Wajue Ma Pendejee na Mameree wanaotamba kwenye nyimbo za Bolingo.

Hii ni Compilation ya mwanadada Sophia wa Kessy na ni jibu la mdau wangu Moris wa Mererani kama ulivyoniomba nikwambia nani ni nani kwenye nyimbo za Congo, nakujibu swali lako mkuu.

Sio jambo geni kusikia majina ya watu mabali mbali yakitajwa kwenye nyimbo, angalia hapa utajua

CHIEF DIDI KINUANI LE MILLIONAIRE

Didi Kinuani a.k.a.DIKINI au ukipenda mkingereza waweza muita Didi Stone au Didi mzee wa mawe mkiswahili yeye ndio mfadhili mkubwa kwa muda mrefu wa Mahasimu wawili Le Roi De La Forret Werrason a.k.a.papaa na Exocee pamoja nae Le Rambow du Zaire a.k.a.Papaa na Didi stone Koffi Olomide, pia na wanamuziki wengine wengi kasoro Souverain Leadeur ya Ba Wengee BCBG JB MPIANA MUKULUMBA a.k.a.papaa na Daida. Kwa faida tu ya wasiojua huyu jamaa ndio aliyezaa na mke wa JB Mpiana baada ya kutengana na JB Mpiana kwa takriban miaka 7 na kuzaa naye mtoto mmoja lakini baadaye walirudiana na JB na wako wote mpaka sasa, Didi Kinuani ni mfanyi biashara mkubwa sana wa madini ya Almasi na mshirika wa karibu wa Rais Kabila pia, katika nyimbo nyingi hata za hapa nyumbani pia unaweza kumsikia amiwa ameibwa amekuwa mfano wa kuigwa huko kongo kwa kuchangia si tu secta ya muziki lakini pia hata ma hospitali na hata kufikia hatua ya kununua vyo mbo vya muziki kwa kuwagaramia na wakati mwingine kuwasafirisha wanamuziki wa kongo barani ulaya na kuwatangaza kupitia kampuni yake ya group de kin.

 

ZADIO CONGOLE aka ZK aka ZADIO BEECEEBEEGEEQUE

Zadio Congole, huyu pia ni ‘mpigaji” ambaye alifaikiwa kupata pesa anaishi huko Ubelgiji (shengheni kwa ujumla) na ni mshabiki mkubwa wa JB Mpiana ambaye kwa kiasi kikubwa amejitolea pesa na muda katika bendi hii, Zadio ndiye mfadhili mkubwa wa show za JB Mpiana na amejizolea umaarufu kupitia muziki huku JB akiwa ameshamtungia nyimbo takribani tatu mpaka sasa huku wimbo wa Zadio au ZK ambao unapatikana kwenye album ya Quel Est Ton Probleme.

 

TABOU FATOU aka TABOU FATOU TOP MODELLE

Mwanamuziki Faustin Ipupa Nsimba aka Fally Ipupa Di Caprio, Album yake ya “Droit Chemin” ndiyo Album bora ya Mwaka 2007/2008, Albamu hiyo  iliuza sana takribani miaka miwili mizima. katika Album hiyo kuna wimbo unaitwa “Liputa” kwenye huo wimbo amededicate kwa Taboo Fatou ” Mama na Compressor”(pichani), huyu ni Mfanyabiashara Mrembo anaishi Belgium, ana miliki maduka kadhaa ya Nguo huko Paris(France) na Beligium,na inasemekana zile Pamba zote za Fally, Taboo Fatou ndiyo anamvalisha, kwa wale wapenzi wa JB Mpiana watumbuka katika Album yake ya Kwanza(Solo) Feux D’Lamour,kuna wimbo unaitwa “Top Model” utampata humo Tabu Fatou.

 

MERE MALOU “MADAME YA POTO”

Marehemu Mama Mere Malou akiwa na Papa Wemba enzi hizo, Hawa waliwahi kuwa wapenzi.

Pichani juu ni Marehemu Mama Mere Malou “madame ya poto“ akiwa na Papa wemba enzi hizooo Mama Mere Malou alikuwa Mkongo anayeishi Paris Ufaransa, alishiriki kwa kiasi kikubwa kuukuza na kuutangaza muziki wa Kongo bara Ulaya, alikuwa ndio mdhamini na mpokezi wa wanamuziki wa Kongo kila wakifanya ziara Ufaransa, Pia Mere Malou ndiye alikuwa mke wa kwanza wa mwanamuziki  Wemba.

Mere Malou a.k.a.Nanyangoo alikua mwanamama simple shabiki mkubwa sana wa papa wemba,kuna video walipiga wenge original pale paris wakiwa stage moja na papa wemba mwana mama huyu anaonekana akipanda stejini kumtunza mzee wembadio shungu a.k.a.papa wemba na kukumbatia,kulikua na minong’ono mingi sana katika jamii ya wacongo duniani jinsi mama huyu alivyopata utajiri,hayo tuyaache kwa kuwa hayupo tena duniani.

 

Saghi Sharufa

image

Katika list hii ya wamama yupo pia mwanamama SAGHI SHARUFA “mabele mokonzi” a.k.a. Sharufa la Refference, akimiliki la refference club na kati ya paris pamoja na nyingine Brussels, huyu mama aliwahi kuwa girl friend wa mzee wembadio shungu (papa wemba).

Mama huyu anaonekana pichani siku ya harusi yake alipoolewa na Pastor Bongo,  kwa sasa hasikiki sana,ipo sababu,zamani alikua muislam lakini baadae miaka kama miwili mitatu iliyopita alibadili dini na kuolewa na pastor,hivyo kwa sasa amempokea bwana na amekua akiutumia utajiri wake kueneza neno la mungu,hayuko tena katika muziki wa kidunia,amenzisha redio ya mambo ya mungu ikiitwa ASIFIWE REDIO, Kwa sasa anaitwa ESTHER ELIZABETH si yule mabele mokonzi sharufa la refference tena. Wapo pia kina Igete mboma,

Waombolezaji wakiwa na Papa Wemba siku Mama Mere Malou alipofariki

 

ZACHARIE BABABASWE

Zakari bababaswe mmoja wa ambao pia mie nawakubali waliochangia pia kutagaza vipindi vyao kutokana na interview za DVD ambazo amekuwa akitengeza na kuuza ulaya lakini pia kupitia kipindi cha lingala facile amekuwa akifanya mambo ma kubwa kwa sasa .

Tchacho Mbala

 

TCHACHO MBALA

Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo. Shukrani kwa Big Producer Maghambo.

WAPO WENGI SANA KAMA KINA KASHOGII, KINA YAKUZA DEBS,Boris Bondo, Bebee Ramadhani, Papito Mbala, Zamalenga, Cedric Okitundu, apokalips Bella na USA, na wengine wengi ambao sijataja majina yao i hope umewasikia sana na umekuwa ukijiuliza kwanini wanaibwa ingawa mwisho wa siku kwa namna moja ama nyingine nathubutu kusema jamaa hawa wanamchango mkubwa na wamesaidia sana kuutangaza muaiki wa Congo ulaya na kwingineko africa wamekuwa wakiwatunza wanamuziki na kuwapa suport .

Hapa nyumbani pia watu kama hawa wapo wengi sana nitakuletea picha zao na kile wanacho kifanya muda si mrefu na nikiwa na imani na wao pia bado wanayo nafasi ya wakishirikiana na wanamuziki kuutangaza muziki wetu wa Tanzania nje ya Tanzania tukishirikiana nao kama wadau wa sekta ya burudani kwakuwa miongoni mwao ni wafanya biashara wakubwa na maarufu na wana uwezo wa kusuport vijana wa kitanzania kwa kila namna.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: