From UK to Spain with LOVE!

June 13, 2009

Cristiano-Ronaldo-Long-10 Hatimaye timu ya soka ya Uingereza ya Manchester United imeafiki kitita cha fedha kilichovunja rekodi ya mauzo ya mchezaji duniani cha paundi milioni 80 kwa Criostiano Ronaldo ajiunge na Real Madrid.

Taarifa kutoka klabu ya Old Trafford imesema "United imeafiki kuiruhusu Real Madrid kufanya mazungumzo na mchezaji".

Taarifa hiyo imeongeza kueleza kwamba uamuzi huo umekuja kutokana na maombi ya Ronaldo mwenyewe baada ya "kwa mara nyingine kuonesha hamu ya kuondoka".

United imelezea zabuni hiyo kwa mshabuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kama isiyokuwa na masharti na kuongeza wanatumaini makubaliano kamili yatafikiwa mwishoni mwa tarehe 30 mwezi huu wa Juni.

Imefahamika kwamba fedha za uhamisho zitapatikana kwa meneja wa Mashetani hao Wekundu Sir Alex Ferguson kwa ajili ya kuwekeza katika soko la usajili.

Madrid tayari mapema wiki hii ilimsajili kiungo mshambuliaji Mbrazil kwa kitita inachosemekana ni paundi milioni 56 na kukipiga kumbo kiasi kilichokuwa juu cha fedha kumsajili mcghezaji duniani, kilichokuwa kikishikiliwa cha paundi milioni 45.6 ambacho Real ililipa kumpata Zinedine Zidane 2001.

Madrid pia inaelezwa kuwa na uchu kuwachukua Xabi Alonso wa Liverpool, David Villa wa Valencia na winga wa Bayern Munich Franck Ribery.

Kati ya mambo ambayo inasemekana Kocha Fergurson alitilia mkazo ni nidhamu binafsi ya Mchezaji huyo kwa maisha yake binafsi jambo ambalo wadadisi wa kimichezo wanasema Ronaldo asipojiandalia atamaliza mchezo wake Spain kwani huko Maisha ya kujiachia ni  zaidi ya uingereza.


Cristiano Ronaldo.

Maamia ya mashabiki wanasaubiri kuona je Ronaldo majaliwa yake kwa maisha mapya ya mpira ambapo kwa timu ya Manchester United yamekuwa yamafanikio makubwa.


Manchester yaendelea kusomba Mataji

August 11, 2008

Gary Neville of Manchester United lifts the Community Shield after Manchester United won the FA Community Shield match between Manchester United and Portsmouth on August 10, 2008 at Wembley Stadium in London. Manchester United won the game 3-1 on penalties after the game finished 0-0. AFP PHOTO/IAN KINGTON (Photo credit should read IAN KINGTON/AFP/Getty Images)
Gary Neville wa Manchester United akiwa amenyanyua Ngao ya Hisani baada ya kushinda kwenye mchezo wao na Portmounth hapa jana 10.08.08, Mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki, Manchester ilishinda 3-1 kwa penati baada ya kumalizika kwa suluhu ya 0-0.


Man na Orlando Pirates uwanjani leo Durban Afrika ya Kusini

July 22, 2008
Man U

Man U

Captain Rio Ferdinand wa Manchester United , wa tatu toka shoto, akiwaongoza wenzake kwenye mazoezi katika uwanja wa ABSA Stadium huko Durban, South Africa, jana jioni, July 21, 2008, Timu ya Manchester United leo inacheza na Orlando Pirates ya Afrika ya kusini kwenye mechi Vodacom Challenge.


%d bloggers like this: