EXTRA BONGO YAZIDI KUWABAMBA MASHABIKI NDANI YA MEEDA SINZA

April 30, 2013

Mkurugenzi wa Extra bongo Ally Choki akiimba mbele ya mashabiki wake (Hawapo Pichani) ndani ya Ukumbi wa Meeda sinza jana Usiku wakati bendi yake ilipokuwa ikiburudisha pande pande hizo

Kushoto ni mwimbaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo Athanas akiwa na Mwimbaji pekee wa kike wa bendi hiyo Khadija Mnoga a.k.a “Kimobitel” ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake wa “Mgeni” wakishoo luv mbele ya kamera yetu ndani ya ukumbi wa Meeda Sinza jana usiku wakati Bendi yao ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo.

Kushoto ni mmoja wa marapa bora wa muziki wa dansi Totoo Ze Bingwa akirap ndani ya Meeda sinza wakati Bendi anayopigia mzigo Extra Bongo ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo na kulia ni Banza Stone a.k.a Generale akimpa big up.

Maua ya Extra Bongo mzigoni

Wakata nyonga maarufu kwa sasa wa Extra bongo wakiongozwa na nyamwela wakiwapagawisha mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Meeda Sinza jana usiku

Waimbji bora wa Extra bongo kulia ni Rogert Hega a.k.a Katapila wakiimba ndani ya Meeda Sinza jana usiku

Rapa bora wa Extra bongo Kabatano (Kulia) akigani moja ya jimbo zao bora huku akipewa sapoti na nguli wa muziki wa dansi Banza Stone mwana masanja wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza maeneo ya Sinza katika ukumbi wa Meeda jana usiku.


Fimbo ya Bakadja; Mapenzi yanapofananishwa na Fimbo ya Mkoloni na Tshala Muana akimshirikisha Meje 30

April 30, 2013

Alipokaribia kufanya uchaguzi wa kwanza tangu aingie madarakani Rais Joseph Kabila aliwaandalia chakula na kuwaita wanamuziki wote wakubwa Ikulu ya Kinshasa na kuwaomba wamuunge mkono kwani Muziki unanafasi kubwa sana kwenye ushawishi nchini DRC. Baada ya chakula Rais Kabila alikuwa na mazungumzo na kila mmoja wao huku wakichanganyika na kupata vinywaji. Katika mazungumzo na Tshala Muana Malkia wa Mutuashi Rais kabila pamoja na mambo mengine alimuuliza ni vipi watafanya kurithisha muziki wao kwa vijana wadogo, na hapo ndipo Tshala Muana akaamua kumlea Meje 30 na kumtambulisha kwenye ulimwengu wa muziki wakatamba na vitu kama Delastage ambacho kinapendwa sana.

Hapa tunauangalia wimbo Fimbo ya Bakadja ambao Tshala Muana amemshirikisha Meje 30 tena, Wimbo huu unaelezea jinsi bidada shosti alivyoumizwa na penzi la mwanaume akifananisha maumivu yake na kiboko cha Bakadja, Bakadja enzi za ukoloni kama unakumbuka wakoloni walikuwa wakitoa adhabu ya viboko kwa waliokuwa wanashindwa kulipa kodi au kukaidi amri za viongozi, Na hawa wachapaji unakuta kwenye kijiji yuko mmoja ana anaogopwa mnooo!!!.

Adhabu zile zilikuwa ni za Viboko na unachapwa hadhani zilikuwa zinauma physically na emotionally kwa sababu zilikuwa zinadhalilisha sana fikiria mtu mzima unachapwa mbele ya watoto.

Mapenzi bado ni kitendawili na kila siku yamekuwa yakiimbwa na wanamuziki wengi ama kutokana na wao yaliyowakuta ama ndugu zao ama rafiki zao ama watu wao wa karibu. Meje 30 analalamika kwenye wimbo anamlalamikia huyo mwanaume na kuwaambia watu hata kwenye makaburi kuna waliokufa sababu ya mapenzi. ama kweli mapenzi yanaumiza na nyimbo kama hizi zitaendelea kuimbwa kila uchao kwani kadri siku zinavyokwenda mapenzi yanazidi kuwa kizungumkuti hasa haya ya Digital ndio balaa.

Nakuacha na wimbo huo sikiliza Rhumba hilo na nipe maono yako.


Kizomba Dance ni nomaa jombaaa!!!

April 25, 2013

Kwa vile tunasherehekea Muungano naomba niwape video hii ya Kizomba Dance kama burudani kwenu, ikiwa mahsusi kwa Le Suveree Mukulu Mabamba Abiud pamoko sana jombaaaa!!!


Tutu Kaluji aamua kumuimbia Bwana

April 25, 2013

Mwanamuziki Tutuu Caludji ambaye aliwahi kutamba na bendi ya Wenge Musica na Wenge BCBG ameamua kumuimbia bwana baana ya kutoka kivyake na kutoa albamu yake moja sokoni.

Albamu hii inasemwa itaingia sokoni ifikapo katikati ya mwaka huu, ijapo kuwa haijasemwa itakuwa na nyimbo ngapi lakini tutafahamishana hapa hapa.

Ikumbukwe kuwa Pamoja na kuwa atalaku Kaluji pia alikuwa mtunzi ambapo kibao kama Tchico Londonien kilikuwa ni utunzi wake na kilibamba sana.


Demi Tour yakwake Werasson Ngiama Makanda

April 25, 2013

 

Anaitwa LE ROI DE LA FORRET” NOEL NGIAMA WA MAKANDA a.k.a.WERRASON hii ilikuwa kipindi chake cha mwanzo cha kujitawala alipotoka na album yake ya Kibuisa Mpipa kama sijakosea maana hii ilikuwa ni Bonus Truck. Wakati huo bado akiwa na wataalamu wake kama akina Ferre na bado hajakimbiwa na wanamuziki wengi ambao kwa sasa wanatamba sana.

Wimbo huu aliuimba kwa mahadhi ya Congo Rhumba, mdau wanguHadj le Jbnique (Mnazi mkubwa sana wa JB Mpiana)  ye alinikumbusha mbali sana kuwa album hii ilipikwa na mtaalamu wa Congo Rhumba ajulikanaye kama L.NZIMBI ikumbukwe kuwa huyu ndiye mpishi wa albamu ambayo mpaka leo inauza ya FEUX DE L’AMOUR” yakwake Jemedari SOUVERAIN LEADEUR YA BA WENGEE JB Mpiana ambayo aliitoa kama solo enzi kundi la Wenge Musica BCBG halijaparanganyika.

Huu ni moja ya nyimbo ambazo mimi binafsi Werasson amenifurahisha na kama ningepata nafasi ya kukutana naye na kumshauri ningemshauri a stick kwenye nyimbo hizi za taratibu kama unataka kuamini tafuta kitu inaitwa Blandine, Kiukweli hakuna mtu wa muziki anaweza kukisikiliza kitu BLANDINE asifurahi,pale kazi ilifanywa na ikafanyika,vichwa vyenyewe wmmm wakati huo vilikuwa vinatisha,maanake ulikuwa ni mkusanyiko wa vocals za FERRE GOLA,pia kulikua na JDT,alikuwapo ADJANI,AIMELIA LIAS “DEMINGONGO”,BEBEE NDOMBE na SERGE MABIALA.Pia nakiri mzee mzima LE ROI DE LA FORRET WERRASON alifanya vizuri sana katika album nzima kiujumla lazima tuwe fair katika hilo na kufanya vizuri huko mimi binafsi nashawishika kuamini kwamba kulitokana na kwamba alitulia kwa muda kuitayarisha ndio maaana ikatoka na ubora ule,sio siku hizi kila kukicha album mpya.

 

Wakati huo wa Kibuisa Mpipa, huu ni wimbo ambao huku kwetu hauku heat lakini ni moja ya nyimbo ambazo nazipenda sana kwa Wesasson, Pia kuna vitu kama Koffi Ayiana ambacho niliwahi kukiandikia pia siku za nyuma. Kwa ufupi angalia nyimbo zinazombeba zaidi Werasson ni nyimbo hizi za taratibu zenye mahadhi ya Congo Rhumba ambayo Mkongwe JB Mpiana ni champion kwenye hizo najua ma werasonique mtabisha kwa hili lakini ni wazi na halipingiki.

Truck hii hii ni maalum kwa Werasonique wooote Sadiq Tiger, Papaa Maendeka, Boss Chizenga, Moto Mkubwa Halid Mmanzi, Mdau wangu Steven na wapenzi wote wa Blog hii, Mukubwa Hadji Heshima kwako kiongozi na mnazi wa Wenge


Cheka Kispoti; Obama na Ellen wakiondoka Malewa

April 23, 2013

Angalia jinsi mwanamama wa kizungu alivyokuwa akirudi Bolingo hapo sambamba na Baraka Obama Rais wa Marekani, hahahaha amakweli Malewa Kiboko.


Detresse toka Magie ya Koffi Olomide

April 23, 2013

Ni kipindi ambacho Mwanamuziki Koffi Olomide alisemwa kuwahi kuwa na timu nzuri mnoo, kwangu mimi hii ndio ilikuwa Dream Team ambapo watu kama akina Suzuki 4×4 walikuwepo, akina Willy Bulla ambaye kiukweli binafsi nilimpenda sanaaa.

wiki ijayo Inshallah tutajaribu kudadavua kwa undani nini kilipelekea mpaka hii timu ikapanguka na waliondoka walienda wapi na kwa nini waliondoka. yote hayo utayapata hapa hapa Spoti na Starehe. Hii ni kufuatia mazungumzo na mmoja wa wanamuziki wa Koffi alipofanya ziara hapa, aliongea mu kilingala sana ilibidi kutafuta mtu wa kufanya tafsiri ili tusije potosha maana.

Naomba nikuache na kibao Detresse ukijikumbusha the Dream Team ya Quartier Latin ya wakati huo.


%d bloggers like this: