Wanamuziki Congo watamuunga tena mkono Kabila mwaka huu?

Mwaka juzi kulikuwa na habari toka Congo ya kuhusu Serikali kupinga wanamuziki wa huko kuwataja wanasiasa kwenye nyimbo zao,

Hii imekuja baada ya fujo kuzuka kwenye baadhi ya majukwaa ya burudani kufuatia watu kuvutana kwa hisia za kisiasa na pia serikali haikuongelea sana bali wajuvi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema ni katika kuleta nidhamu na kuitakasa sura ya serikali kwa jamii. Muziki unanafasi kubwa sana kwa Congo kwani ni moja ya burudani ambazo zina ushabiki kama ulivyo wa mpira sehemu nyingine na unakusanya watu wengi, hivyo basi nguvu yake kwa umma ni kubwa.

Wimbo huu hapo juu ulipigwa na JB Mpiana wakati wa kampeni iliyomrudisha Joseph Kabila Madarakani. Kwa hiyo hata Rais asiimbwe tena?

Humu utamsikia JB Mpiana, utamsikia Rio, Caludji na wengineo katika Rhumba hii kwa ajili ya kampeni ya Kabila, Mwaka huu Kabila anakutana na Chuma tiene Tisekedi ambaye naye amejizolea umaarufu na anaonyesha kutoa upinzani kwa Kabila hasa.

Katika uchaguzi uliopita Kabila aliungwa mkono na wanamuziki wengi akiwamo Adolph Dominguez, Tshala Muana, Reddy Amis, Emeneya, Mbilia Bell na wengineo wengi.

Miaka ya karibuni  ilishuhudia mwanamuziki Koffi Charles Olomide akiingia matatizoni na serikali baada ya kutoa wimbo wenye muelekeo wa kisiasa, Wimbo huo uliojulikana kama Musouksouk ukiwa unaongelea mpasuko na msukosuko wa kiasiasa unavyoipeleka Congo Mrama. Mpasuko huo ulikuwa kati ya Kabila Upande umoja, Jean Pierre Bemba Gombo ambaye kwa wakati huo alikuwa mmoja wa Makamu wanne wa Uraisi huko Congo, Mbaye mwaka 2006 kwenye uchaguzi alipata Kura nyingi akiwa ni wa pili baada ya Raisi Kabila.

Advertisements

3 Responses to Wanamuziki Congo watamuunga tena mkono Kabila mwaka huu?

  1. Anonymous says:

    huu ni wimbo vote for kabila wa jb mpiana uchaguzi uliopita

  2. Hadj Le Jbnique says:

    mama mokonzi mbilia bell nae hakubaki nyuma 2006 kumpigia debe Joseph Kabila kabange Mwana ya Muzee,msikie hapa tene ameimba mkiswahili fasaha kabisa

  3. Quite nice web site and exceptional and articles.useful layout, as share good stuff with excellent strategies and concepts.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: