Meseji ndio chanzo cha kupigwa Rihanna

February 17, 2009

Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa Gossip.com mwanamuziki Rihanna ametoa ushirikiano na kusema kuwa chanzo cha ugomvi wao ni meseji aliyoingia kwenye simu ya mpenzi wake Chris Brown ambayo ilitoka kwa mwanamke mwingine, ndipo Rihanna alipotaka kujua kulikoni na kuja juu akiamrisha arudishwe nyumbani kwani wawili hao walikuwa kwenye gari moja ya Chris Brown. habari zinasema wakiwa njiani Rihanna alijifanya akiongea na simu na rafiki yake akimueleza kuwa “…Jamaa ananishusha nyumbani hakikisha kuwa polisi wapo…” anavyodai yeye alifanya hivyo kwani anamjua mpenzi wake huyo ngumi mkononi na alikuwa akitishia kumpiga kumbe ndio alipalilia makaa na kufanya Chris Brown ambaye alikuwa akiendesha kuanza kumshishi kupigo ambapo anadai alimpiga kwa kutumia kiwiko (kipepsi).

Marafiki wa Rihanna wanasema kitendo cha mwanamuziki huyo kulamba kipigo ni kitu cha kawaida kwani hata mwaka jana wakati wa 2008 American Music Awards Rihanna alipanda jukwaani akiwa na plasta ambayo alidai ameficha mikwaruzo ambayo vyanzoo vya habari vinasema ni kipondo.

Hakuna ambaye alikubali kutoa maeleezo kati ya wawili hawa lakini mwanamuziki Chris Brown kupitia akaunti yake ya Face book inayopatikana kwa Christopher Maurice Brown amebadilisha sehemu ya mahusiano toka “in relationship” to “Single” na status yake kusomeka “…mtaanza kujua tabia zake halisi sasa” ambapo wadadisi wa mambo wanasema kuwa wawili hao kila mmoja mkorofi.

Kama vipi isome mwenyewe hapa hehehehe

Pia gonga hapa uone jinsi wazee wazima walivyomdaka mshkaji


Chris Brown alivyokatisha usiku wa Valentine kwa mashabiki wa Rihanna Malaysia

February 16, 2009

rihanna_sexynow_cw__580034g Kitendo cha mpenzi wa mwanamuziki Rihanna kupigwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake Cris Brown kimelaaniwa na mashabiki wa muziki hapa Malaysia ambapo Rihanna alikuwa atumbuize siku ya tarehe 13 usiku kuamkia siku ya wapendanao uwanja wa Shah Alam jijini Kuala Lumpur. Onyesho ambalo waandaaji walishamaliza kuuza Tiketi zake siku nyingi.

Wakizungumza kuchangia mada kwenye radio maarufu ya Kiss Fm mashabiki hao waliokuwa wakipiga simu wameomba kituo hicho cha Radio kusitisha kupiga nyimbo za Rihanna katika kuonyesha hasira na hisia zao kwa alichokifanya.

Awali mwanamuziki Rihanna ambaye ziara yake ilileta utata kwa kupingwa na baadhi ya Jumuiya za kidini zenye msimamo mkali kwa kile walichodai mavazi ya mwanamuziki huyo hayaendani na mila na utamaduni wa Malaysia ambayo ni nchi inayofata dini ya Kiislam. Baada ya vuta nikuvute ambayo jumuiya hizi zilisema zingefanya maandamano makubwa waandaaji walilazimika kufanya vikao vya pamoja na Meneja wa Rihanna na kukubaliana kuwa Rihanna atavaa vazi la heshma kitu ambacho ni nadra sana.

Rihanna ametokea kujizolea umaarufu duniani na hivi karibuni alifanya onyesho nchini Singapore ambapo idadi kubwa ya Mashabiki walisafiri kwa kukodisha mabasi kwenda kumshuhudia mwanamuziki huyo huko Singapo ambapo ni mwendo wa masaa sita kwa Basi.

Rihanna alipata michubuko usoni, kwenye feez na kuvuja damu kwenye pua baada ya kipigo hicho.


Ziara ya Rihanna MAlaysia utata mtupu…!

January 22, 2009
Rhanna

Rhanna

Mwanamuziki toka nchini marekani Rihanna anatarajiwa kuzuru nchini Malaysia February 13. Katika nchi ambayo inatawaliwa kwa sheria za dini ya Kiislam ni vigumu kuona onyesho la mwanamuziki kama Rihanna amabaye anakawaida ya kupagawisha mashabiki kwa mavazi yake ambayo yanarandana na umbo lake lenye mvuto kwa kila jicho.

Chama cha Pan-Malaysian Islamic Party kimekuwa cha kwanza kuipinga ziara ya mwanamuziki huyu nchini malaysia kwa madai kuwa haina manufaa kwa wamalay sana sana itaharibu culture ya wamalay . Katika waraka wao PAS wanasema kuwa hawaungi mkono hata kidogo ziara ya mwanamuziki huyu na kutaka serikali kuivunjilia mbali ziara ya mwanamuziki huyu.

Ikumbukwe kuwa waandaaji wa The Pussycat Dolls waliishia kulipa fine ya Dola 3000 na kufungiwa kwa muda maalum kufanya shughuli za burudani baada ya kuchezesha wanamuziki nusu uchi hapa Malaysia.

Hivi karibuni PAS waliongoza mamia kwa maelfu ya waandamanaji kulaani mauaji ya Wapalestina huko Gaza, katika maandamano hayo ambayo yaliishia kwenye uwanja kubwa wa mpira wa Sha Alam, viongozi wa PAS waliwaasa wananchi wa Malaysia kugomea bidhaa za Marekani ikiwemo Coca Cola, Star Bugs, Mc Donald na nyinginezo.

.

Lihana: Washabiki wangu wananipenda kama nilivyo, kwa sauti, mavazi, kucheza.


%d bloggers like this: