SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – IV

Kuzaliwa Kwa Wenge Musica Maison Merre (WMMM) na miaka yake mitatu ya Mwanzo

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko kadhaa leo tunaitazama Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, shukrani za kipekee ziwaendee watu hawa wafuatao kwa kufanikisha kuisimamisha Wenge Maison Mere kwa namna moja ama nyingine:

Wa kwanza ni mtu mmoja anaitwa Sankara De Kunta, huyu mtu alijitoa sana kuwasaidia kina Werrason kujijenga,jamaa alikua na kazi moja tu, kuwachafua Jb mpiana na Koffi Olomide na kumpandisha na Kumsifia Werrason, na kwa kweli alifanikiwa sana, jamaa alikua na vituko huyu hapa nafasi haitoshi, lakini aliipromote sana maison mere na hasa werrason binafsi, ilifikia wakati Tata Sankara ambae awali alikua mnazi mkubwa wa Adolphe Dominguez tangu enzi za wenge musica original alikua akipita mitaani huku akiimba Balingaki Baboma Werra eeeeh! akimaanisha wanataka kumuua werra, akiwataja mahasimu wa Werrason,alikua akiimba kwa style ya aina yake kiasi cha kuwafanya wengi wamuonee huruma sana Werrason wakidhani pengine ni kweli Werrason yuko hatarini kuuwawa kumbe ulikua usanii wa Tata Sankara.

image

Mtu mwingine nyuma ya mafanikio ya mwanzo mwanzo ya maison mere ni Zackarie Bababaswe, yeye pia alisaidia sana kuwa promote maison merre kupitia shows zake mbalimbali lakini na yeye pia akiitumia nafasi hiyo hiyo kutengeneza pesa binafsi, si unajua tena strategy maarufu ya “helping the weaker to overcome the stronger” halafu baadae na wewe unanufaika na hiyo strongness ya uliemsaidia.

Pia mtu mwingine aliewasaidia sana kina Werra kujijenga maison mere ni kiongozi wa wenge el paris Marie Paul, huyu aliwasaidia kutokana na connection yake na Werrason binafsi. Werra na Marie Paul wanatoka kijiji kimoja, pamoja na Reddy Amisi, pamoja na King Kester, lakini kwa sasa Werrason na hawa ndugu zake hawaongei wala kusalimiana, hali ya mahusiano miongoni mwao imekua ikilegalega kadri siku zinvyosonga mbele hasa kati ya Werrason na Marie Paul kiasi cha Marie Paul kutohudhuria hata mazishi ya baba yake Werrason miezi michache iliyopita. Msaada mkubwa ambao Marie Paul aliipatia maison mere kutokana na connection yake na werrason ni kuwaambia mashabiki wake na Wenge El Paris kiujumla wote wampe support Werrason na bendi yake na pia akawapa Maison Mere wanamuziki wake wawili, JDT Mulopwe na Manda Shante ambae baadae alijitoa hata hivyo (Kwa wasiomjua Manda Chante ni yule mwenye sauti kali kweli wimbo wa Kalay Boing wa Wenge Musica BCBG enzi hizo.

 

Wera na madai ya Nguvu za giza.

Pia habari za chini ya kapeti zinasema Marie Paul pia alimpa Werrason “Nguvu Zake” ambazo zinaelezwa kuwa ndio chanzo cha chuki za hali ya juu miongoni mwa watu hawa kutoka kijiji kimoja, kwani inaelezwa kuwa Werra badae hakurudisha “nguvu” hizo alizopewa kama walivyokubaliana,hapa sitaki kuingia sana lakini kwa congo hayo ni mambo ya kawaida sana. Kwa mnaoelewa Lingala mkisikiliza vizuri hapo chini kwenye video hiyo mtamsikia mwenyewe Marie Paul akiyaelezea hayo mambo ya “nguvu zake” anazozililia kwa Werrason, alijaribu kukwepa kwepa lakini mtangazaji akambana kwenye kona mpaka akafunguka. Msikilize mwenyewe hapo “Le Roi Pele” Marie  Paul anavyosema

Msikilize Marie Paul akiongelea mambo kadha wa kadhaa humu

Inasemekana nguvu hizo zinatoka kijijini kwao tu ,zilimtoa King Kester enzi zile za “kidengune”nadhani wengi mnakumbuka alivyotamba, baadae Reddy Amisi nae akazitumia, halafu ikaja zamu ya Marie Paul nae ndio akampa Werrason.

Tukiacha mazungumzo hayo baada ya habari,sasa tuende moja kwa moja kutazama zoezi la kusaka wanamuziki kwa ajili ya kuisuka Maison Mere,nani alikua wa kwanza,nani alifuatia na waliwatoa wapi hao wanamuziki twende pamoja.

 

FERRE ajiunga na WMMM akiwa ni Mwanamuziki wa Kwanza kuwa Recruited

Kutokana na wanamuziki wengi wa WENGE MUZIKA 4X4 TOUT TERRAIN kuondoka na Kumfuata Jb Mpiana kama tulivyoona huko nyuma,Werrason,Didier Masela na Adolphe Dominguez wakatakiwa kujipanga upya kwa kusaka watoto wa congo wenye vipaji vya muziki waweze kuwa recruit,kazi haikua rahisi pia,kwanza walianza na Ferre Gola ambae alikua ana hang tu baada baada ya kukimbizwa na Aimelia Lyase “Demingongo” kule Bcbg,hivyo na yeye akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kujiunga maison mere baada ya waanzilishi hao watatu Werra, Masela na Adolphe.

Vita Imana ni moja ya Tungo HAI za Ferre Gola ndani ya WMMM inayotamba mpaka wa Leo. Wimbo huu Uliimbwa tena akiwa kivyake.

 

Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya wajaribiwa WMMM

Kutoka hapo official recruitment ikawa imeanza, baada ya Ferre ku join kundini mwanamuziki aliyefuatia kujiunga na maison mere ni Bob Lorenzo, baadae akaja JDT kama tulivyoona huko nyuma kwamba aliletwa na Marie Paul kutoka kwenye bendi yake ya wenge el paris ili kumsaidia home boy wake Werrason, halafu akaja Baby Ndombe alipitia kwenye mchujo na alifaulu kwa upande wa uimbaji na alifaulu majaribio pia kama mpiga bass, baadae tena rafiki wa siku nyingi wa werra toka enzi za wenge musica ambae pia alikua mdau mkubwa wa wenge muzica enzi hizo WASENGA KIMPUNI akawaleta vijana kadhaa kutoka BANDAL (wenge musica home town), vijana hao ni huyu Fally Ipupa Celeo na Mtaalamu wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya ambao walikua wanapiga bendi moja ya mtaani huko Bandal, baada ya hapo akaja mpiga drums Maradona (the second ever true drummer wa iliyokuwa wenge musica original) ambae walijiunga maison mere kipindi kimoja na Papy Kakol ambaye yeye alitoka katika group ambayo Fally Ipupa wakati fulani alikua ndio atalaku namba moja wa hiyo group kabla ya kuanza kuimba, baada ya hapo akaja kijana mmoja mwenye kipaji cha hali ya juu, kijana ambae alikua ametokea katika bendi ya JOLINO iliyokuwa chini ya uongozi wa Rio Kazadi “Rio de Janeiro” ambae kwa sasa ni muimbaji wa bcbg, pia huko JOLINO ndiko alikotokea Chai Ngenge muimbaji wa bcbg pia, kijana huyo si mwingine bali BILL CLINTON.

 

Fally Ipupa Afanya Interview WMMM

Baadae tena Adolphe Dominguez akawaleta kundini SERGE MUBIALA na DIDIER LACOSTE wote walikuja kuibeba sana maison mere kwenye safu ya uimbaji, pamoja nao Adolphe alimleta pia mpiga kinanda Thiery Synthe, baadae Adjani nae akajiunga akitokea bendi ndogo ya mtaani, then akaja mpiga rythm guitar Kojack, baada ya hapo wakawajaribu tena mamia ya vijana wa congo miongoni mwao ni atalaku Brigade na muimbaji CHOU LAY (mtoto wa EVOLOKO) Lakini bahati mbaya Chou Lay hakuchaguliwa baada ya majaji kumuona Bob Lorenzo ni bora zaidi kutokana tu mvuto wa sura yake lakini hakua muimbaji mzuri kuliko Chou Lay, mwanzo tuliona Fally Ipupa akiletwa kwenye usaili, nadhani mtakua mnajiuliza ilikuwaje, je alifeli usaili?

Jibu ni kwamba hapana, hakufeli usaili, sasa kwanini hakujiunga? jibu ni kwamba Fally alijiondoa kwenye usaili mwenyewe kutokana na kuwa na mapenzi makubwa na Quartier Latin ya Koffi Olomide bendi aliyokua akiipenda toka akiwa bado kijana mdogo na kwa mujibu wa Willy Bula (kaka yake na Blaize Bula) anasema Fally pamoja na Bouro Mpela (mdogo wa Alain Mpela) walikua wakimsumbua mara kwa mara enzi hizo wakimuomba awaunganishie wapate nafasi ya kujaribiwa Quartier Latin ya Koffi Olomide ambayo yeye Willy Bula alikua mmoja wa wanamuziki huko, Bula baadae alifanikiwa kumshawishi Koffi awajaribu wadogo zake hao lakini baada ya majaribio Bouro Mpela ndio akawa wa kwanza kufaulu majaribio na kujumuishwa kundini huku Koffi akimwambia Fally aendelee kujifua na wao QL watakuwa wanafuatilia maendeleo yake na wakati mwingine kujumuika nae mazoezini na kwenye local shows za QL, hivyo Fally akaona asije akajiaribia mipango yake na Quartier Latin kwa kujiunga na Maison Mere,ndipo akajitoa kwenye usaili, nadhani kuna watu walimshauri asifanye haraka, aisubiri QL, hivyo basi Fally hatuwezi kumuhesabu kama ex-maison mere, hakuwahi kujiunga nayo japo alijaribu.

 

image

Hii ni moja ya Albamu ambazo zimefanya vizuri sokoni

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi,nini kilifuata,tuendelee kufuatana hapa hapa siku ya jumatano ambapo tutakamilisha miaka mitatu ya WMMM na baadaye tutaangalia walivyoendelea.

Huu ni mfululizo wa Historia ya Wenge Musica na kwa kuanzia tunajaribu kuangazia kilichopelekea JB Mpiana na Werrason kutengana na miaka ya mwanzo ya bendi husiki huku tukitazama kwa kina jinsi wanamuziki walivyopatikana na walioondoka na kwa nini waliondoka. Simulizi hiizi za kusisimua kwa wapenzi na wanafamilia wa Wenge ni za pekee na zitakujia hapa hapa kwenye Blog yako ya Spoti na Starehe.

Nawaacha na Kibao Heritier Itere toka kwake Werrason Ngiama Makanda, Hiki kilikkuwa katika Albamu ya Pentagone wakati huo wakifanya kazi pamoja.

Salamu zangu za dhati kwa Werasonique woote ndani ya Blog hii nadhani mmeridhika na habari za bendi yetu ya WMMM. Shukrani a kipekee kwa Papaa Henry Kasapira nakati ya londone, Juma Mukubwa Muzee ya Air Port, Le Big Prodyuza Maghambo tuko pamoja, Papaa Julie We Ston weeee Ndenge nini papaa?, Papaa Hadji Le Becebegeeque Nambari wan!! Uko Juu Papaaa, Mamaa Tabou Fatou ya Tanzanie weeeee Kitokoooooo, Papaa Farid Wa Muscat, Mamaa Perovee, Mukubwa Shabani, Papaa Mwalimu wa Muheza Waambaze Mgoshi?,  Sadik Titanike weeee, Alain Kamangu Merci Mingi papaa, Mamaa Fatuma Mtanga tuko Pamoja Meree, Samson wa Delila karibu sana, Mke Mimi nakati ya Ujiji Chighoma, Ubeleji na wachangiaji na Wasomaji wote tuko pamoja na Asante kwa support yenu, kwa wale wanaonitumia email na kunipigia simu pamoja sana najitahidi kujibu email zenu wote.

Merci Mingi, Till then…. Kama uko kwa Facebook basi ungana na page yetu kwa kubofya join/like hapo juu kulia basi utapata habari live kwenye notifications zako kila tunapochapisha kitu kipya.

Kama unaswali au maoni tafadhali niandikie piusmicky@yahoo.co.uk au nitwangie Hotline no. +255713 666616

27 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – IV

 1. Ntilya J says:

  Mukulu Bilanga Papaa Pius nimefurahi sana kuijua Werasson na WMMM maana mi ni Werra Damu ingawa simchukii Babaa na Daida, Nafurahishwa sana na story hii na nimekuwa niifuatilia sana tangu imeanza, ulinipa kazi ya kuchukua watu 8 kuwapeleka kwenye Cafe ila tulizuiwa ikabidi nianze ku Print moja baada ya nyingine na hatimaye leo umefikia ya Werra.
  Usichoke unatukuna sana Mukulu
  Merci mingi Papaa

  Ntilya – Mbeya Mwanjelwa Sokoni

 2. PDJ says:

  Kumbe chupu chupu fally ajiunge wmmm sijui pangekuwaje..pangetosha kweli?

 3. papa kasapira nakati ya london says:

  merci mingi papa pius mimi nishabiki mkubwa sana wa j’b mpina(BIN ADAM) ila kwa mashabiki wa wera nafikiri mmejisomea hapo juu jamaa hana kipaji zaidi ya ubinafsi,chuki,majungu na kutumia nguvu za giza naomba tu tuendele kufuatilia hii history ya WMMM then tutajua sababu za wakina papa one Adolf, presida Didier Masela ,Bill Clinton,Prince,Kenekene,Rio David,Celeo na The king of the new generation Fere Gola mwana Bandal etc why walimkimbia Igweeeee!

 4. Fatuma Mtanga says:

  Kweli mengi hatukuyajua thanx a lot kwa kutufungua macho jamani,naona mambo hayaishi na sisi kiu haiishi pia,japo sijui kilingala nimempenda sana mwanadada anaemuhoji marie paul hapo juu,ananikumbusha enzi za marehemu amina chifupa na africa bambataa pale clouds fm, mungu amuweke pahala pema peponi.

  amina chifupa R.I.P. Mama,naamini ungekuwepo tungekuwa pamoja hapa.

 5. Mamaa President says:

  Nilikua sijaingia siku mbili tatu humu si unajua tena computer zenyewe za kumvizia boss atoke kwanza,leo nimesoma mpaka nikawa nasisimka,hii stori kwa kweli hainishi hamu mwenzenu,inabidi nifanye mpango niiprint tu,i cant wait kwa kweli.

 6. papa kasapira nakati ya london says:

  Pedeshee papa pius can you please confirm hizi habari kama ni kweli au ni uzushi je ni kweli the best mkaanga chips ever in the history of Wenge Musica BCBG 4*4 Tout Terrain Original TITINA AL CAPONE amefariki dunia? ndenge zalii papa pius

 7. Mukubwa Shabani says:

  Nimejaribu kufuatilia habari hizo za titina toka kumekucha hapa leo mpaka muda huu hakuna taarifa hizo,nimeongea na watu wangu wa karibu paris lakini hawana habari hizo mpaka sasa.Ngoja tusubiri kama kweli tutajua si unajua dunia ni kijiji siku hizi.

 8. werrasonique wa ukweli says:

  stori ya wenge maison ndio imeisha!mbona umetupunja bana maison mere….ilikuwaje kumeguka kwa masela,dominguez na badae kina bill clinton?

 9. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo […]

 10. piusmickys says:

  Simu ya Titina ya Dubai inaita tuu na Page yake ya Facebook haina comments zozote za Msiba. NAdhani bado ni mzima

  • papa kasapira nakati ya london says:

   thanx a lot papa pius na mukubwa shabani ntafikisha ujumbe kwa wana wenge wa londone kwamba habari hizo zilikua ni uzushi merci.

  • Cbd Anxiety says:

   I got to book mark your website. Very helpful info particularly the last part. I really liked your post. I really enjoyed seeing this. It is crazy how incorrect I was.

 11. Anonymous says:

  Kaka nilikua naifuatilia hiyo interview ya Le Roi Pele Marie Paul na huyo mwanadada mwanzo mpaka mwisho,jamaa kaongea mabo mengi sana i wish watu wote humu tungekua tunaelewa lingala,kiukweli mngefaidi sana wandugu,dada kweli anaijua kazi yake maana alikua anamchokonoa jamaa kama hataki vile,mwenyewe kasema yote,pia kuna mahali katika interview hiyo Alain Mpela afande nae alituma ujumbe wa simu kwa mtangazaji akieleza kwamba na yeye anafuatilia kwa kutazama mahijiano hayo,dada alipomwambia Marie Paul Kwamba Alain Mpela ametuma ujumbe wa simu kwamba anafurahia na kufuatilia mahojiano hayo Marie Paul akacheka na kumwita jina flani la utani ambalo anamtaniaga,basi raha tupu kuona licha ya kwamba hawako pamoja kikazi sasa lakini bado wanacheka na kutaniana,nimeipenda hiyo interview kiukweli

 12. waziri dewa says:

  Asante sana kwa habari nzuri kama hizi,nani kama wewe kaka,jibu hakuna.wewe ndio unakamatisha mutanzania

 13. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo […]

 14. […] Aimelia aliondokaje Wenge BCBG gonga hapa. Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne LD_AddCustomAttr("AdOpt", "1"); LD_AddCustomAttr("Origin", "other"); […]

 15. […] yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo […]

 16. Frank says:

  Umejitahidi sana ktk uchambuzi lakini haya ni mapungufu kutokana na uchambuzi wako

  1.Hujatupa sababu kwanini Marie Paul alijitoa na kuanzisha Wenge el paris

  2.Kwanini Jb Mpiana aliamua kutumia nembo ya bendi na jina la bendi kutoa albamu ya Ndomboloo yenye nyimbo kama masuwa,papito n.k ,Kutokana na albamu hii ndipo mgogoro ulipo anzia kwani hata mr.mapato wa bendi Werrason hakujua mpango wa Jb ni nini? Kutokana na mkanganyiko wa kimaslahi juu ya albamu hii waanzilishi wa bendi Werrason Ngiyama na Didier masela waliamua kujitoa ila Aldoph Dominguez alifuata upepo wao,na walipotoka mwanzo bendi yao iliitwa Wenge Musica Espirit ya bien (Wenge yenye tabia nzuri)albamu ya kwanza yenye nyimbo kama likelema,kalayi boeing 2,na baadae wakabadili na kuwa Wenge Maison Mere ambapo wimbo wa Sololar bien (ongea vizuri) unamtaka jb aongee ukweli na sikupotosha ambako amefanya kupitia albamu ya titanic kuhusu chanzo cha mpasuko wao japo hawajamtaja moja kwa moja ila maudhui ya wimbo ndivyo yalivyo.Na mpaka leo upotoshaji huo bado unafanywa kama ulivyoeleza kwenye sababu zako

  3.Tunaomba utupe sababu kwanini Aldoph Dominguez kutoka Wenge Musica Maison Mere na kuanzisha kundi lake La Wenge Tonya tonya.

 17. james masele says:

  Nimegundua werrason hawezi simama peke yake kwani sijaona wimbo alioimba peke yake kama ambavyo JB hufanya. Nisaidien kama kuna,mdau anaujua wimbo wowote alioutunga na kuuimba Werra mwanza mwisho.

 18. james masele says:

  Hi… Papa Pius! Naomba tafsiri ya wimbo ” no coment shengen ” kwa faida ya BCBG’s woooote bila kumsahau Mh. Steven Masele!

 19. Anonymous says:

  hi big boss, tafadhali sijasoma historia hii ya kugawanyika kwa wenge musica sehemu ya I, II NA III. Nitazipataje?

 20. saidr380 says:

  good music maker.wenga musica bcbg

 21. Emanuel Masanja says:

  Nimefurahi sana kukutana na hii kitu. Mie ni shabiki sugu wa mziki wa Congo na nilikuwa sifahamu mengi kuhusiana na wenge music bcbg lkn leo nimepata majibu. Huwa nikisikiliza miziki ya Congo najiona akili imekaa vizuri na kujiona kama maisha nishayapatia kumbe hola! napenda sana live concert za JB MPIANA na hadi sasa nimeamua kutembelea Kishansha japo nipaone tu kulingana na starehe zinazoletwa na wanamziki wa Congo. Pamoja na kupenda miziki hiyo cha ajabu sijui hata tafasiri ya nyimbo hizo! Hivi sasa nyimbo ninazotaka kufahamu maana yake ni 48HEURS na OMBA wa JB MPIANA.

 22. Hendrick mtui says:

  Nimekukubali Mkuu, Hii ni kitu adimu sana. Mimi ni Shabiki kindaki ndaki wa JB mpiana. Kwa ujumla Natamani siku moja wenge BcBg iliudi jukwaani watumbuize japo kwa siku moja wakiwa pamoja kama zamani. NAMAANISHA WAWEPO WOTE… JB MPIANA, WERWSON NGIAMA MAKANDA, DOMININGUEZI, BLAIZE BULA, ALAN MPELA, CLITON, DIDIER MASELA, EMELIA, TOTO CALUGI, PIPINAA, ALAN MAKABA, NA WENGINEO. Sijui ni kwa nini vitu vizuri havidumu. kweli tembea ulimwenguni uone mambo (tembe na mokili emoni makambo)

 23. Wonderful post however , I was wondering if you could write a litte more on this topic? I’d be very grateful if you could elaborate a little bit more. Cheers!

 24. I believe this is certainly an informative publish and it truly is experienced and extremely handy. I would prefer to thank you for that efforts you’ve produced in writing this informative article.

 25. Once I thought about factors like: why such data is totally free right here? Whenever you compose a book then no less than on promoting a guide you receive a percentage, for the reason that. Thank you and good luck on informing persons additional about this.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: