Collabo kwa inanogesha muziki zaidi.

October 25, 2011

Sikiliza Huu wimbo wa Mzee wa Busara toka kwa Nature na Inspekta enzi hizo (Si video Rasmi)

Kuna vitu ambavyo huwa kila siku naombea kitokee tena kwenye burudani ya muziki wa Bongo Flava:-

1. Kuwaona Hard Blasters wanafanya kazi pamoja tena.

2. Kuwaona Nature na Inspector wakifanya kazi pamoja tena

3. Kuendelea kumsikia Mr. Paul akizirudia nyimbo za zamani

4. Niwasikie Mandojo na Domokaya

5. Kuwasikia GWM wakiimba tena

Oamoja na wengineo lakini ningependa kuwatolea mfano Nature na Inspekta au Hard Blasterz (Terry, Jay na Willy).

Kwa kiasi kikubwa collabo ya hawa watu wawili ilileta muamko kwenye sekta nzima ya burudani ya Bongo Flava kwani ilikuwa inatoa hadhi hasa ya Flava za Bongo, Namkumbuka mmoja wa watangazaji wa wakati huo Mike Mhagama akiwa Radio One aliitaja hii Collable kama hazina ambayo wangeendelea basi wangeleta mabadiliko makubwa sana kwenye sekta nzima ya Muziki wa kizazi kipya.

Wakati huo haikuwa rahisi kupenya kwenye uzio wa nyimbo kama Bongo Dance ambapo Bendi za Dance nazo zilikuwa zimeleta mageuzi kwa kutumia Mirindimo ya Ki Congo na Muziki wa Dance ndipo zikazaliwa Bendi kama African Revolution, Twanga Pepepta, TOT, Diamond sound na muendelezo wa bendi jizo.

Hivyo basi vijana wakawa wameachwa nyumba na kujiliwaza kwa muziki toka Magharibi na ndipo huu muziki wa kizazi kipya ulipoaanza na kupitia mageuzi na vikwazo kadha wa kadha kwani wakati huo ulikuwa ukijulikana kama mziki wa kihuni.

Picha ya Maktaba ikiwaonyesha The Hard Blasters, Terry kushoto,   Prof Jay (kati) na Biggie Willy (Kulia)

Nakubaliana na kila  mmoja wao kwenda solo kwani inampa uwanja mpana zaidi lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa kwenye makundi siku zote kila mmoja ana nafasi yake, kuna wengine wanajua sana kupanga sauti wengine kupanga vina na wengine kupanga mpokezano. Mfano kwenye bendi ya Wenge Muzika wakati huo kulikuwa na mtu anaitwa Blaise Bulla kwenye wimbo utamsikia Verse moja tuu ila kazi yake kubwa alikuwa kupanga sauti na wakati mwingine hata kushauri kuwa beti hii haifai kuimbwa na wewe ikiimbwa na fulani italeta mguso zaidi.

Muziki wa Bongo Flava unatofautiana na Genge (wa KEnya) kwani wao ni Commercial zaidi wakilenga kuchezesha watu na wakati mwingine hupati maana kwenye wimbo mzima hata wakihojiwa wanashindwa kusema mziki ulilenga nini. Tofauti na muziki wetu ambao unalenga kutoa ujumbe na kuburudisha na ndio maana utaona kila mtu anajitahidi kumshirikisha mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti ambayo pia inapatikana kwenye makundi, na utao nyimbo nyingi ambazo mtu ameshirikisha mwingine zimewatoa sana.

Hivyo basi ni muhimu kwa makundi ya muziki kuthamini mchango wa kila mmoja tumeshuhudia makundi kama HArd Blasters baada ya kupanguka mmoja tuu amefanikiwa kutoka na wengine wamebaki waki piga kwata kwenye sekta ya burudani. Kuna ladha ambayo tunaikosa kama wapenzi napenda kumsikia Pro. Jay lakini naikosa ladha ya Loon T (Terry), naikosa ladha ya Biggie Willy (Baba Walter).  Hivyo usia wangu ni kwamba mnatutia kilema mashabiki wenu ambacho mkipanguka mnatupa kazi kuikubali hali halisi.


AY atua India

March 1, 2011

AY akiwasili ndani ya INDIA kwenye uwanja wandege wa kimataifa wa BANGAROLE,Leo 1st March atapiga ndani ya Blue  Waves Bangarole then tarehe 5th atakamua Hyderabad,picha zaidi zoinakuja.

Posted with WordPress for BlackBerry.


Kambarage kutambulisha albamu ya Sugu “VETO”

June 23, 2009

sugualbum Mwanamuziki mkongwe kwenye fani ya muziki wa kizazi kipya 2Proud aka SUGU anakuja na abamu yake mpya inayokwenda kwa jina la VETO yenye nyimbo takribani 10.

Akiongea na dawati la Spoti na Starehe Prodyuza wa albamu hiyo Stiggo Ibrahim wa S&S Records aliyekuwa kundi la Deplowmatz amesema kuwa Albamu hiyo imeshirikisha wanamuziki vichwa akiwemo Balozi Dola Soul, Yeye mwenyewe Stiggo, Prof Jay na vichwa kibao.

Tayari kibao cha kuitambulisha albamu hiyo kiko mtandaoni kikienda kwa jina la Kambarage akiwa anatimiza miaka 10 tangu afariki na Sugu anatoa Albamu yake ya 10.

Mr II kama alivyozoeleka anasema binafsi yake amekuwa na mafanikio sana kwenye mtanange huu wa Muziki wa kizazikipya na kusema kuwa hii ni Albamu yake ya mwisho ikiwa ni albamu ya 10 kwenye mwaka wa 10 wa kifo cha Mwalimu Julius KAmbarage Nyerere ambaye anasema kuwa yeye ni Nyerere wa RAP!


Bongo Flava ndani ya CNN tena, ni AY

June 13, 2009

Yeah ni mara nyingine tena tunagonga anga za kimataifa kwa Mwanamuziki Ambwene Yesaya baada ya Nakaaya Sumari ku fanya mahojiano na kituo kikubwa cha Television cha CNN,

AY mwanamuziki ambaye amekuwa na historia ndefu mpaka kufikia hapo alipo ameweza kuwa kati ya wanamuziki wachache wa kizazi kipya ambao tunaweza kusema waanzilishi ambao wako juu tangu wameanza mpaka sasa.

Safari hii hajahojiwa lakini kipindi kimemuongelea ikiwa ni sehemu ya kipindi maalum cha CNN Inside Africa.

Ama kwa hakika hii ni hatua kubwa kwa wanamuziki na huu muziki wetu kwani ni njia rahisi ya kuitangaza nchi kama mikakati ikifanyika na kuwapa ajira vijana ambao wanaweza kuelimisha na kuburudisha wakati huo huo.

Unataka kujua wameongelea nini basi bonyeza player hapo chini upate kuona.


Prodyuza Stiggo afanya kweli unyamwezini!!

June 8, 2009

cccx

Stiggo Mwamba producer Ambaye Kazi zake anafanyia jijini New York USA Amefanya kazi mpya ambayo ni Babkubwa Ndani ya Track iyo mistari imefanywa na msanii Cashmere. Spoti na Starehe iliwahi kufanya mahojiano na Nguli huyu wa Bongo Flava (Gonga hapa).

Kwa kusikiliza Truck hiyo bonyeza kitufe uende Baabu Kubwa

Stiggo pia anafanya kazi na wanamuziki tofauti na kwa sasa anatengeneza Nyimbo ambayo itajumuisha wanamuziki kadhaa akiwemo Beezy na Shanice ambao mwenyewe anawakubali kinoma.


Wimbo Mpya wa AY – Leo

March 19, 2009

Mwanamuziki ambaye kwa kiasi kikubwa amepata mafanikio makubwa katika Sekta ya Muziki wa kizazi kipya AY hivi karibuni aliachia nyimbo yake mpya Leo.

Nyimbo ambayo imeshika chat kwenye radio show mbalimbali akiongea nami asubui hii AY ambaye anarejea Kesho nyumbani Tanzania akitokea ziara yake ya USA amesema kuwa Video ya nyimbo hiyo ambayo imetengenezwa na Ogopa Djs wa Kenya na imefanyiwa jijini Dar es Salaam, pia AY aliongeza “…video ni noma sana nimezidi kuinvest zaidi ili ziweze kuchezwa kwenye stations kubwa zaidi na kubadilisha soko lilipo kwa sasa kama unavyoona kazi ilivyo”.

Gonga Hapa ukapate kuisikia nyimbo hii

KWa hiyo wapenzi wa muziki kaeni mkao wa kula video iko njiani,

Kwa wanaopenda Lyrics ya wimbo huo gonga hapochini

Read the rest of this entry »


Mahojiano ya Nakaaya na CNN-Inside Africa

March 18, 2009

Mwanamuziki Nakaaya Sumari jana alionekana kwenye kipindi cha CNN Inside Africa, si kitu kigeni lakini kwa wanamuziki tena muziki wa Kizazi kipya ambao ulianza kwa kutokukubalika haya ni mafanikio makubwa sana kisanaa na kisanii pia.

Aliongea nini aliulizwa nini bonyeza kitufe upate kuona mwenyewe


Sir Nature atambulisha Single

January 15, 2009

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Sir Juma Nature leo mchana amefanya utambulisho wa wimbo wake mpya uitwao ULEVI kutoka kwenya albamu yake mpya ya tano inayoitwa TUGAWANE UMASIKINI yenye jumla ya nyimbo kumi.
Mmoja wa wasaniii wa karibu wa msanii huyo,Rich One ameiambia JIACHIE leo mchana kuwa wimbo huo wenye mabadiliko makubwa tayari umekwishasambazwa kwenye vituo kadhaa vya redio mbalimbali za hapa jijini Dar na kwingineko.
“Kwa hiyo leo tunaanza utambulisho wa singo ya kwanza inayoitwa ULEVI,ikiwa kama utambulisho wa albamu hiyo iliyorekodiwa ndani ya studio za Bongo Records chini ya prodyuza mahiri P-Funk, na albamu kuanzia wiki ijayo itaingia sokoni tayari kwa mauzo”amesema Rich One .
Habari na MichuziJr gonga hapo upate habari kamili

Spika Sitta afagilia Bongo Fleva

August 28, 2008
Samuel Sitta

Samuel Sitta

SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, Samuel Sitta, amesema anawazimia sana wasanii wa kizazi kipya (Bongo Fleva), akiwemo wanamuziki Jackline Ntuyabaliwe ‘Kyline’, Bushoke na Ali Kiba.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati alipokuwa akiongezea kwenye jibu la aliyewahi kuwa Waziri wa Michezo ambaye sasa ni Wazari wa Nchi Ofisi za Makamu wa Rais (Muungano), Seif Khatib aliyesema vijana wa Bongo Fleva waachwe wajimwage kwa sababu kila enzi ina vitabu vyake na vijana hao wanatoa burudani kwa Watanzania. Awali, Mbunge wa Nyang’wale, James Msalika (CCM), alitaka kujua serikali inasema nini juu ya mitindo ya mavazi kwa vijana wa sasa na muziki wa kizazi kipya, Bongo Fleva, ambao unaonekana kumomonyoa utamaduni wa Tanzania.


%d bloggers like this: