Lady Jay Dee ni zaidi ya mwanamuziki

April 30, 2009

n590146649_2170467_667435

Ukinitajia mwanamuziki Lady Jay Dee kwangu ninayojinsi  ninavyomuangalia mwanadada huyu. Napenda sana ubunifu alionao na jinsi anavyoimba kwa kutumia sauti asilia ambayo inaandikika kimuziki, nikiwa namaana kuwa muziki wake uko kwenye Note za kimuziki hasa na hivyo kutompa kazi prodyuza yeyote au wapiga vyombo wake.

Nilipopata nafasi ya kuongea na Maneno Uvuruge (Gonga hapa usome mahojiano naye)ambaye kwa wakati fulani aliwahi kufanya kazi na Machozi Band yake Lady Jay Dee anasema kuwa kati ya watu alifanya kazi nao basi hatomsahau Lady Jay Dee kwani walikuwa wakiongea lugha moja “unajua kama mtu anayeimba anaimba kwenye note hupati taabu mpiga ala, ila kama muimbaji anatoka nje ya note anakupa taabu wewe kumfunika ili washabiki wasielewe, alisema Uvuruge ambaye anapiga Solo kwenye Band ya Kilimanjaro Connection inayopiga muziki nchini Malaysia kwa sasa.

Kwangu mimi Lady Jay Dee ni zaidi ya Mwanamuziki.

Hivi karibuni mwanamuziki huyu alitembelea huko mikoa ya kusini na kugawa Vyandarua kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Malaria na huko alikutana na Mwanamuziki maarufu Barani Africa Balozi wa Malaria Afrika Princess Vyone Chaka Chaka.

11

Lady Jay Dee akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda huko Ntwara.

12

Akichangia jambo pamoja na Waziri Mkuu na Yvone Chaka Chaka Kulia.

n590146649_2161315_1150291

akiwa Hospitali na kugawa Vyandarau kwa akina mama wajawazito

Sikiliza kibao cha Siwema toka kwake Lady Jay Dee anayepiga gitaa mwanzo kulia ni Maneno Uvuruge.


Asante kwa kuwa sehemu ya Maisha Plus

April 30, 2009

IMG_0185 “…Kwa kutazama kwako vipindi vya Maisha Plus, kusoma habari zinazolihusu shindano na kutoa maoni, moja kwa moja ulikuwa sehemu ya Maisha Plus.
Timu nzima ya Maisha Plus inakushukuru wewe kwa kuchukua muda wako na kulifuatilia shindano hili, hii ndiyo ilikuwa sehemu kubwa ya mafanikio yetu kwa kuwa tulikulenga wewe.
Kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili umekuwa nasi bega kwa bega kutuunga mkono katika hili, tunautambua mchango wako kwa kuwa wewe ni sehemu ya shindano hili.
Tunamshukuru mungu kwa kuweza kulifanya shindano hili kuwa kubwa na lenye mafanikio na zaidi ya yote limekuwa sehemu ya kuwajenga na kuwaburudisha Watanzania.
Mwisho wa msimu huu ndio mwanzo wa maandalizi ya shindano la msimu ujao, tunaamini utakuwa na subira ukiwa na imani na sisi kuwa tukuandalia kitu kingine kizuri na chenye manufaa.
Mungu akubariki kwa sehemu ya mafanikio ya Maisha Plus.
regards”
Julieth Kulangwa


Justin Timberlake na Lupe Fiasco kupanda Mlima Kilimanjaro

April 30, 2009

 JustinTimberlake460 Mwanamuziki Justin Timberlake na Rapper Fiasco Lupe wataungana na muimbaji Kenna katika kampeni ya Maji safi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Nia ya kupanda mlima kilimanjaro ni kuchangia mradi ambao ulianzishwa na Kenna ambaye ni mzaliwa wa Ethipia, ikumbukwe kuwa nyingi ya nchi za Africa bado suala la Maji safi ni kitendawili.

Justin amesema kuwa anakuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa wiki ili kuzoeza mapafu yake kwa ajili ya kubeba hewa ya Oksijeni ya kutosha ambayo inahitajika sana wakati wa kupanda mlima huo wenye urefu wa M 5800.

Tutapanda kwa wiki nzima huku tukiwa na mzigo wa paundi karibu 30 mgongoni, kazi ni kubwa mbele yetu alisema Timberlake akiongea na GQ.

Naye Kenna alisema ”Baba yangu nusura afariki kwa ajili ya tatizo la maji miaka hiyo…” nina marafiki wengi sana ambao wako tayari kusaidia kampeni hii hivyo ni lazima tuifanikishe alisema Kenna.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Guardian wastani wa wapandaji 10 hufariki kila mwaka katika harakati za kuupanda mlima huo mrefu kuliko yote Barani Afrika.

Waandaaji wamepanga upandaji ufanyike kipindi hiki cha majira ya kipupwe.

Nakuacha na kibao Whats Goes Around Comes Around toka kwake Justin Timberlake!!


Manchester City wamtolea macho Eto’o

April 29, 2009

Samuel Eto'o

Eto’o has scored 32 goals in 42 games so far this season

Klabu ya Manchester City imefanya mazungumzo na Klabu ya Barcelona juu ya mchezaji Samuel Eto’o BBC imeripoti.

Etoo ambaye kwa sasa ameingiza kimiani magoli 32 kwenye mechi 42 alizocheza msimu huu ameonyesha kiwango kizuri hasa baada ya kupona ambapo kulikuwa na hati hati ya majaliwa yake.


Mambo ya Elle Fashion Show @ Mid Valley Mega Mall

April 27, 2009

Katika pitapita zangu jumapili nikaingia Mid Valley Mega Mall nikiwa na rafiki yangu Yatie Mwaki, nilikutana na hii Fashion Show iliyokuwa imeandaliwa na Elle Fashion, nikaona si vibaya kama nitashare na wadau wangu walao picha mbili tatu, Mamaa Shamim upoo?. Maonyesho haya yalikuwa kwa ajili ya kuonyesha nguo mpya na kulikuwa na punguzo kubwa la beo 30% to 70% kwa waliohitaji kufanya biashara karibuni Malaysia.

11

2

3

4

5

6

8

64


MISS TANZANIA EU 2009 REGISTRATION continues!!!!

April 27, 2009
Washiriki wa mwaka jana

Washiriki wa mwaka jana

MISS TANZANIA EU 2009 REGISTRATION continues!!!!

Application Form for Miss Tanzania European Union

www.misstanzania.eu

Mashindano haya ya urembo yatashirikisha warembo wakitanzania toka nchi za jumuiya ya Ulaya (Schengen) yatafanyika Essen Germany.

Washindi 3 wa mwanzo watawikilisha warembo wengine huko United kingdom katika mashindano ya Miss Tanzania Europe mwishoni mwa mwezi Juni.

Jiandikishe sasa!!

info@misstanzania.eu

+49 174 45656 44


Weekend njema wadau!!

April 24, 2009

Weekend ndio hiyo kama kawaida nakuacha na kibao Liberez kibao hiki ni maalum kwa washkaji zangu Mama Sophia Kessy, Le Suvereign Maghambo, Mukulu Ling’ande (mna nini bwana?), Jeff Msangi, Robbie Mzee Wa Upang, Rasheed na Danny, Muafirika hehehe Mutu ya Mbeya, Mukubwa Six, Mgosi Tameem na Abel, Mamaa Ghaty, Mamaa Joy Mwaisa na wengine wooooote!! Weekend njema Chakuchoma kwa sana, nawamiss kinoma washkaji!!


%d bloggers like this: