Tony Nyadundo, Mfalme wa Nyimbo za Wajaluo

Tony Nyadundo

Tony Nyadundo

Tony Nyadundo ni mzaliwa wa Kanda ya Ziwa huko Kenya. Anatokea katika kabila la Wajaluo (Luo), Tony Nyadundo amejipatia umaarufu kwa aina ya mziki wake na ni jambo la kawaida kupita mitaani na kusikia nyimbo zake zikichezwa. Aina ya muziki wake inajulikana kama Ohangla (Muziki toka kanda ya Ziwa) na sasa yeye anajulikana kama Mfalme wa Ohangla.

Tony ni mmoja wa wanamuziki walifaidika na muziki wake na kuufanya muziki huo kukubalika na rika lote. Tony pamoja na kaka yake anayejulikana kwa jina la Jack Nyadundo naye anapiga aina ya muziki kama wa Tony kama mdogo wake naye anakubalika sana kwenye Muziki na umaarufu wao ni mkubwa hasa Sehemu ambazo Wajaluo wanatoka. Tony ambaye anatamba na nyimbo kama Dawa ya Mapenzi,Isanda Gi hera, Obama na nyinginezo nyingi ameshafanya matamasha ya muziki nchi mbali mbali ikiwemo Ujerumany na USA pia achilia mbali hizi za Afrika. Umaarufu huu unafuatia aina ya muziki wake ambao unajumuisha ala za asili, uchezaji pamoja na uimbaji ambao huvutia kwa taratiibu na kuupandisha toka Mziki wa Vilabu vya Pombe, Bar mpaka sasa zimbo zake zinapigwa hata kwenye Kumbi za Burudani zikichanganywa na Genge, muziki maarufu wa Kenya.

Mwaka 2006 alitoa albamu yake iliyoitwa Obama. Ikiwa ni kumuenzi Seneta Barak Obama wakati huo ambaye Baba yake ni Mzaliwa wa Kenya kama Nyadundo. Wakati wa tamasha la Kisima Music Award mwaka 2007 alishinda kwenye kundi la Muziki wa kiasili. Tony ambaye binafsi anaweza kutumia ala zote za kiasili, muziki wake anatumia ala za kiasili tupu isipokuwa kinanda cha kupuliza tuu amefanikiwa kuweka utamaduni na muziki huo katika chati ya Muziki kitaifa na kimataifa.

Bonyeza Player upate Uhondo wa mwanamuziki Tony Nyadundo, Ukiangalia kwenye hii Video Utamuona Waziri Mkuu Raila Odinga, Prof Anyang Nyong, na wajaluo wengine ambao wapo kwenye nafsi za juu kichama(ODM) au kiserikali.

One Response to Tony Nyadundo, Mfalme wa Nyimbo za Wajaluo

  1. install Stair lifts

    Tony Nyadundo, Mfalme wa Nyimbo za Wajaluo | Spoti na Starehe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: