Malaika hawa wanahitaji Msaada wako

September 7, 2011

image

Familia ya bw na bibi Edwin Dosantos wakazi wa kimara jijini dar es salaam,wanahitaji msaada wa hali na mali kuweza kuwalea watoto wao mapacha watatu..walio na umri wa miezi 2.msaada unaohitajika zaidi ni MAZIWA AINA YA LACTOGEN namba 1. AU PESA TASLIMU..Kwa sasa wazazi wa watoto hawa hawana kipato chochote hali ilio walazimu kuomba msaada..kwa mawasiliano 0719909085 AU O654 336459.

Unaweza kutumia huduma ya TIGO PESA  au acc no 01000038882 EDWIN SANTOS MBAKIZAO. benki ya posta


Werrason akimbiwa na wanamuziki watatu

September 7, 2011

Mwanamuziki Ngiama Makanda anazidi kupata pigo baada ya kukimbiwa na mwanamuziki wake Fabregas, Miel na Heritier Watanabe. Awali Werrason alikanusha habari hizi akidai kuwa Heritier ni mgonjwa na Miel pamoja na Fabregas wanamuuguza huko ulaya jambo lililopelekea wadadisi kuhoji sana kwani si kawaida wakati WMMM wanasubiriwa kwenye show kubwa ya FIKIN ambayo wanamuziki hawa tegemezi lazima wawepo.

Kwa mujibu wa habari zilizomo kwenye mitandao maarufu wa Digital Congo ni kuwa sasa imebainika Fabregas ameondoka na Heritier pia hii ni kufuatia ugomvi wake na Mwanamuziki mwenzie ajulikanaye kama Tadhe baada ya Heritier kutoa wimbo wake wa Con­fession intime. Tutawaletea habari zaidi lakini kwa sasa habari ndio hiyo.


Wazee wa Ngwasuma wakikamua…

September 7, 2011

image

Wazee wa Ngwasuma, kutoka kushoto, Patchou Mwamba ‘Tajiri’, Mohamed Kingombe ‘King Blaise’ na Muleziri Boyange ‘Mulemule’ wakikamua. Patchou Mwamba kijana anayekuja juu sana kwenye ulimwengu wa Movie mpaka anawatisha mashabiki wake wa Muziki kuwa anaweza kubobea zaidi kwenye Movie na  kuachana na Muziki. Patchou niliongea naye anasema ataendelea kukamua kote kote na kwa mashabiki wa Muziki anakuja na kitu si cha mchezo.


Wanamuziki Congo watamuunga tena mkono Kabila mwaka huu?

September 7, 2011

Mwaka juzi kulikuwa na habari toka Congo ya kuhusu Serikali kupinga wanamuziki wa huko kuwataja wanasiasa kwenye nyimbo zao,

Hii imekuja baada ya fujo kuzuka kwenye baadhi ya majukwaa ya burudani kufuatia watu kuvutana kwa hisia za kisiasa na pia serikali haikuongelea sana bali wajuvi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema ni katika kuleta nidhamu na kuitakasa sura ya serikali kwa jamii. Muziki unanafasi kubwa sana kwa Congo kwani ni moja ya burudani ambazo zina ushabiki kama ulivyo wa mpira sehemu nyingine na unakusanya watu wengi, hivyo basi nguvu yake kwa umma ni kubwa.

Wimbo huu hapo juu ulipigwa na JB Mpiana wakati wa kampeni iliyomrudisha Joseph Kabila Madarakani. Kwa hiyo hata Rais asiimbwe tena?

Humu utamsikia JB Mpiana, utamsikia Rio, Caludji na wengineo katika Rhumba hii kwa ajili ya kampeni ya Kabila, Mwaka huu Kabila anakutana na Chuma tiene Tisekedi ambaye naye amejizolea umaarufu na anaonyesha kutoa upinzani kwa Kabila hasa.

Katika uchaguzi uliopita Kabila aliungwa mkono na wanamuziki wengi akiwamo Adolph Dominguez, Tshala Muana, Reddy Amis, Emeneya, Mbilia Bell na wengineo wengi.

Miaka ya karibuni  ilishuhudia mwanamuziki Koffi Charles Olomide akiingia matatizoni na serikali baada ya kutoa wimbo wenye muelekeo wa kisiasa, Wimbo huo uliojulikana kama Musouksouk ukiwa unaongelea mpasuko na msukosuko wa kiasiasa unavyoipeleka Congo Mrama. Mpasuko huo ulikuwa kati ya Kabila Upande umoja, Jean Pierre Bemba Gombo ambaye kwa wakati huo alikuwa mmoja wa Makamu wanne wa Uraisi huko Congo, Mbaye mwaka 2006 kwenye uchaguzi alipata Kura nyingi akiwa ni wa pili baada ya Raisi Kabila.


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – V

September 7, 2011

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya

 

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi. Ikafanya official show yake ikiendelea kutumia jina la WENGE MUSICA BCBG 4X4, Lakini baadae wakaachana na neno BCBG kwa kuwa lililetwa na kuwa introduced hapo WENGE MUSICA original enzi hizi na Jb Mpiana, Badala yake wakaweka la kwao “MAISON MERE” hivyo ikawa sasa wao ni WENGE MUSICA lakini MAISON MERE sio tena BCBG. Wenge Maison Mere maana yake wakimaanisha Wenge yao ndio Wenge Mama au Wenge Makao makuu ikiwa na makao yake makuu ZAMBA PLAYA ndani ya Kinshasa.

Je hilo jina MAISON MERE lilibuniwa na nani? alikua ni Werrason? jibu hapana, alikua ni Didier Masela? jibu hapana, je alikua Tata Mobitch Adolphe Dominguez? jibu pia hapana. Ukweli ni kwamba jina Maison Mere lilibuniwa na kupendekezwa na Baby Ndombe! Hilo ndio jibu sahihi.

Tukiacha hilo la jina bendi ilianza Rais akiwa Adolphe Dominguez huku Werra de la Forre akiwa makamu wa rais na artistic director pia, Didier Masela akiwa Chef d’orchestre. Baadae  ya muda kidogo ikaonekana Werra ndio awe rais kutokana nadhani na mvuto wake kwa mashabiki ambao tayari walikwishaanza kumshindanisha na Jb Mpiana wa Bcbg. Wakati huo huo JAPONAIS ambae alijiunga akitokea kwa Jb mpiana akapewa cheo cha artistic director alichokuwa nacho Werra akiwa pia makamu wa rais wa bendi.Na maandalizi ya album yao ya kwanza ile FORCE INTERVENTION RAPIDE yakawa yamekamilika, wakairelease hiyo album huku dogo FERRE GOLA akipewa aimbe vocals za Jb Mpiana.

Hapa muhimu kukumbuka kwamba album ya TITANIC ya BCBG Kiukweli ilikua imetayarishwa kwa pamoja na iliyokuwa wenge musica original kwa maana ya kwamba pia kina werrason walishiriki maandalizi ya album hiyo na walishaifanyia mazoezi na pia kupiga show. Kama utatazama nakusikiliza vizuri video hiyo hapo chini ambayo ni moja kati ya live concert za mwisho mwisho za wenge musica original ikiwa pamoja utaweza kusikia mipigo iliyokuja kusikika kwenye titanic baadae, hapa ilichezwa na kina werrason ndani ya wenge original, ukisikiliza vizuri mwishoni mwishoni mwa hii video utausikia mpini ambao baadae ulikuja kusikika kwenye wimbo wa borkinafaso uitwao Serge Palmi unaopatikana kwenye album ya Titanic, hapa Burkinafaso alikuwa anawachezesha kina Werrason huo mpini wake wa solo ambao baadae waliucheza kina Jb kwenye titanic.

 

Kuibuka kwa Bill Clinton

Kwa hiyo kiufupi ni kwamba album ya titanic ilikua iwe album ya wenge musica original ikiifuatia pentagone ambayo ndio album ya mwisho ya wenge musica original kama kundi. Tukiachana na hayo, mwaka 1999 mwimbaji kijana Heritier Bondongo akajiunga na maison mere then wakafanya album yao ya pili wakiita SOLO LA BIEN ambayo kiukweli ilipata mafanikio makubwa sana sokoni huku ikimuibua pia BILL CLINTON na kumfanya awe kipenzi cha mashabiki katika ulimwengu wa wapenzi wa muziki wa Congo kutokana na kazi yake nzuri na style yake ya kipekee ya atalaku aliyokuja nayo ambayo naweza kusema ndio iliyomtoa Tutu Kaludji sokoni na style yake iliyokuwa imekamata sana kabla ya ujio wa BILL CLINTON na pia baada ya kung’atuka Roberto Ekokota kwenye muziki.

Album hiyo pia ikafungua milango kwa maison mere kuanza kupata mikataba minono ya kwenda kupiga shows ulaya ambako walifanikiwa kumrecruit mpiga guitar kiraka PATIENT KUSANGILA ambae kina werra walikua nae wenge musica original lakini alibaki kwa Jb baada ya mgawanyiko lakini baada ya muda mfupi akamtosa Jb baada ya concert ya bcbg kule zenith 1999 baada ya kupewa nafasi finyu ya kupiga guitar kwenye show hiyo kama tulivyoona huko nyuma katika mfululizo wa makala haya. Baada ya kuachana na JB kusangila alibaki Paris akiishi huko ndipo kina werra walipoenda na maison mere wakamkuta na kumshawishi ajiunge nao.

 

Mimiche amrithi Masela kwenye Bass Guitar

imageMambo yakaendelea, wakiendelea kupata kazi nyingi ndani na nje ya africa, badae wakiwa katika tour nyingine Canada CHRISTIAN MABANGA ambae alikua amerithi nafasi ya  DIDIER MASELA (aliyekua amejiondoa kundini baada ya tour ya ulaya) kama Chef d’orchestre akaugua ghafla ikabidi abaki Canada kwa matibabu zaidi, ndipo Ferre Gola akapewa nafasi hiyo, akawa Chef d’Orchestre na wakarelease album ya TERRAIN EZA MINE ikiwa ni album ya tatu ya kundi kabla ya album binafsi ya werrason, ile KIBUISA MPIPA. Baada ya Masela kuondoka kundini ikabidi waanze mpango wa kumsaka mrithi wake katika bass guitar, ndipo wakampata MIMICHE kutoka kwenye bendi ya PEPE KALLE 

 

Patient Kusangira ajitoa WMMM 

Then wakapata deal nyingine ya kusafiri kwenda kupiga paris, lakini kabla ya kuelekea paris walitakiwa kupitia  Congo Brazaville kwanza, wakiwa katika pilikapilika za maandalizi ya safari hiyo, ndipo KUSANGILA akaachana na Maison Mere kutokana na jina lake kuondolewa katika kikosi kitakachosafiri kuelekea Brazzaville na baadae Paris, kitendo ambacho kilionekana na wengi akiwemo Kusangila mwenyewe kama ni adhabu ya kisasi toka kwa werrason kutokana na ugomvi wao wa siku nyingi toka Wenge Musica original uliosababishwa na mwanamama mchezo show pekee wa wenge musica original kipindi hicho NANA SUKALI.

image

Ikumbukwe kuwa Werre alishawahi kufanya jaribio la kumfukuza Kusangila wenge original lakini Jb na viongozi wengine kundini hawakukubaliana na adhabu hiyo kali dhidi ya Kusangila kwa kuwa walikuwa wakifahamu kinachoendelea kati ya watatu hao kundini yani Werra, Kusangila na Nana Sukali, hivyo ikaonekana ni wivu wa kimapenzi tu na badala yake wakapendekeza asimamishwe tu na si kufukuzwa kabisa, hivyo kitendo hiki cha kuachwa katika safari ya ulaya bila ya sababu za msingi kikatafsiriwa na wanaojua historia ya wawili hawa werra na kusangila kama ni muendelezo tu wa ugomvi wao wa siku nyingi sababu ya mwana mama Nana sukali. Pia werra aliwahi kufanya jaribio la kumtimua Tutu Kaludji kwa kutomuheshimu yeye Werra kama kiongozi na badala yake kumheshimu zaidi Jb na Viongozi wengine kundini.

 

WMMM yafanya Show ya Bercy na Aimelia Lyase atambulishwa rasmi kwa mashabiki.

Baada ya kujiondoa Maison Mere Kusangila kwa msaada wa marafiki zake Sam Tshintu na Modogo akarudi zake Paris. Kwa upande wa bendi ya Maison Mere baada ya kumaliza kazi Brazaville wakachukua zao flight kuelekea Paris, na kupiga ndani ya BERCY Show yenye mafanikio makubwa sana na isiyosahaulika miongoni mwa wapenzi wa maison mere, watu walijaa kupita kiasi na ndipo Werra alipopachikwa jina la Le PHENOMENA na Pia ndio siku werra alipomtambulisha Aimelia Lyase Demingongo kama mwanamuziki mpya wa Maison Mere akitokea kwa mahasimu wao wakuu wenge bcbg.

 

Dominguez ajitoa WMMM

image

Pichani ni Dominguez alipiokuja nchini, hapa akibadilishana namba na Steven Kanumba wa Bongo Movie

Baadae mwaka 2001 “Big Tata” Adolphe Dominguez nae akajitoa, bendi sasa ikawa ya Werrason peke yake.Kwa upande mwingine   mwanamuziki “mtata” na mzee wa kuhamahama Ali Mbonda akatimka Maison Mere na kurudi bcbg na baadae mwishoni mwa 2001 akarudi tena Maison Mere, JAPONAIS nae akaondolewa kwenye nafasi kama Artistic Director, nafasi yake ikachukuliwa na fundi, mtaalam wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya.

Next kuzaliwa kwa Le Marqius de Maison Mere, nini chanzo cha vijana kufanya uasi huo na kwa nini hawakufanikiwa licha ya kuanza kwa kishindo?, tutajua zaidi.

Natuma salamu kwa Bana Werason wote Mukulu Timothy Banda shukrani sana kwako kwa mchango wako kwenye blog hii, La Suvereign Maghambo, Mukubwa Chizenga, Muddy Saloon, Choki na Nelly nakati ya Kinondoni, Japhet Malya muzee wa Koffi na WMMM, Abdul Tall na wapenzi wote wa Werason.


JB Mpiana na Werrason Ngiama ndani ya Congo Rhumba; Nani zaidi?

September 7, 2011

JB Mpiana na Werra

Werrason na JB katika Video zao mpya.

Na The Romantic

Hapa leo tuna video za nyimbo mbili za mafahali wawili, Ya kwanza ni video ya wimbo Bologna ambao Jb amemtungia rafiki yake aitwae Patric Bologna, wimbo huu upo kwenye album mpya ya Jb na Bcbg iitwayo Sayons Serieux ambayo imeingia sokoni na video ya pili ni wimbo Likambo wa werrason ambao unapatikana kwenye album yake mpya Malewa Part 2.

Kitu kizuri hapa ni kwamba wote wamezipiga nyimbo hizo katika mtindo wa taratibu wa  Congo rhumba ambazo mara nyingi ndio zimekua anga za Jb, Werra this time kasema hapana na mimi nitafanya Congo Rhumba ili wale wanaosema siwezi waone, Kama kawaida mdau kazi yako hapo ni rahisi tu, zitazame  hizo video na toa maoni yako. Mimi binafsi ni mpenzi wa sports cars, hayo magari waliyotumia hawa waungwana wawili sio siri nimeyakubali,vjapo siwezi kusema la nani ndio limenikuna zaidi lakini lipo moja nimelipenda zaidi, kwa sasa na reseve comments zangu kidogo.

Bologna ya JB Mpiana

 

Mzee mzima Igwe katika album yake mpya akaja na kitu hii hapa

Likambo ya Werrason in Congo Rhumba

Arsenal yapata pigo Vermaelen aumia tena

September 6, 2011

Mlinzi wa kati wa Arsenal Thomas Vermaelen hatacheza soka kwa muda unaokisiwa mwezi mmoja baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kifundo cha mguu wake wa kushoto.

Thomas Vermaelen

Thomas Vermaelen

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 aliumia wakati wa mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Udinese.

Ni pigo jingine kwa Gunners, ambayo imeuanza msimu kwa kuchechemea na hivi karibuni mchezaji mwengine Jack Wilshere ameumia na hatacheza soka kwa miezi mitatu kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu.

Vermaelen msimu mzima uliopita hakucheza kutokana na kuumia kifundo cha mguu mwengine, ambao pia ulifanyiwa upasuaji.

“Haya ni matibabu yanayofanana na aliyopata katika kifundo cha mguu wa kuume mwezi wa Januari mwaka huu na hayahusiani na kuumia kwake kwa msimu uliopita,” taarifa ya Arsenal ilifahamisha zaidi.

“Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mashauriano na daktari bingwa aliyeshauri afanyiwe upasuaji kuzuia tatizo lisiwe la kudumu.”

Vermaelen aliumia wakati Arsenal ilipoishinda udinese mabao 2-1 tarehe 24 mwezi wa Agosti na klabu hiyo ilikuwa na matumaini asingehitajika kufanyiwa upasuaji.

Lakini alipasuliwa mjini Stockholm siku ya Jumatatu na sasa atakosa mechi dhidi ya Swansea, Borussia Dortmund, Blackburn, Shrewsbury, Bolton, Olympiakos na Tottenham.

Mlinzi huyo wa zamani wa Ajax hakucheza tarehe 28 mwezi wa Agosti siku Arsenal ilipoadhiriwa na Manchester United kwa kutandikwa mabao 8-2, lakini licha ya kukosa mechi hiyo msimu huu amecheza karibu mechi zote za Arsenalde.

Per Mertesacker, aliyejisajili na Arsenal muda mfupi kabla ya kufungwa dirisha la usajili, huenda akaitwa haraka kuziba pengo la Vermaelen, wakati walinzi wengine wa kati Laurent Koscielny, Johan Djourou na Sebastien Squillaci huenda mmoja wao akawa matumaini ya Arsene Wenger kwenye safu ya ulinzi.

Arsenal msimu huu imeshafungwa mabao 11 na hadi sasa inashikilia nafasi ya 17 ya msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi moja tu baada ya mechi tatu.


Sayons serieux vs Malewa 2 Generiques

September 6, 2011

Leo hapa tuna video mbili ambazo ni generique  zinazopatikana katika album mbili mpya za mafahali wawili katika muziki wa congo,Tunayo video ya sayons serieux ambayo ni album mpya ya wenge bcbg ya kwake JB MPIANA kwa upande mmoja na tunayo video ya techo malewa 2 ambayo ni album ya wenge maison mere ya kwake Le Roi De La Foret Werrason,mdau unaombwa kuzitzama vizuri generique hizi mbili halafu utuambie wewe kwa maoni yako nani amefanya vizuri kuliko mwenzake kwenye video hizi mbili? Mapenzi binafsi unaweza kuyaweka pembeni kidogo ili uwe fair.

Baada ya kuzitazama generique hizi,tutaanza pia kutazama nyingi moja moja za Wenyewe Jb na Werra na pia zilizotungwa na vijana wao zilizomo kwenye album mbili hizi,mwisho tutajua nani amefanya vizuri zaidi ya mwenzake,je ni JB na sayons serieux yake ama Werrason na Malewa 2 yake?tutajua.Kwa sasa pata video hizi mbili,then toa maoni yako.

Merci mingi kwako Mukulu The Romantic kwa kuwezesha mambo meeeengi humu ndani. Pamoko sana mukulu kwa support.

 

Kisha Peruzi na hii utoe maoni yako. Kama kawaida hapa haturuhusu lugha chafu wala hakuna kugombana si unajua muziki wenyewe unataka usmat kuanzia mavazi mpaka mambo fulani.


sayons serieux sokoni

September 6, 2011

Habari njema kwa wapenzi wa wenge bcbg,mzigo wa DVD ya Sayons serieux umeingia sokoni,kazi kwenu wadau kupita katika maduka ya muziki kuilizia hiyo DVD,habari za kuasisimua ni kwamba zimetoka kwa pamoja na album ya wenge Maiso Mere Malewa No.2. Nani atafunika kwenye mauzo? tutajua. sio siri jb sasa ame improve kwenye video.


Hongera kaka Venture

September 6, 2011

314895_282121711801192_100000100973443_1333217_3124147_n

Kila la Heri DJ Venture katika maisha yako mapya ya ndoa, Mungu wajalie muweze kuwa na ndoa yenye amani na furaha tele.


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – IV

September 4, 2011

Kuzaliwa Kwa Wenge Musica Maison Merre (WMMM) na miaka yake mitatu ya Mwanzo

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko kadhaa leo tunaitazama Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, shukrani za kipekee ziwaendee watu hawa wafuatao kwa kufanikisha kuisimamisha Wenge Maison Mere kwa namna moja ama nyingine:

Wa kwanza ni mtu mmoja anaitwa Sankara De Kunta, huyu mtu alijitoa sana kuwasaidia kina Werrason kujijenga,jamaa alikua na kazi moja tu, kuwachafua Jb mpiana na Koffi Olomide na kumpandisha na Kumsifia Werrason, na kwa kweli alifanikiwa sana, jamaa alikua na vituko huyu hapa nafasi haitoshi, lakini aliipromote sana maison mere na hasa werrason binafsi, ilifikia wakati Tata Sankara ambae awali alikua mnazi mkubwa wa Adolphe Dominguez tangu enzi za wenge musica original alikua akipita mitaani huku akiimba Balingaki Baboma Werra eeeeh! akimaanisha wanataka kumuua werra, akiwataja mahasimu wa Werrason,alikua akiimba kwa style ya aina yake kiasi cha kuwafanya wengi wamuonee huruma sana Werrason wakidhani pengine ni kweli Werrason yuko hatarini kuuwawa kumbe ulikua usanii wa Tata Sankara.

image

Mtu mwingine nyuma ya mafanikio ya mwanzo mwanzo ya maison mere ni Zackarie Bababaswe, yeye pia alisaidia sana kuwa promote maison merre kupitia shows zake mbalimbali lakini na yeye pia akiitumia nafasi hiyo hiyo kutengeneza pesa binafsi, si unajua tena strategy maarufu ya “helping the weaker to overcome the stronger” halafu baadae na wewe unanufaika na hiyo strongness ya uliemsaidia.

Pia mtu mwingine aliewasaidia sana kina Werra kujijenga maison mere ni kiongozi wa wenge el paris Marie Paul, huyu aliwasaidia kutokana na connection yake na Werrason binafsi. Werra na Marie Paul wanatoka kijiji kimoja, pamoja na Reddy Amisi, pamoja na King Kester, lakini kwa sasa Werrason na hawa ndugu zake hawaongei wala kusalimiana, hali ya mahusiano miongoni mwao imekua ikilegalega kadri siku zinvyosonga mbele hasa kati ya Werrason na Marie Paul kiasi cha Marie Paul kutohudhuria hata mazishi ya baba yake Werrason miezi michache iliyopita. Msaada mkubwa ambao Marie Paul aliipatia maison mere kutokana na connection yake na werrason ni kuwaambia mashabiki wake na Wenge El Paris kiujumla wote wampe support Werrason na bendi yake na pia akawapa Maison Mere wanamuziki wake wawili, JDT Mulopwe na Manda Shante ambae baadae alijitoa hata hivyo (Kwa wasiomjua Manda Chante ni yule mwenye sauti kali kweli wimbo wa Kalay Boing wa Wenge Musica BCBG enzi hizo.

 

Wera na madai ya Nguvu za giza.

Pia habari za chini ya kapeti zinasema Marie Paul pia alimpa Werrason “Nguvu Zake” ambazo zinaelezwa kuwa ndio chanzo cha chuki za hali ya juu miongoni mwa watu hawa kutoka kijiji kimoja, kwani inaelezwa kuwa Werra badae hakurudisha “nguvu” hizo alizopewa kama walivyokubaliana,hapa sitaki kuingia sana lakini kwa congo hayo ni mambo ya kawaida sana. Kwa mnaoelewa Lingala mkisikiliza vizuri hapo chini kwenye video hiyo mtamsikia mwenyewe Marie Paul akiyaelezea hayo mambo ya “nguvu zake” anazozililia kwa Werrason, alijaribu kukwepa kwepa lakini mtangazaji akambana kwenye kona mpaka akafunguka. Msikilize mwenyewe hapo “Le Roi Pele” Marie  Paul anavyosema

Msikilize Marie Paul akiongelea mambo kadha wa kadhaa humu

Inasemekana nguvu hizo zinatoka kijijini kwao tu ,zilimtoa King Kester enzi zile za “kidengune”nadhani wengi mnakumbuka alivyotamba, baadae Reddy Amisi nae akazitumia, halafu ikaja zamu ya Marie Paul nae ndio akampa Werrason.

Tukiacha mazungumzo hayo baada ya habari,sasa tuende moja kwa moja kutazama zoezi la kusaka wanamuziki kwa ajili ya kuisuka Maison Mere,nani alikua wa kwanza,nani alifuatia na waliwatoa wapi hao wanamuziki twende pamoja.

 

FERRE ajiunga na WMMM akiwa ni Mwanamuziki wa Kwanza kuwa Recruited

Kutokana na wanamuziki wengi wa WENGE MUZIKA 4X4 TOUT TERRAIN kuondoka na Kumfuata Jb Mpiana kama tulivyoona huko nyuma,Werrason,Didier Masela na Adolphe Dominguez wakatakiwa kujipanga upya kwa kusaka watoto wa congo wenye vipaji vya muziki waweze kuwa recruit,kazi haikua rahisi pia,kwanza walianza na Ferre Gola ambae alikua ana hang tu baada baada ya kukimbizwa na Aimelia Lyase “Demingongo” kule Bcbg,hivyo na yeye akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kujiunga maison mere baada ya waanzilishi hao watatu Werra, Masela na Adolphe.

Vita Imana ni moja ya Tungo HAI za Ferre Gola ndani ya WMMM inayotamba mpaka wa Leo. Wimbo huu Uliimbwa tena akiwa kivyake.

 

Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya wajaribiwa WMMM

Kutoka hapo official recruitment ikawa imeanza, baada ya Ferre ku join kundini mwanamuziki aliyefuatia kujiunga na maison mere ni Bob Lorenzo, baadae akaja JDT kama tulivyoona huko nyuma kwamba aliletwa na Marie Paul kutoka kwenye bendi yake ya wenge el paris ili kumsaidia home boy wake Werrason, halafu akaja Baby Ndombe alipitia kwenye mchujo na alifaulu kwa upande wa uimbaji na alifaulu majaribio pia kama mpiga bass, baadae tena rafiki wa siku nyingi wa werra toka enzi za wenge musica ambae pia alikua mdau mkubwa wa wenge muzica enzi hizo WASENGA KIMPUNI akawaleta vijana kadhaa kutoka BANDAL (wenge musica home town), vijana hao ni huyu Fally Ipupa Celeo na Mtaalamu wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya ambao walikua wanapiga bendi moja ya mtaani huko Bandal, baada ya hapo akaja mpiga drums Maradona (the second ever true drummer wa iliyokuwa wenge musica original) ambae walijiunga maison mere kipindi kimoja na Papy Kakol ambaye yeye alitoka katika group ambayo Fally Ipupa wakati fulani alikua ndio atalaku namba moja wa hiyo group kabla ya kuanza kuimba, baada ya hapo akaja kijana mmoja mwenye kipaji cha hali ya juu, kijana ambae alikua ametokea katika bendi ya JOLINO iliyokuwa chini ya uongozi wa Rio Kazadi “Rio de Janeiro” ambae kwa sasa ni muimbaji wa bcbg, pia huko JOLINO ndiko alikotokea Chai Ngenge muimbaji wa bcbg pia, kijana huyo si mwingine bali BILL CLINTON.

 

Fally Ipupa Afanya Interview WMMM

Baadae tena Adolphe Dominguez akawaleta kundini SERGE MUBIALA na DIDIER LACOSTE wote walikuja kuibeba sana maison mere kwenye safu ya uimbaji, pamoja nao Adolphe alimleta pia mpiga kinanda Thiery Synthe, baadae Adjani nae akajiunga akitokea bendi ndogo ya mtaani, then akaja mpiga rythm guitar Kojack, baada ya hapo wakawajaribu tena mamia ya vijana wa congo miongoni mwao ni atalaku Brigade na muimbaji CHOU LAY (mtoto wa EVOLOKO) Lakini bahati mbaya Chou Lay hakuchaguliwa baada ya majaji kumuona Bob Lorenzo ni bora zaidi kutokana tu mvuto wa sura yake lakini hakua muimbaji mzuri kuliko Chou Lay, mwanzo tuliona Fally Ipupa akiletwa kwenye usaili, nadhani mtakua mnajiuliza ilikuwaje, je alifeli usaili?

Jibu ni kwamba hapana, hakufeli usaili, sasa kwanini hakujiunga? jibu ni kwamba Fally alijiondoa kwenye usaili mwenyewe kutokana na kuwa na mapenzi makubwa na Quartier Latin ya Koffi Olomide bendi aliyokua akiipenda toka akiwa bado kijana mdogo na kwa mujibu wa Willy Bula (kaka yake na Blaize Bula) anasema Fally pamoja na Bouro Mpela (mdogo wa Alain Mpela) walikua wakimsumbua mara kwa mara enzi hizo wakimuomba awaunganishie wapate nafasi ya kujaribiwa Quartier Latin ya Koffi Olomide ambayo yeye Willy Bula alikua mmoja wa wanamuziki huko, Bula baadae alifanikiwa kumshawishi Koffi awajaribu wadogo zake hao lakini baada ya majaribio Bouro Mpela ndio akawa wa kwanza kufaulu majaribio na kujumuishwa kundini huku Koffi akimwambia Fally aendelee kujifua na wao QL watakuwa wanafuatilia maendeleo yake na wakati mwingine kujumuika nae mazoezini na kwenye local shows za QL, hivyo Fally akaona asije akajiaribia mipango yake na Quartier Latin kwa kujiunga na Maison Mere,ndipo akajitoa kwenye usaili, nadhani kuna watu walimshauri asifanye haraka, aisubiri QL, hivyo basi Fally hatuwezi kumuhesabu kama ex-maison mere, hakuwahi kujiunga nayo japo alijaribu.

 

image

Hii ni moja ya Albamu ambazo zimefanya vizuri sokoni

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi,nini kilifuata,tuendelee kufuatana hapa hapa siku ya jumatano ambapo tutakamilisha miaka mitatu ya WMMM na baadaye tutaangalia walivyoendelea.

Huu ni mfululizo wa Historia ya Wenge Musica na kwa kuanzia tunajaribu kuangazia kilichopelekea JB Mpiana na Werrason kutengana na miaka ya mwanzo ya bendi husiki huku tukitazama kwa kina jinsi wanamuziki walivyopatikana na walioondoka na kwa nini waliondoka. Simulizi hiizi za kusisimua kwa wapenzi na wanafamilia wa Wenge ni za pekee na zitakujia hapa hapa kwenye Blog yako ya Spoti na Starehe.

Nawaacha na Kibao Heritier Itere toka kwake Werrason Ngiama Makanda, Hiki kilikkuwa katika Albamu ya Pentagone wakati huo wakifanya kazi pamoja.

Salamu zangu za dhati kwa Werasonique woote ndani ya Blog hii nadhani mmeridhika na habari za bendi yetu ya WMMM. Shukrani a kipekee kwa Papaa Henry Kasapira nakati ya londone, Juma Mukubwa Muzee ya Air Port, Le Big Prodyuza Maghambo tuko pamoja, Papaa Julie We Ston weeee Ndenge nini papaa?, Papaa Hadji Le Becebegeeque Nambari wan!! Uko Juu Papaaa, Mamaa Tabou Fatou ya Tanzanie weeeee Kitokoooooo, Papaa Farid Wa Muscat, Mamaa Perovee, Mukubwa Shabani, Papaa Mwalimu wa Muheza Waambaze Mgoshi?,  Sadik Titanike weeee, Alain Kamangu Merci Mingi papaa, Mamaa Fatuma Mtanga tuko Pamoja Meree, Samson wa Delila karibu sana, Mke Mimi nakati ya Ujiji Chighoma, Ubeleji na wachangiaji na Wasomaji wote tuko pamoja na Asante kwa support yenu, kwa wale wanaonitumia email na kunipigia simu pamoja sana najitahidi kujibu email zenu wote.

Merci Mingi, Till then…. Kama uko kwa Facebook basi ungana na page yetu kwa kubofya join/like hapo juu kulia basi utapata habari live kwenye notifications zako kila tunapochapisha kitu kipya.

Kama unaswali au maoni tafadhali niandikie piusmicky@yahoo.co.uk au nitwangie Hotline no. +255713 666616


Msimamo wa Barclays Premier Ligi mpaka leo Tarehe 4 September 2011

September 4, 2011

image


Wajue Ma Pendejee na Mameree wanaotamba kwenye nyimbo za Bolingo.

September 4, 2011

Hii ni Compilation ya mwanadada Sophia wa Kessy na ni jibu la mdau wangu Moris wa Mererani kama ulivyoniomba nikwambia nani ni nani kwenye nyimbo za Congo, nakujibu swali lako mkuu.

Sio jambo geni kusikia majina ya watu mabali mbali yakitajwa kwenye nyimbo, angalia hapa utajua

CHIEF DIDI KINUANI LE MILLIONAIRE

Didi Kinuani a.k.a.DIKINI au ukipenda mkingereza waweza muita Didi Stone au Didi mzee wa mawe mkiswahili yeye ndio mfadhili mkubwa kwa muda mrefu wa Mahasimu wawili Le Roi De La Forret Werrason a.k.a.papaa na Exocee pamoja nae Le Rambow du Zaire a.k.a.Papaa na Didi stone Koffi Olomide, pia na wanamuziki wengine wengi kasoro Souverain Leadeur ya Ba Wengee BCBG JB MPIANA MUKULUMBA a.k.a.papaa na Daida. Kwa faida tu ya wasiojua huyu jamaa ndio aliyezaa na mke wa JB Mpiana baada ya kutengana na JB Mpiana kwa takriban miaka 7 na kuzaa naye mtoto mmoja lakini baadaye walirudiana na JB na wako wote mpaka sasa, Didi Kinuani ni mfanyi biashara mkubwa sana wa madini ya Almasi na mshirika wa karibu wa Rais Kabila pia, katika nyimbo nyingi hata za hapa nyumbani pia unaweza kumsikia amiwa ameibwa amekuwa mfano wa kuigwa huko kongo kwa kuchangia si tu secta ya muziki lakini pia hata ma hospitali na hata kufikia hatua ya kununua vyo mbo vya muziki kwa kuwagaramia na wakati mwingine kuwasafirisha wanamuziki wa kongo barani ulaya na kuwatangaza kupitia kampuni yake ya group de kin.

 

ZADIO CONGOLE aka ZK aka ZADIO BEECEEBEEGEEQUE

Zadio Congole, huyu pia ni ‘mpigaji” ambaye alifaikiwa kupata pesa anaishi huko Ubelgiji (shengheni kwa ujumla) na ni mshabiki mkubwa wa JB Mpiana ambaye kwa kiasi kikubwa amejitolea pesa na muda katika bendi hii, Zadio ndiye mfadhili mkubwa wa show za JB Mpiana na amejizolea umaarufu kupitia muziki huku JB akiwa ameshamtungia nyimbo takribani tatu mpaka sasa huku wimbo wa Zadio au ZK ambao unapatikana kwenye album ya Quel Est Ton Probleme.

 

TABOU FATOU aka TABOU FATOU TOP MODELLE

Mwanamuziki Faustin Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa Di Caprio, Album yake ya “Droit Chemin” ndiyo Album bora ya Mwaka 2007/2008, Albamu hiyo  iliuza sana takribani miaka miwili mizima. katika Album hiyo kuna wimbo unaitwa “Liputa” kwenye huo wimbo amededicate kwa Taboo Fatou ” Mama na Compressor”(pichani), huyu ni Mfanyabiashara Mrembo anaishi Belgium, ana miliki maduka kadhaa ya Nguo huko Paris(France) na Beligium,na inasemekana zile Pamba zote za Fally, Taboo Fatou ndiyo anamvalisha, kwa wale wapenzi wa JB Mpiana watumbuka katika Album yake ya Kwanza(Solo) Feux D’Lamour,kuna wimbo unaitwa “Top Model” utampata humo Tabu Fatou.

 

MERE MALOU “MADAME YA POTO”

Marehemu Mama Mere Malou akiwa na Papa Wemba enzi hizo, Hawa waliwahi kuwa wapenzi.

Pichani juu ni Marehemu Mama Mere Malou “madame ya poto“ akiwa na Papa wemba enzi hizooo Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa, Pia Mere Malou ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mwanamuziki  Wemba.

Mere Malou a.k.a.Nanyangoo alikua mwanamama simple shabiki mkubwa sana wa papa wemba,kuna video walipiga wenge original pale paris wakiwa stage moja na papa wemba mwana mama huyu anaonekana akipanda stejini kumtunza mzee wembadio shungu a.k.a.papa wemba na kukumbatia,kulikua na minong’ono mingi sana katika jamii ya wacongo duniani jinsi mama huyu alivyopata utajiri,hayo tuyaache kwa kuwa hayupo tena duniani.

 

Saghi Sharufa

image

Katika list hii ya wamama yupo pia mwanamama SAGHI SHARUFA “mabele mokonzi” a.k.a. Sharufa la Refference, akimiliki la refference club na kati ya paris pamoja na nyingine Brussels, huyu mama aliwahi kuwa girl friend wa mzee wembadio shungu (papa wemba).

Mama huyu anaonekana pichani siku ya harusi yake alipoolewa na Pastor Bongo,  kwa sasa hasikiki sana,ipo sababu,zamani alikua muislam lakini baadae miaka kama miwili mitatu iliyopita alibadili dini na kuolewa na pastor,hivyo kwa sasa amempokea bwana na amekua akiutumia utajiri wake kueneza neno la mungu,hayuko tena katika muziki wa kidunia,amenzisha redio ya mambo ya mungu ikiitwa ASIFIWE REDIO, Kwa sasa anaitwa ESTHER ELIZABETH si yule mabele mokonzi sharufa la refference tena. Wapo pia kina Igete mboma,

Waombolezaji wakiwa na Papa Wemba siku Mama Mere Malou alipofariki

 

ZACHARIE BABABASWE

Zakari bababaswe mmoja wa ambao pia mie nawakubali waliochangia pia kutagaza vipindi vyao kutokana na interview za DVD ambazo amekuwa akitengeza na kuuza ulaya lakini pia kupitia kipindi cha lingala facile amekuwa akifanya mambo ma kubwa kwa sasa .

Tchacho Mbala

 

TCHACHO MBALA

Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo. Shukrani kwa Big Producer Maghambo.

WAPO WENGI SANA KAMA KINA KASHOGII, KINA YAKUZA DEBS,Boris Bondo, Bebee Ramadhani, Papito Mbala, Zamalenga, Cedric Okitundu, apokalips Bella na USA, na wengine wengi ambao sijataja majina yao i hope umewasikia sana na umekuwa ukijiuliza kwanini wanaibwa ingawa mwisho wa siku kwa namna moja ama nyingine nathubutu kusema jamaa hawa wanamchango mkubwa na wamesaidia sana kuutangaza muaiki wa Congo ulaya na kwingineko africa wamekuwa wakiwatunza wanamuziki na kuwapa suport .

Hapa nyumbani pia watu kama hawa wapo wengi sana nitakuletea picha zao na kile wanacho kifanya muda si mrefu na nikiwa na imani na wao pia bado wanayo nafasi ya wakishirikiana na wanamuziki kuutangaza muziki wetu wa Tanzania nje ya Tanzania tukishirikiana nao kama wadau wa sekta ya burudani kwakuwa miongoni mwao ni wafanya biashara wakubwa na maarufu na wana uwezo wa kusuport vijana wa kitanzania kwa kila namna.


Misri haitotetea taji lake la Afrika

September 3, 2011

Na BBC

Wakati michuano ya kuwania nafasi za kushiriki fainali za Kombe la Mataifa mwakani nchini Gabon na Eqautorial Guine yakiendelea, bingwa mtetezi, Misri imeishiwa maarifa.

Misri

Misri imeshindwa kuendelea na uhodari wake katika soka

Hii ni baada ya Timu hiyo kujikuta mwisho wa kundi lake ikiwa na pointi mbili kutoka mechi tano. Misri ilichapwa 2-1 hapo jana ilipochuana na Sierra Leone.

Senegal kwa upande mwingine imejishindia nafasi kushiriki fainali za Guinea na Equatorial Guinea kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Congo mjini Dakar.

Kwingine Libya ilitoa kimasomaso licha ya vita na kupata ushindi wa bao moja dhidi ya Msumbiji kwenye uwanja wa kuazima mjini Cairo, huku Malawi na Tunisia zikitoa sare ya 0-0 il hali Cameroon ikipasua ngoma kwa kuhesabu matano kama ilivyofanya Ivory Coast mjini Kigali dhidi ya Rwanda.

Timu ijulikanayo kama Chipolopolo ya Zambia ilikuwa na wakati mgumu dhidi ya visiwa vya Comoros lakini hatimaye ukakamavu wa Comoro ulivunjwa na Zambia kuifunga na hivyo kupanda kilele cha kundi lake. Hata hivyo itabidi Chipolopolo isubiri mchuano wake dhidi ya Libya mjini Lusaka ambapo mwakilishi wa kundi hilo atabainika.

Cameroon ilikawia kupata kasi dhidi ya Mauritius mjini Yaounde lakini ilionyesha makucha yake katika kipindi cha pili ambapo Choupa Moting akifunga mawili kati ya matano yaliyowawezesha Simba wa nyika kuthibitisha nafasi yao kwenye fainali za Gabon na Eq.Guinea mwakani,

Ingawaje bado kuna walakini wa kushiriki licha ya kuonekana kama washindi wa pili wenye matokeo mazuri.

Mjini Cairo bao la Libya lilifungwa na Rabiyah Lafi na nchi hiyo iliyotumia bendera ya uongozi mpya wa waasi una hakika ya kushiriki fainali mwakani.

Ingawa Malawi ililazimishwa sare ya kutofungana ikisaliza matumaini ya kufuzu katika mechi yake ya mwisho nyumbani.

Mali ikapiga hatua kubwa kwa bao 3-0 katika mchuano wa kundi A dhidi ya Cape Verde mjini Bamako.
Hata hivyo itabidi Maliisubiri matokeo ya mechi kati ya Zimbabwe na Liberia kujiandalia safari ya kuingia fainali.

Ivory Coast ilisafiri kwenda mjini Kigali ikiwa tayari imeisha jihakikishia kushiriki fainali lakini hilo halikuwazuia nyota wake kuinyunyizia Rwanda mabao matano bila majibu.

Namibia ikajipatia bao la lala salama dhidi ya Gambia mjini Windhoek. Mfungaji alikua Tangeni Shipahu, matokeo ambayo yanaiweka Namibia sawa kwa pointi 3 na Gambia ingawa nyuma kidogo ya Burkina Faso.

Malalamiko ya Namibia kwamba Burikina faso ilitumia mchezaji asiyestahili Timu hizi zilipopambana bado yameweka kivuli juu ya kundi zima na CAF bado haijafikia uwamuzi kuhusu madai hayo.


Van der Vaart aumia kutocheza wiki 6

September 3, 2011

Kiungo wa Spurs Rafael van der Vaart huenda asicheza soka kwa muda wa hadi wiki sita baada ya kuumia msuli wa paja.

Rafael van der Vaart

Rafael van der Vaart

Mchezaji huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, aliumia wakati Tottenham ilipocharazwa nyumbani kwao mabao 5-1 na Manchester City.

Tottenham wapo mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka ya England baada ya kupoteza mechi zao zote mbili za ufunguzi dhidi ya Manchester United na Manchester City.

Meneja wa Spurs Harry Redknapp ameliambia gazeti la Sun: “Hilo ni jambo la mwisho kabisa kulisikia. Ni jeraha baya na alikuwa katika hali nzuri kimchezo.”

Kiungo mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji muhimu tangu alipojiunga na Spurs akitokea Real Madrid kwa kitita cha paundi milioni 8 mwaka 2010.

Van der Vaart atakosa mechi za Ligi Kuu dhidi ya Wolves, Liverpool na Wigan, na pia mechi dhidi ya watani wao wa jadi Arsenal katika uwanja wa White Hart Lane.

Pia hataweza kuanza kuichezea Spurs katika kampeni za ligi ya kuwania kombe la Europa, ikiwemo mechi dhidi ya PAOK Salonika na Shamrock Rovers.


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – III

September 2, 2011

 

image

Pichani ni JB Mpiana akiwa na ma stage show wake wakiwa katika moja ya show za Wenge BCBG

Baada ya majuzi kuona jinsi akina Tshai Ngenge, Acolpa Alba, Rio na wengineo walivyoingia Wenge BCBG sasa tunaendelea na jinsi Wanamuziki wengine walivyoingia na kutoka BCBG.

Makala Hii ni muendelezo wa Sehemu ya Kwanza ambayo tuliona vile Wenge Musica BCBG ilivyo vunjika, na Sehemu ya Pili ttukaona Jinsi Wenge BCBG ilivyoundwa na sasa tuko Sehemu ya Tatu.

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA. Sasa Endelea…

Wakiwa katika maandalizi ya safari hiyo ya Paris, bahati mbaya Blaize Bulla akapata viral infection kwa muda mrefu, hivyo akashindwa kuungana na wenzake kwenda safari hiyo. Lakini anadai alipokuwa kwenye hali hiyo JB na Makaba walimtosa, hawakumjali sana yeye wala afya yake badala yake wao wakawa focused kwenye mafanikio ya concerts hizo hasa ikizingatiwa hizo ni kumbi kubwa na zenye heshima ya pekee na wao ndio wamepata nafasi ya kwanza kutumbuiza huko kabla ya mahasimu wao MAISON MERE, hivyo walipania kufunika, kutokana na hatua hiyo Blaize Bula inasemekana alihuzunika sana,kuapa kuamua kuitosa BCBG rasmi akiwa kitandani na bendi ikiwa ulaya.Lakini inaonekana ni wazi Blaize Bula alikua akimlenga zaidi Jb Mpiana kwani ndio anaeishi Kinshasa ambako yeye alilazwa. Kwani kama tulivyoona huko nyuma makaba wakati huo alikua tayari ameshahamia ulaya akiungana na wenge pale inapokua na show za huko na wakati wa kurekodi album na alikua akifanya hivyo toka enzi za wenge original ikiwa katika siku zake za mwisho mwisho hivyo basi hata this time BCBG walikutana nae hukohuko. Hilo la Blaize Bulla likabaki Kinshasa.

image

Pichani ni Werason, JB Mpiana na Blaise Bulla wakitumbuiza mwishoni mwa miaka ya 80 huko Congo

 

Bendi ikasafiri bila Blaize Bula mpaka Paris.Lakini wakiwa katika maandalizi kuelekea siku ambayo watapiga zenith ambako ndio walipangiwa kupiga kwanza kabla ya olympia,ulizuko mgogoro kati ya JB na Makaba,mgogoro ambao chanzo chake kilikua ni makaba kutokubaliana kabisa uamuzi uliochukukuliwa na bendi huko Kinshasa ku-recruit wanamuziki wapya ambao makaba aliona kama hawakuwa na uwezo wa kutosha kuwa wanamuziki wa wenge BCBG  mpya,hapa tukumbuke kwamba katika mtiririko wa vyeo walivyopeana makaba alikua ndio artistic director hivyo hakuwakubali wasanii wapya yani Jules Kibens, Rio, Chai Ngenge na Genta.

Mgogoro huo ulidumu mpaka siku ya show yenyewe ndani ya zenith  dakika chache kabla ya kupanda stejini kuanza show kulitokea majibizano ya maneno baina ya marafiki hao yaliyopelekea mpaka JB Mpiana kulia machozi baada ya Alain Makaba kutumia maneno makali sana yaliyofanana na matusi dhidi yake, JB aliumia sana moyoni kwani kazi ya ku recruit aliifanya Blaize Bula, Jb akasusa kupanda jukwaani hali iliyopelekea showa rasmi ichelewe kuanza huku kina Alain mpela na Aimelia wakiwa wanaendelea kuimba nyimbo za utangulizi stejini, ikabidi mkewe Jb, mama Amida Shatur pamoja na rafiki yake JB waliekuwa pamoja maisha ya utotoni JDL ambae wakati huo alikua ni mpiga keyboard wa Wenge El Paris waingilie kati kumsihi JB apande stejini kwani wapenzi hawatawaelewa kabisa hasa ikizingatiwa Blaize Bula nae hayupo (JDL kwa sasa yuko na bcbg kama muimbaji).

Sehemu ya Show ya Zenith ilivyokuwa

Baadae Jb akakubali na kupanda stejini akiwa amevaa crown ya mfalme kichwani na koti refu lenye rangi ya dhahabu akisindikizwa na Tutu Kaludji ukumbi mzima ukizizima kwa kushangilia na moja kwa moja akashika mic na kuanza kuimba wimbo wake COURAGE kwa hisia kali na masikitiko makubwa, huku akiwataja wakongwe Papa Wemba, Pepe Kalle, Adui yake wakati huo Koffi Olomide (japo alipomtaja watu walizomea) huku akisema kwamba yeye ni mdogo kwa hao wote, unaweza kutazama hapo chini jinsi alivyokua akiimba kwa hisia kali wimbo huo siku hiyo,ambapo baada ya huu akaamba mulolo, Parie Bouge (Kin e Bouger) na n.k. mnaweza kuitafuta video hii kamili kwa ambao hamjaiona, mimi huwa hainichoshi kuitazama, ni nzuri sana,imeandikwa JB Mpiana & WENGE bcbg Zenith 1999!
vIDEO:

Wenge alikomelea kwenye kutunga zaidi na vijana walipewa nafasi vijana zaidi, Wimbo huu unaitwa Serge Palmi ukiwa ni utunzi wa kinaja Burkina Faso Mboka Liya aka Burkifaso Kasongo mmoja wa vijana wakongwe kwenye BCBG.

Katika show hii kwa upande wa makaba nae alisusa kabisa kupiga solo, akakaa back stage, mpaka mwishoni kabisa alipobembelezwa sana na wadau wa bcbg ndio akapanda stejini akapiga solo kwenye wimbo omba ambao hupendwa sana na wamama wa congo, tena hakua yule makaba tunaemjua, mcheshi, mchangamfu na mbwembwe nyingi stejini,bali alikua amenuna, mwenye hasira akipiga solo lake huku akiwa amewapa mgongo mashabiki!!mimi mwenyewe nilipoiona hii video enzi hizo 2000 kabla ya kujua kilichotokea nilimshangaa sana makaba kwa style ile ya upigaji gitaa huku amewapa mgongo mashabiki, niliona kama ilikua ni dharau!tafuta video ya live concert hii bora kabisa uangalie vituko hivyo vya prince makaba.

Baada ya show hiyo JB akaamua kuachana na Makaba kwenye show ya Olympia ambayo ndio ilifuata siku chache baadae.Show ambayo ilikuja kuwa voted kama BEST CONGOLESE CONCERT OF THE CENTURY., Baada ya mafanikio ya concert hiyo JB na BCBG kiujumla walikubaliana kumvua rasmi Makaba cheo cha artistic director kwa kumdhalilisha rais wa bendi JB Mpiana, ndipo makaba akakasirika na kuamua kuachana kabisa na kitu kinachoitwa wenge pamoja na kushawishiwa mara kadhaa na werrason ajiunge maison merre.Hii hapa chini ni video ya showa ya OLYMPIA.
VIDEO:

Pata Kitu Process Mambika, Hii ni sehemu ya show ya Olympia–1999 wakati unameza mate.

Baada ya hapo JB na vijana wake mwishoni mwa 1999 wakaingia studio huko huko paris na kufyatua single ya YA PAS MATCH, hawakukaa sana tena mwanzoni mwa mwaka 2000 wakaja na single nyingine iliyokuja kuwika sana PAPITO MBALA REMIX ambao ni wimbo uliokuwa umetungwa na “Teja” ZULEMA Kijana mcongoman lakini akiwa ametumia muda wake mwingi huku Brazzavile akiimbia bendi moja huko mpaka JPS PRODUCTION waliomkuta akizurura Paris na kuamua kumleta Kinshasa ajiunge  maison merre japo werra alimkubali tatizo la  kutumia madawa likamkosesha kazi. Japo alifanya kazi hiyo ya PAPITO REMIX na BCBG kipindi hicho Zulema hakua mwanamuziki wa bcbg, walikutana tu paris na kwa kuwa Kibens waliwahi kufanya kazi pamoja huko Brazaville ndio akamtambulisha kwa Jb wakawa wanafanya mazoezi pamoja nae sasa kwa kuwa ana kipaji cha kutunga ndio katika muda mfupi akatunga hiyo single, kabla bcbg hawajaamua wawe nae ndio JPS wakampeleka kwa Werra japo kwa sasa yuko na BCBG, Jb anamkubali sana sema tatizo lake ndio huo uteja.

Baada ya kuachia single hizo mbili,ndio sasa wakaanza maandalizi ya album ya T.H.bila Blaize Bula wala Makaba,lakini wanafanya mixing ya hiyo album huko paris baada ya kuwa wamesharekodi sauti na vyombo yaani kila mtu kaimba na kupiga sehemu yake kwenye album nzima na imesharekodiwa,ghafla Aimeli Lyase nae akatangaza kujiondoa kundini huko huko Paris na kuamua kuungana na mkewe na mwanae wanaoishi huko Paris akipanga kutoa album yake binafsi ya CONSTAT,nae Burkinafaso ambae Jb sasa ndio ilikua roho yake baada ya kuachana na makaba,akanyakuliwa na wapinzani wao Wenge Maison Merre akiahidiwa kupewa gari na dola 10,000 na wafadhili wa Werrason,mbaya zaidi Burkinafaso hakuondoka peke yake,aliondoka na mpiga gita kiraka wa bass na Rythm Patient Kusangila ambae yeye alikasirishwa na kitendo cha kufanywa mpiga gita namba 2 nyuma ya ACCOMPA ALBA(solo)na Sunda Bass(Bass).

image

Shabiki Nambari One wa BCBG Zadio Kongolo (ZK) akifurahia kumtunza Mpiana

Kuondoka kwa wanamuziki hawa watatu kwa mpigo tena bendi ikiwa studio kulimchanganya sana JB hasa kuondoka kwa Burkinafaso na Aimelia ambao tayari walikua wameshaingiza sauti zao wanasubiri kufanya mixing tu then album iingie sokoni,kukawa hakuna jinsi ikabidi releasing ya T.H. ichelewe kwa sababu walilazimika kurudi tena studio ili kuondoa vocals za Aimelia na sehemu ambazo Burkina faso alipiga solo, japo hawakuweza kufuta mikono ya Burkinafaso kabisa kama walivyofanya kwa sauti ya Aimelia ambayo haisikiki kabisa kwenye TH,Ndio ukiisikiliza T.H. upande wa solo gitaa utaona inafanana sana na TERRAIN EZA MINE ya MAISON MERRE ni kwa sababu zote mbili ni mikono ya Burkinafaso japo FICARE MWAMBA alijaribu kuondoa ondoa athari za burkinafaso lakini wapi.. ikashindikana.

Kwa kuwa burkinafaso mapigo yake aliyopiga kwenye T.H. akaenda nayo vilevile kwenye TERRAIN EZA MINE nadhani alifanya vile makusudi si unajua mambo ya upinzani tena hadi kile kibwagizo cha Souverain premier.. souverain premier binadaaaaaaaaaaam souverain premier jb mpianaaaaaaaa tutu calugi alikibadilisha tu jina tu kwenye T.H., Lakini ukweli ilikua ni cha burkinafaso ndio maana akahama nacho na kina Bill Clinton wakakiimba Burkinafasooo burkinafasoooooo……..Hali iliyopelekea Bill Clinton kwenye ile concert ya WMMM Bercy awapige kijembe BCBG kwa mafumbo,kuna sehemu anasema “BURKINAFASO MOPAYA SOKI ALONGWE AKENDAKA NA NYONSO ATA RIDEAU YA PAMBA (MTU  AKIJA KWAKO AKITAKA KUONDOKA ANAENDA NA KILA KITU ALIKUJA NACHO).

image

Genta Machine akiwa na mdau, huyu ndio ameziba Pengo la Tutuu Kaludji na kuwa Atalaku nambari One wa BCBG

Lakini yote kwa yote mwisho wa siku T.H. ikawa released, JDL yule rafiki wa JB toka maisha ya utoto akajiunga bcbg kama muimbaji si mpiga keyboard tena kama kule Wenge el Paris, baadae rafiki mwingine wa JB toka maisha ya utoto BIKU LEBRUN nae akajiunga akitokea UK ENGLAND, TH ikapata mafanikio makubwa sokoni, ikiwapatia BCBG Kazi nyingi kwa maana ya concerts ulaya, america na hata africa, baadae kijana mdogo sana mpiga solo akijulikana kama Patou Solo akajiunga na bendi kuongeza nguvu lakini hakuwa full time musicien wa wenge bcbg kwa sababu kipindi hicho alikua mwanafunzi akifanya degree yake ya mambo ya sheria na pia akifanya degree ya sound engineering mpaka 2003, pia kipindi hicho hicho wakajiunga Richard  Mukena rafiki mwingine wa jb waliekulia nae sehemu moja,Bogus Bompema na mpiga gitaa anaetumia mkono wa kushoto Pathy Moleso.

Wakarekodi album ya INTERNET ambayo ikawapatia contract ya kusafiri kwenda ulaya kufanya concert ndani ya BERCY,Wakapania sana kwenda kuivunja record iliyokuwa imekwishawekwa na Koffi pamoja Werrason hapo bercy kwa kujaza watu wengi sana.

image

Wanamuziki wa Wenge BCBG wakishambulia jukwaa, Hii ilikuwa show ya Olympia

Watu walijaa lakini si sana kama ilivyokuwa kwa Koffi na Werrason walipopiga hapo siku za nyuma na hii ilitokana na kwamba concert hii ya bcbg hapo Bercy ilifanyika ndani ya siku 11 baada ya ile milipuko ya september 11 marekani, hivyo kwa wageni wengi waishio ulaya na marekani kipindi hicho kilikua kigumu sana kwao kwani askari walikua wakivamia kila penye mkusanyiko wa wageni na kuharass watu na kama mnavyojua tena waafrika wengi huwa tunaishi bila makaratasi kwenye nchi hizi sasa watu wengi wakaogopa kujitokeza kwenye hiyo concert kwa kuhofia mkono wa sheria za uhamiaji, lakini show ilikua nzuri sana chini ya BADIVE.
Hiyo ndio ilikua miaka mitatu ya mwanzo ya uhai wa BCBG.

Stay tuned kwa miaka mitatu ya mwanzo wa uhai wa MAISON MERE,

  • Walianza vipi ku recruit vijana,
  • nani alikua wa kwanza kujiunga baada werra, adolphe na masela? Bill clinton alipatakanaje?
  • Je Wajua kuwa Fally Ipupa aliwahi kufanya Inter View WMMM?

Tutajua hapa hapa Spoti na Starehe, Shukrani za kipekee kwa Papaa Henry Kasapira nakati ya londone, Juma Mukubwa Muzee ya Air Port, Le Big Prodyuza Maghambo tuko pamoja, Papaa Julie We Ston weeee Ndenge nini papaa?, Papaa Hadji Le Becebegeeque Nambari wan!! Uko Juu Papaaa, Mamaa Tabou Fatou ya Tanzanie weeeee Kitokoooooo, Papaa Farid Wa Muscat, Mamaa Perovee, Mukubwa Shabani, Papaa Mwalimu wa Muheza Waambaze Mgoshi?,  Sadik Titanike weeee, Alain Kamangu Merci Mingi papaa, Mamaa Fatuma Mtanga tuko Pamoja Meree, Samson wa Delila karibu sana, Mke Mimi nakati ya Ujiji Chighoma, Ubeleji na wachangiaji na Wasomaji wote tuko pamoja na Asante kwa support yenu

Merci Mingi, Till then….


Stoke yakwama kumsajili Lukaku wa Chelsea

August 31, 2011

Na BBC

Stoke imekwama katika mipango yake ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji mpya wa Chelsea Romelu Lukaku kwa sababu ya kanuni za Ligi Kuu ya England.

Romelu Lukaku

Romelu Lukaku

Romelu Lukaku, aliwasili Stamford Bridge akitokea klabu ya Anderlecht mapema mwezi wa Agosti na alicheza mechi yake ya kwanza na Chelsea siku ya Jumamosi.

Lakini kanuni ya Premier League namba M 7.1 inasema: “Usajili wa muda hautawezekana wakati wa dirisha la usajili ambapo mchezaji amekuwa ndio kwanza amekamilisha usajili na klabu nyingine.”

Wakati huo huo Stoke wamo mbioni kumsajili Wilson Palacios kutoka Tottenham kwa kitita cha paundi milioni 6 na kiungo huyo anajiandaa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Stoke katika siku za karibuni pia imehusishwa kutaka kumchukua mshambuliaji wa Spurs Peter Crouch.

Na vyombo vya habari vya Denmark vimesema mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner huenda yupo njiani kujiunga na Stoke.

Chelsea ilimsajili Lukaku kwa kitita cha paundi milioni 20 tarehe 6 mwezi wa Agosti. Ni mchezaji mashuhuri nchini Ubelgiji baada ya kuwa mfungaji bora katika ligi ya nchi hiyo msimu wa 2009-2010 alipokuwa na umri wa miaka 16.

Alifunga mabao 16 katika mechi 37 za ligi msimu uliopita na akafunga bao lake la kwanza katika mechi ya kimataifa Ubelgiji ilipoilaza Urusi mabao 2-0 mwezi wa Novemba.


Armand Traore wa Arsenal ajisajili QPR

August 31, 2011

Na BBC

Mlinzi wa kusoto wa Arsenal Armand Traore amejiunga na vijana wapya katika Ligi Kuu ya soka ya England QPR kwa kitita ambacho hakijasemwa.

Armand Traore

Armand Traore

Armand Traore mwenye umri wa miaka 21, anaondoka Arsenal baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka mitano akiwa ameshiriki mechi 23, amesaini mkataba wa miaka mitatu na QPR.

Traore anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na QPR chini ya mmiliki wake mpya Tony Fernandes, akifuatiwa na Joey Barton pamoja na Luke Young.

“Nilipozungumza na meneja Neil Warnock alionekana kuwa na matumaini makubwa nami katika klabu hiyo,” alisema Traore.

Traore aliichezea Juventus kwa mkopo msimu uliopita, lakini akawa anatafuta nafasi ya kuwa mchezaji atakayepangwa kila mechi.

Beki huyo atavaa fulana yenye nambari 13 katika klabu hiyo ya magharibi mwa London na Warnock amesema: “Armand amekuwa mchezaji nambari moja niliyekuwa namhitaji kwa muda mrefu.


Per Mertesacker kujiunga na Arsenal

August 31, 2011

Na BBC

Mlinzi wa Werder Bremen anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Per Mertesacker anakaribia kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu ya Arsenal.

Per Mertesacker

Per Mertesacker

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26- ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ya Werder Bremen inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, pamoja ya kwamba yumo katika kikosi cha timu ya taifa hivi sasa, ameruhusiwa kusafiri hadi London.

Mipango ya Arsenal kumsajili Mertesacker, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6 aliyekwishacheza mechi 75 kwa timu ya taifa ya Ujerumani, inaweza ikawa ndio mwisho kwa klabu hiyo kutaka kumsajili mlinzi wa Bolton Gary Cahill.

Lakini Gunners pia wamo mbioni kumsajili beki wa kushoto Mbrazil Andre Santos.

Hatua ya wa meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuimarisha safu yake ya ulinzi, imetokana na timu hiyo kuadhiriwa kwa kuchapwa mabao 8-2 na Manchester United siku ya Jumapili katika Ligi Kuu ya England.

Hivi karibuni klabu hiyo ilimuuza mlinzi wake wa kushoto Gael Clichy kwa Manchester City, na mlinzi wa kuume Emmanuel Eboue kwa klabu ya Uturuki ya Galatasary, wakati siku ya Jumanne imemuuza Armand Traore kwa klabu ya Queens Park Rangers.

Mlinzi wa kati wa Arsenal Thomas Vermaelen aliumia akijiandaa kwa safari ya Old Trafford na msimu uliopita hakuweza karibu msimu mzima akiwa ameumia kifundo cha mguu.

Mertesacker alikuwemo katika kikosi cha Ujerumani kilichoilaza England mabao 4-1 katika Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Na ameitwa tena katika kikosi cha Ujerumani kitakachopambana na Austria katika mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya siku ya Ijumaa baada ya kuumia kisigino mwishoni mwa msimu uliopita.


Pendejee Samuel Etoo Alipomwaga dola jukwaani

August 30, 2011

Ni kawaida kwa wanamuziki wa Congo kuwarusha Mapendejee na Meree safari hii ilikuwa zamu ya Kurushwa Samuel Etoo angalia jinsi alivyomwaga pesa na jinsi alivyomwaga mauno.

Pia utamuona Rogger Milla naye akichezeshwa jukwaani na wasanii hawa.