Koffi na Cindy Wake

October 22, 2013

Amakweli “Thin Line Between Love and Hate” hakuna ambaye aliwahi kudhani Koffi Olomide aliyewahi kuwa hasimu mkubwa wa JB Mpiana leo hii wangekuja kuwa maswahiba, wala hakuna aliyewahi kudhani Koffi na Werra wangeweza kupeana migongo lakini ndio upepo wa muziki wa Congo ulivyo. kama walivyo wasanii wa Bongo Movie hawaishi visa bali na hawa wa Congo hawaishii visa ili mradi wasikauke vinywani mwa mashabiki wao kama sikioni mwao kutokana na muziki mpya.

Natamani mapenzi haya kati ya WERRA na KOFFI yarudi tena lakini this time yawe ya ukweli sio kama hapa solidarity hii kati ya wawili hawa ilikua dhidi ya JB MPIANA, Tunapenda mapenzi na solidarity iwe kwa wanamuziki wote wa Congo ambao miongoni mwao kumekua na mpasuko mkubwa for years now,huyu hampendi yule,yule nae anaungana na mwingine ambae hampendi huyu…mradi tafrani tu,wapenzi tunataka burudani sio ma “beef” yasio na mpango..

Huyu ni Koffi Olomide akiwa na Cindy kipenzi chake, kwa sasa Koffi ametangaza kustaafu mziki akitoa albamu yake ya 20 ambayo anatazamiwa kuitoa December 2013. Je koffi atafanya shughuli gani baada ya hapo? Inawezekana kuwa akageukia biashara ambapo kwa siku za karibuni


Zawadi ya JB Mpiana kwa Zadio Kongolo

October 21, 2013

Na The Romantic mwana BCBG

Huu ni wimbo maalum zawadi ya Jb Mpiana kwa swahiba yake Le Bcbque nambari moko Zadio Kongoloo na Mkewe Carole ambao walifunga ndoa ya kukata na shoka hivi karibuni.

Angalizo: kama wewe sio mpenzi wa Congo Rhumba,usijisumbue kuusikiliza wimbo huu,utakuzingua tu,but kwa wapenzi wa muziki wa taratibu made in congo kama mimi,this is your thing.Enjoy the lyrics,masauti mchanganyika ya mzee mzima mwenyewe Papaa Cherie Mobali ya Mamaa mokonzi Amida Shatur, Nono Fuji pamoja fundi Zulema pia utamsikia anavyoichezea sauti yake, Zulema kalia sana humu.

Patamu zaidi ni pale solo guiter na bass zinapoachiwa zifanye mambo yao.safi sana, hii kamata mamaa nayoo cheza nayee taratibu… yoka elengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Nadhani mkuu wangu Nderumaki utakuwa umesuuzika hapo.


GS1 Yakabidhi Barcode kwa Professor Jay

October 21, 2013

IMG_0315

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.

IMG_0319

Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajube wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.

IMG_0323

Profesa Jay akionyesha kwa wanaandishi wa habari (hawapo pichani) mfano wa hundi/bango alilokabidhiwa likiwa na Barcode kwa Bidhaa yake.

IMAG0735

Pichani Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.

 

Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode.

Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.

Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.

Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.

Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.


Shai Ngenge akwaruzana na Familia kwa kuondoka BCBG

October 18, 2013

DCF 1.0

Mwanamuziki Shai Ngenge aliyejiondoa kwenye kundi la Wenge BCBG ameingia kwenye mgogoro mpya na familia yake baada hivi karibuni kuibuka mgogoro bai  L’honorable Senado.

Hayo yamesemwa na watu wa karibu na  L’honorable Senado ambaye ni rafiki mkubwa wa Papa Wemba na mwenye mapenzi makubwa na Wenge BCBG, kwa mujibu wa habari zinasema kuwa Shai Ngenge ambaye kwa kiasi kikubwa alidumu na bendi kwa takribani miaka kumi na tano kuondoka kwake ni pigo kwa bendi na kwake yeye binafsi, alipoulizwa kuhusiana na hilo Shai alisema kwa sasa asingependa kundeleza malumbani kwani yuko bize akitaarisha albamu yake ya solo ambayo anatazamia aitoe mapema mwakani, “kuna nyimbo ambazo nilianza kufanya mazoezi na BCBG ambazo nimeondoka nazo kama Duo de Paris na Quantité d’amour ambazo zimo kwenye albamu itakayotoka.

Shai Ngenge aliondoka Wenge BCBG katikati ya mwaka huu kwa kile kilicho ripotiwa kuwa ni kutokuelewana kwake na mpiga drumz wa Wenge BCBG Seguine Mignon ambaye sio tu kuwa swaiba wa JB Mpiana bali JB anamlea kama mwanaye, jambo linalopelekea yeyote anayegombana na Suguine kuwa hatarini kiajira na maisha yake ndani ya bendi kuwa magumu.


Shai Ngenge akwaruzana na Familia kwa kuondoka BCBG

October 18, 2013

DCF 1.0

Mwanamuziki Shai Ngenge aliyejiondoa kwenye kundi la Wenge BCBG ameingia kwenye mgogoro mpya na familia yake baada hivi karibuni kuibuka mgogoro bai  L’honorable Senado.

Hayo yamesemwa na watu wa karibu na  L’honorable Senado ambaye ni rafiki mkubwa wa Papa Wemba na mwenye mapenzi makubwa na Wenge BCBG, kwa mujibu wa habari zinasema kuwa Shai Ngenge ambaye kwa kiasi kikubwa alidumu na bendi kwa takribani miaka kumi na tano kuondoka kwake ni pigo kwa bendi na kwake yeye binafsi, alipoulizwa kuhusiana na hilo Shai alisema kwa sasa asingependa kundeleza malumbani kwani yuko bize akitaarisha albamu yake ya solo ambayo anatazamia aitoe mapema mwakani, “kuna nyimbo ambazo nilianza kufanya mazoezi na BCBG ambazo nimeondoka nazo kama Duo de Paris na Quantité d’amour ambazo zimo kwenye albamu itakayotoka.

Shai Ngenge aliondoka Wenge BCBG katikati ya mwaka huu kwa kile kilicho ripotiwa kuwa ni kutokuelewana kwake na mpiga drumz wa Wenge BCBG Seguine Mignon ambaye sio tu kuwa swaiba wa JB Mpiana bali JB anamlea kama mwanaye, jambo linalopelekea yeyote anayegombana na Suguine kuwa hatarini kiajira na maisha yake ndani ya bendi kuwa magumu.


Werrason na Mahombi ndani ya Ifound A Way; Werasson akiwa kivingine.

October 18, 2013

 

Wanamuziki wa Congo wengi kwa sasa wanajaribu kutoka na kuingiza ladha tofauti kwenye muziki wao hasa kwa kuwashirikisha wanamuziki wenye haiba tofauti. Wimbo huu unaitwa I found a Way wakwake Mahombi msanii anayeishi huko Sweden akimshirikisha Werasson Ngiama makanda wakaimba mahadhi ya Afri Pop ambayo kiukweli Werasson ameutendea haki.

Hii ni katika kujipenyeza kwenye masoko ya Ulaya na America ambako wanaongea lugha nyingine tofauti na Lingala, Swahili ama Kifaransa. Tayari Fally Ipupa ameshatoka na Olivia na ana nyimbo mbili zenye lugha ya Kiingereza Sweet Life na French Kiss ambazo zimebamba vilivyo sokoni. Mwanamuziki Ferre Golla naye alitangaza kumshirikisha Celine Dion na Rick Ross kwenye albamu yake ijayo. Msikilize Werrason unipe maoni yako, Uwanja wako Erick Tiger na Papaa Richard Malewa.

Ijumaa Kareem


CD Baby mkombozi wa Kuuza nyimbo kirahisi mtandaoni.

October 15, 2013

image

Suala la kuibiwa kazi za wasanii ni kilio cha kila siku toka kwa wasanii, lakini wengi wetu tunachelewa kwa sababu inawezekana uvivu wa kutafuta njia mbadala au mawazo mgando ya kufata utaratibu uliopo bila kuwaza ni jinsi gani unaweza kutanua soko lako.

Wasanii wakubwa wote hawategemei kuuza CD au DVD zao mitaani na kwenye Traffic Lights kwani kuna mfumo ulionyooka ambao nawawezesha wao kufatilia mauzo ikiwa ni pamoja na kuuza wenyewe Online kwa kutumia nyenzo kama iTune Store, CD Baby na nyinginezo.

Njia ya kuuza miziki Online inafanya uwe na uwanda mpana zaidi wa soko kwani unaweza kumuuzia shaiki wako aliyeko nje ya nchi kwa urahisi bila kwenda dukani au kutoka nyumbani kwake bali kwa kubofya tuu.

CD Baby ni kampuni ambayo inajishughulisha na kuuza nyimbo kupitia mtandao wa kijamii ikiwamo Facebook na mingineo, hii ni njia rahisi ya kuwafikia hao mashabiki wako (funs) wako kwani kwa ulimwengu wa sasa katika kila vijana wasomi wa mijini kumi at least nusu yake wanajihusisha na mitandao ya kijamii hasa facebook.

Hii ni njia rahisi sana ya kuwafikia mashabiki na kuongeza soko kwa kutumia mitandao hii ya kijamii kwa wasanii wetu. Dunia kwa sasa haiitengi Tanzania kuwa kijiji bali tunatakiwa kwenda na mabadiliko ya sayansi na Technolojia ili kuweza kukabilia na changamoto ya soko huria ambalo linaifanya dunia kuwa kijiji kwa kutumia teknojia hii ya mawasiliano.

Malalamiko ya wasanii wetu kuhusiana na wizi wa kazi zao kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na usambazaji mbovu wa kazi zao, jambo linalopelekea uchakachuaji kufanyika, wengi wa wasanii wanalalamika kupunjwa na mfumo wa usambazaji wa sasa ambapo msanii ananafasi ndogo ya ufatiliaji wa taarida za usambazaji na masoko.

Pamoja na kuwa na changamoto kadhaa kwenye mfumo husika ambapo wengi wa mashabiki hasa wa mitandaoni huishia kupakua (download) hizi nyimbo bila kulipa gharama zozote mtandaoni. jambo hili si tu linarudisha nyuma kimalipo bali linafanya uhuhishaji na urasimishaji wa sekta nzima kuwa mgumu kwani asilimia kubwa ya mapato ya nyimbo husika hayaendi kwa mwanamuziki mwenyewe na husihia mikononi mwa wajanja wachache ambao wanadownload hizi nyimbo na kutengeneza CD mitaani na kuiza.

Changamoto hii ni kubwa kwani kwa CD Baby inamtaka mwanamuziki kutotoa wimbo wake kwenye mitandao bali kuipeleka kwao kwa kwa utaratibu wa sasa wazalishaji huwa wanasambaza hizo nyimbo mpya ikiwa kama kuzitambulisha kwa mashabiki ambao mwisho wa siku hawanunui CD.

Suluhisho la hili ni kwa wanamuziki na wazalishaji wa Muziki wenyewe kutosambaza nyimbo zao na kutumia wauzaji walioidhinishwa na kunakuwa na Radio Version ambayo itatumika kama Promo kwa redio na kama mtu anaipenda basi aende kwenye maduka yaliyorasmi na ama mitandao ya kijamii kama hii ya CD Baby na kununua huko.

Ili uweze kuuza kupitia CD Baby unatakiwa kuwa mwanachama wa CD Baby ambapo utajiandikisha na kufungua duka lako kwenye mtandao. Unatakiwa kujaza Contact info zako, pili unajaza njia za malipo.

Nini Kinatakiwa?

Kwanza mwanamuziki anatakiwa kuwa na Barcode. Barcode inawezesha wimbo wako kuweza kupatikana na inatumika kama namba maalumu ya utambulisho wa wimbo wako. Barcode kwa wanamuziki wa Tanzania zinatolewa na GS1 Tanzania Pekee. Hawa ndio watoaji Pekee wa Barcode kwa bidhaa  za Tanzania. mbali na CD Baby kutoa huduma hii ya Barcode ambayo utalipia dola 20 kwa kila Albamu, bado inashauriwa kuchukua Barcode kwa GS1 Tanzania ambao pamoja na mengine utapatiwa Barcode ambazo si zitakutambulisha duniani bali zitakutambulisha kwa kuwa zina kiambishi cha nchi ambacho ni 620.

Unaweza kuwasiliana na Gs1 Tanzania kwa barua pepe: info@gs1tz.org au Simu Namba 0713666616 na 0713720725 kwa maelezo zaidi.

 

Account yako inaweza kutumikaje?

Sell your music on iTunes Kwa kuwa na account na CD baby utaweza kuuza nyimbo na CD zako kwenye iTunes, Amazon MP3, CDBaby.com, na nyingine nyingi zinazouza nyimbo kwenye mtandao. 

Wiki ijayo tutaangalia CD Baby inavyoweza kusambaza Wimbo na CD Yako kwenye mitandao mingine ikiwemo Amazon, Google Music, Itune, Rhapsody na kwingineko.

Imeataarishwa na Pius Pius Mikongoti, Afisa Muandamizi wa GS1 Tanzania watoaji wa huduma za Barcode.


Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema.

October 11, 2013

Ingawa wimbo huu maarufu toka kwa Wenge ya JB Mpiana unajulikana kama utunzi wake JB Mpiana kiukweli kabisa Wimbo huu ni utunzi wake kijana machachari Zulema ambaye ni bonge la kipaji ambacho kiukweli kwangu naona kinapotea.

Zulema ni muimbaji mzuri ambaye kwa kipidi kirefu amekuwa akisumbuliwa na uteja kwa utumiaji wa madawa ya kulevya. JB Mpiana aliamua kumsaidia Zulema kama mdogo wake na kuna kipindi alipelekwa kwa wataalamu na kupatiwa ushauri nasaha ana alitangazwa kuacha matumizi ya madawa hayo.

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Nakutakieni Weekend Njema, Natumai Meree Gladys nakati ya Moshi utakuwa umefarijika sana na sauti ya Afande ambaye anasikika uzuri humu. Kiukweli kila mtu ameutendea haki wimbo huu na Verse yake kiujumla. Sikiliza unipe maoni yako.


QPR ya Uingereza yaipiga jeki TSCSA ya Mwanza

October 8, 2013

QPR

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe wa tatu toka kulia akiwa na Viongozi wa timu ya QPR ya Uingereza wakipokea mfano wa hundi iliyokabidhiwa kwa Tanzania Street Children Sports Academy ya Mjini Mwanza, wa Pili kutoka Kulia ni Mtani Yangwe Kiongozi wa TSCSA, na aliyeshika Camera ni Israel Saria mdau wa michezo na Mtanzania anayeishi nchini Uingereza.

Hii inafuatiwa na mualiko na kutembelewa awali na Viongozi wawili wa QPR huko Mwanza ambapo Gareth Dixon na Martino Chevannes walitembelea kituo cha Kuleana cha Jijini mwanza na pamoja na mambo mengine waliahidi kusaidia watoto hao.

TSCSA ni asasi isiyokuwa ya kiserikali na na isiyojiendesha kwa faida ikiwa na makao yake makuu jijini Mwanza ambayo inajishughulisha na kuendeleza michezo kwa watoto wa Mitaani. Timu ya TSCSA imeshashiriki ziara kadhaa za nje ya nchi. Picha kwa hisani ya Mtani Yangwe.


Zenith yathibitisha Onyesho la JB Mpiana

October 4, 2013

Hatimaye ule utata wa kama onyesho litafanyika umetatuliwa na waandaaji wa onyesho hilo huku Taasisi ya uendelezaji utamaduni na wamiliki wa ukumbi maarufu wa Zenith wamethibitisha onyesho hilo kwa kuweka tangazo la onyesho hilo linalotazamiwa kufanyika Dec 21.

JB Mpiana alikuwa nchini Ufaransa mwezi September na inasemwa kwenye ndege walikuwa na hasimu wake Werasson Ngiama Makanda ambaye pia amesaini kupiga onyesho kwenye ukumbi huo huo bado tarehe haijapangwa.

Swali linabaki je onyesho litafanyika bila fujo au kipingamizi kutoka kwa Bana Congo???


WIMBO GRACE À TOI GERMAIN : Nung’uniko la HUBA la JB Mpiana

October 4, 2013

Mapenzi yanauma, Mapenzi yanatesa, mapenzi yanasumbua, mapenzi yanakondesha, kipindi JB Mpiana anatunga na kutoa wimbo huu ndio kipindi ambacho mapenzi yalimtesa sana, hebu fikiria mkeo wa ndoa anachukuliwa na mtu unayemfahamu, anaenda naye sehemu ambazo mlikuwa mkikatiza wote, anakaa na marafiki wengine ambao walimuita shemeji akiwa na wewe na sasa wanamuita shemeji akiwa na mtu wa karibu yako?

Hii ni hali tete sana kimahaba kwa mtu maarufu kama JB Mpiana na hayo ndio yaliyomkuta kwa mkewe Kipenzi Amida Shatur mama na Daida pale mkewe kipenzi alipochukuliwa na tajiri Didi Kinuani  Mkurugenzi na mmiliki wa Groupe Dikin kampuni yenye makampuni chini yake pamoja na mambo mengine wanauza madini. Lakini kwa sababu ya upendo wa kweli Mamaa Amida alirudiana na JB Mpiana pamoja na kuwa alifanikiwa kuzaa mtoto na Didi mtoto aliyepewa jina la DIAM ikiwa ni kifupi cha majina yao, mtoto mwenyewe ndio huyo aliyebebwa na JB pichani chini akiwa na familia nzima.

19436

Ijumaa ya leo naomba nikuache na tafsiri ya Wimbo Grace A Toi Germain utunzi wa Suveree Mukulu Bin Adamu Jean Bedel Tshituka Mpiana Papa Cheri Papa Matikakana Baba ya Bana Sultan. Shukrani za Kipekee kwake Kamarade Lubonji wa Lubonji kwa mtohoo huu merci mingi sana kwako Suveree.

Au sommet du mont blanc Je re-salue November… : Kileleni mwa Mlima (Mont Blanc pokea salaam zangu November…
Amour eloko oyo esalema pona banso : Upendo kitu kilichoumbwa kwa ajili ya wote
Eclaquer nga porte na zolo mawa nanga : Leo hii Pendo lanifungia mlango usoni maskini mie!!!
Natikali isolée na couloir ya déception : Najikuta nikiwa mpweke nikijazwa na majonzi,Simanzi na masikitiko
Bolingo eboyi kosekisa nga : Pendo lanikosesha raha na tabasamu
Mawa efandeli nga na matama :Huzuni wajichora chavuni mwangu
Efungoli robinet ya pinzoli : Na kufungua Bomba la machozi
Soki ezalaki mayi ya Regideso : Ingekua machozi yangu ni maji ya Bomba ya (REGIDESO)Shirika la maji huko Congo
Mbele baye kolongola compteur : Basi kama tayari Bomba limesha fungwa kutokana na uwingi wa mtiririko wa maji
Bolingo po’nini Yo okomi Moselu na maboko manga Lokolaaaa ngolooo ?: Pendo kwanini watereza mikononi mwangu kama Samaki?
Germain Souries-moi : Germain Nionyeshe Tabasamu lako
Je t’en supplie (Je t’en supplie) : Tafadhali
Ba scenes ya ba amoureux Nakoma komona lokola bilili ya télévision(Germando) :Kwangu mimi kuwaona wawili wapendanao ni jambo ambalo silijui tena,Hua natizama kama picha kwenye TV (Germando)
Germain Souries-moi Je t’en supplie :Germain Nionyeshe Tabasamu lako Tafadhali
Koyenga yenga lokola kipekapeka Oyo azangaka fololo : Nikiwa nahaha mitaani kama kipepeo kinacho tafuta Uwa!!!
En me promenant nalokotaki la photo d’un jeune très sympa : kutokana na Mihangaiko hayo nimebahatika kuokota Picha ya Kijana Maridadi
j’avais bien voulu que djo ango asekisa nga : Ningependelea Kijana alieko kwenye Picha anionyeshe Tabasamu lake (anichekeshe)
photo ezalaka sourde pe muette : Kumbe picha hua haisemi wala haisikii
ordinateur ya nzambe par la prière epesaki nga identité naye nyonso : Baada ya kuingia kwenye maombi nikaenda kwenye computer ili nipate kujua vitambulisho vyake.
Germain Germando Rue de l’amour (Rue de l’amour) : Jina lake Germain Germando Unakaa kwenye Mtaa wawapendanao
Tu vis dans un oasis qui s’appelle affection : Unaishi kwenye OASIS inayoitwa Upendo
C’est pourquoi je t’aime (je t’aime) Germain Germando : Nikwamaana hiyo nakupenda (Nakupenda) Germain Germando
Rue de l’amour (Rue de l’amour) : Mtaa wa wapendanao
Germando T’es la musique de mon affection : Wewe ni wimbo niupendao
de nature aux couleurs d’un martin pêcheur Germando en… :Mwenye aina na rangi ya Kingfisher Germando…
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
Dedication : Heiin kombo nanga oyebi Adjola suba motema humm : Helin Jina langu walijua Adjola Suba moyo humm
kombo nanga oyebi iii Jacky Lomata Ya Germando : Jina langu walijua!!! Jacky Lomata kaka yangu Germando, Bébé mobondo Jean Tekbwe
Nzambe sala likamuisi Nzambe euh sala likamuisi oooh : Mungu Tenda maajabu Mungu fanya maajabueee!!!
Yanga Amida akoma à zéro mètre nanga : Naomba Mpenzi wangu Amida awe sana karibu nami,Daida Soraya Junior Fari
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
(Afande) nafikiri ni Portuguese language anayejua tafsiri yake haya!!!
Eyukera sentre amore Christian Bashila
Eyukera sentre amore Riva Menga
Eyukera sentre amore Max Mwanza
Eyukera sentre amore Renaud Busiko
Eje kamunere vaka Fanfan Longa
Grâce à toi Germando Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa
Mwana ya moto ata omelisi ye libele na butu :Mtoto asiekua wakwako utampa ziwa (kumnyonyesha) usiku kutwa na akapatwa na usingizi
na tongo tango akolamuka akotuna wapi baboti baye :Asubuhi atakapo amka ataanza kulia wapi walipo wazazi wake
Hernestine Mambweni ata yo okendeee : Hernestine Mambweni Hata kama waondoka…
Quand j’avais atteint l’âge de raison,Senado me disait : Nilivyo timiza age of reason
Senado kaniambia :
L’orgueil est la seule force de l’imbécilité :Jehuri ndio nguvu pekee za kijinga
Adida Royz
Bababi bobo bababi bobobo bobo bobo ubo
Grâce à toi Germando (Charles Kabuya) Loboko nanga edivorcer na litama : Kutokana na wewe Germando kilio changu kimeisha,wafanya niondoe mkono wangu kwenye shavu
Riche ou pauvre tout le monde a droit A l’amour : Tajiri kama vile Maskini sote tunayo haki ya kupendwa

Ijumaa Kareem kwako Papaa Farid Al-Shukairy Mukulu wa Bakulu Merci mingi Papaa kila nikivaa Kanzu na Kofia nakukumbuka asante sana,  MaMeree Gladys nakati ya Moshi, heshima kwako, Hadji Le Jeebeeneeque umepotea sana mkuu, Sadiq Tiger Werasonique damu, Papaa Richard Malewa, Dj wangu Kipaso heshima kwako na mashabiki na wasomaji wote wa Blog yetu.


%d bloggers like this: