo baadae Jb akamtambulisha Adolphe kwa Werrason na wengine kundini ambapo wakaanza kumfundisha muziki Adolphe hapo hapo kundini huku yeye akilipa fadhila kwa kuwafadhili upande wa mavazi kupitia utajiri wa babake!

Kitabu kimeongelea mambo mengi hatuwei maliza ngoja nitoe dondoo za alichozungumzia werra kuhu su maisha yake binafsi.Katika maisha yake binafsi werra anasema alikutana na mkewe kipenzi Mama Pastor Silvie Mampata akiwa shule kupitia rafiki yake kipenzi wakati huo aitwae Wasenga Kipuni.Sylvie alikua ni binti wa mfanyabiashara tajiri na aliutumia utajiri wa babake kuisadia sana wenge huyu mama kupitia kwa werrason.

Kuhusu mgawanyiko kitabu kinaeleza kwamba ni uamuzi wa Jb kurekodi “Feux de l’amour” kwa kuwashirikisha wanamuziki wengine toka nje ya wenge kama alivyofanya Alain Makaba kwanza kwenye album yake solo iitwayo “Pile ou face” hapo ndipo mgogoro wa kiuongozi ulipoanza kuibuka,ambapo baada ya mafanikio ya Feux de l’amour Jb kwa kushirikiana na SIMON SIPE ambae ndie alikua meneja wao akisimamia kila kitu mpaka production zao wakanogewa na kutaka kutoa album nyingine solo ya pili ya Jb,hapo ndipo werra alipokasirika na kuitangaza album yake Kibuisa mpipa huku akiwa hana hata nyimbo moja wakati huo akiitangaza ila tu alitaka kumuonyesha Jb kwamba hawezi kutoa album solo ya pili wakimtazama tu.

Baada ya hapo bendi ikagawanyika na werra  ili kushindana na Jb akawa na mawazo ya kuanzisha tu bendi haraka haraka na kuanza kuperfom matokeo yake akachemsha sana mwanzoni kwenye concerts zake za awali zikawa “flop” mpaka ndugu zake wanaotoka kijiji kimoja kina Marie Paul wakamuonea huruma na kuamua kumsaidia ambapo Marie alimpa bure mwanamuziki wake JDT na yeye mwenyewe akawapata watu kama Didier Lacoste,Adjan n.k. ndipo mambo yakaanza kwenda vizuri sasa na kutoa FORCE INTERVENTION RAPIDE.

Ambapo badae mwandishi wa kitabu hiki nae alimpa wazo werra la kutarget zaidi concerts za watu wa kawaida kuliko za VIP kama wafanyavyo Bcbg,pia werra akapata msaada mkubwa toka kwa mamaa Tshala muana,baadae wakapata kazi ya kwanza ulaya kwa kualikwa kwenda kupiga London ambapo muandishi wa kitabu hiki alifanya kazi ya ziada kwa ku organize umati wa watu kwenda kumpokea werra na bendi yake airport katika safari ambayo masela aliachwa kin na ikawa mwisho wako kundini.


%d bloggers like this: