MSIKILIZENI KIJANA ” DEPLICK ” WIMBO ” CRI DE BILENGI “

August 31, 2014

MIEZI KADHAA BAADA YAKUJIONDOA KWENYE GROUP ” WENGE MUSICA MAISON MÈRE ,KIJANA DEPLICK, INGAWA ALBUM YAKE,BADO YASUBIRIWA, KATUPIA KIBAO CHA KWANZA ILIMPATE KUSIKIA UHONDO,KADHALIKA,MUWEZE KUMSAPOTI KATIKA KAZI ZAKE.

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI,UPATE KUUSIKILIZA NA KUONA VIDEO YA WIMBO ” CRI DE BILENGI ”

USISITE KUTOA MAONI YAKO

ASANTENI

Lubonji Wa Lubonji

 


VIJANA WA TANO MACHACHARI WA WENGE MUSICA MAISON MÈRE

August 29, 2014

10560451_714487741955059_9175257174060878161_o

Haya!!! WEWE KAMA MPENZI KWELI WA MUZIKI ,HASA WA WENGE MUSICA MAISON, BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI, KISHA TUTAJIE MAJINA YA WOTE AMBAO WANAPATIKANA KWENYE PICHA ILIO HAPO JUU!!! ANZIA KUSHOTO NENDA KULIA !!!

Lubonji wa Lubonji

 


TUNAENDELEA KUWALETEA VITU VIPYA!!! FERRE GOLA TENA HUYOO!!!

August 27, 2014

 

BURUDIKA KIDANSI NA FERRE GOLA NIKABORONINA JESUS DE NUANCES !!!

KAWALETEA WIMBO MPYA ” PILI PILI YA MBUMA ”  UNAOPATIKANA KWENYE SINGLE ” PETITE YA QUARTIER “, AMBAYO IMETENGENEZWA KWAAJILI YA MATANGAZO YA MDHAMINI WAKE KIWANDA CHA BIA ” PRIMUS “.

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UPATE KUUSIKILIZA WIMBO AUDIO, VIDEO IPOKWENYE MATAYARISHO TUTAWAWEKEA BAADAE!!!

Lubonji Wa Lubonji

 

 


MSHAHARA WA KAZI NI MALIPO TIZAMENI ( FERRE GOLA / FALLY IPUPA )

August 27, 2014

1396955_681203195295122_2653493686008963393_o

VIJANA HAO WAWILI WAMEAMUA KUFANYA KWELI,

KULIA KWENYE PICHA NI JUMBA LA FERRE GOLA TAYARI KAZI IMEKWISHA MALIZIKA

KUSHOTO PICHANI NI JUMBA LA FALLY IPUPA, BADO UJENZI WAENDELEA!!!

TUNAZIDI KUWAPONGEZA

 

Lubonji Wa Lubonji


MPYA HIYO YA FERRE GOLA – KATSHOU KATSHOU #AUDIO

August 27, 2014

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UPATE KUSIKILIZA WIMBO MPYA WA FERRE GOLA ” KATSHOU KATSHOU ”

VIDEO YAKE ITATOLEWA HIVI KARIBUNI

 

Lubonji Wa Lubonji


WERRASON YUKO KWENYE HARAKATI YA KUFUNGUA KAMPUNI YA UUZAJI NA UNUNUZI WA MADINI

August 27, 2014

10569061_707900342613799_7717490699149915144_n10485516_707900192613814_5157759356185635112_o

 

Bofya kwenye kichwa cha Habari

KATIKA MPANGILIO WAKUJISTIRI KWENYE MAISHA YAKE PAMOJA NA FAMILIA HUKO MBELENI,

MSANII MAARUFU WA MUZIKI INCHINI CONGO WERRASON NGIAMA MAKANDA,YUKO KWENYE HARAKATI YA KUFUNGUA KAMPUNI KUBWA YA UUZAJI NA UNUNUZI WA MADINI.

KAMPUNI HIYO IJULIKANAYO KWA JINA LA ” EXAUGLA “, YAANI MCHANGANYIKO WAMAJINA ZA MABINTIE   (EXAUCÉE na GLADY ).

KUPITIA KAMPUNI HIYO, MADINI MNAYO YAHITAJI MFANO KAMAVILE (Dhahabu, Almasi, Shaba na Colbats… ) YANAPATIKANA.

TUNAMTAKIA KILA LA KHERI LE ROI DE LA FORET.

Lubonji Wa lubonji


FERRE GOLA KAIMBA MZEE MWENYE WIVU, KAMLENGA NANI ? MSIKILIZENI

August 26, 2014

KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI WILLY, FERRE GOLA KAIMBA WIMBO WA MZEE MWENYE WIVU.

BONYEZA KWENYE KICHWA CHA HABARI  UPATE TAFSIRI YA MANENO YAKE.

 

Eloko oyo Bolingo Ezalaka Sukali na ebandeli / MAPENZI HUA MATAMU PALE TUU UHUSIANO BADO UPO MWANZONI !!!

Amitié mpe ezalaka sukali soki boyokani / URAFIKI MZURI  NIWAKATI WATU WANAISHI KWA MAELEWANO

Kasi tango mosusu ekomaka bololo soki Moto akaniseli Moninga naye Mabe / WAKATI MWENGINE URAFIKI WAINGIWA NA DOSARI , NIHASA PALE MMOJA KATI YENU HUMFIKIRIA VIBAYA MWENZIE.

Vieux Jaloux abongami akomi na Camps ya Ba adversaire, / MZEE MWENYE WIVU KESHA GEUKA,NA KWASASA YUKO UPANDE WA WAPINZANI .

Akomi kosalaka contre attaque na vie nangai / KAYALETA MASHAMBULIZI YAKE HADI MAISHANI MWANGU

Bakale oyo mukulu alobaka nayoka mpe na sango kasi lelo oyo,namoni yango na miso / VIKWAZO NA VIPINGAMIZI KAVIZUNGUMZIA MUKULU ( JB MPIANA ),NILIKUA NIKIVISIKIA, KWA LEO HII YAMENIKUTA NAMI PIA.

Nasengi na SHABANI RECORD aya kotongela nga ndakoo !!! nabaye!/ OMBI LANGU LIMWENDEE SHABANI RECORD ILI AJE KUNIJENGEA NYUMBA, NIMECHOKA MIMI

Navivre nangai na KINKOLE que na KIN oyo, Vieux Jaloux akoma kokana ngai / NIENDE ZANGU NIKAISHI MAENEO YA KINKOLE, KWA HALI ILIVYO SASA HAPA JIJINI KINSHASA YANITISHA, MZEE MWENYE WIVU KAONEKANA MWENYE CHUKI SANA NAMIMI.

Lokola Soso na Mpese / CHUKI ALIONAYO KWANGU NIKAMA YA KUKU NA MENDE

Lokola Mpuku na Nyau / KAMA YA  PANYA NA PAKA

Lokola Le Loup et l’ Agneau / KAMA MBWA MWITU NA KONDOO

Nzambeee, Nzambee, Nzambe Alaah zala mokengeli nangai / BABA MUNGU WANGU WEWE NDIE MLINZI WANGU WA PEKEE !!!

Bamambo nini ngai na sala ya mabe,mpo baboma ngai likulusu / NIKIPI KIBAYA NILICHO KITENDA HADI NIWEKWE MSALABANI!!!

Lokola baboma Yesu masia eh!!! / KAMA ALIVYO SULUBIWA YESU MASIA !!!

Soki Ngai Mpe nasalaki mabee eh !!! likunya na bango eleki makasi ba Jaloux eh !!! / INGAWA NAMI PIA NINAYO MAKOSA YANGU, ILA WIVU WAO WAPITISHA KIPIMO!!!

Mauwa na nga basombela yango masanga mpe basala feti / MATATIZO NINAYO KABILIANA NAYO,KWENU NYINYI NI FURAHA,MNASHEHEREKEA KWA KILEO

Balinga se moto azanga Bango basepela, mpo bakabela ye,nasima baloba avivraki mpo na bango / RAHA YAO NIKUMUONA MTU KATESEKA,WAMLETEE MSAADA, HUKU WAKIMSIMANGA ETI BILA SISI ANGEISHI VIPI HUYO?

lubonji Wa lubonji

 

 


WEEKEND NJEMA NA VIDEO MPYA YA ROGA ROGA, WIMBO ” CONTENTIEUX “

August 24, 2014

 

JUMAPILI NJEMA NA ROGA ROGA, Wimbo Mpya ” CONTENTIEUX ” Bofya kwenye Kichwa cha Habari

 

Lubonji Wa Lubonji


NI KWELI KOFFI OLOMIDE KAKOPA KWA JB MPIANA DOLA 30.000 $ ?

August 21, 2014

 

NI KITUGANI KINACHOENDELEA KATI YA JB MPIANA NA KOFFI OLOMIDE ? BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UPATE MAELEZO ZAIDI!!!

Tofauti zinazo jitokeza hivi karibuni kati ya Wasanii hao wawili yatujia vigumu kabisa kujua kiini chake.

Kwanza ifahamike kwamba ma SUPERS STARS haoWote wawili ni Majirani, wanaishi JIJINI KINSHASA kwenye Mitaa ya kifahari mahala panapo julikana kwa jina la ” Montfleury “.

Yasemekana Mzozo wa siku hizi Umeibuka kutokana na kitendo cha JB MPIANA kushindwa kumpa Mualiko Jirani yake KOFFI OLOMIDE, wakati alipo andaa SHEREHE kabambe yakumhenzi Bintie DAIDA kwa ajili ya B’Day yake yakutimiza miaka 18, Tarehe 14-07-2014, Wakati wapo Wasanii na Watu wengine Maarufu waliopata fursa ya kuudhuria napia kuwa mashahidi kwa Tukio hilo ambalo liliacha Gumzo JIJINI KINSHASA. Pamoja nakuwepo na waalikwa wengi,  Watu walipatwa na mshangao pale walivyo muona Kama Mgeni Rasmi ( WERRASON ),walikuwepo pia ( ADOLPH DOMINGUEZ, FALLY IPUPA )…

Siku Chache Baadae, KOFFI OLOMIDE  kwa Upande wake,kaandaa pia SHEREHE kwa Ajili ya B’Day ya Binti yake DIDI-STONE ambae katimiza umri wa Miaka 15.

JB MPIANA huku akiendelea na Shughuli zake, kakaa kimya bila kujali yale yanayopita kwa Jirani, Mtu wakwanza ambae Tumemsikia kwenye Vyombo vya Habari,ni KOFFI OLOMIDE,kamtupia mwenzie kwa kusema : ” KWAKWELI MIMI KUNAWAKATI MWENGINE YANIJIA VIGUMU  KUWAELEWA  KABISA WATU WENGINE, MTU KASHINDWA KABISA KAZI YA MUZIKI,ANACHOKIJUA KWA SASA NI MAJUNGU PEKEE, WALA SI MIMI NILIE MCHUKULIA MKEWE!!! CHUKI YA NINI JAMANI !!!  MIMI SIPO HUKO KABISA “.

Hapa yatubidi tukumbushia kidogo, Wakati bado wanaelewana , KOFFI OLOMIDE, Tumemsikia akimtolea sifa Nyingi sana JB MPIANA siku ya B’Day yake Tarehe 02-06-2014, Namnukuu : ” TUNAPO CHUNGUZA VIZURI KWENYE KAZI YA MUZIKI INCHINI CONGO, MA STARS KATIKA FANI YA MUZIKI WAPO WAWILI, NAO SIWENGINE BALI NI MIMI NA JB MPIANA “.

SASA NANI KAJAKUWASHA MOTO ?

Mtu ambae kajiingiza kwenye Mzozo huo ni Chizi wa Mfalme WERRASON anaejulikana kwa jina la SANKARA DE KUNTA. Yeye kamkingia Ubavu JB MPIANA,kwa kumtolea khashfa KOFFI OLOMIDE pale alivyo tamka kwamba, HUYO MZEE NIMPUUZI TUU, WALA HANA LOLOTE, MWACHENI HUYO KAISHA KABISA, KWANZA MADENI YAMEMZIDI ,HADI KAENDA KUKOPESHA KWA JB MPIANA, KIUMBE ALIE MWEMA WA WATU KAMGEA DOLA 30.000.

Maneno hayo, yamemkera vibaya sana KOFFI OLOMIDE, Kwenye video nilio iambatanisha na Post hii, MOPAO MOKONZI katoa maneno ya khebei kwakusema : ” SINA LAKUSEMA,MIMI NAWASIKILIZENI TUU, NA KAMA UNALO LAKUONGEA, BASI NENA YALE YALIO NA UKWELI,SI LAZIMA KWAKO WEWE KUJIFICHA  MGONGONI  MWA MTU MWENGINE. NAKUOMBA NENDA KWENYE TV,NA UONYESHE KWA MAANDISHI YANAYO THIBITISHA MATAMSHI YA HUYO MSEMAJI WENU, AMBAE KADAI  KWAMBA NIMECHUKUA KUTOKA MIKONONI  MWAKO PESA. KWELI KAMA WEWE NI MWANAUME WA UHAKIKA, BASI FANYA HIVYO ILI UKWELI UDHIHIRIKE !!!

 

LUBONJI WA LUBONJI


HATIMAE FERRE GOLA KAJIELEZA ” SINA UPINZANI NA WERRASON “

August 20, 2014

 

KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI ” WILLY “, FERRE GOLA KAONGELEA MAMBO MENGI KUHUSIANA NA GROUP LAKE,KUJIONDOA KWA BAADHI YA WANAMUZIKI, NA MZOZO ULIOPO KATI YAKE NA WERRASON. ( KWA MAELEZO ZAIDI BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI ).

FERRE GOLA : KWANZA SALAMU ZANGU ZIWAFIKIE MASHABIKI WANGU, NAPIA WAPENZI WOTE WA MUZIKI AMBAO WANATUFWATA KWA WAKATI HUU. UMUHIMU WA MTU KUFANYA MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI UPO WAKATI PALE LIPO NENO AU JAMBO JIPYA LA KUONGELEA.

WALA MSIWACHUKULIE WATU WANAO FWATILIA MAMBO TUYAFANYAYO SISI KAMA WAJINGA, SIONI HAJA YAKUJA KWENYE TV WAKATI SINA JIPYA LAKUZUNGUMZIA. TAKRIBAN MIEZI SITA AU SABA SIJAONEKANA KWENYE TV.

MTANGAZAJI : Bado twasubiria kutolewa kwa Single ya Mdhamini wako, Mda mrefu umepita sasa,Ipo Tarehe kamili ambayo Single hiyo itatolewa Rasmi?

FERRE GOLA : Tumesha maliza kazi kubwa ya Single ” PRIMUS PETITE YA QUARTIER “, Tatizo lilijitokeza lipo kwa upande wa Mdhamini wetu, kaomba Wimbo uwe mfupi wa Dakika 6 Kwa ajili ya matangazo ya Kibiashara,wakati sisi tulikua tayari tumesha tengeneza Wimbo wa Dakika 9. kwa maana hiyo,tumelazimika kurudi tena Studio ili tuyafanye marekebisho kama yaliyo hitajika.Kwa wakati huu tupo katika maandalizi ya Video Clip.

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Siku zahivi karibuni, Tumegundua kwamba wapo Vijana wengi walio jiondoa kwenye Group lako,Tatizo ninini hasa? Kosa latokana na wewe, au lipo kwa wale Vijana  ambao Wewe ndie umewalea katika Muziki,na kwasasa hawaridhishwi na utendaji wako wa kazi !!!

FERRE GOLA : Kama nilivyo kuambia hapo awali, Takriban Miezi saba sijapita kwenye Runinga,hakuna Mtu kanisikia napiga kelele kutokana na hili wala lile,yamaanisha Mambo yangu si mabaya. Ntakupa Mfano wa Album ” BOITE NOIRE “, Unapo chunguza Hit Parade Mbalimbali,utagundua Imeshikilia nafasi nzuri, Ipo kabisa kileleni, Kama si nafasi ya kwanza basi ni yapili nakadhalika… Sioni kitugani kitakacho nifanya nilalamike.

MTANGAZAJI : Kitendo cha Vijana hao kujitengua kwenye Orchestra yako,hakikupi shida? mbona wamesha ondoka wengi?

FERRE GOLA : Kumbuka mwanzoni nilivyotoa Album yangu ya kwanza ” SENS INTERDIT “,nafikiri nilikua Mwenyewe,peke yangu . Kwa wale Vijana walio jiondoa, ntakalo lisema ni kwamba,” NAWATAKIA KILA LA KHERI HUKO WAENDAKO “.

MTANGAZAJI : Hayo huyanenayo niyamoyoni kweli?

FERRE GOLA : Ndio, nayatoa moyoni mwangu kwa uhakika, Mimi bado mchanga, ndo kwanza naanza,Mwaka 2006,huoni kabisa niponipo!!! Jamani !!! Walio jiondoa,nawatakia maendeleo mema huko waliko. Wapo baadhi yao ambao bado tunaendelea na mawasiliano,wananipigia simu kunijulia hali!!!

MTANGAZAJI : Kwamfano Mtu kama CHIKITO hua anakupigia simu?

FERRE GOLA : Ndio, CHIKITO mara nyingi tunawasiliana naye

MTANGAZAJI : Yaani kumbe hajadanganya, kaniambia hua anakupigia simu na mnaongea mara kwa mara!!!

FERRE GOLA : CHIKITO ni Mwanamuziki pekee aliejiondoa na ambae hadi leo bado mawasiliano haijakatika.Hua ananipigia simu na kunifaarifu jinsi gani maendeleo yake yalivyo kwa sasa. Hata wakati yuko Inchini Angola,tuliendelea kuwasiliana.

MTANGAZAJI : Inamaana CHIKITO kesha jiondoa kabisa kwenye Group lako!!!

FERRE GOLA : Kanipigia Simu siku mbili zilizo pita, Anahitaji nimkabidhi Hati yake ya kusafiria,Nikamwambia nakumuelewesha kwamba, wakati ulivyo jiunga na Group, hujaja na Pasipoti,na Unavyo amua kujiondoa ni haki yako, basi Nenda kamavile hujawa na PASIPOTI. Tuliongea kiustarabu kila Mtu kamuelewa mwenzie.

MTANGAZAJI : Si unaweza ukamgea hiyo PASIPOTI kama zawadi,yule ni Mwanao, kwanza alikua akikuita  BABA ” PAPA HERVE ” .

FERRE GOLA : Wala sioni haja yakuongelea maneno mengine ilimradi tuu nikuridhishe wewe!!! hivi unacho ongelea hapo Ni Mwanamuziki au Wanamuziki !!!

MTANGAZAJI : Ninacho hitaji kufahamu ni kwamba Hujapatwa na huzuni wowote,wakati wamejiondoa Vijana wako? ntawataja CHIKITO, NICODEM, R-KELLY !!!

FERRE GOLA : Sikiliza, kuna itilafu kidogo katika usemi wako, Wapo Wanamuziki waliojiondoa na wapo pia wale ambao niliwaachisha kazi.

MTANGAZAJI : Kweli ? Wapo walio fukuzwa kazi wakajidai kujiondoa? basi yapo mengi tulikua hatuyajui kabisa!!!

FERRE GOLA : Mikokotano si kazi yangu hasa, kwakifupi, nawatakia kila la kheri,iwe wale waliojiondoa,au wale niliowaondoa mimi.Hivi waweza nikumbusha ni Nyimbo gani walizo zitunga hao waliojiondoa?

MTANGAZAJI : Walikua wakichangia kwenye Nyimbo za Orchestra yako

FERRE GOLA : Kwani Orchestra yangu inajina gani?

MTANGAZAJI : JET SET

FERRE GOLA : Wala sikwali, Umeshawahi kunisikia wapi nikasema Jina la Orchestra yangu ni JET SET ?

MTANGAZAJI : Sasa naomba uniambie, Orchestra yako inaitwaje ?

FERRE GOLA : Inaitwa FERRE GOLA!!!

MTANGAZAJI : FERRE GOLA MUSICA

FERRE GOLA : Tayari umeshaongezea neno Musica ( kacheka )!!!

MTANGAZAJI : Yamaanisha Pindi tunapo ongelea Orchestra yako, Tunakuzungumzia kwanza wewe!!!

FERRE GOLA : Kwani Wewe wafikirije ? Kwajumla, sioni tatizo lolote wakati Wanamuziki wanaamua kujiondoa kwenye Group,hali hii wala si leo ndo imeanza kujitokeza,limeshakua jambo la kawaida!!!

MTANGAZAJI : Kujiondoa kwao wala hakukupi Shida yeyote!!!

FERRE GOLA : Shida yanini sasa ? Tizama kwenye Album ” BOITE NOIRE “, Wengi kati ya Wanamuziki walio changia wapo wala sioni tatizo kabisa. Mimi hua nawapenda Vijana wangu wote, hata kwawale walio ondoka,nilikua pia nawafurahia.

MTANGAZAJI : Unayo yasema hapo si kwania mbaya !!!

FERRE GOLA : Baadhi ya Wanamuziki wote waliopitia kwangu,wamejengeka vizuri kabisa,nimewafua vilivyo,ninao uhakika wanao uwezo wakujitetea vilivyo popote pale wanapo hitajika.

MTANGAZAJI : Lipo Swali nataka lijibiwe kwa uwazi, Imewahi kutokea siku ukaitisha mkutano,ukakaa na Vijana wako na mkayaongelea hasa Matatizo yao khususan yale yanayo ambatana na maswala ya Pesa ?

FERRE GOLA : Bila kujisifu, Mimi niko miongoni mwa wale wachache ambao wanajua kuwatunza vilivyo Wanamuziki. Wote niliwahi kuwanunulia Magari aina ” MERCEDES-BENZ ”

MTANGAZAJI : Kumbe yanayo zungumzwa ni kweli!!!

FERRE GOLA : Wala sikwamba najigamba, Hapana,Kwenye miaka miwili au mitatu iliopita,Vijana wangu wote niliwagea zawadi ya Gari.na wale walioondoka wameondoka pia na MAGARI YAO .

MTANGAZAJI : Ni kweli?

FERRE GOLA : Ndio, Wengi wananijua kwa upande huo, Mimi sio Mtu bahiri. Orchestra yangu ipo sawa, tunajijenga vizuri, Siku za hivi karibuni Mtatuona mimi na Group langu nzima kwenye vipindi vyenu. Kwa sasa tupo kwenye matayarisho ya Album Mpya,Jina litatolewa baadae.

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Upo uvumi uliozagaa kana kwamba Umewaruhusu Vijana wako waweke Nyimbo zao kwenye Album ambayo kwa sasa bado ipo Jikoni.

FERRE GOLA : Mbona swali lako mwenyewe sinalo jibu? hayo wayatoa wapi ?

MTANGAZAJI : Siri yavujishwa na wahusika wenyewe !!!

FERRE GOLA : Yapo mambo mengine hayastahili kutolewa ovyo Inje ya Group, ipo Mikakati ya kisiri ya Orchestra ambayo hutolewa kwa wandishi wa Habari kwa Mda unaohitajika.

MTANGAZAJI : Watu wanakuchulia wewe kama mpinzani wako Mkuu ni FALLY IPUPA, Ikawaje leo hii ukahamishia upinzani wako kwa BOSS wako wa zamani WERRASON ?

FERRE GOLA : Hayo ndo maswali uliyo yatayarisha kwakuniuliza leo?

MTANGAZAJI : Wala simimi, ni Watu wanao hitaji ufafanuzi zaidi kutokana na hayo tunayo yasikia na kuyaona siku hizi.

FERRE GOLA : KINACHO HITAJIKA KUFAHAMIKA HAPA NI KWAMBA ” MIMI SIMTU KABISA WA MALUMBANO ” NA WALA SINA UPINZANI NA MTU YEYOTE ULE .

MTANGAZAJI : Kweli huna Matatizo na Mtu yeyote ?

FERRE GOLA : Ndio ukweli wangu huo,sina tatizo na Mtu.

MTANGAZAJI : Wewe ni Mtu mwenye Kinyongo ?

FERRE GOLA : Hapana!!!

MTANGAZAJI : Unao uhakika kwa hayo majibu yako? huoni kama Watu manyumbani kwao watashindwa kukuelewa?

FERRE GOLA : Sina Kinyongo na Mtu, labda yawezekana,Mimi ni Mwanadamu wa kawaida kama wengine, yaweza ikatokea Mtu kaamka vibaya akawa mwenye kununa, ila jioni kicheko kikamrudilia!!! na ndivyo maisha yalivyo.

MTANGAZAJI : Habari kuhusu Album ” 13ème APOTRE ” ya MOPAO MOKONZI KOFFI OLOMIDE, makubaliano yalikuaje?

FERRE GOLA : Kuna siku nilikua matembezini, Barabarani nikamuona Mzee KOFFI OLOMIDE, kwa heshima nikamfwata na kwenda kumtolea Salaam, kafurahi kuniona ndipo kapendekeza nijumuike naye kwa kuchangia kwenye Album yake. na nikampa ahadi kwamba ntakapokua na Mda ntapitia kwenye Studio ili nipate kuchangia kwenye Album hiyo. NILICHO KIFANYA NIKUTIMIZA KAULI YANGU.

MTANGAZAJI : Watu wanasema KOFFI OLOMIDE yuko nyuma yako,kakusapoti kwa hayo uyatendayo, Kuna Timu imeundwa Mkiwa WEWE FERRE GOLA, FABREGAS, na KOFFI OLOMIDE, huku pande nyingine lipo Group la akina WERRASON,JB MPIANA na FALLY IPUPA !!! hayo umewahi kuyasikia?

FERRE GOLA : Kwanza natoa Samahani sana kwa Wote wanaonisikiliza kwa wakati huu, Kwakweli mimi siyajui nasipo kabisa kwa hayo yote ulioyazungumzia, Wenda kwasababu hua siku hizi mwenye kusafiri sana Inje ya Inchi, taarifa hizo sina. kilichokua cha ukweli ni kwamba ” NIMECHANGIA KWENYE ALBUM YA KOFFI OLOMIDE “. zaidi ya hayo mimi siyajui .

MTANGAZAJI : FERRE GOLA, Wewe ni kijana mwenye sauti ilio nyororo, Mbona hatujakuona sana ukifanya Featuring na WASANII wakigeni ? au Huna Meneja mzuri anaeweza kukutangaza vilivyo?

FERRE GOLA : Willy Swali hilo huo unalipenda sana!!! Mbona natoka kufanya Featuring na KOFFI OLOMIDE LE GRAND MOPAO MOKONZI

MTANGAZAJI : Wasanii wakimataifa kutoka Inchi nyingine

FERRE GOLA : Kila Mtu anayo mikakati yake.

 

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

 

 


KOFFI OLOMIDE KAWACHEZA RUMBA ” TCHATCHO ” RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE DENIS SASSOU NGUESSO NA MKEWE WIMBO ” N’GOULI “

August 18, 2014

 

INGAWA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA WAINGIA DOSARI KATI YA INCHI ZA CONGO BRAZZAVILLE NA CONGO KINSHASA, KWANZA NI KITENDO CHA INCHI YA CONGO BRAZZAVILLE  KUWASAKA NA KUWATIMUA KWA NGUVU WA HAMIAJI HARAMU INCHINI HUMO,AMBAO WENGI WAO NI RAIA KUTOKA CONGO DRC, PILI NI KUTOKANA NA PENDEKEZO LA RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE ” DENIS SASSOU NGUESSO ” LAKUTAKA INCHI YA CONGO DRC IRUDILIE JINA LAKE LA ZAMANI LA ” ZAIRE “. NA PAPO HAPO RAIS WA CONGO KINSHASA ” JOSEPH KABILA ” KAMJIBU KWA KUMDHIHAKI KANA KWAMBA ” INCHI YA CONGO BRAZZAVILLE INGELISTAHILI KUA MMOJA KATI YA MIKOA YA CONGO KINSHASA, NA RAIS DENIS SASSOU NGWESSO ANGETEULIWA MKUU WA MKOA HUO.

LICHA YA MALUMBANO HAYO,KOFFI OLOMIDE, KAALIKWA KAMA MGENI RASMI NA RAIS DENIS SASSOU NGUESSO  KWENYE SIKUKUU YA KUSHEHEREKEA UHURU WA INCHI YA CONGO BRAZZAVILLE, SHEREHE ILIOFANYIKA  KWENYE MJI WA ” SIBITI ” TAREHE 15-08-2014.

WAKATI AKIWA JUKWAANI, KOFFI OLOMIDE KASEMA ” INGAWA YEYE NI RAIA WA INCHI YA ZAIRE, ILA KAJIVUNIA MAENDELEO AMBAYO KAYAONA  INCHINI  CONGO BRAZZAVILLE.

KASEMA KWAKE YEYE RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE, NDIE MZURI WA USO NA UMBO KUWAZIDI MA RAIS WOTE BARANI AFRICA.

KOFFI OLOMIDE KAIMBA WIMBO ” N’GOULI ” UNAO PATIKANA KWENYE ALBUM ” MONDE ARABE “, WIMBO HUO AMBAO NI UTUNZI MAALUM KWA AJILI YA MAMA “ANTOINETTE SASSOU NGUESSO ” YEYE AMBAE WAPINZI WAKE HUMPACHIKA JINA LA ” N’GOULI “, LIKIMAANISHA ” MAMA “.

MAMA ANTOINETTE NA MMEWE RAIS WALISHINDWA KABISA KUJIZUIA, WALISIMAMA NA KWENDA KULISAKATA RUMBA ” TCHATCHO “.HUKU WAKIFWATIWA NA UMATI WAWAALIKWA.

UTAMSIKIA KOFFI OLOMIDE AKIIMBA KWENYE WIMBO HUO  ” MAMAN N’GOULI NA PAPA NGUESSO NZAMBE ABATELA BINO EBELE ” / MAMA NA BABA NGUESSO ,MWENYEZI MUNGU AWAZIDISHIE NYINGI ZAIDI.

 

LUBONJI WA LUBONJI

 


WERRASON NA JB MPIANA WAMPONGEZA PAPA WEMBA KUTOKANA NA NDOA YAKE YA KANISANI

August 18, 2014

 

PAPA WEMBA : Shukrani zangu za dhati zimwendee MAMA huyu ambae si mwengine bali ni MKEWANGU,Yeye kanivumilia katika kipindi cha Miaka 44. Yeye ni Shahidi kabisa wa Uhuni wangu wote niliokua nao katika kipindi chote hicho. Kutokana na hayo yote, Ndipo nikachukua Uamuzi wa kumleta Kanisani,Kanisa lililo nikuza katika Imani yangu ya Ukristo,Nimemleta Mke wangu Ilitupate kuungana wote kwa pamoja katika IMANI. ASANTE SANA MKE WANGU

MAMA AMAZONE : NI KWANGU MIMI KUKUSHUKURU KWA HESHIMA ULIONILETEA!!!

JB MPIANA : PAPA WEMBA MZEE EKUMANYI LE KURU YAKA, ambae kwa siku hizi kajulikana zaidi kwa jina la ” MAÎTRE D’ÉCOLE “, WEWE NI MKUZAJI WA VIPAJI, KAMA LEO HII BAADHI YA WATU HUJITOKEZA NA KUA MA STAR, NIKUTOKANA NA MCHANGO WAKO ULIO MKUBWA.

Kwakweli sisi Wadogo zako, Sisi Wanao,tunayo furaha sana kuona Umetuletea Heshima. Waheshimisha kabisa Kazi ya Muziki Inchini Congo.Waondoa Doa kubwa machoni mwa watu ambao wengi kati yao hufikiria kwamba kazi ya Muziki niya WAHUNI. Kwakweli kwangu mimi Kitendo cha Wewe kufunga Ndoa,kimeniletea raha sana moyoni mwangu.Wamuheshimisha MAMA mbele ya MWENYEZI MUNGU,Wahitimisha hitaji kubwa ambalo Wanawake wengi hua wakilisubiria maishani mwao. ” KUVAA USHUNGI WA NDOA ” .

Katika Imani yetu ya Kikristo,Mwanmke hufunga Ndoa Mara moja,wala si mara mbili, KITENDO CHENU CHA KUFUNGA NDOA BAADA YA MIAKA 44 YA KUISHI KWA PAMOJA, BASI NI JAMBO MUHIMU KABISA NA SOMO TOSHA KWAKWELI. Ni mangapi ya Shari kama vile ya Raha mlioyapitia? Ila uamuzi wa mwisho ni kufunga Ndoa tena Kanisani. Kunakipindi fulani Mlifanya dhiara kwenda ROMA, na huko Mkakutana na PAPA ambae kawabariki,kwa wakatiule,mlikua bado si Wanandoa, Kwasasa Nyinyi ni Bwana na Bibi Harusi. TUNAWASHUKURU SANA KWA HILO. NAWATAKIA KILA LA KHERI,NAHISI NA SISI PIA TUPO MBIONI KUZIFWATA NYAYO ZENU. ASANTE SANA PAPA WEMBA, HONGERA SANA KWAKO MAMA AMAZONE MUKARAME.

WERRASON : Nashukuru sana kwakunipa kauli, Kwakweli Tukio la PAPA WEMBA kufunga Ndoa,limefwatwa na Wengi Uliwenguni kote. Kilicho kizuri zaidi nikuona twaheshimika sisi WANAMUZIKI.

KWETU SISI, YEYE NI BABA,KAKA,TAYARI YUKO NA WAJUKUU,PIA ANAO WADOGO WENGI,NA MAMILIONI YA WATU WAPO NYUMA YAKE NA HUA WANAMPENDA.

Kwa siku hizi,Watu walipuuzia sana Tendo hilo muhimu la kufunga Ndoa, wakati hata katika Biblia yapo maandishi yanao tushurutisha tufunge Ndoa. NDOA NIKUMUHESHIMISHA MKEO MBELENI MWA MWENYEZI MUNGU, NA MACHONI MWA BINADAMU.WAONYESHA KWAMBA WEWE NA MKEO NI KITU KIMOJA,MWILI MMOJA.

Nafikiri katika Kipindi kirefu cha Miaka 44,Wamejenga Maisha yao kwa pamoja,Wamezaa watoto, kadhalika wametokea kuwapata Wajukuu wengi. KWAKWELI FURAHA ILIOJE KUONA WAMEHITIMISHA AGANO LA NDOA.

Kitendo hicho ni Heshima kubwa kwa sisi Wasanii hasa wanamuziki. MAMA AMAZONE, KATIKA KIPINDI CHOTE HICHO CHA MAISHA YENU NA PAPA WEMBA, YAPO MAMBO MENGI YALIYO JITOKEZA,YA HUZUNI KAMA VILE YA FURAHA, NTAKUOMBA UYASAHAU KABISA YALE MABAYA,NA UYAPEKIPAUMBELE KAULI MBILI MUHIMU ZAIDI NAZO NI : ( SAMAHANI NA ASANTE ).

Binafsi niliudhuria Sherehe ya Ndoa yenu nikiongozana na MAMA PASTEUR (SYLVIE MAMPATA ) NILIPATWA NA FURAHA TELE MOYONI MWANGU. Watu wengi walijitokeza kuwa mashahidi wa tukio hilo,Maandalizi yalikua mazuri sana, NIKASEMA MOYONI KWAMBA : KITENDO HICHI NDO SALIO LA MWISHO LA PAPA WEMBA ,HATIMAE KAFUNGA NDOA.

KWAKWELI PAPA WEMBA, SISI WADOGO ZAKO HATUNA BUDI KUZIFWATA NYAYO ZAKO,KWETU SISI WEWE NI MFANO, NI KWAMAANA HIYO HUA NAKUITA ” KOCHA “.

Kitendo chenu cha Kufunga Ndoa, ni somo kubwa kwa wengi, yaani Watu Mnakaa kimapenzi kwa miaka kadhaa,Mnazoeana,Ni jambo la kawaida Kwa matatizo kujitokeza wakati Watu mnaishi kwa pamoja, ila mnakabiliana nayo,mwisho wa mwisho mkaja kuchukua uamuzi wa kufunga ndoa, RAHA ILIOJE ? na Baada ya Ndoa nikipi kingine cha muhimu zaidi kilicho salia maishani mwa Mwanadamu? hakuna!!!

MZEE BOKOUL ( PAPA WEMBA ) Ni Mtu mwenye Ushahuri mwema. KWAKO WEWE MAMA AMAZONE, NAJIONA MTU MWENYE RAHA SANA, WEWE NI DADA YANGU. ASANTE SANA

LUBONJI WA LUBONJI


TUONGELEE WENGE MUSICA KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA SEHEMU YA SABA

August 14, 2014

TUNAENDELEA NA SIMULIZI YA MPIGA GITA WA WENGE MUSICA ORIGINAL, BURKINA FASO MBOKA LIYA (SEHEMU YA SABA ) UKITAKA KUSOMA SEHEMU ZA MWANZONI,ZIPO KWENYE FACEBOOK, UKURASA WA ( MUZIKI NA LUBONJI ).

UKITIZAMA VIDEO, BASI ANZIA KWENYE 01:08:30 HADI 01:18:00

MTANGAZAJI : Swali langu nilakutaka kujua nikitu gani kilicho wafanya BLAISE BULA na ALAIN PRINCE BAKABA  wajiondoe kwenye Group WENGE MUSICA BCBG?

BURKINA FASO MBOKA LIYA : Sikiliza, BLAISE BULA kutokana na Tabia yake, si Msemaji sana? yaani ni mpole, Mara ya kwanza nimemuona kakasirika na nikamuelewa,ni wakati bado tupo ” WENGE MUSICA ORIGINAL “,Kipindi ambacho mzozo wapamba moto,hali ilikua Mbaya sana.Kiliitishwa kikao kwenye Hotel INTERCONTINENTAL JIJINI KINSHASA, ili tupate kuyajadili matatizo yetu. BLAISE BULA, kapandwa na hasira hadi kidogo amguse mwilini DIDIER MASELA. Kwa bahati nzuri akina ALAIN PRINCE MAKABA na Wengine wakaingilia kati. Kutokana na Fujo kuzidi kua nyingi, basi Askari wakaja kututimua wote Nje. BLAISE BULA kamshutumu DIDIER MASELA kwamba simchapa kazi, bali ni Mtu mwenye kupenda hela kupindukia.

Uamuzi wa BLAISE BULA kujiondoa kwenye Group ” WENGE MUSICA BCBG “, ulisababishwa na mawasiliano kuwa mabaya sana kati yake na JB MPIANA. BLAISE BULA, kwa mara kadhaa kamuomba JB MPIANA wakae chini ili wapate kuyamaliza tofauti iliokua ikijitokeza kati yao. JB MPIANA akawa hapendelei kabisa mazungumzo yawepo, kadhalika kwa upande wa ALAIN PRINCE MAKABA, JB MPIANA kawa anamkwepa kila siku wakati mwenzie kamuomba wakae chini na kuyatatua tofauti ilio jitokeza kati yao. Mimi mwenyewe hapa, JB MPIANA kanifukuza kama Mbwa.

MTANGAZAJI : Kakutimua Mkiwa  wapi? wakati bado mpo Ulaya au JIJINI KINSHASA !!!

BURKINA FASO : Hebu nenda kawaulize Vijana wa TOTTENHAM,watakuongelea mkasa ulionikuta kwa kirefu. Walijua Jina ambalo kanipachika JB MPIANA!!!

MTANGAZAJI : Jina gani hilo?

BURKINA FASO : MUNDUNDU

MTANGAZAJI : MUNDUNDU ikiwa na maana gani?

BURKINA FASO : Akimaanisha Mwenyeji wa Mkoa wa BANDUNDU ( KWAO WERRASON ). Kwa Mtizamo wake, Wote ambao wanatokea kwenye Mkoa huo,basi ni maadui zake.

MTANGAZAJI : Ikafikia wakati BLAISE BULA kaamua kujiondoa

BURKINA FASO : ( Kacheka sana ) Sioni umuhimu wa hilo swali lako

MTANGAZAJI : Swali langu linamaana saana, Watu wengi walinipigia simu kwa madhumuni yakutaka kujua hali halisi ya mambo ilivyokua ikijitokeza kwenye Group ” WENGE MUSICA “.Tunaomba ufafanuzi zaidi, Wakati BLAISE BULA kajiondoa, Je ALAIN PRINCE MAKABA alikua wapi?

BURKINA FASO : Kuna kipindi fulani,tulipata tenda ya kusafiri na kwenda kufanya SHOO JIJINI PARIS,Kwenye Ukumbi wa ZENITH,Dhiara hiyo ikaja kujitokeza kua ndefu zaidi kupindukia,kwasababu, tulilazimika kwenda hadi CANADA kufanya SHOO,na tukafanya SHOO nyingine nyingi tuu kwenye baadhi ya Inchi za AFRICA, Kabla ya uamuzi kuchukuliwa wa sisi wote kurudi JIJINI KINSHASA.

Ndipo ALAIN PRINCE MAKABA, kaamua kubaki zake ULAYA ( BRUSSELS ),Huku Group nzima likarudi KINSHASA. Tukiwa tayari KINSHASA, BLAISE BULA kamuomba JB MPIANA wakae chini Wazungumze na kuyasawazisha tofauti zao. JB MPIANA kawa mwenye kuonyesha dalili zote za Mtu asiekubali muafaka wowote upatikane, kawa anamkwepa mwenzie. HATAKI TENA USHIRIKIANO NA BLAISE BULA, ” NIA YAKE KUU NI KWAMBA BLAISE AONDOKE KWENYE GROUP ILI ABAKI MWENYEWE KIONGOZI MKUU ” Nafikiri unanielewa !!!

MTANGAZAJI : Ndio, nimekupata vizuri

BURKINA FASO : Yaani Wewe wajitahidi suluhisho lipatikane, Huku Mwenzio hana haja nawewe tena. Kwa hapa ntaongezea mfano wangu Binafsi. Kutokana na Matatizo ambayo nilikua nakabiliana nayo, Nilijitahidi kwa nguvu zangu zote kumtafuta JB MPIANA Ili tupate kuzungumza bila mafaanikio, kila siku akawa ananikwepa, Hadi ilivyofikia siku Mmoja nikachukua uamuzi wakumfwata Nyumbani kwake. Gari nililokua nikitembelea,lilikua Bovu sana,limechakaa vibaya sana, halikua hata na siti.

MTANGAZAJI : Gari kama hilo, ikawaje ukawa unazunguuka nalo?

BURKINA FASO : Mimi nikama Askari, kwa wakati huo,nilikua wala sina uamuzi mwengine, Laa sivyo, ingenijia vigumu kweli kuchakarika katika kazi zangu. Nikaendelea kulitumia Gari langu bovu, na nikalipachika jina ( POURQUOI OZONGELI SOUVERAIN !!! ). ikimaanisha ( KWANINI WAKUBALI KUMFANYIA KAZI SOUVERAIN !!! ” JB MPIANA “.

Tatizo kubwa kwa ma Boss wetu wa Muziki Inchini CONGO, Ubinafsi wazidi kipimo, Kwanza ni wao, wengine hapana!!! Kwakweli ninayo hasira kali sana na jamaa hawa, Mimi nilifanya kazi kwa kujituma, nilikua nafanya kazi kwa bidii na moyo wangu wote,kwa faida ya wajinga hao!!!

MTANGAZAJI : Mbona watumia matusi? unawaita wajinga !!!

BURKINA FASO : Sioni tusi nilitumialo kwa hapa, Mjinga ni Mtu asie elewa kitu. Mwenyewe hapa kama waona nashindwa kuelewa,basi rukhsa kuitwa Mjinga.

MTANGAZAJI : Naona waongea kwa Jazba BURKINA FASO, Tafadhali, Ondoa hasira ili upate kujieleza vizuri na Watu wapate kukuelewa.

BURKINA FASO : Mimi ni Mtu mzima sasa, BABA wa Familia, ninao watoto watatu,Wakiume mmoja kafwatiwa na mapacha wawili. Kwakweli Mimi sikua Mtu wakuja kuanzia Upya Maisha yangu ULAYA, wakati nilikua tayari nimeanza kujijenga vizuri.Nilikua na mipangilio mingi sana,hadi nikaanza mikakati ya kufunga Ndoa. Roho mbaya na Ubinafsi wa hao Jamaa vyafanya Mtu karudi Nyuma kabisa, na mipangilio yote Uenda na maji.

Watumishi wa Shetani hao, Walaji, Wanyonyaji, kutokana na Ubinafsi, na Dhulma yao, Sisi wengine tunaharibikiwa na Maisha.

Kweli Nakubali Mimi pia ninamakosa yangu, sipotena kwenye Group lake,sasa tizama alivyo fanyiwa Kijana CHAI NGENGE,kwani kafanya kosa Gani? kwakua naye pia ni Mwenyeji wa Mkoa wa BANDUNDU. ( Kacheka ).

MTANGAZAJI : Haya matatizo yote unayo yazungumzia leo hii, kwani wakati Ulivyokua kwenye Group,mbona hujamuongelea BOSS wako JB MPIANA? kuyatoa yote yaliko Moyoni mwako?

BURKINA FASO : Utaongeaje na Mtu wakati mwenyewe hataki kabisa? Pindi unapotaka mazungumzo,yeye hukukwepa. Jamaa hao wanaishi maisha ya kinafiki,machoni mwa Watu wa Inje,hujionyesha kama wao ni Watu wema,kumbe maadui wakubwa!!!

MTANGAZAJI : Sasa kwa hawa Wanamuziki ambao kwa wakati huu wako na JB MPIANA, kwani bado hawajagundua ubaya wake? au Ndo kesha badirika !!!

BURKINA FASO : Inategemea, Unaona Mtu kama mimi na JB MPIANA, tunalingana kiumri,Tofauti kabisa na hawa Vijana waleo walio zaliwa kwenye miaka ya 90, Sisi tumezaliwa kwenye miaka ya 60. tunayo Mawazo na Mtazamo ulio tofauti kabisa na hawa Vijana wa leo. Wakati Mimi nasuka mikakati jinsi gani niyaboreshe maisha ya baadae ya wanangu,Kijana wa leo, bado mafikira yake ipo kwenye Kiatu, ” NIVIPI ATAKAVYO FAANIKIWA KUNUNUA BASKET MPYA “. Watu kama hao ndo JB MPIANA na moyo wake wa kishetani hupendelea kufanya nao kazi. Watu wasiokuwa na malengo yeyote, hawana Mke wala Mtoto.

MTANGAZAJI : Tuambie, Ninini kilichotokea hadi JB MPIANA kachukua Uamuzi wakukuachisha kazi kwenye Group ” WENGE BCBG “.

BURKINA FASO : Sikiliza, Mambo ya ndani kati ya JB MPIANA na WERRASON,ntashindwa kabisa kuyaongelea hapa,kwakua yanawahusu Wenyewe. Sababu iliopelekea Mimi na JB MPIANA tukorofishane ni mmoja tuu ” NILIENDA KUFANYA KAZI NA WERRASON,WAKATI ALIPO NIHITAJI KUMSAIDIA KWENYE ALBUM KIBWISA MPIMPA “.

MTANGAZAJI : Wakati wewe bado upo mwanamemba wa WENGE BCBG

BURKINA FASO : Ndio, Basi naomba utulie nipate kujieleza… ITAENDELEA…

 

 

 


FALLY IPUPA KAWASHA MOTO JUKWAANI INCHINI MAREKANI

August 13, 2014

 

FALLY IPUPA,Kazaliwa JIJINI KINSHASA TAREHE 14-12-1977

Kama ilivyo kwa baadhi ya wengi wa vijana wa JIJI LA KINSHASA, FALLY IPUPA kaanza Muziki kwenye Kwaya ya Kanisa, Kisha kajiunga na vikundi Mbalimbali vya Mtaani. Kundi la mwisho alikotokea kabla ya kujiunga na Group QUARTIER LATIN INTERNATIONAL YA KOFFI OLOMIDE Mwaka 1999, lajulikana kwa Jina la  Group ” TALENTS LATENTS ”

KESHATOA ALBUMS 3

1. DROIT CHEMIN IMETOLEWA MWAKA 2006 .
ilisambazwa na LABEL ” OBOUO MUSIC ” ya DAVID MONSOH. ILIPEWA TUZO LA GOLD DISC. JIJINI PARIS

Kwenye Album DROIT CHEMIN kapata ushirikiano wa Wasanii wenye uwezo mkubwa kabisa kimuziki, wakiwemo :

 • Montana Kamenga
 • Modogo Abarambwa
 • Luciana Demingongo
 • Dédé Djasco
 • Tripason
 • Serge Mabiala
 • Jimmy Vondo-Vele “Saxo-Tenor”
 • Barbara Kanam
 • Ben J

Upande wa Gita, Kapata Msaada wa Wataalamu wa fani hiyo, ntawataja :

 • Felly Tyson
 • Fofo Le Collégien
 • Ramazani Fulutini
 • Beniko Popolipo
 • Maika Munan
 • Binda Bass
 • Michel Bass

KWENYE DRUM WALIKUWEPO WAKALI ZAIDI :

 • Titina Mbwinga
 • Champion Djikapela
 • Djoudjou Music

MA PERCUSSIONNISTS WALIKUWA :

 • Jimmy Mbonda
 • JM Bolangasa

REPA AKIWA KIJANA APOCALYPSE CENDRE AKISHIRIKIANA NA FALLY IPUPA MWENYEWE.

*** UNAPO ISIKILIZA ALBUM HII ” DROIT CHEMIN ” UTAGUNDUA UTAMU WAKE, KUTOKANA NA MCHANGANYIKO WA NGOMA ZA KIAINA YAKE. HUWEZI KUCHOKA KABISA KUCHEZA UNAPO SIKILIZA VIBAO KAMA :

1. DROIT CHEMIN2. LIPUTA3. SOPEKA ( Featuring na BEN J )

4. ASSOCIE

5. MABELE

6. ATTENTE

7. 100 % LOVE ( Featuring na BARBARA KANAM )

8. ORGASY

9. BAKANDJA

10. NAUFRA – KETCH

11. PRINCE DE SOUTHFORK ( Featuring na MODOGO ABARAMBWA )

12. KIDIAMFUKA

*** KUTOKANA NA ALBUM ” DROIT CHEMIN “, FALLY IPUPA KAPEWA TUZO NYINGI KADHAA :
.MWAKA 2006, KAPEWA TUZO LA MWANAMUZIKI BORA WA KIUME KWENYE MUSIC AFRO CARIBBEAN,
2006, KAPEWA TUZO MBILI KWENYE BLACK MUSIC IKIWEMO LA MWANAMUZIKI BORA WA MWAKA WAKIUME.2006,KAPEWA TUZO LA CLIP BORA ” DROIT CHEMIN ” INCHINI BENIN.2006, KAPEWA TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA INCHINI COTE D’IVOIRE.
.MWAKA 2007, KAPEWA TUZO CÉSAIRE MSANII BORA WA AFRICA (PARIS).MWAKA 2008, KAPEWA TUZO LA KORA ,MSANII BORA WA AFRICA YA KATI

 

2. ARSENAL DE BELLES MÉLODIES NDIO ALBUM YA PILI YA MSANII FALLY IPUPA,ILIYO TOLEWA MWAKA 2009, CHINI YA USIMAMIZI WA LABEL ” OBOUO MUSIC ” YA DAVID MONSOH ,HADI KWA WAKATI HUU, ALBUM HIYO TAYARI IMESHA CHUKUA TOZO LA PLATINIUM DISC.

Ni Album ambayo Mnapatikana ndaniemo Nyimbo 16, zikigawanywa kwenye CD 2.

Kwenye CD ya kwanza Mnapatikana Nyimbo hizi :

1. Bicarbonate
2. Cadenas
3. Tshô
4. Travelling Love
5. Une Minute
6. Délibération
7. Chaise Electrique (featuring Olivia)
8. Nyokalessé
9. Mon Amour
10. Catafalque
11. La Jungle

CD ya Pili zipo hizi :

1.Arsenal Des Belles mélodies,2. 5ème Race, 3.Orphelin Amoureux, 4.Lourdes, 5.Sexy Dance ( Featuring Krys ).
*** ALBUM ARSENAL DES BELLES MÉLODIES ILIZIDI KUMUONGEZEA FALLY IPUPA SIFA NYINGI,NA KUMFANYA APOKEE PIA TUZO MBALIMBALI,ZIKIWEMO :TUZO TATU kwenye NDULE AWARDS, MWAKA 2010.( ALBUM BORA, CLIP BORA “WIMBO CHAISE ÉLECTRIQUE”, NA WIMBO ” DELIBERATION ” KUTEULIWA KAMA WIMBO BORA ). MWAKA HUO 2010,KAPEWA TUZO LA ” GOLD MICRO ” NA JIJI LA BRUSSELS,KAMA MSANII BORA WA DIASPORA YA CONGO.
KAPOKEA PIA TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA YA KATI KWENYE SOUNDCITY VIDEO AWARDS. KACHUKUA TENA TUZO MBILI YA “MAMA” KWENYE MTV AFRICA (MSANII BORA KUTOKA KWENYE JUMUIYA YA INCHI ZINAZO TUMIA LUGHA YA KIFARANSA, NA WIMBO “SEXY DANCE”UKATEULIWA CLIP BORA.
MWAKA 2011,KACHUKUA TUZO INNE KWENYE MOAMAS AWARDS JIJINI “NEW YORK” IKIWEMO TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA. MWAKA HUO 2011,KAPEWA TUZO NYINGINE MBILI KWENYE OKAPI AWARDS ( MSANII BORA WA KIUME,NA “BICARBONATE” WIMBO BORA ).

KWENYE ALBUM ARSENAL DE BELLES MÉLODIES, FALLY IPUPA KAPATA USHIRIKIANO WA WATU MAARUFU KADHAA WAKIWEMO :

 • Olivia Longott (Mwimbaji)
 • Krys (Mwimbaji)
 • Maika Munan (GITA)
 • Ramazani Fulutini (GITA)
 • Fofo Le Collégien (GITA)
 • Rigo Star (GITA)
 • Pathy Bass (Bass)
 • Michel Bass (Bass)
 • Champion Djikapela (DRUM)
 • Brice Malonga (SYNTHESIZER)

3.ALBUM YAKE YA TATU ” POWER KOSA LEKA ”

Kwenye Album hii, FALLY IPUPA kawatumia zaidi vijana wa ORCHESTRA YAKE ” F Victimes “.

Album ” POWER KOSA LEKA ” Iliwekwa sokoni tarehe 04-04-2013,Ilipokelewa vizuri sana na Mashabiki wake, kadhalika pia na wapenzi wa Muziki. zaidi ya CD 30.000 zilinunuliwa katika kipindi cha siku 30.

FALLY IPUPA kawa Mtu si wakutambulishwa tena, kachukua uamuzi wa kuachana na Label “OBOUO” ya DAVID MONSOH,yule ambae kamtoa gizani, na kujiunga na LABEL kubwa zaidi Duniani ya ” UNIVERSEL  A-Z “.

” KOSA LEKA ” INAZO NYIMBO 22, ZILIZO WEKWA KWENYE CD 2.

CD 1 .

1. Hustler is Back
2. Ndoki
3. Bruce
4. Émeraude
5. Anissa
6. Nourrisson
7. Power “Kosa Leka”
8. Cri d’Alarme
9. Mikitisa
10. Amour Assassin
11. Service
12. Sweet Life “La Vie Est Belle”

CD 2 .

1. Terminator
2. Double Clic
3. Pene Pene
4. Likukuma
5. Sony
6. Oxygène
7. We Are The World
8. 1000% Mawa
9. Mokek’s
10. Skype

KUTOKANA NA ALBUM HII, FALLY IPUPA KAPEWA TUZO KADHAA :

.Mwaka 2013, KAPEWA TUZO LA MSANII BORA WA AFRICA,KWENYE TRACE URBAN MUSIC AWARDS.

Kwenye mwaka huo, 2013,KAPEWA TENA TUZO MBILI KWENYE NDULE AWARDS, ( ALBUM BORA ” POWER KOSA LEKA ” NA VIDEO BORA WIMBO ” SERVICE ”

Mwezi wa Saba Mwaka Huu 2014, KACHUKUA Tuzo la AFRIMMA kama Mwanamuziki Bora wa Kiume Africa ya kati.Jijini DALLAS.

FALLY IPUPA,kashiriki kwenye MTV ALL STARS, akiambatana na Wanamuziki wenye Majina Makubwa, akina :

Snoop Dogg ,2Face Idibia, Flavour na wengineo…

Mwezi huu Tarehe 04 hadi 06, FALLY IPUPA,kawa mmoja wa WASANII walio pokea Mualiko kutoka kwa BARACK OBAMA, ili apate fursa ya kushiriki kwenye kikao cha Ushirikiano na Maendeleo kati ya Marekani na Inchi za Africa.

HIKI NDICHO KIKOSI CHA WANAMUZIKI WA GROUP LAKE,KILICHO SHIRIKI KWENYE ALBUM “POWER KOSA LEKA “:

A) TIMU YA WAIMBAJI :

 • Atele Kunianga
 • Tony Buangi
 • Junior Mutukua
 • Pitchen Kalombo
 • Masudi Dady
 • Mopiwi Cousto Lufuluabo
 • Michel Lufua
 • Marc Vobi Iseboya
 • Youssouf Mabiala
 • Ambassy Bourgeois
 • Nathan Munkala
 • Maiko Mbula
 • Batuseka Ping-Pong
 • Fally Ipupa

B) MA REPPA WALIKUA HAWA :

 • Identité Selenga
 • Gecamines Kasangidi
 • Guelord Boussol
 • Doubai Mutamba
 • Kabuya Mulamba
 • Tramontina Ekofo
 • Baby Tangofor
 • Yannick Luzolo
 • Fally Ipupa

C) WAPIGA GITA :

 • Alvarito Nymi
 • Petit Kurukuru
 • Serge Liaki
 • Felly Tyson
 • Nsimba Pezo-Zagalo
 • Willy Zola
 • Tumba Bass
 • Wallo Liyeye Bass

DRUMS :

 • Arnaud Kayembe
 • Franck Kapaya
 • Cambodge Motul

PERCUSSIONISTS :

 • Shoumen Lunguila
 • Mata Suangolo.

SYNTHESIZER :

 • Billy Muyoyo
 • Mijo Synthé

MSANII FALLY IPUPA KESHA TOA PIA SINGLE TATU :

 • Naza Cot’Oyo : Ilitolewa Mwaka 2008 (Spot ya Matangazo kwa ajili ya Mdhamini wake Kiwanda cha Bia Skol BraCongo)
 • French Kiss : (Single iliyo tolewa Mwaka 2011)
 • Original (Single Iliotolewa Mwezi wa Inne Mwaka 2014), FALLY IPUPA kapata sifa nyingi sana kutokana na Single ” ORIGINAL ” Wimbo ambao unawika sana kwenye Ulimwengu wa Muziki, Kwenye Wimbo huu FALLY IPUKA Kasema yeye ni MuAfrica na kakipa kipaumbele Utamaduni wa KIAFRICA. KATIKA KIPINDI KIFUPI CHA MIEZI MITATU,WIMBO HUO UMESHATIZAMWA KWENYE YOUTUBE ZAIDI YA MARA 1000.000.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 


MPYA HIYO YA EXTRA MUSICA ( ROGA ROGA ) WIMBO Fièrement Congolais

August 10, 2014

 

MALIZIA WEEKEND YAKO NA EXTRA MUSICA, WIMBO Fièrement  Congolais

WIMBO MAALUM KWAAJILI YA MDHAMINI WAKE AMBAE NI KAMPUNI YA SIMU ” AZUR ”

LUBONJI WA LUBONJI


HATIMAYE PAPA WEMBA KAFUNGA NDOA NA MAMA “AMAZONE “

August 10, 2014

WAHENGA WANASEMA ” KAWIA UFIKE ”

BAADA YA MIAKA 44 YA MAISHA YA KAWAIDA KWA PAMOJA NA KWA UAMINIFU, MWANAMUZIKI MKONGWE INCHINI CONGO JULES PRESLEY SHUNGU ( PAPA WEMBA ),JANA TAREHE 09-08-2014 KAFUNGA NDOA YA KIDINI NA MKEWE MARIE-ROSE LUZOLO,MAARUFU KWA JINA LA ” AMAZONE ” KWENYE KANISA KATOLIKI ” SAINT JOSEPH ” JIJINI KINSHASA.

WANANDOA HAO WANATARAJIA KUSHEHEREKEA HARUSI YAO KWA MDA WA SIKU TATU, YAANI JANA TAREHE 09, LEO TAREHE 10.SIKU HIZO MBILI, SHEREHE NI KWA AJILI YA WATU MAALUM ( WANANDUGU NA MARAFIKI ).

TAREHE 12 -08-2014 LITAANDALIWA TAMASHA KUBWA KUHUSIANA NA SHEREHE YA HARUSI  HIYO, NA WATU WOTE WANA KARIBISHWA, KHUSUSAN KWA WALE WAPENZI WA RUMBA NA MZEE FULA NGENGE.

KUTOKANA NA TAARIFA ZILIZO TOLEWA NA  MR  JEAN – FELIX BEJE BESALA,AMBAE NDIE MKURUGENZI WA GROUP VIVA LA MUSICA,WATU WENGI MAARUFU KUTOKEA SEHEMU MBALIMBALI, ( AFRICA,ULAYA NA MAREKANI ) WAPO TAYARI JIJINI KINSHASA KWA NIA YAKUA MASHAHIDI WA TUKIO HILO MUHIMU.

MUALIKO UMETOLEWA PIA KWA BAADHI YA WASANII MBALIMBALI WA AFRICA ILI WAJE KUHUDHURIA NA KUFANYA SHOO KADHAA MBELE YA WANANDOA. VIKIWEMO VIKUNDI ” BANA POTO POTO “, ” MATITI MABE “, ” EXTRA MUSICA ” …

WAKIWA TAYARI WAMESHA ZAA WATOTO SITA,PAPA WEMBA NA AMAZONE WALIFUNGA KWA MARA YA KWANZA NDOA YAO YA ASILI KWENYE MIAKA 1970.

SWALI LAKUTAKA KUJUA KWANINI KAAMUA KUFUNGA NDOA YA KANISANI BAADA YA TAKRIBAN MIAKA 40 KUPITA? JIBU LA PAPA KURU YAKA NI KWAMBA : ( MIMI NI MUUMINI WA KANISA KATOLIKI,NAPENDELEA NITAMBULIWE HIVYO NA DHEHEBU HILO ). TAYARI KWENYE MIAKA KADHAA ILIOPITA TULIPATA FURSA YA KUBARIKIWA NA PAPA WA ROMA BENEDICT XVI.

YAANI TUNAHITIMISHA SAKTAMENTI YA NDOA KAMA ILIVYO PENDEKEZWA NA NENO LA MUNGU.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 


KOFFI OLOMIDE KASEMA BOSSI WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO NI YEYE

August 10, 2014

HUU NI UJUMBE WA KOFFI OLOMIDE

 

SALAMU ZANGU ZIWAFIKIE POPOTE MLIPO, NI MIMI KOFFI OLOMIDE QUADRA KORAMAN.

WAPO WATU WALIO NIJIA NA KUNITAARIFU KWAMBA,IPO NJAMA MBAYA INAYOUNDWA KWA AJILI YA KUNIDHURU.

WATU MNAPO KOSA LAKUZUNGUMZA WAKATI MKIALIKWA KWENYE TV, BASI JINA LA KOFFI OLOMIDE HALIONDOKI MIDOMONI MWENU.ETI KOFFI NA HILI,KOFFI NA LILE !!! ( KACHEKA SANA ).

BASI MNACHOTAKIWA KUFAHAMU NI KWAMBA, TAJIRI KIONGOZI WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO NI MIMI.HAYO NINAYO YATAMKA,WALA SI KOSA LANGU,MSINILAUMU KWA HILO,ANAEPASWA KULAUMIWA NI BOB MUNDABI,AMBAE KWA SASA NI MAREHEMU,NDIE ALIE TANGAZA RASMI KUA KOFFI OLOMIDE NDIE LEADER WA WANAMUZIKI WOTE WA CONGO.

ASIE KUBALIANA NA MANENO HAYO, BASI RUKHSA KWAKE AENDE AKAMUULIZE BOB MUNDABI.MIMI SIKO TENA HUKO.

WAPO BAADHI YA WATU AMBAO WANAJIDAI KAMA WAO NI MA LEADER,NA UTAKAPO CHUNGUZA KIUNDANI, UTAGUNDUA KWAMBA HAWAJAWAHI KUTUNGA HATA WIMBO MMOJA,WALA KULETA DANSI MPYA YEYOTE. KAZI YAO KUU NIKUNILETEA KHASHFA ILI WASIKIE NATAJA MAJINA YAO, SIWEZI KUJISHUSHIA HADJI KWAKUWARIDHISHA WAO HATA KIDOGO.

KWA SIKU YA LEO, NIPO KWENYE MAANDALIZI YA ALBUM 13 ème APÔTRE, NA WALA SINA MDA WA MALUMBANO.

MIMI NI KOFFI,FANYENI MTAKAVYO, WALA HAMTONIFIKIA. KWANZA YUPO YULE MMOJA AMBAE KAZI YA MUZIKI IMEMSHINDA KABISA,KESHA IKUMBATIA FANI YA MAVAZI. KAWA MWEUPE KAMANINI, HADI WATU HUFIKIA KUMCHANGANYA WAKIFIKIRIA KAMA YEYE NI CHOTARA,KUMBE SIVYO!!!

KATIKA DHIARA YANGU YA HIVI KARIBUNI INCHINI ANGOLA,WATU WAHUKO WALINIPACHIKA JINA LA ” PATRAO ” IKIMAANISHA ” BOSS “.FURAHA YANGU ITAKUAJE SIKU MOJA ITOKEE MOJA WA WANAMUZIKI WA CONGO ASIFIWE KAMA MIMI.

KWAKWELI MIMI SIELEWI KABISA, MTU KASHINDWA KABISA KAZI YA MUZIKI,KAZI ALIYONAYO KWA SASA NI MAJUNGU.KAMCHUKIA JAMAA KWAKUA KAMCHUKULIA MKE.JAMANI MIMI SIPO HUKO KABISA.

NIACHENI NICHAPE KAZI ZANGU,NIPENDE USINIPENDE,HUO NI UAMUZI WAKO. UMESHINDWA KABISA NA KAZI,UNAKUA KWENYE MITINDO YA MAVAZI.

UONGO HAUNA FAIDA,BALI UKWELI WAZAA MATUNDA MEMA.

WEEKEND NJEMA KWA WOTE.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 


KWA MTAZAMO WANGU CHIKITO KAJIONDOA KWA FERRE GOLA

August 8, 2014

Ingawa kashindwa kutamka kwa uwazi kana kwamba Kajiondoa kwenye Group ” JET SET ” ya FERRE GOLA, Dalili zaonyesha uwezokano mkubwa kwa CHIKITO kutaka kujitegemea mwenyewe.

Kutokana na Mahojiano kati yake na Mtangazaji AICHA OKOKO, CHIKITO kasema kwa wakati huu,yeye hutizama kwanza Maisha yake ya hapo Baadae. Kwa mtazamo wake,hajaona mafaanikio kamili kwa kipindi cha miaka 9 aliokaa akiwa na FERRE GOLA.

Kutokana na sababu hiyo, CHIKITO kachukua Uamuzi wakuingia Studio akiwa kwenye matayarisho ya Album ” BOMBE HIROSHIMA “itakayo tolewa mwishoni mwa mwaka huu.

Alipo ulizwa na Mtangazaji AICHA OKOKO swali lakutaka kujua kana kwamba Kajiondoa rasmi kwenye Group ” JET SET LES GAULOIS ”  inayo ongozwa na FERRE GOLA, CHIKITO kashindwa kujibu kiufasaha, katoa majibu ambayo hayaendani kabisa na Swali kwakusema ” WANACHO KISUBIRIA WATU KWA SASA NI ALBUM BOMBE ATOMIQUE “. Album ambayo kutokana na maelezo yake itakua bora zaidi na itapokelewa vizuri na Mashabiki wake.

CHIKITO, katoa Mfano wa Kijana ambae bado yuko Nyumbani kwao akiishi na Mama yake Mzazi,Pindi anapo gundua Mambo hayaendi vizuri kwa Hapo Nyumbani,ni wajibu wake kutaka kujitegemea hadi kufikia kuchukua Uamuzi wakuondoka Nyumbani kwao na kuhamia sehemu nyingine.

CHIKITO kaendelea kusema kua,Mtoto Mmoja anaweza kuondoka Nyumbani na kuyaanza maisha yake ya Pekee,hilo linaeleweka, Sasa endapo Watoto watatu huchukua Uamuzi kama huo tena kwa wakati mmoja, sasa hapo ninani atakae laumiwa? Mzazi au Watoto.

Mtangazaji AICHA OKOKO wala hajamuachia CHIKITO kaendelea kumbana na maswali, Kamrudisha kwanza kwenye Historia yake mwenyewe kwa kusema : ( CHIKITO, WEWE NI MTU ULIE LELEWA NA FERRE GOLA,KAKULETA KWENYE GROUP LAKE UKIWA BADO MDOGO, WOTE TUMESHUHUDIA HILO,LEO HII KWELI WAWEZA KUMSALITI FERRE GOLA ?).

CHIKITO kamjibu kwakusema : Kadri Umri unavyo zidi kusonga mbele, Ndipo pia Mabadiriko makubwa hujitokeza maishani mwa Mwanaadamu. Ndio, Nakubali kweli Nimeanza Muziki nikiwa Mdogo, Ila kwa wakati huu Mimi sasa ni Mtu Mzima, na siko radhi tena kudangwanywa tena kwa kupewa PIPI.

Kwa sasa Mimi CHIKITO nimesha elewa Mambo ya ulimwengu huu jinsi yalivyo, Wakati sasa wawadia kwa mimi kuonyesha Kipaji changu na Uwezo nilionao, Kwangu mimi Muziki upo kwenye Damu.

AICHA OKOKO kaendelea kumshushia CHIKITO, kamwambia Aibu ilioje kwako wewe kujiondoa kwa FERRE GOLA, bila hata kumtaarifu, ukachukua uamuzi wa kusafiri kutoka JIJINI KINSHASA na kwenda INCHINI ANGOLA kimya kimya,wala hujachukua fursa ya kuomba hata Hati yako ya kusafiria.

CHIKITO kamjibu kwa kusema : ” MWANA MAYELE AYEBAKA KO PRÉPARER LOBI NAYE / MTOTO MJANJA NA MWENYE AKILI NI YULE AMBAE ANAJUA KUJIAANDAA KWA AJILI YA MAISHA YAKE YA YA BAADAE.

Sina lolote la Ubaya nitakalo liongelea lihusianalo na huko niliko tokea. Majibu kutokana na maswali yote mliyonayo, na ambayo yana husiana na Mimi, Mtayapata kwenye Album ” BOMBE HIROSHIMA “.

Swali la Udadisi la Mtangazaji AICHA OKOKO kutaka kujua kama CHIKITO yuko na mpango wa kujiunga na WENGE MUSICA MAISON MÈRE, CHIKITO KAKATAA KABISA KWA KUSEMA WALA HANA MPANGO HUO. Kaendelea kusema, Kipaji alicho nacho ndicho chawafanya watu kujitokeza na kutaka kumsaidia na kumsapoti, kati yao akiwemo Mdhamini Mkubwa wa GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE anae julikana kwa Jina la GERVAIS NFUTILA LIYEBO.

AICHA OKOKO kamwambia kwa mara nyingite CHIKITO kua YEYE NI MTU ASIEKUA NA SHUKRAN,BAADA YA MIAKA 9 KWENYE GROUP LILILO KULEA NA KUKUJALI HADI UKAPELEKWA ULAYA,UKAPEWA FURSA YA KUIMBA JIJINI PARIS KWENYE UKUMBI WA ZENITH.

Jibu la CHIKITO ni kwamba, NI SAHIHI KABISA, NIMEKAA HUKO KWA KIPINDI CHA MIAKA TISA, KWANI NYINYI MLIKUA MKIPENDELEA NIKAE HADI MIAKA 30? WAKATI MIMI NIKIWA SINA KITU ? IKITOKEA LEO HII MUNGU AEPUSHIE MBALI KIFO KINANIKUTA, NANI YULE ATAKAE WAJALI WANANGU?

NAOMBA NIPENI NAFASI PIA NA WAKATI ,NDIPO MTAKAPO GUNDUA KIPAJI CHANGU!!! MNIELEWE KAMA MULIVYO WAELEWA WENGI KABLA YANGU. WAKATI NDO HUU WAWADIA KWA CHIKITO KUDHIHIRISHA KIPAJI CHAKE.

KAMALIZIA KWA KUSEMA YEYE HAYUPO FB,WALE AMBAO WANATUMIA JINA LAKE FB NI MATAPELI.

MTU AKITAKA KUWASILIANA NAE BASI AMTAFUTE KWENYE NAMBA HIZI 00243997838041 / 00243822954474.

*** KAMA WIKI MMOJA ILIOPIA, MSEMAJI MKUU WA WERRASON, SANKARA DE KUNTA akiwa kwenye Ndege JIJINI PARIS, KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI PAPY GENE, KASEMA UHAKIKA ALIONAO NI KWAMBA, PINDI CHIKITO ATAKAPO MALIZA SHUGHULI ZAKE HUKO ALIKO INCHINI ANGOLA, ATAKUJA MOJA KWA MOJA KUJIUNGA NA GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE .

LUBONJI WA LIBONJI

 


MUZIKI NA MAADILI YA UMMA INCHINI CONGO DRC

August 4, 2014

KATIKA UCHAMBUZI WANGU HUU, NIMEWEKA VIDEO AMBAYO YAONYESHA UKEUKAJI WA MAADILI YA UMMA  KUTOKANA NA MUZIKI. TIZAMA KWENYE VIDEO HII ANZIA DAKIKA YA ( 58:55 hadi 1:01:10 ). ASANTENI

 

Baadhi ya Wanamuziki Inchini CONGO DRC,katika Nyimbo zao hutumia Maneno Machafu,huku Wanenguaji wakicheza bila Aibu hadi wengine hufikia hatua ya kuvua kabisa Nguo zao na Kuonyesha sehemu zao za siri.

Ingawa Imefikia wakati fulani Serekali ya CONGO imechukua hatua ya kudhibiti vitendo vichafu kwenye Muziki,kupitia WIZARA YA UTAMADUNI NA SANAA, wakati lilipoundwa ” BODI YA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MAMBO YAPOTOSHAO UMMA KWENYE MUZIKI “.

Licha ya kuwepo Shirika hilo, Bado wapo Wanamuziki ambao wanaendelea bila woga wowote kwenda kinyume cha sheria nakuyafanya hayo wayatakayo wao.

Kumbukeni zipo aina ya Dansi zilizo vuma sana wakati, Maneno yake yalikua ya Upotovu wa Jamii :

1. KOFFI OLOMIDE kaimba ( MAMAN PESA SIMA, PAPA ATUBA TONGA ) akimaanisha MAMA LETE NYUMA, BABA ACHOME SINDANO.

2. WERRASON ( yeye katuletea Dansi MFUENI = MATAKO, pia na DANSI MWANA NATIKAKA MOKE SIMA EKOLI akimaanisha KABINTI NILIKAACHA BADO KADOGO LEO HII KANAJAZA TAKO KAMA NINI ).

3.JB MPIANA nae hajabaki nyuma,na Dansi ( EZO SUA EZO SALA PASI, SIMBA NGA MALEMBE. akimaanisha YANICHOMA,YANIUMIZA KWELI,NENDA TARATIBU.

Mifano ni nyingi sana,ionyeshayo utovu wa nidhamu na Upotevu wa Maadili ya Umma kwenye Muziki. Hebu jifikirie wewe Mzazi na Watoto wako Sebuleni mkitizama Video iliojaa na Maneno machafu kama hayo,huoni kama ni Aibu tupu!!!

Licha ya Mimi Binafsi kua Mpenzi Mkubwa wa Rumba, Naona upo upungufu fulani kwenye Bodi ya Mamlaka ya kudhibiti mambo machafu kwenye Muziki.Haifanyi kazi yake ipasavyo kwakutoitekeleza majukumu yake vilivyo.

KATIKA DESTURI NA MILA ZETU KWA SISI WA AFRICA,MAMBO KAMA HAYO HUA HATUPENDEZWI NAYO HATA KIDOGO.

Mambo kama hayo, na Vitendo kama vivyo, ni Moja ya sababu iliopelekea Vijana wa Diaspora wa CONGO, wanao julikana kwa jina la ” COMBATTANTS ” kuja juu na kupinga vikali aina ya Muziki kama huo, kwa madai kwamba SIKU HIZI MUZIKI WATUMIWA VIBAYA KWA KUPOTOSHA JAMII NA KUMDHALILISHA MWANAMKE.

Kwenye Miaka Kadhaa iliopita,Ilikua vigumu kwa Mwanamuziki kuimba maneno machafu,pasipokua na Sheria kufanya kazi yake. Kumbukendi kipindi ambacho Sheria kali imechukuliwa Dhidi ya Wanamuziki KOFFI OLOMIDE na NYOKA LONGO,walipo swekwa jela Mwaka 1993 JIJINI KINSHASA, kutokana na Dansi ” ETUTANA EH YANGO NA YANGO ” VIACHENI VIGONGANE VYENYEWE KWA VYENYEWE.

Sasa ingawa siku za huko Nyuma,Sheria ilikua ikifanya kazi na kuwapa adhabu kali kwa wale ambao wanaharibu maadili ya Umma kupitia Nyimbo zao, Kwa nini leo hii Wanamuziki wanaipa sheria kisogo, na kufanya yale wayatakayo bila kua na woga wowote?

Je! Hali hii ya sababishwa na Viongozi wenyewe wa Serekali,ambao hujisahau kutokana na Maslahi yao binafsi,kwakua kupitia Wanamuziki hujipa umaarufu zaidi wanapo tajwa mara kwa mara kwenye NYIMBO ?( LIBANGA ).

WENGI TULISHEHEREKEA KUONA SEREKALI YA CONGO IMEWATUNZA WANAMUZIKI KWA KUWAPA TUZO KUTOKANA NA KAZI YAO, NI WAJIBU PIA WA SEREKALI HIYO KUSISITIZA NA KUSHIKIZA MASWALA YA MAADILI MEMA KWA WANAMUZIKI,KWAKUA WAO NDIO KIOO CHA JAMII.

LUBONJI WA LUBONJI

 

 

 


CLAUDIA BAKISA FEAT FABREGAS

August 2, 2014

 

MALIZIA WEEKEND YAKO NA WIMBO ” AMOUR EN OR ” CLAUDIA BAKISA FEAT FABREGAS METIS NOIR

 

 

 

 


%d bloggers like this: