Serengeti yaja na Saidia Stars ishinde!!

December 29, 2009

Meneja uhuasiano wa kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kiwandani hapo kuhusu promosheni ya shangilia Taifa Stars inayoanza kesho wakati timu hiyo itakapocheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Ivory Cast Januari 4 na 7 jijini Dar es salaam Ivory Coast inajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Angola.

Promosheni hiyo itawafanya mashabiki mbalimbali wa soka katika baa mbalimbali kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Bia za Serengeti, Kofia, Fulana na jezi za timu ya Taifa pamoja na tiketi za kuingilia katika michezo hiyo, wanaofuatia katika picha ni meneja mkuu wa kampuni hiyo Mr Kagusa, Bahati Singh meneja matukio na promosheni na mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa.


Mjadala wa Maximo Jamii Forum

December 29, 2009

Kwa wadadisi na wapenda mijadala ninapozungumzia Jamii Forum wananielewa, Kuna mjadala unaendelea kule kuhusu maendeleo na majaliwa ya Taifa Stars chini ya kocha Marcio Maximo.

Mjadala ulianza toka kwa mdau JP (kifupi), naye alisema:-

Mambo vipi members wa jambotz,e bwana kuna kitu kinanzingua…hivi maximo anaona kama watanzania ni wa jinga..e,
nasema hivi kwa kukumbuka kauli yake aliyeitoa wakati alipoenda na stars kuweka kambi kule brazil,
alisema…anawapeleka kwenye ardhi yenye harufu ya mpira sio hapa bongo,ambapo hakuna hewa nzri ya mpira,haya ni ma2si na hajawahi kuomba msamaha kwa kauli yake hyo,jamani huyu mtu atimuliwe hafai kuwa kocha hata cvs zake hazijulikani?

 

Majibu ya Mdau wa kwanza

Kwako,Bro John P.

Kila binadamu hufanya makosa nadhani tunaweza kukubaliana hapo.Na kama kila siku unaweza kufanya kosa jipya na kujifunza kutokana na hilo kosa ,inakuwa vema sana na sana.Tatizo au uvivu ni kuwa tunafanya makosa then hatutaki kukubali kuwa tulifafanya kosa na kujifunza kutokana na kosa hilo au lile.Huo ndio udhaifu wetu,bila shaka na hata huyo Maximo,kama ulivyomtambulisha.

Read the rest of this entry »


Petit frere Guy Digital alipowachengua Nairobi Dec hii.

December 29, 2009

[image]
Shikito ambaye alianza kuimba akiwa kijana mdogo sana na kujizolea umaarufu mkubwa kwa sauti yake, Kijana huyu anamkosha sana rafiki yangu Ally Tandika tajiri wa simu.
[image]
Petit frere Guy Digital, Jina ambalo kwa sasa ndio wanamuita kwa kuifanananisha sauti yake na sauti ambazo tayari zimeingizwa kwenye mashine za kisasa za muziki kuchujwa!!. Kwa wanaofatilia mtu mwingine ambaye aliitwa hivyo ni Lola Mwana “Lola Digital” ambaye alikuwa kwa mwanamuziki Def Defao.

 

[image]
Fere hujituma sana awapo jukwaani na ana pumzi sana kwani nyingi za nyimbo zake huimba beti ndefu na pia huhitajika kucheza, yaitaji pumzi haswa.
[image]
Who’s the atalaku? Binafsi simjui jina lakini kwa waliosikiliza Albamu mpya ya Fere Gola watakubaliana na mimi jamaa anatisha.

[image]
Mukulu Bilanga FEre Gola

[image]
Mwasi kitoko, nadhani ushasikia sana hiyo!!

[image]
Boss akionyesha uwezo wake

[image]
Follow the leader, Mzee mzima Fere Gola akiwaongoza vijana wake.

[image]
Shikito akipagaisha watu

[image]
Bendi Nzima


Tangazo la wadhamini

December 28, 2009

showroom

We are a one-stop Exclusive Car Accesories located at Lumumba Street next to Royal Chief Restaurant in Dar es salaam.

Our wide range of Cars Accesories is exclusively imported from

UAE,Singapore,Malaysia,Japan,China and Thailand. Our Contacts: 0719700001, 0718306060, 0754268578, 0784949127.


Man U waongeza kasi

December 28, 2009

image

Manchester United wamekataa kupigwa kumbo kwenye ngazi ya ligi kuu ya Uingereza kwa kuitandika Hull 3-1 na kurejea katika nafasi ya pili ambayo ilikuwa imetwaliwa kwa muda mfupi na Arsenal.

Ushari wa Wayne Rooney ulivuna goli kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Hull walisawazisha kupitia penalti ingawa walijifunga na kuwapa Manchester United nafasi ya kuwabana na kuwakandamiza zaidi.

Bao la tatu lilifungwa na Dimiter Babatov, ushindi ambao uliwarejesha vijana wa Alex Ferguson katika nafasi ya pili.

Kwa sasa Man U wamecheza mechi 19, sawa na Chelsea ambao wanashikilia nafasi kwanza kwa pointi mbili.

 

Na BBC


Yanga mabingwa wa Tusker

December 28, 2009

image

Wachezaji wa Timu ya Yanga wakisherehekea Ushindi baada ya kunyakua Kombe la Tusker katika mchezo wa Fainali ambapo waliwalaza wapinzani wao Sofa Paka ya Kenya 2-1. Picha na Michuzi

TIMU ya Yanga imefunga mwaka kwa 2009 kwa kishindo baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Tusker kwa kuichapa Sofapaka kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga walilazika kusubili hadi dakika tano za mwisho kuanza kusherekea ubingwa wao kwa mabao yaliyofungwa na Mrisho Ngassa (90 dk), na Boniface Ambani (85dk).

Mabingwa hao wa Tanzania wamefanikiwa kujinyakulia shilingi milioni 40, huku ndugu zao Simba wakijinyakulia nafasi ya tatu Mil 10 na Wakenya hao Sofapaka washindi wa pili walijinyakulia Mil 20.

Mshambuliaji Jerryson Tegete alikabidhiwa zawadi yake ya ufungaji bora Mil 2 baada ya kufunga jumla ya mabao 6 kwenye michuano hiyo, huku Mafunzo ya Zanzibar imepata tuzo ya timu yenye nidhamu.

Gonga hapa kusoma zaidi.


Arsenal yashamiri kwa kuitandika Villa

December 28, 2009

image

Nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas alionyesha ushujaa wake kwa kuiongoza timu yake kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Aston Villa.

Fabregas ambaye ana jeraha alikuwa amehifadhiwa kama mchezaji wa akiba.

Lakini mnamo dakika ya 57, huku mambo yakiwa tasa kati ya timu zote mbili, Meneja Arsene Wenger, alimwachilia nyuki Fabregas kutimua mishale.

Haikumchukua muda kabla ya kutumbukiza mawili kwenye wavu.

Hata hivyo ilidhihirika kwamba jeraha lake Fabregas ni sugu na akaondolewa.

Hata hivyo, Arsenal walikuwa wamedhibiti mechi, Abou Diaby akaongeza la tatu.


%d bloggers like this: