Aifola: Kibao cha “ukweli” cha Linex nusura kimsimamishe kizimbani.

image

Binafsi huwa naupenda sana huu wimbo hasa maudhui yake na ujumbe uliomo ndani, kwa kweli mghani amefanikiwa kuiteka hadhira na kufikisha ujumbe vilivyo. Alipoookuwa akiongea na kipindi cha Wanawake Live mtunzi na muimbaji wa Wimbo huuu Linex amesema kuwa alipokuwa akishoot wimbo huu kwa bahati mbaya alimpiga kibao cha ukweli bidada aliyekuwa Video Queen kwenye video hii jambo lililopelekea bidada kununa, “alikasirika na ilichukua muda mpaka akawa poa na tuliendelea na scene nyingine….” alisema Linex na kuongeza “…Kibao kile nilijikuta kama napata hisia za ukweli na kikanitoka kweli…”.

Baada ya Video kutoka na ku hit mwanadada yule alimpigia simu Linex na kumwambia kuwa amemdhalilisha na hivyo anataka kumpeleka mahakamani, “Nilimuita tukaongea akasema anataka nimlipe milioni moja si unajua mtaani watu wamemshika masikio….” aliongeza Linex, mi nilikubali nikampa laki tano mambo yakaisha mpaka sasa ni washkaji na tunachekiana hata kwenye simu.

Ujumbe, Melody na Sauti

Rafiki yangu Mngoya Ahmedi Juma Lukuta wa Kibanda Kicheba Kwa Semkope Muheza anasema Wali wa Nazi hauhitaji mboga yenye mbwembwe hahahahaha. hii ni misemo ya kiswahili ambayo inahitaji mtu atulie aweze kuelewa mtu anamaanisha nini. Ukimsikiliza Linex  anaimba kutokana na sauti yake ilivyo hakilazimishi wala habani pua, hatii mbwembwe kwenye sauti yake.

Huyu bwana Linex mi namkubali sana ni mara chache sana kuniona mimi naweka post za Bongo Flava hapa ila kwa wanaojua muziki huu umepigwa kwenye mahadhi ya Afri Zook/Pop na utasikia Solo Gitaa linauongoza huu muziki kwa mbaali.

Linex ni mwanamuziki ambaye mi napenda kwa sauti yake tuu na jinsi anavyoipangilia na kuimba kwa hisia, kijana ametulia sana na anajua ni nini anakifanya ili kuwaridhisha mashabiki wake, kiukweli kijana anatunga sana na anajua kuifikia hadhira, hata kwenye live show stage performance yake sio mbaya “ Imbeni nyimbo zote mnazozijua, lakini najua. kimoyo moyo najua mnakiri kwamba mpaka sasa, Aifora kutoka kwa Linex ndio wimbo bora wa mapenzi kwa kipindi chote hiki cha kufunga mwaka, Nibishieni maana hamkawii….” anasema Henry Mdimu Bloga, muandishi na mchambuzi makini wa muziki wa Bongo Flava na Habari za burudani wa gazeti la Mwana Spoti. Mdimu anahaki ya kusema hivyo jaribu kuuusikiliza huuu wimbo, ujumbe, melody na sauti kisha niambie mawazo yako.

6 Responses to Aifola: Kibao cha “ukweli” cha Linex nusura kimsimamishe kizimbani.

 1. Anonymous says:

  Linex Bhana Mwachen Atambe! Mauruc Mtawa Toka Lindi Uku

 2. Anonymous says:

  Kaka Linex Xalima Imekaa Poa Xana! Mauruc Mtawa Toka Lindi *0789097528*

 3. Its my good pleasure to go to your site and to love your terrific posts here. I like it a whole lot. I can truly feel that you simply paid a lot awareness for those articles, as all of them make sense and therefore are quite helpful.

 4. After I thought about things like: why this kind of info is at no cost here? When you create a guide then at the least on promoting a book you receive a percentage, since. Thank you and great luck on informing persons extra about it.

 5. MTony says:

  Hello, is anybody here interested in online working?
  It is simple survey filling. Even $10 per survey
  (ten minutes of work). If you are interested, send me email to hans.orloski[at]gmail.com

 6. Appreciating the hard work you put into your blog and in depth information you offer. It’s awesome to come across a blog every once in a while that isn’t the same old rehashed material. Excellent read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: