TIMU YA TAIFA YA POOL KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA, PARIS UFARANSA

October 30, 2010
Meneja wa Bia ya Safari lager,Fimbo Buttalah (kati) akizungumza mbele ya vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika leo,wakati wa kutangazwa kwa timu ya Taifa ya Pool itakayoshiriki mashindano ya Dunia huko nchini Ufaransa mapema mwezi ujao.Kushoto ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho na kulia ni Katibu mkuu Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Pool,Dennis Lungu,akitangaza kikosi chake chenye wachezaji saba ambao wataondoka nchini tarehe 6,Novemba kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia.wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Godfrey Muhando (nahodha),Omary Akida,Mohamed Iddy,Issa Mkindi,Felix Atanas pamoja na Vaileth Mrema (mshichana pekee katika timu hiyo).kulia ni Mwenyekiti wa Pool Taifa,Isack Togocho.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kukamilisha mipango yote ya kuipeleka timu ya taifa ya Pool katika mashindano ya dunia yatakayofanyika katika jiji la Paris, nchini Ufaransa mwezi Novemba. Read the rest of this entry »

Adha ya kivuko saa nyingine!!

October 30, 2010

...

Abiria wakihamaki huku PAntoni ya Mv Magogoni baada ya mlango wake kushuka kabla PAnton haijatia nanga, matukio ya namna hii ni hatari kwani yanaweza kusababisa maafa.


Hii Mlimba hii!!

October 30, 2010

...

Wiki iliyopita nilikuwa kijijini kwetu Mlimba huko Ifakara – Morogoro, Mara ya mwisho nilikwenda kukiwa hakuna hata umeme lakini majuzi nimeshangaa watu wanakula Ligi ya Uingereza kama Dar, Pia huduma muhimu za barua pepe na kurambaza zinapatikana tena mtandao wa kasi tuu. HAya ni mageuzi kwa kweli.


Jangwani jioni ya leo

October 30, 2010

Jangwani

Yamebaki masaa kabla ya Watanzania kufanya uamuzi mkubwa.

Kesho ni siku ya kupiga kura, Picha hii imepigwa dakika chache baada ya Chama Cha Mapinduzi kuhitimisha kampeni zao kiaina pae katika viwanja vya Jangwani jioni hii.


Tumpigie kura zetu Lady Jaydee ili ashinde PAM Awards,

October 29, 2010

Lady Jay Dee

Jinsi ku VOTE,
Andika 36 acha nafasi halafu andika Lady Jay D. Tuma kwenda namba +256 752 600 100. Lady Jaydee anatanguliza shukrani za dhati kwenu wana Bongo Flava..


ALIKIBA NDANI YA CHICAGO

October 29, 2010

Ali Kiba (kulia) akiwa na 2Face Idibia wakipitia mistari.

 


Shime twendeni tukapige kura!!

October 29, 2010

 

http://1.bp.blogspot.com/_stxylFr6jLM/TMhW5zVD9pI/AAAAAAAAy_A/jZNSJVejXCQ/s1600/Picha+Nye.jpg

 

Kama wazee hawa walithubutu kusimama kwenye msururu mrefu hivi ili wapige kura, itakushinda nini wewe baba,wewe mama,wewe kaka,wewe dada wewe kijana,kusimama foleni na kupiga kura shimeshimee watanzania tukapige kura,mabadiliko yataletwa na kura yako.katika picha hapo juu wa nne kushoto ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa kwenye foleni ya kupiga kura.


%d bloggers like this: