Kivumbi Arsenal na Chelsea, Man Utd v Man City

November 30, 2008

Mashabiki kushangilia au kulia leo?

Mashabiki kushangilia au kulia leo?

LIGI Kuu ya Uingereza inaendelea tena kwa kuikutanisha miamba nane inayowania kutwaa taji hilo.

Miamba hiyo inayoshuka viwanja tofauti leo ni Chelsea ambayo itaikaribisha Arsenal, huku Man City watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi Manchester United, Portsmouth wao watakuwa wakikipiga na Blackburn, huku Tottenham wakipepetana na Everton.

Pamoja na kuwepo mechi zote hizo, macho na masiko ya mashabiki yatakuwa kwenye viwanja viwili vya Stamford Bridge ambako Chelsea na Arsenal zitakuwa zikitoana jasho na Uwanja wa Eastlands ambako Manchester City na Manchester United zitavaana.

Chelsea wataingia uwanjani kwa nia ya kuondoka na pointi tatu ambazo ni mhimu kwao, ili waendelee kujihimarisha kileleni mwa ligi hiyo, wakati Arsenal watakuwa na nia kama hiyo, ili waweze kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Wakati timu hizo zikiwa na nia hiyo, Manchester wao wataingia uwanjani kusaka pointi tatu, ili kupunguza pengo la pointi ambazo inazidiwa na vinara wa ligi hiyo Chelsea na Liverpool, wakati Manchester City wao watakuwa na ni ya kuzitwaa pointi hizo, ili nao waweze kujiweka sawa katika mbio za kuwania ubingwa huo.

Mechi ya Chelsea na Arsenal itazikutanisha timu ambazo kila moja imewahi kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara tano, lakini Chelsea ikiwa ikiizidi Arsenal kwa kufanya vizuri katika misimu michache iliyopita, ambapo klabu hiyo ya Stamford Bridge haijamaliza misimu mitano ikiwa nje ya timu mbili bora wakati Gunners wao hawajawahi kugusa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Blues wataingia uwanjani wakiwa na rekodi ya kutofungwa, huku wakiwa kileleni mwa ligi wakiizidi pointi 10 Arsenal, ambayo imeshindwa kushinda mechi nne kati ya tano zilizopita, ingawa katikati mwa wiki hii ilifanikiwa kutinga hatua ya mtoano katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.


Masikini Mramba, aikosa ndoa ya Binti yake!!

November 30, 2008

Binti Aifena Mramba, mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Basil Mramba akitoka Kanisa la Mt. Petro Oysterbay, Dar es Salaam jana mara baada ya kufunga pingu za maisha na Bw. Evans Msiba. Bw. Basil Mramba alikosa kuhudhuria harusi ya bintiye baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana licha ya unafuu uliotolewa na mahakama. (Picha na Zuberi Mussa Majira)

Binti Aifena Mramba, mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bw. Basil Mramba akitoka Kanisa la Mt. Petro Oysterbay, Dar es Salaam jana mara baada ya kufunga pingu za maisha na Bw. Evans Msiba. Bw. Basil Mramba alikosa kuhudhuria harusi ya bintiye baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana licha ya unafuu uliotolewa na mahakama. (Picha na Zuberi Mussa Majira)

BI.AIFENA Mramba, binti wa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Fedha, Bw. Basil Mramba, amefunga ndoa na Bw. Evans Msiba, bila shamrashamra za aina yoyote kufuatia baba yake (Mramba) kushitakiwa na kukosa dhamana katika kesi inayomkabili na mwenzake, Bw. Daniel Yona, ya kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.

Washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na makosa zaidi ya 10 yanayohusiana na uzembe wanaodaiwa kuufanya wakiwa kazini na kulisababisha taifa hasara ya zaidi ya sh bilioni 10.

Ndoa hiyo ilifungwa Dar es Salaam jana katika Kanisa la Mt. Petro huku kukiwa hakuna shamrashamra kama ilivyozoeleka kwenye sherehe za harusi. Aifena na Evans walitoka nje ya kanisa hilo wakiwa wameshikana mikono wakiwa tayari mke na mume, tabasamu angavu juu ya uso wa Bibi harusi likiashiria matumaini mapya ya maisha yake ya ndoa. Soma Majira kwa Habari Zaidi


Taifa Stars yaichapa Sudan 3-1

November 30, 2008

Wachezaji wa Taida Stars wakishangilia

Wachezaji wa Taida Stars wakishangilia. Picha na Mwananchi

NI raha, raha tupu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya ushindi mzuri wa Taifa Stars wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan katika mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania.

Ushindi huo umeifanya Tanzania kujiweka pazuri kwa mchezo wa marudiano na kuanza kupigia mahesabu safari ya Ivory Coast kwenye fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN, Julai mwakani.

Stars sasa inahitaji sare ya aina yoyote iweze kukata tiketi ya fainali katika mchezo wa marudiano utakaofanyika kati ya Desemba 13 na 15.

Katika mchezo huo ambao Stars walianza kwa mashambulizi tangu dakika ya kwanza baada ya Athumani Idd kupaisha mpira akimwangalia kipa wa Sudan Akram Elhad.

Stars wakionekana kutulia na kupanga mashambulizi ya kushitukiza waliliandama lango dakika tano za kwanza lakini Jerry Tegete mara zote hakuwa makini. Katika dakika ya 12, nusura Haruna Moshi ‘Boban’ aipatie Stars bao baada ya kupiga shuti kali na kipa wa Sudan, Elhad kulipangua.

Gonga hapa kusoma zaidi gazeti la Mwananchi


Waziri mkuu aruhusu YOGA MAlaysia lakini…

November 28, 2008

Mikao mbalimbali ya Yoga

Mikao mbalimbali ya Yoga ambayo National FATWA Committee inasema haifai kwa akina mama wa Kiislam

Wazirimkuu wa Malaysia Abdullah Ahmad Badawi amesema jana kuwa Michezo ya mazoezi ya viungo ya YOGA ambayo ilikuwa imezuiliwa na kupigwa marufuku kabisa kwa jamii ya kiislamu nchini humo inweza kuendelea kama baadhi ya marekebisho yakifanywa.

Mchezo wa YOGA ulitangazwa kuzuiliwa na kutangaziwa FATWA kwa yeyote ambaye atajaribu kuishiriki mapema wiki iliyopita na baadhi ya majimbo zaidi ya nane yalishaipitisha kuwa sheria kabla ya Waziri mkuu kutolea maelezo.

Kwa mujibu wa baraza la kiislamu la  National Fatwa Council, lilitangaza kupiga marufuku YOGA kwa waislamu kwa kusema kuwa inaingilia imani kwa jumuiya ya waislam na baadhi ya mikunjo yake si vyema kufanywa na jamii ya Waislamu hasa akina mama. lakini uamuzi huo ulionyeshwa kupingwa si tu na jamii ya waislamu wenyewe bali hata viongozi na baadhi ya majimbo kam Selango lilisema suala hilo inafaa lirudishwe kwa wananchi wao waamue.

Mwanamama akifanya Yoga

Mwanamama akifanya Yoga

“Nimewaambia baraza kuwa kama michezo hiyo itafanyika bila kuwa na malengo ya kuharibu au kuingilia imani ya mtu ni bora wakaiacha iendelee kwani kwa upande mwingine inafaida kwa jamii” alisema Abdulah.

Yoga ni mchezo ambao mchezaji hutakiwa kutulia na kufuata mienendo kwa step huku akili akiwa ameipumzisha jambo ambalo wachezaji husema huwapeleka mawazo mbali na mara nyingi kiutokwa na jasho jingi. hicho kipande ndicho kinasemwa kinaingiliana na imani.


Serikali Malaysia yazuia onyesho la mwanamuziki toka Indonesia

November 28, 2008

Inul

Inul

Mamlaka ya Halmashauri ya jiji la Kuala Lumpur (DBKL) imekataa maombi ya waandaaji wa onyesho la mwanamuziki toka Indonesia Inul Daratista, kwa kile kinachosemwa masuala ya kiusalama.

Akizungumzia uamuzi huo ofisa wa DBKL alisema kuwa awali ilipangwa mwanamuziki huyo maarufu kuwa na onyesho katika uwanja wa taifa wa Burkit JAril siku ya jumamosi tarehe 29 lakini ombi lake limekataliwa.

Imefahamika kwamba Mwanamuziki Inul haruhusiwi kutokana na miondoko yake ambayo inasemekana haiendani na maadili ya dini ya kiislam.Maofisa wa DBKL wanasema kuwa waandazi walishafahamishwa toka jumatatu.

Hii ni mara ya pili kwa mwanamuziki huyo kunyimwa kibali cha kufanya onyesho awali ilikuwa mwezi july.

Kwa mujibu wa asasi za kidini zilisema zitaandamana kupinga onyesho hilo jambo ambalo DBKL wamesema litahatarisha amani.

Malaysia ni nchi inayofuata dini ya Kiislam kwa mujibu wa dini hiyi mwanamke hatakiwi kuacha wazi baadhi ya maungo kama anavyofanya mwanamuziki huyu awapo jukwaani kwani hata cheza yake inasema inahamasisha ngono.

Gonga player upate kionjo cha mwanamuziki huyu machachari jukwaani (kiuno bila mfupa).


Tunawakilisha

November 28, 2008

Katambuga

Katambuga

Shavu kwa wadau wangu wa Kuala Lumpur si unaona wanavyowakilisha chata Katambuga!!


Mrembo wa Afrika Mashariki kupewa gari la kifahari

November 28, 2008

Lena Calist kushoto akimuonyesha Balozi Leandre Bagegwanubusa wa Burundi magari yatakayolewa kama zawadi kwa washindi wa shindano hilo. Picha na Mzee wa Full Shangwe!!

Na Majuto Omary wa Mwananchi

MSHINDI wa mashindano ya Miss East Africa yaliyopangwa kufanyika Desemba 19 mjini Bujumbura, Burundi atapata gari aina ya Lexus Rx 300 lenye thamani ya dola za Kimarekani 35,000 waandaaji wa mashindano hayo, Rena Events Limited wametangaza.

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Rena Callist alisema kuwa mshindi wa pili atapata dola 5,000 na wa tatu dola 3,000 wakati wa nne na wa tano watapata dola 500 kila mmoja. Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: