KANUMBA ALIKIJUA NA KUKIPENDA SANA KIBAO HIKI..

April 13, 2012

Na Hadji Le JBnique

“naijua hii inaitwa Fimbu ya bakandja…..yaani bakora ya bakandja”-Haya ni maneno ya marehemu Steve Kanumba aliyoniandikia baada ya mimi na yeye kubadilisha maneno kwa njia ya e mail kuwahusu wanamuziki wa kike wa kizazi kipya katika muziki wa lingala,hapa nawazungumzia Cindy Le Coeur anaefanya kazi na Koffi Olomide akiwa kama artistic director wa kundi la QL la Koffi Olomide na Meje 30 anaefanya kazi mamaa Mokonzi Mbilia,Nimeyakopi na kuyaweka hapa bila kuhariri neno hata moja lengo likiwa ni kumkumbuka mdau mwenzetu huyu kwenye tasnia hii ya muziki wa LINGALA

R.I.P.” KANUMBA THE GREAT PIONEER MOTO WA VOLCANO” kama ulivyopenda kujiita mwenyewe,mbele yetu nyuma yako ulale pema kamanda 


“Vibrators” za Maison Mere balaaa!!

April 13, 2012

Nilikuwa najadili jambo na Papaa Julie We Ston Liberko kuhusu muziki wa Congo mara nikaingia kwenye library yangu nikamuwekea hii Live ya Werason nilitaka awaangalie stageshow wa Werrason na kumsikiliza Flam Kapaya anavyofanya vitu vyake, kiukweli hii ni moja ya DVD za Werasson ambazo huwa sichoki kuziangalia. Hiki kiliwahi kuwa kikosi bora kabisa cha WMMM wadada hawa walikuwa wanajituma sana, angalia na wewe uniambie.


%d bloggers like this: