ona Cheche za Mbwana Samatta na TP Mazembe

July 26, 2011

Moise Katumbi; A Man Behind TP Mazembe

April 4, 2011

Mh. Gavana Moise Katumbi

 

Anaitwa Moïse Katumbi Chapwe alizaliwa 28 December 1964)Ni Mfanyabiashara na mwanasiasa.

Moise Katumbi ni mheshimiwa Gavana wa jimbo la  Katangaambalo liko kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo. Huyu ni Gavana wa kwanza wa kuchagukliwa na wakati anakuwa Gavana alikuwa na umri wa miaka 42 tu.

Katumbi ni mdogo wake Raphael Katebe Katoto, mfanyabiashara mkubwa wa Kongo ambaye anaishi Ubelgiji ( Belgium).

Moise pamoja na biashara nyingine anamiliki kampuni ya uchimbaji madini  Africo Resources, Ltd ambapo ana shea kubwa humo.

Katumbi anakubalika sana kwa watu wake kwa maendeleo na jinsi alivyoleta mageuzi na utulivu. Akiwa na asili ya mchanganyiko Baba ni Myahudi anaitwa Nissim Soriano, Huyu ni mmoja wa Wayahudi wengi waliolowea Congo kutoka visiwa vya Rhodes, Lakini mama yake ni raia wa Congo.

Katumbi anachukuliwa kama mfano wa kuigwa kwani akiwa na miaka 13 anasema hapo ndipo alipoanza kutengeneza pesa kwa kuuza samaki8 na faida yake ya kwanza ilikuwa kama dola 40$. toka hapo aliendelea mpaka alivyo ssasa.

Jimbo lake la Katanga kwa sasa linamaendeleo likiwa na miradi mikubwa ambapo ameweza kuvutia hata wawekezaji toka USA na Europe ambapo wamewekeza vya kutosha.

 Alichaguliwa Gavana wa Katanga mwaka 2007, baada ya ya kuchaguliwa Moise Katumbi alihakikisha na kusimamisha usafirishaji wa Coper Ore ambapo aliwalazimisha wachimbaji kujenga viwanda ili kutengeneza ajira, na viwanda vya kusindika ore kuwa chuma vikajengwa jimboni kote.

Katumbi pia alilazimisha wawekezaji wote kwenye sekta ya madini kulima angalao hekari 500 za mahindi namazao mengine ya kuchakula kwa ajili ya kuchangia chakula kwa jamii jambo ambalo limetoa kilio cha njaa na kutoa ajira pia kwa wakazi wa vijijini. Si hivyo tu bali pia makampuni haya kwa kushirikiana na uongozi wa Jimbo serikali iliyochini yake wanamikakati ya kufufua ufuaji mkubwa wa umeme kwa ajili ya kutumika na makampuni makubwa ya uwezaji jimboni humo.

Katumbi binafsi amekuwa chachu ya maendeleo kwa kuchangia miradi ya maendeleo kama shule, maospitali, visima vya maji safi na michezo huku akiwa ndio mfadhili namdhamini mkuu wa kiboko ya Simba TOUT POISSANT MAZEMBEE ENGLEBERT ambayo jana imeitoa kamasi Klabu ya Simba kwa kuichabanga mabao 3-2 na kuifungasha virago.

Fuatilia hapa hapa nitakujuza ushiriki wake kwenye TP Mazembe.


Mpira hauna Uzalendo

April 2, 2011

Shabiki akiwa amevalia Bango lenye Maandishi TP Mazembe 6-0 Simba eneo la Ferry Kigamboni Dsm, Homa ya mpambano wa marudiano baina ya TP Mazembe na Simba umepamba moto huku Ikiwa imebaki siku moja tu timu hizo kurudiana kwenye uwanja wa Taifa Jijini D’Salaam.

Posted with WordPress for BlackBerry.


%d bloggers like this: