Soyons Serieux ya BCBG yaendelea kutesa Kinshasa

September 30, 2012

Tangu kutoka albamu ya Wenge BCBG ya Soyons Serieux imeendelea kutesa mitaa ya Kinshasa.

Kwa mujibu wa mtandao maarufu na unaoaminika wa Digital Congo albamu hiyo bado inatesa kwenye mauzo, kupigwa mitaani kwenye radio na hata kwenye sherehe. “albamu hii inanyimbo nyingi nzuri na zenye mvuto na kupigwa kifundi ambazo yeyote mpenda muziki hawezi kuacha kuzisikiliza hivi karibuni…” ilisema sehemu ya habari hiyo.

Hayo pia yamedhihirika hata upande wa pili wa Mto Congo yaani Brazaville ambako JB na kundi lake la Wenge wanapendwa zaidi, amekuwa akipata mialiko mingi ya huko na kila mara kupata interview za magazeti ama radio na hata kwenye vituo vya luninga. hii ni kuthibitisha jinsi gani kazi ya Binadamu Mukullu Papaa Cherie inavyokubalika.

Habari hiyo imemalizikia kwa kuwakaribisha wapenda muziki kwenye show ya BCBG kwenye kiota chao cha Crystal Club leo jumapili kilicho kwenye barabara ya June 30 kupata burudani mwanana. Nakuacha na kibao Bologna ambacho binafsi nakipenda sana ambacho kiko kwenye albamu hiyo ya Soyons Sirieux. Jumapili njema waungwana


Heritier Watanabehuenda akatimuliwa Wenge Musica Maison Merre

September 30, 2012

Mwanamuziki Heritier Watanabe wa WMMM

Mwanamuziki nguli na mwenye sauti ya Radi Heritier Watanabe toka kundi la Wenge Musica Maison Merre WMMM linaloongozwa na Grand Tata Werasson Ngiama Makanda anaweza kutimuliwa kundini.

Watanabe ambaye siku za karibuni amekuwa akigonga vichwa vya habari hasa baada ya kurejea kundini mwanamuziki wa siku nyingi wa kundi hilo Japonaise na kupewa uongozi. kumekuwa na vita ya kugombea madaraka kati ya Japonaise na Watanabe na kwa kiasi fulani Watanabe ambaye tangu awali anatabia ya utukutu amekuwa haheshimu ratiba za mazoezi, anagombana na wenzake kwenye kundi na hata kiongozi mkuu Werasson amekuwa hamsikilizi kilisema chanzo cha habari hizi.

Watanabe ambaye wiki mbili zilizopita aliachwa na bendi yake ilipokwenda kutumbuiza Muanda huko jimbo la Bas- Congo ikiwa nai adhabu baada ya kupayuka kwenye vyombo vya habari kuwa kuna upendeleo kwenye kundi lake na ye kuona kama hatendewi haki. Habari pia zimesema mwanamuziki Mwingine Papii Kakol aliwahi kupata adhabu kama hiyo pale alipoonyesha utovu na nidhamu wakati wa mazoezi ya “Zamba Playa” ni baada ya kukwaruzana na Wata, Wajuzi wa mambo wanasema kutoonekana kwenye show ile na hata juzi jumapili kwenye Show ya Kisenso hakuwepo inawezekana ndio byebye.

Mgogoro wa uongozi ambao washabiki wanauhusisha na matajiri ambao wanauhusiano na hasimu mwingine Koffi Olomide ambaye awali alikuwa rafiki mkubwa wa Werasson na sasa yuko kambi ya Jb Mpiana, habari zinasema kuwa Watanabe anachochewa na watu wa nje asikubali kuwa chini ya Japonaise  ambaye tangu arejee kwenye bendi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miaka kumi amekuwa gumzo kila bendi inapopiga.


Usiku wa sauti na Diamond Sound sasa mwezi Ujao

September 28, 2012

adolp mbinga

Adolph Mbinga

alain mulumba kashama

Allain Mulumba Kashama

elly chinyama

Elly Chinyama

Ibonga Katumbi Jesus

 

richard mangustino (2)

Richard Mangustino

ONYESHO la Usiku wa Sauti na Marafiki kweli ambalo litakaowakutanisha wanamuziki mbalimbali waliowahi kupigia bendi ya Diamond Sound ‘Dar es Salaam Kibinda Nkoi’ pamoja na wanamuziki wengine nyota nchini utafanyika mwezi ujao.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Endless Fame inayoandaa onyesho hilo, Zulfa Msuya amesema mjini Dar es Salaam kuwa, kusogezwa mbele kwa onyesho kumetokana na baadhi ya wanamuziki kuwa safarini huku wengine wakiwa katika kazi ya kurekodi na bendi zao.

“Tumelazimika kusogeza mbele onyesho hili kwa sababu walengwa wakuu walikuwa safarini, wengine walikuwa wana kazi ya kurekodi, kwa hiyo hawakuweza kuanza mazoezi kwa muda uliotakiwa, lakini sasa wamesharejea wote na wako tayari kuanza kambi kwa ajili ya siku hiyo,” amesema.

Zulfa amesema wanamuziki hao watakuwa wakifanya mazoezi katika ukumbi wa Princess Hall pale Sinza, Mapambano na mazoezi hayo yatachukuwa wiki mbili.

Naye kiongozi wa Diamond Sound, Ibonga Katumbi ‘Jesus’ amesema wanataka kufanya onyesho ambalo litakuwa historia, hivyo bila timu yote kukamilika isingekuwa rahisi wao kuanza mazoezi.

“Sisi hatujakaa pamoja zaidi ya miaka 12, ili kupata muziki wenye kiwango cha juu ni lazima tukae si chini ya wiki mbili kufanya mazoezi, ili watu wasikie ladha ile ile waliyokuwa wakisikia TCC, Silent Inn.

“Wasisahau kuwa tutapiga pia nyimbo za Beta Musica, sasa mtu kama Adolph hakuwepo Beta, Kata Nyama amepiga Beta wimbo mmoja, lakini kuna wanamuziki kaka zetu watakuwepo pia nyimbo zao ni za miaka ya 1980 huko nao lazima zifanyiwe mazoezi, tuko makini kuhakikisha tunafanya hili kwa ufanisi mkubwa,” amesema.

Jesus amesema kuanzia wiki ijayo utaratibu wa muda wa kuanza mazoezi, ukumbi na matangazo mengine mbalimbali yataanza kutoka kwa nguvu kwenye vyombo vya habari. Ameongeza pia kuwa hata nyimbo zingine zitaanza kusikika katika mapigo tofauti lakini zikiimbwa na wanamuziki wote wa zamani.


Wenge Re Union palikuwa hapatoshi

September 27, 2012

CLAN WENGE wenyewe kila mmoja kwa wakati wake mewahi kuungama kuwa hawana uhasama nje ya jukwaa na tofauti zao zipo kwenye kazi tuu na hili limethibitishwa karibuni walipojumuika pamoja kwenye msiba wa mwanadada Monica Ceres wa Wenge BCBG na hata msiba wa Madillu na hata Werasson alipopata ajali JB Mpiana na Adolph walikuwa wakwanza kufika.

Katika vitu naombea kukutana nacho kwa macho yangu makavu ni mjumuiko kama huu tena, hiiilikuwa ni mwaka 2010 walipojumuika tena kwenye jukwaa moja Werrason, Blaise Bula, Tata Adolphe Dominguez,  Didier Masela Vandomas, Alain Makaba Prince, Emelia Liase Doming’ong’o, Alain Mpela Afande kasoro JB mpiana ambaye alikuwa yuko Paris Ufaransa kwa ajili ya kumalizia Albamu yake.


Angalia Audition ya Maisha Plus Dar jinsi ilivyovunja record !!!

September 25, 2012

Nyomi hili liliambiwa litasailiwa siku inayofuata, baada ya majaji kuzidiwa

Washiriki Nyomi wakiwa wanasubiri zamu yao ilibidi siku isogezwe mbele ili walao waweze kudahiliwa.

Wow. We knew we were going to get a big crowd for our two day audition in Dar lakini hatukujua ingekuwa hivi, asante kwa wote mnaotuunga mkono, you all made this possible. Washiriki waliojiotokeza ni wengi kuliko matarajio yetu.

Wakati Audition zinafikia tamati, vipindi navyo vimeanza kuruka hewani kila siku kuanzia saa nne kamili usiku ndani ya TBC1, catch all the drama, all the laughs, all the lessons.

IMG_1822

IMG_1873

Baadhi ya vijana waliojitokeza


Usiku wa Mayenu ndani ya Mzalendo Pub

September 21, 2012

USIKU wa MAYENU leo FURAHIDAY ndani ya Mzalendo Pub, miLLennium tOwers, Dar es SaLaam, TZ ni Hatareeee, njoo ukutane na WATU wa NGUVU.


Wimbo Liberation wa Wenge Musica BCBG

September 21, 2012

Tunaendelea na kukokotoa nyimbo zetu za Lingala, Wimbo huu umetungwa na Aimelia Lyase Doming’ong’o wa Wenge BCBG toka Albamu ya Titanic ambayo ilikuwa ni moja ya Albamu zao za kwanza kabisa.

Wimbo huu binafsi naupenda sana na hasa verse ya Afande Alain Mpela ambaye kiukweli sijui ni kwanini ameamua kuondoka kundini kwani pamoja na jitihada zake bado hajafanya vizuri kabisa.

Aimelia Lyase ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa akifanya vizuri sana na Wenge BCBG naye aliamua kutoka kivyake, nitakuleteeni story kwa nini Lyase aliamua kuondoka BCBG na kwa sasa yuko wapi, maisha yake ya Muziki siku zijazo.

Kama nilivyosema tafsiri hiii si rasmi hivyo mwenye kuweza atie nyama zaidi.

LIBERATION

WENGE BCBG (TITANIC)

AIMELIA LIASO

Baloba kutu nalingaki yo Na moyeke Po motindo tolingani epesi solo folie yaaa, Bolingo tango ekobandaka ngonga ekobeta teo tokomi kolingana malembe malembe Na bolingo oo ekoti motema milema na milema Charles Kabuya boni yo Sali boye

· Wamesema kwamba ninakupenda Kwa juju Kwa sababu tumependana Kama vichaa, Penzi linapoanza halipigi kengele na huanza taratibu taratibu Charles Kabuya kwa nini unafanya hivyo.

Titi yaka tuna ngai, Elili yokotuna nga Oya Aimelia Liaso talaka Na biso Te, Oya Alain Mpela nga nakoloba nini mokolo ya kozonga Na Mboka Na nga Mboka ya Bapapa mpe Bamama babota biso oo.

· Titi njoo uniulize Kivuli chako huja kuniuliza O Aimelia Liase nyumbani, Nchi ya akina baba Na mama walimozaliwa.

J.B Mpiana tunela nga ye, Po nini Alain otalaka nga ee Oya Cele Bula nga nakolela nini mokolo akozonga Na Mboka Na nga Mboka ya Bapapa mpe Bamama babota biso oo.

· J.B Mpiana niulizie Kwa nini Alain waniachia hivyo O Cele Bula nitaliaje lini siku atakaporudi nyumbani Nchi ya akina baba na mama walimozaliwa.

Po nini, Ponini, Po nini Nzambe, Mokili ekomi bongwana bongwana likambo ya somo Po Na biso bato ya Mokili boyokani ikeleve Charles yaka yaka kopelisa mwinda Na ndako yango molili Cele yo Charles kabuya Na nga aa

· Kwa nini, Kwa nini, Kwa nini mungu Duniani kigeugeu Ni jambo la huzuni sisi watu Duniani tusikilizane Charles njoo, Njoo unurishe/Ung’arishe chumba changu Giza Limezidi Charles Kabuya wangu.

Nayebisaki yo wuta kala Charles Kabuya, Nalobelaki yo wuta kala Mike Toto oo, Je pourrais pas te quitter amie d’ amour Yawe talela nga likambo lelo nga nakomi na pasi na nga bapasi na nga Alain afuta…………………….

· Nilikuambia tangu zamani, Nilikuzungumzia mapema Mike Toto sitokuacha rafiki wa Kimapenzi Mungu nitazame mkasa huu, Leo nimetekwa katika matatizo Matatizo yangu atalipa Alain……………

Soki bolingo ewutaka Na Nzambe Te nde ngai nazanga yo ozali fleur oyo naloni pembeni ya ebale mwinda aa mpe malasi ya vie na nga aa

· Kama mapenzi yasingetoka Kwa mungu ningekukosa wewe ni ua nililopanda pembeni ya bahari wewe ni taa pia manukato ya maisha yangu.

Ayenhe yoyo nalela bolingo Na nanga wuta bomwana, Nalela mama mokonzi Grace Nzenga Na ngai Namona Mbemba akokola Na mabele Nalela Souverain Patchou nalela matabisi alima masoi ………….

· Ayenhe nimekua nikililia penzi langu tangu utotoni Nalia mama mkubwa Grace Nzenga wangu Nimemuona Mbemba akikulia Ziwani Namlilia Mfalme Patcho

Oyebi bolingo batango mosusu epesaka liboma Papito Mbala Tate moko Pinzoli Na miso ekokita se po ya souci nayo Bolingo makasi Aladji Djambo manase ya Mbula nakopola sepo ya souci ya vie chance Na Kavungu Ni mokonzi…………………

· Waelewa kwamba mapenzi wakati mwingine husababisha mauaji Papito Mbala, Machozi yanidondoka juu ya Penzi la nguvu Aladji Djambo nimelowa na mvua kwa ajili ya Kavungu mkubwa………..

 

Shukrani za kipekee kwa mashabiki wangu nimefarijika nimepata email toka kwaEmmanuel Msigwa toka Pride FM Radio ya Mtwara pamoja sana mukubwa. Nawatakia Ijumaa Kareem


%d bloggers like this: