Gongolamboto tuko pamoja na Japani tuko nanyi pia.

March 30, 2011

...

FAIR PLAY; Mshabiki akionyesha bango la kuwafariji Gombo la Mboto na Japan pia, Hii ilikuwa kwenye mechi uwanja wa Taifa baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kati. Sehemu ya mapato ya mechi hiyo ambayo ni asilimia moja (1%) yalitolewa kwa ajili ya waathirika wa mabomu wa Gongo la Mboto, na jana wametangaza kuwa takribani Tsh Milioni moja na ushehe ikiwa ni asilimia moja ya Milioni mia imetolewa kwa ajili hiyo.


Stars yainyoa New zealand 2-1

June 4, 2009

b13

Kikosi cha Taifa Stars kilicho wanyoa Netherland jana

Timu ya Taifa Taifa Stars usiku wa kuamkia leo imewapa zawadi watanzania baada ya kuichapa timu ya Taifa ya New zealand kwa mabao 2-1. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja Mpya wa Taifa, Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kufungwa bao ambalo lilipatikana dakika ya 10 baada ya beki wa Stars kuunawa mpira ndani ya box, Muda mchache baadaye Stars walisawazisha kwa bao safi la kichwa lililopachikwa na mchezaji Jerry Tegete.

Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mamia ya mashabiki na kurushwa Live duniani kote ulikuwa wa pande zote kwani timu zilishambuliana kwa zamu na kama si makosa ya hapa na pale basi wallah tungewaumia. Bao la pili la Stars lilifungwa na mshambuliaji anayekuja juu Mwinyi Kazimoto. Mpaka kipyenga cha mwisho Taifa Stars 2-1 New zealand.

Shukrani kwa mdau wangu Robert Mwafrika kwa habari hii, Picha na Michuzi.


Justin Timberlake na Lupe Fiasco kupanda Mlima Kilimanjaro

April 30, 2009

 JustinTimberlake460 Mwanamuziki Justin Timberlake na Rapper Fiasco Lupe wataungana na muimbaji Kenna katika kampeni ya Maji safi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Nia ya kupanda mlima kilimanjaro ni kuchangia mradi ambao ulianzishwa na Kenna ambaye ni mzaliwa wa Ethipia, ikumbukwe kuwa nyingi ya nchi za Africa bado suala la Maji safi ni kitendawili.

Justin amesema kuwa anakuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa wiki ili kuzoeza mapafu yake kwa ajili ya kubeba hewa ya Oksijeni ya kutosha ambayo inahitajika sana wakati wa kupanda mlima huo wenye urefu wa M 5800.

Tutapanda kwa wiki nzima huku tukiwa na mzigo wa paundi karibu 30 mgongoni, kazi ni kubwa mbele yetu alisema Timberlake akiongea na GQ.

Naye Kenna alisema ”Baba yangu nusura afariki kwa ajili ya tatizo la maji miaka hiyo…” nina marafiki wengi sana ambao wako tayari kusaidia kampeni hii hivyo ni lazima tuifanikishe alisema Kenna.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Guardian wastani wa wapandaji 10 hufariki kila mwaka katika harakati za kuupanda mlima huo mrefu kuliko yote Barani Afrika.

Waandaaji wamepanga upandaji ufanyike kipindi hiki cha majira ya kipupwe.

Nakuacha na kibao Whats Goes Around Comes Around toka kwake Justin Timberlake!!


%d bloggers like this: