Nionavyo mimi: Akina TID wako wengi

July 25, 2008

Habari za kuwekwa ndani kwa mwanamuziki Khalid Mohammed AKA TID wiki hii zimewastua wengi hasa wapenzi wa muziki nchini na nje ya nchi kwa ujumla. Hii inatokana na comments ambazo zimekuwa zikiwekwa kwenye blog mbalimbali zilizoweka habari za mwanamuziki huyu. Ikumbukwe TID alihukumiwa kwenda Jela baada ya kumuumiza kijana mwenzie wakiwa katika ulevi wa pombe.

Sio kama natetea au nataka kulaumu maamuzi ya chombo cha dola au wale wanaomuhurumia la hasha, lakini ninachotaka kusema huu ndio utaratibu wa kawaida na hukumu za kawaida za kimahakama kwa maisha ya watanzania walio wengi. Kuna watu ambao kwa kiasi kikubwa wamelaumu kitendo cha hakimu cha kumhukumu TID kutumikia mwaka mmoja jela kwa kosa la kumuumiza mtu, kosa ambalo kimsingi wangeweza kulimaliza nje ya mahakama au kama ni hukumu wengi walitegemea kuwa angelipishwa fine, kwa vile kosa hili huchukuliwa kiwepesi hata watu wengi hawakujua kama TID ana kesi ila walistukia wakisoma vichwa vya habari TID aswekwa rumande, au TID atupwa Segerea na vingine vinavofanana na hivyo, Wapo walioko ndani na ni hukumu hata ya miaka miwili au mitatu kwa kosa la kuiba kuku, haya yote tunayasoma kwenye magazeti ya jioni (Dar Leo na Alasili) ambayo ni maarufu kwa kuandika kesi kama hizi. Kwa vile hawa hatuwafahamu huwa tunasoma kama story na kupita na kwa kuwa huyu tunamjua basi imemstua kila mmoja wetu. Ninachotaka kusema ni kesi nyingi za watu kama hawa wanatumikia vifungo na wengine kufia jela au kutoka na magonjwa ya kuuambukizwa kwa sababu ya makosa kama haya ya akina TID au tuseme makosa ya wizi wa Kuku.

Utaratibu wa kuitumikia jamii

Mwaka 2006 mwanzoni Nikiwa mwanafunzi huku Singapore nilivunja sheria ya barabarani na kugeuza gari kwenye traffic lights (Uturn) kosa lile lilirekodiwa kwenye video ya polisi jioni kurudi nyumbani nilikuta karatasi ya fine (huku wanaita Denda) ikinitaka kuripoti kwenye kitengo cha Polisi Jamii ( Singapore Westland Police Station) nilipofika nilionyeshwa kosa langu na kusomewa shtaka papo hapo, kisha nilitakiwa kuchagua adhabu ya kwanza ikiwa ni kuendesha gari la kumwagilia maua kwa wiki 3, Pili kufanya usafi Hospitali ya serkali (Singapore University Hospital), tatu Kufanya kazi za kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima, hizi zote ni kwa wiki tatu na unatakiwa kufanya masaa 12 kwa wiki, hivyo utapanga mwenyewe utafanya masaa mangapi kwa siku. Hii inafanya wewe kwa vile umekosa unaitumikia jamii na utakuwa huru nyumbani kwako. na kama utakaidi hili basi kifuatacho ni jela na kazi ngumu.

Hapa tunajifunza nini? Kimsingi kwa kosa la TID na wengine wenye makosa kama yake kwa kuwaweka jela ni kumaliza hela ya serikali bure kwani atahitajika kulishwa na hii ni nguvu kazi ambayo unaiweka ndani kwa mwaka mzima. Inasemwa hakuamini aliposomewa shtaka kwani alitarajia atasomewa hukumu kwa kutakiwa kulipa fine au kwenda jela au vyote viwili, hii inatoa mwanya kutunisha mfuko wa serikali kwa fine zinazokusanywa. Kwa nini tusitatumie hawa watu kufanya shughuli za kijamii kutokana na kipaji au ujuzi ulionao, nadhani hili lingemanya mtu ajifunze zaidi kwani kwa kumuona TID akifagia Muhimbili kungefanya wengine waogope makosa madogo madogo na kujifunza zaidi.

Binafsi napinga kuwapeleka jela watu wenye makosa kama ya TID. Ni kutumia pesa ya Kuwepo kwa kitengo cha polishi shirikishi au polisi jamii kunaifanya vyombo vya dola kufanya kazi karibu zaidi na jamii na kuifanya jamii kuona ni sehemu ya majukumu yao. Hii inasaidia kupunguza makosa madogo madogo katika jamii pia. Leo tunasoma kwenye gazeti moja la kila wiki kuwa wababe wa gereza walifurahia kumpokea TID gerezani wakiahidi kumfanyia kitu mbaya akiwa huko ili akitoka akahadithie, Je unafikiri kama atafanyiwa kitu mbaya huyu mtu akitoka utakuwa umemsadia au ndio umemharibu kabisa? itamfanya mtu kuwa na visasi zaidi au na roho mbaya zaidi na kufikiria ni jinsi gani na yeye atamlipizia aliyesababisha haya yote. Kwa njia moja au nyingine yapasa tuwe na njia mbadala kwa makosa akama haya. Ni mtazamo tu wadau.

Nakuacha na kibao nilikataa cha Top Band TID akimshirikisha Mr Blue na Q Chilla.


TID aswekwa Segerea!

July 23, 2008
TID

TID

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D jana amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.
T.I.D mwenye umri wa miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya wilaya ya Kinondoni baada ya Hakimu huyo kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashtaka.
katika utetezi wake TID aliiomba mahakama imhurumie kwani alitenda kosa hilo sababu ya ulevi na kuwa familia yake inamtegemea hasa mama yake.
Hata hivyo Hakimu Kalombola alitoa hukumu hiyo kwa kumwambia mshtakiwa “kwa vile huwezi kujimudu ukilewa na huwezi kujizuia kunywa na kuhukumu uende jela mwaka mmoja ujifunze ili usiwe unakunywa hizo pombe” Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: