Chapuo hadi kieleweke…!!

August 11, 2008

Brazil's Olympic soccer player Ronaldinho, center, carries a drum as he arrives in Qinhuangdao, Monday, Aug. 11, 2008. Brazil, which will play against host China in Qinhuangdao on Wednesday, is trying to win the Olympic title for the first time.
Mchezaji wa Brazil timu ya Olympic ya soka ya wanaume Ronaldinho Gaucho akiwa amebeba “chapuo” walipokuwa wakiwasili mjini Qinhuangdao, leo Aug. 11, 2008. Chapuo ni kijigoma kidogo kwenye ngoma ya Wazaramu ya Mdundiko ambacho kikianza kupigwa hakizimwi hadi ngoma iishe. Brazil wamedhamiria kuchukua kikombe hiki kwa mara ya kwanza.


Chelsea kumchukua Kaka kwa dau la kuvunja rekodi ya mwaka!

July 20, 2008
Kaka huenda akaenda Chelsea

Kaka huenda akaenda Chelsea

LONDON: Mchezaji wa AC Milan nyota Mbrazili Kaka anakaribia kutua kucheza English Premier League kwa klabu ya Chelsea kwa kile kinachosemwa rekodi ya dunia ya uhamisho ya Paund £80milioni (sawa na 100mil euros), alisema mshauri wa Kaka jana.

Kama kaka ataondoka itakuwa pigo kwa mshambuliaji Ronaldinho ambaye alisema amefurahi sana kucheza timu moja na Kaka na ni katika vito vilivyomfanya asisite kuhamia timu hiyo ni kuwepo kwa Kaka. na msemaji wa Kaka ambaye ni Meneja wake binafsi Diogo Kotscho aliongeza kuwa pande zote mbili ziko tayari kumaliza deal hiyo na kuifanikisha.

“Real Madrid walitaka kutoa euro 90milioni msimu uliopita kwa mchezaji Kaka lakini Milan hawakuwa tayari kumuachia kwa wakati huo, alisema” Kotscho akiongea na gazeti la The Guardian.

“Wakati huu ni tofauti na nafikiri huu ni muda muafaka wa kufanya hii deal, ni wakati pekee tunafikiri huu mpango twaweza ufanikisha na hii ni kwa sababu ya hali ya kifedha iliyopo klabuni hivyo ni muda muafaka kumalizana na jambo hili”.

Kama Kaka atakwenda Chelsea basi mashabiki wanaipa nafasi kubwa kwa kampeni yake ya kuchukua vikombe vyote viwili ambao ndio mission ya mmiliki wa klabu hiyo alipomkabidhi jahazi Philipe Scollari.

Wakati huo huo Chelsea imekataa mpango wa Real Madrid wa kubadilishana Samuel E’too na wao wamtoe Didie Drogba. HAbari kamili inakuja.


%d bloggers like this: