SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I)

image

SURA MPYA YA BLOG NA MAMBO MAPYA!!!

Mengi yamesemwa sana kuhusiana na kuparanganyika kwa kundi hili na hatimaye kutokea Wenge zaidi ya sita huku mbili kubwa ya JB Mpiana na ya Werason zikionyesha upinzani wa hali ya juu.

Kuanzia wiki hii nitakuwa nikiwalete Makala ya Historia Ndefu ya WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE. Ilikujua nini Hasa kilitokea baada ya kupata mwanya wa mmoja wetu kuongea na mtunzi wa kitabu cha Historia hiyo. Makal hizi zitakuwa zikikujia Kuanzia leo Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ikiwa ni muendelezo, hivyo usikose kupita hapa Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, kujua kwa undani nini kilitokea na kusababisha bendi hii ya kizazi cha nne cha Musiki wa Congo kuparanganyika, ungana nasi kwenye masimulizi haya ya kusisimua EXCLUSIVE. Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

imageNilibahatika kukutana na mdau mmoja mwana familia mwenzetu wa wenge ambae yeye amekwenda mbali kidogo,ameamua kuandaa kitabu maalum kwa ajili ya Clan ya wenge “THE STORY OF CLAN WENGE”,Kitabu ambacho mimi kwa mtazamo wangu nadhani kitatusaidia sana wana wenge family dunia nzima tujue nini hasa kilitokea mpaka wenge musica bcbg 4×4 Tout Terrain original kutokuwepo tena ulimwenguni na kuifunga kabisa ama kuipunguza mijadala ya malumbano baina ya wana familia wa iliyokuwa wenge musica ya ukweli.

Kitabu kitakua katika lugha mbili,kitakua mkifaransa na mkilingala lakini nimejaribu kumshawishi akiweke pia mkingereza ili watu wa afrika mashariki pia waweze kukisoma na kukielewa kwani nimemueleza kwamba pia sehemu hizo na zambia,malawi,zimbambwe ambako wanaongea zaidi english wapo wanafamilia wengi sana wenge,ameniahidi kulifanyia kazi hilo,hivyo likifanikiwa nadhani itakua ni fursa nzuri hata kwa wasiojua french au lingala kufahamu kilichojiri hasa kwa kuwa mwandishi amejitahidi sana kuzungumza na wahusika wakuu wa iliyokuwa wenge musica original kuanzia wanamuziki viongozi mpaka wanamuziki wa kawaida,mapromota mpaka maproducer na wadau wa karibu sana.

So stay tuned,kama kawaida yetu hapa,habari zote za muziki na wanamuziki wa congo na kinachoendelea katika muziki wa congo kila wakati sisi tutakua wa kwanza kuzipata zikiwemo hizi za kitabu hiki.

Lakini kwa kuwa nilifanya nae mazungumzo ya kina muhisika wa kitabu hiki,leo nitadodosa kidogo yaliyomo ndani ya kitabu hicho kwa kuwa nimefanikiwa kuzipata dondoo zake,ila naomba kudiclare interest kabla ya kuanza kwamba mimi ni mnazi mkubwa wa JB japo simchukii WERRA pia,ila kwa kuwa leo nimeruhusiwa kukaa kwenye jukwaa hili la heshima hapa juu joho langu la ushabiki naliweka kando ili niweze kuwa fair,hivyo mtaona sehemu ambazo jb atakua alichemsha nitamgonga bila kujali,sehemu ambazo werra alikua right nitampa credit zake bila hiyana.Twende pamoja sasa:

imageArticle hii ni sehemu tu ya kitabu husika ambayo inaelezea zaidi miaka mitatu ya mwanzo ya kila kundi yaani wengee BCBG kwa upande mmoja na wengee MAISON MERRE kwa upande wa pili,itatusaidia kujua nani alifanya nini na jinsi gani baadhi walijitoa tena kwenye hizo wenge mpya mbili baada ya muda mfupi.Lakini kwanza lazima tufahamu nini hasa kilikua chanzo cha wenge musica bcbg 4×4 kuvunjika.

WENGE iligawanyika na kusambaratika vipande viwili mwaka 1997 December kufuatia sintofahamu kati ya JB MPIANA na WERRASON, Huo ndio ukweli japo unauma. Yapo mambo mengi yalizungumzwa na yanaendelea kuzungumzwa kufuatia hiyo sintofahamu iliyopelekea mtafaruku huo wa mafahali hao wawili,wengine wakidai chanzo alikua ni mwanamke,wengine wakidai JB MPIANA alikua akikerwa na udhaifu wa WERRASON Katika udhibiti wa mapato ya bendi (werrason alikua ndio mtunza fedha wa bendi ikumbukwe) lakini pia kuna wengine wamekua wakidai chanzi ilikua ni chokochoko za Mzee Papa Wemba na Koffi Olomide ambao inasemekana walikua wakiionea wivu wenge kutokana na kuwa iliundwa na vijana wadogo wakati lakini ikawa haikamatiki kwa mafanikio.

Yote yanaweza kuwa majibu lakini sababu hasa iliyopelekea sintofahamu hiyo na hatimaye wenge kusambaratika kwa mujibu wa wahusika wenyewe ilikua ni mambo mawili,kwanza kabisa mafahali hao wawili iligundulika kwamba ni vigumu kwao kufikia malengo na matarajio yao ya hali ya juu waliyokua wameshayaingiza vichwani mwao wakiwa pamoja,kila mmoja alitaka kumpanda mwenzie kichwani awe mkubwa yeye,na jambo la pili alikua ni producer wao SIMON SIPE,yeye aliona anapata hasara ku deal na lundo la viongozi 6!(JB,WERRA,MAKABA,MASELA,DOMINGUEZ,BLAIZE BULA) ambao ukifanya nao kazi wote walikua wakihitaji treatment sawa, sasa ili kubana matumizi akaona ni bora kwa upande wake awepo kiongozi mmoja ambae atakua anadeal nae kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali yahusuyo production,na mapato yatokanayo na concerts na mauzo ya cd ambayo pia yalikua yakisimamiwa na SIPE,Hapa ikjitokeza kitu inaitwa Less Leaders Mo Money…!

image

Kwa hiyo mwanzoni mwa 1998,WENGE BCBG ikazaliwa ikijulikana mwanzoni kama WENGE MUSICA BCBG Lakini baadae wakaondoa neno MUSICA kutokana na kwamba Didier Masela ambae ndio muanzilishi wa hilo jina hakuwamo kundini humo,yeye alibaki na Adolphe na Werra,wakaamua kumuachia MUSICA yake.Sasa mpaka hapa tunaona BCBG ndio ilikua bendi ya kwanza ku exist,

Hivyo ili kutochanganya mambo nitaizungumzia kwanza miaka mitatu ya mwanzo ya BCBG then MAISON MERRE nitamaliza nayo.

Usikose Jumatano kwa kujua kwa undani kuhusu miaka mitatu ya Wenge BCBG ya JB Mpiana na kuondoka kwa watu kama Dominguez, Aimelia, Ali Mbonda na wengineo. Kama una lolote tuandikie piusmicky@yahoo.co.uk au tuma sms 0713 666616.

Hapa nitakuacha na kibao cha Promesse bouboule ikiwa ni utunzi wake shujaa Allain Mpela, hiki ni moja ya vibao vilivyowatambulisha kwenye jukwaa la muziki kitaifa na kimataifa. Salamu zangu za dhati kwako Big Producer Maghambo, Hadji Le Bcbgeeque, Jema Mandali nakati ya USA, Papaa Julie We Eston Ndenge nini Papaa, Mamaa Salma Jaruf nakati ya London, na funs wote wa Blog yangu nawatakia Eid El Fitr Njema. .

68 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I)

 1. Farid wa Muscat says:

  Ama kweli hapo umepatia kweli Mzee Pius yaani hakuna blog inayotoa kitu watu wanapenda kama yako na watu wote tumeridhika kabisa tena tunakuomba usichoke kutuletea burdan ya miziki tolingi na motema ya bana wenge. MERCI MINGI PATRON

 2. Mamaa Perovee says:

  Nimefurahishwa sana na hii habari natamani ingekuwa inatoka kwenye gazeti ili niliweke kumbukumbu.
  Pius Uko juu sana

 3. mukubwa shabani says:

  Pius unaonaje ukianzisha gazeti la weekly au hata monthly kama vipi kwa kushirikiana na huyo anaejiita le jbnique na wadau wengine ambao wamekua wakitufungua macho kuhusu muziki tuupendao lakini hatuzipati taarifa zake,idea hiyo brother maana stori kama hii kwenye gazeti au magazine ingependeza sana naamini wengi wanapenda kujua mengi sema hawana access ya mtanda,pia waandishi wamagazeti wa burudani wakiiona hii wataicopy na kuichapisha wapate sifa za bila jasho,jipangeni bwana japo sisemi huku tuache hapana

 4. Mwalimu Mkumbe-muheza,Tanga says:

  Kazi nzuri..japo umekatiza uhondo tunasubiri mkubwa P

 5. MAMAA TABU FATU LA TANZANIANE says:

  Naona raha sana,sijui kwanini sikujua mapema kwamba haya mambo yanapatikana huku jamani…wamiliki itangazeni hii blogu jamani kuna blog za ovyo ovyo tu lakini maarufu kuliko blogu kama hii yenye mambo bomba hasa kwa sisi wapenzi wa bolingo,hii ipeleke kwa michuzi uwaonjeshe waifuate huku,na uhakika wakiingia huku watanasa kama mimi nilivonasa,hii imekua ni kama home page yangu sasa.

  Asante sana bwana muandishi

 6. piusmickys says:

  Poa poa tuko pamoja hapa ni Yenu mwanzo mwishoooo!!

 7. Fred Mosha says:

  Wenge Musica BCBG ilikuwa bendi ya kupigiwa mfano ila mimi nilikuwa napenda sana tungo za Werra ndani ya BCBG kama Suprise Kapangala, Coco Madimba Kaskin, Amour Nick D na Kalayi Boeing hata sasa mimi ni mdau wa Werra japo Mpiana naye anafanya vizuri

  Fred Mosha

 8. Anonymous says:

  Ni kweli Wera alikua na tungo nzuri lakini kwa Presso JB Mpiana hakutia mguu. JB ni balaa na hata sauti yake hata Koffi haipati. Nampenda sana JB na rumba zake pia. Nimefurahi sana kupata hii habari. endelea kutupa mambo matamu kama haya.

  Man of Style

 9. kihwelo, c. says:

  kaka mi nimekubali,wala sijabisha. nasubiri j’tano

 10. Anonymous says:

  Nashukuru nimepata taarifa ambayo nimetafuta kwa siku nyingi bila mafanikio. Kusema kweli Werra ni kiboko ni mwimbaji na mtunzi mzuri sana wala hatumii nguvu ktk uimbaji wake.

 11. Sadik Titanike says:

  siku zote ulikuwa wapi kaka? hii habari nasoma huku nasisimka vinyweleo nimeipenda mnooo yaani km naangalia sinemaa. napenda blog zinazohangaika kuleta habari km hivi hongera mukulu

 12. Alain Kamangu says:

  Mkubwa Pius ahsante sana kwa makala hii yako. Nataka kukujulisha kuwa katika yote haya yaliyoongelewa juu ya mgawanyiko wa Wenge ni kwamba utawala ulikuwa mbovu, na si Papa Wemba wala Koffi waliotaka kuivinja Wenge.

  Kumbuka, Papa Wemba ni mshauri ama alikuwa ni mshauri mkubwa wa Mpiana mpaka Mpiana alimshirikisha katika ile albamu yake ya Ndombolo na kuimba naye wimbo mmoja wa Calvaire Solitaire.

  Kwa kila Mcongolais (Mzaire) anajuwa kuwa Mpiana ndiye aliyekuwa chanzo cha kuvunjika Wenge kwani alikuwa anaringa sana na alikuwa hana tungo nzuri zaidi ya ile ya Kin Ebouger (1990-1991). Alikuwa anaringa kwa sababu alikuwa na mashabiki lukuki kwa ajili ya uchezaji na uchekeshaji wake.

  Tungo kali za BCBG zilitungwa na Blaise Bula Engineer ama La Voix Du Wenge (sauti ya Wenge), na Werra.

  Ni kweli Wenge walikuwa na viongozi 6 na kila mmoja alitaka utawala. Wenge ilikuwa doomed kuvunjika kwani wakati ulifika watengane na ndiyo maana walikuwa wanafanyiana vituko kwani baada ya Makaba kutoa albamu yake minong’ono ikaanza ndani ya kundi. Wengi walimlaumu sana Makaba kwa kutoa ile albamu ila Mpiana aliunga mkono kwani naye pia alifuatia kufanya hivyo kwa kutoa ile albam yake ya Ndombolo Ya Solo.

  Na baada ya hapa ndipo uhasama ukaanza kwani kina Makaba (swahiba wa Mpiana), na Blaise Bula wakawa upande wa JB Mpiana, kina Chouchou de Tout Le Monde (Ado Dominguez Ebondja Elongo) na President Masela wakawa upande wa Werra.

  Ikumbukwe kuwa Mpiana siyo muasisi wa Wenge Musica. wasisi wa Wenge ni Masela President na Werra, Mpiana alikuja Wenge baada ya muda kidogo na alikuta bendi imejijenga tayari.

  Baada ya mtafaruku wa muda mrefu ndipo Werra na masela wakahamua kuachana na Mpiana na kundi lake na wao kuunda Wenge Musica Maison Mere (yaani Wenge Musica ya asili ama Mama ya Wenge) kwani waasisi ni hao kina Masela na werra siyo Mpiana.

  Baada ya kusambaratika kwao, kina Blaise Bula na Makaba nao wakatoka kwenda kuunda Wenge zao na huku kina Masela na Dominguez wakatoka kwenda kufanya hivyo hivyo.

  Ila kwa bahati mbaya katika Wenge zote hizi ni Werrason pekee ndiye aliyeweza kudumu mpaka leo hii nakuandikia huu ujumbe. Mpiana toka 2005 hana jipya ni kama kaishiwa na hapa Kin watu wameshaanza kumuona mbabaishaji tu. Yeye hupiga nyimbo za matangazo ya bia tu na promosheni lakini hamna kipya kwake.

  Binafsi namfagilia sana Engineer Bula ila naye kwa bahati mbaya naona kaishiwa siku hizi si kama yule wa enzi zile za Ave Maria.

  Ninayo stori ndefu sana ya Wenge ila siwezi kubandika hapa mpaka nione hiko kitabu na kukisoma. Ahsanteni!

  • piusmickys says:

   Merci Mingi Kamangu, Fatilia hapa kesho kujua sehemu ya pili na Ijumaa utasoma sehemu ya Tatu na ya Mwisho.
   Kumbuka hapa tumeongelea Miaka mitatu ya hizi Wenge Mbili na Sababu ya Werason na JB Mpiana kutengana.

   Karibu Sana

   • Alain Kamangu says:

    Nimekupa mukubwa na merci mingi a vous aussi!

   • Seated App says:

    I actually felt my brain growing when I browsed your post. My life will be changed forever because of this. Pinterest professionals would agree with your website. My girlfriend is trying to discover more about this issue. Hello from Ohio.

  • Nonana says:

   You hate Mpiana too much

   • Alain Kamangu says:

    Hapana, si kweli. Ila ukweli ndiyo huo juu ya kuvunjika kwa wenge. Sipe ni kweli alisababisha kuvunjika kwao ila Mpiana na Werra walikuwa na vita baridi among them. So this band was doomed to die. Hayo kuhusu mimi kumchukia Mpian na mawazo yako na sikubishii kwani fikiria unavyotaka wewe.

  • Hadj Le Jbnique says:

   Eeh!hii kali pamoja na ujanja wangu wote wa kuifuatilia wenge sijawahi kuisikia wenge mpya iliyoanzishwa na Alain Prince Makaba,labda jamaa yetu kutoka Kinshasa ututajie jina la hiyo wenge ya makaba,maana wenge zinazojulika ni hizi,bcbg ya papaa na daida le souvereign binadam jb mpiana a.k.a.salvatory de la patria mwana congo,Wenge Maison Merre ya kwake Werrason De La Forret papa na Exocee,Wenge Tonya Tonya ya Le Big Tata Mobitch Adolphe Dominguez,Bendi ya Blaize Bulla japo sidhani kama anaiita wenge,hiyo ya wenge iliyoanzishwa na makaba baada ya kutoka BCBG ni ipi?Ninavyojua Alain Makaba baada ya kuachana na Bcbg hajawahi kuanzisha wala kujiunga na bendi yeyote licha ya kubembelezwa kila kukicha na werrason ajiunge nae,amekua akikataa na kujikita katika studio yake huko ubelgiji akiwa kama producer wa muziki

   Papa wemba kweli alikua mshauri wa JB lakini na Koffi le Rambow du Zaire nae alikua msahuri wa Werra pia japo siku hizi wamekua ndio maadui wakubwa.

   Alieivunja wenge SIMON SIPE,Werra na Jb walitumika tu.Jb hakua muanzilishi sawa tunakubali wote wala hakuna asiejua hilo,yeye alikuja baadae,lakini je kabla ya kuja Jb wenge ilikua inajulikana na nani?ilikuwaje bendi ikawa kimya mpaka Jb alipokuja kuitoa mafichoni na MULOLO na KIN E BOUGE yake?na je ilikuwaje kina Werra waanzilishi mpaka wakampisha wakuja JB awe kiongozi wao?unadhani kwa nini walikubali kutawaliwa na mgeni?

   Halafu unasema Werra na Masela walitoka kwenda kuanzisha Maisono Merre,halafu badae eti Adolphe akatoka kwenda kuanzisha wenge tonya tonya,hapa unachanya mambo,Adolphe alitoka pamoja na kina Werra na Didier Masela Kwenda kuianzisha hiyo Maison Merre,japo Werra baadae aliwazunguka wenzake kwa kuwatumia vijana kuwahujumu kina Adolphe,mpaka kuna wakati ilikua paris kwenye concert vijana wa werrason kina Bill clinton walimvizia Adolphe na kubandika Big G kwenye Kiti chake huko back stage ili akikalia big g nguo iharibike ashindwe kupanda stejini werra atawale pekee yake,kaa hapa zipo stori nyingi zinakuja huko mbele u will see things,utaona mpaka Marquis de maison merre ilivyozaliwa.Tatizo Werra kwenye mambo ya hela anapunja sana.

   Jb hana kitu zaidi ya matangazo ya bia,hii nayo kali,ina maana huko kinshasa album mpya ya jb soyons serieux haijafika bado?

   Aaah poa bwana ni mtazamo na mahaba yako lakini

   • Alain Kamangu says:

    Kijana sikia. Kabla ya kujibu mapigo ama shutuma tafadhali naomba usome tena reply yangu ndipo unijibu nami nitakufafanulia kama hujanielewa:

    Yes Mpiana alikuja Wenge baadaye na kutoa changamoto kwenye nyimbo zake za awali. Wenge ilianzishwa mwaka 1983 na ikawa mafichoni miaka yote hiyo. Katika kipindi hiki walitoa nyimbo nyingi tu underground kwani bado walikuwa wachanga mno na walikuwa hawajapata a big break yet.

    Kama sijakosea, kuna siku moja nafikiri mwaka 1987 mishoni ilitokea tamasha moja la muziki wa Jeune Vedette hapa Kinshasa na Wenge chini ya kina Aime Buanga, Ya JB Papa na Daida, Werra, Bula, Ado Dominguez na wengineo walitoa fora sana pale Commune Societe de Bandal (Bandalungwa). Na mwaka uliofuatia wakaalikwa kwenye Television national OZRT na kuanza kutambulika kwa fujo kwani kipindi hiki bendi nyingi zilikuwa zikiishi Ulaya na ngome ya Zaiko Langa Langa ilisambaratika na muziki ule wa lika la Zaiko (Papa Wemba, Bozi Boziana, Evoloko Jocker, Le Grand Zaiko Wawa, Minzoto, Choc Stars ya Ben Nyamabo, Victoria Eleison) nyinginezo nyingi tu zilikuwa zinafifia.

    Hapa ndipo Wenge ikapata a big break. Kwani walikuja na nyimbo kama vile Mulolo (JB Mpiana), Ave Maria (Ya Blaise Bula), A Moi Nicky D (Werrason)…yaani palikuwa patamu sana, na walikuja na ule mtindo wao wa Bouger, Bouger…..ah Kin na biso…mawa trop, yaani kweli ilikuwa raha tupu kipindi kile.

    Nirudi kwenye makala yako ama majibu yako.

    Nilisema kina Werrason, Masela, na Tata Mobitchi (Dominguez) walijiengua na kuanzisha Wenge Musica Maison Mere na kumuachia JB na Wenge BCBG.

    Pale Maison Mere nako Werra alikuwa anabania sana pesa na kukosana na Dominguez kitendo kilichomfanya naye ajitoe kwenda kuunda bendi yake mwaka 2001.

    Mkaba yeye hutoa albam zake kama a solo artist ila anajiita kama Makaba Du Wenge Musica ili atambulike zaidi kibiashara. Na Blaise Bula naye anafanya hivyo hivyo. Bula bendi yake inaitwa Ponderation 8 ya Ingineur Blaise Bula de Wenge Musica.

    Kiukweli ni kwamba kuna Wenge Musica ama Wenge 5 tu ndizo zinazofahamika.

    (1) Wenge Musica ya Mpiana (Wenge Musica BCBG)
    (2) wenge Musica ya Werrason (Wenge Musica Maison Mere)
    (3) Wenge Musica ya Marie Paul (Wenge Musica Aile Paris)
    (4) Wenge Musica ya Aime Buanga (Wenge Musica Kumbela)
    (5) Wenge Musica ya Tata Mobitchi (Wenge Tonya Tonya)

    Nimechoka kuandika naishia hapa. Ila tambua kuwa hii bendi ya Wenge ilikuwa doomed kufa kwani werra na Mpiana walikuwa na vita bariidi miongoni mwao haswa kwa kuwa Mpiana si muasisi wa wenge na yeye Mpiana ndiyo alitaka atambulike kama muasisi wa Wenge kitu ambacho kilimkera werrason.

   • Alain Kamangu says:

    Ningependa siku ukipata muda uje hapa Kin uone nani anayekamata soko la muziki hapa. Ni kweli JB ana wapenzi wake ila kimuziki kaishiwa hana jipya JB. Yaani anapitwa hata na kina Kabose, Fally, na Ferre….Mawa trop!

   • Didistone says:

    kamungu mpiana kaishiwa?kaka tafadhali kidole na macho,na hii hapa chini vipi…

   • Mukubwa Shabani says:

    “Mpiana alitaka “atambulike” muasisi wa wenge kitu ambacho kilimkera werrason”.Hapa sijamuelewa mukubwa wa kinshasa anamaanisha nini,alitaka atambulike na nani hivyo?
    Hivi huyu jb alikua na nguvu kiasi gani na ujasiri wa namna gani kiasi awakute watu tayari na kitu chao then yeye aliyeletwa tu tena kaletwa na makaba ambae nae alikua wakuja pia aweze kuwaovertake waasisi wote na yeye kukaa mbele na bendi kuendelea kutoa album na kupiga shows since 80’s mpaka 90’s bila ridhaa ya hao waasisi?hii katika hali ya kawaida haiwezekani japo tuko mbali na kinshasa.

    Mimi nasema hivi…kama unamuona mbwa yuko juu ya mti usiulize amepandaje uliza nani alimpandisha kwani katika hali ya kawaida mbwa hawezi kupanda juu ya mti bila kupandishwa.

    Melesi mingi.

   • Hadj Le Jbnique says:

    Kwanza kabisa naomba kusema kwamba mapendo au ombi lako la kunitaka nije kwanza kinshasa sijalikubali sitakanyaga hapo labda Jean Pierre Bemba awe rais.Pili bwana mkubwa sisi tuna comment on kile uliandika,nikukumbushe kwa kunukuu bila kuhariri neno hata moja,kuna sehemu uliandika hivi:

    “Baada ya mtafaruku wa muda mrefu ndipo werra na masela wakaamua kuachana na mpiana na kundi lake na wao kuunda wenge musica maison mere” mwisho wa kunukuu.Sasa nataka kujua haya maneno uliyaandika wewe mwenyewe au kuna mtu aliyagushi na kupoteza maana uliyokusudia?Maana hapo hatujaona jina Adolphe Dominguez likitajwa kwenda kuanzisha maison mere.

    Then ukaendelea kuandika nanukuu tena:

    “Baada ya kusambaratika kwao,kina Blaize Bula na Makaba nao wakatoka kwenda kuunda wenge zao na huku kina Masela na Dominguez wakitoka kwenda kufanya hivyo hivyo”.mwisho wa kunukuu.Sasa soma sawa maandishi yako halafu upime mwenyewe kama hukustahili kujibiwa vile.

    Jb mpiana anapitwa mpaka na Kabose Bulembi na hiyo “ELECTION” yake aliyoirelease! hapa sina comment

    Ila kuna mahali naomba nichangie kidogo,umesema wenge walimlaumu makaba ku release solo album,hapa nadhani unamaanisha ile album ya “POILE OU FACE” mwaka 1995 .Walimlaumu kwanini sasa?hukutufafanulia.Mi nadhani labda ungesema Werrason alimlaumu makaba kwa hiyo album labda japo mimi sijawahi kusikia hilo.Lakini iweje wamlaum,mbona yeye alifanya hiyo album kwa kuwashirikisha watu watatu tu toka wenge,ambao ni Titina,Le grand chibuta roberto ekokota na jb,wengine hawakuwa member wa wenge maana alimshirikisha mzee Sam mangwana,Dindo yogo,Luciana Demingongo,Abby Suriya,Ballou Cante na King Kester Emeneya ambae wengine wanamwita victoria eleison sijui kwanini.

    Halafu JB hajawahi kutoa album inayoitwa ndombolo labda unamaanisha Feux de L’amour,tukubali tukatae mitafaruku ndani ya wenge haikua baina ya werra na jb tu,kama mfuatiliaji wa mambo hapo kin december 1997 sijui kama ulikua umeshaingia congo,ndani ya Grand Kin Hotel kulifanyika concert ya wenge ambayo hakuna mpenzi wa muziki hasa wa wenge ndani ya congo ataisahau maana concert hiyo in all names ikabatizwa
    as “concert de la separation” baade, Tafuta video uone kilichotokea baina ya werra na blaize bulla mbele ya papa wemba ambae alikuja hapo kama mualikwa,Kiufupi tu ni kwamba Sele na Werra siku hiyo walitukanana sana,Sele akamwambia Werra maneno hayo “rafiki yangu kila siku unaota uwe kama mimi,uwe kama Jb,uwe kama Makaba,hizo ni ndoto kaka yangu” mwisho wa kunukuu.Hapo ndio utaona vile joto lilivyokuwa kali kundini humo kwa wanamuziki wote sio issue ya werra na jb pekee kama unavyodai.Otherwise tuko pamoja cuz constructive criticism are most welcome to me alwayz

  • MUKONGO says:

   MABWANA NA MABIBI WA EAST AFRICA tANZANIE ….MI NAFURAIA KUONA MUSIC WETU SOTE TUNAPENDA NA PIA LUGHA YA KISWAHILI. MIE NITATOFAUTIANA KIDOGO NA WALIOTANGULIA KWA KUELEZA MOJA YA UKWELI….

   WENGE NI BAND ILIOKUWA NA MUSICIE WENGI …ILA IKUMBUKWE KWAMBA KATIKA HAWA MUSICIE JB ALIKUWA MASIKINI NA DECATION YAKE KWA BAND NA USISAHAU VOCAL(SAUTI) NDIO ILIMUWEKA MBELE…MFANO MUDOGO.MUNAJUA KOFFI NA PAPA WEMBA WALIKUWA KWENYE BAND MOJA,LAKINI PAPA WEMBA ALIKUWA JUU SANA SHAURI YA SAUTI YAKE NA KOFFI ALIFUNIKWA NA SAUTI YA PAPA WEMBA..KOFFI ALIONDOKA NA AKAJARIBU KUPIGA MUSIKI AMBAO ULIKUWA MUSIKI WA POLE POLE SANA…
   NIRUDI KWA JB NA WERA…JB SAUTI YAKE NDIO ILIMUWEKA
   PALE NA NIUKWELI MABOSS WALIKUWA WENGI NA YEYE JB HAKUKUWA NA FARANGA HIVO ALIANZA KUPATA PESA ZAIDI NAKUFUNIKA WENGINE..

   ILE KUSEMA JB HAKUWA NA NYIMBO MUSURI SI KWELI…PALE ALIPOTOA MIMBO YA Feux de Amour http://www.youtube.com/watch?v=tX6T1QCNA8M&feature=related
   PIA WATU WENGI CONGO WALIKUWA WANASEMA JB TALENT YA KUANDIKA MIMBO SASA ALISEMA ATAFANYA NYIMBO NYINGI SANA..NA WENGI WALISEMA WENGE YA JB INGEKUFA LAKINI ALIJITAIDI NAKUPATA CONTRACT KATIKA COMPANY ZA BEER KABLA YA MUSICIAN YEYOTE CONGO…

   PRACTICE KATIKA BAND YEYOTE NI MUHIMU SASA WERRA HAKUKUWA AKIWAPO NA HIYO ILIFANYA BAND YAO YA MWANZO HAIKUKUWA NA ALBAM NYINGI NA JB ALIPENDA KUTOSHA ALBAM NYINGI…

   SIKU INGINE WAPENDWA…SOTE TUNAPENDA MUSIC WA WERRA NA JB ..FERRE GOLLA NA WENGINE

   MUKONGO

  • Farid wa Muscat says:

   Patron Kamangu Naomba tuwasiliane ,sijui nitakupata vipi?

 13. chembera says:

  mkubwa,hata mimi nashangaa kitu kizuri kama hiki kilikuwa wapi muda wote huo…ngoja nisubiri sehemu inayofuata nitachangia…ubarikiwe

 14. EDMAS says:

  Bro kamangu nakuaminia kaka.

  Nanukuu “Kwa hiyo mwanzoni mwa 1998,WENGE BCBG ikazaliwa ikijulikana mwanzoni kama WENGE MUSICA BCBG Lakini baadae wakaondoa neno MUSICA kutokana na kwamba Didier Masela ambae ndio muanzilishi wa hilo jina hakuwamo kundini humo,yeye alibaki na Adolphe na Werra,wakaamua kumuachia MUSICA yake.Sasa mpaka hapa tunaona BCBG ndio ilikua bendi ya kwanza ku exist”,

  Hapa sikubaliani na mwandishi, vile baada ya sintofahamu hiyo hawa watu waligawana vyombo na kila kitu kilichohusu bendi hiyo, na akina werra wakawa na haki ya kulitumia jina la Wenge Musica, mpiana na wenzie wakaamua kujiita wenge BCBG. Mpiana ndie alikuwa wa kwanza kutoa albam ikafuatiwa na werra mwezi mmoja baadae. hivo si kwamba BCBG ndio ilianza ku-exist.

 15. Hadj Le Jbnique says:

  Subiri huko mbele utaona jinsi kina werra walivyoanza upya ku recruit vijana waunde bendi mpya,kumbuka wao walibaki watatu tu,sasa bendi gani ya watu watatu kaka,ulishawahi kuiona bendi dizaini hiyo,bila shaka jibu lako litakua hakuna bendi ya watu wa watatu,mbele utaona walivyoita vijana wa congo toka kila kona wanaohisi wana vipaji vya muziki waje kujaribiwa,walijitokeza wengi akiwemo huyu Fally Ipupa,sasa ilikuaje fally hakujiunga,je alifeli au nini kilitokea,fuatana na muandishi

 16. […] kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. […]

 17. Fatuma Mtanga says:

  Thank u very much ndugu mwandishi,mimi nilikua siijui hii blogu nimetka kule kwa michuzi,kumbe mambo iko huku sibanduki,ndio kwanza nakaa kitako,napenda miziki ya bana kongolee ile mbaya.lete vitu tunasubiri

 18. samson says:

  Hii Baab kubwaa!!Nakumbuka niliwahi kununua Radio kubwa yenye CD Deck ya juu kwa ajili ya kusikiliza nyimbo za WENGE

 19. […] Hii ni muendelezo wa Sehemu ya Kwanza ambayo tuliona vile Wenge Musica BCBG ilivyo vunjika, na Sehemu ya Pili ttukaona Jinsi Wenge BCBG […]

 20. PDJ says:

  mimi nasema hivi mashabiki wa werra mashabiki wa mpiana wote tolingana jamani,tuache kurumbana na kugombana,wote wanajitahidi kufanya kazi nzuri na sasa hivi wenyewe wanaelewana nasikia mpaka wanafanya kazi za matangazo ya kampuni ya bia ya huko kwao pamoja,sisi tunatoana macho hapa

 21. Alain Kamangu says:

  Mukongo acha uongo. Koffi Olomide hata siku moja hajawahi kuwa mwanamuziki wa Viva La Musica (Papa Wemba). Kumbuka wakati Papa Wemba alipojitoa Yoka Lokole (hii ni Clan ya Zaiko Langa Langa) akaanzisha Viva La Musica mnamo mwaka 1976. Kipindi hiki Koffi alikuwa mwanafunzi Ulaya, ila alipokuwa anarudi likizo huku Kin alikuwa anaalikwa na Papa Wemba kuimba naye kwani nyimbo nyingi za Viva La Musica za awali alikuwa anatunga Koffi. Yaani Koffi alikuwa anaitungia bendi nyimbo wakati yeye yupo Ulaya anasoma lakini hajawahi kuwa mwanamuziki wa Viva La Musica hata siku moja, huu ni uwongo. Koffi alipoanza music alikuwa anatunga nyimbo na kuchagua nani wa kuimba naye, na mara nyingi alikuwa anaimba na bendi zilizo juu kwa kipindi kile kama Viva La Musica na Zaiko Langa Langa.

 22. Alain Kamangu says:

  PDJ nakubaliana na wewe. Hapa watu watalumbana lakini suluhisho alitapatikana. Kiboko ya yote hii ni kuwa mwenye uwezo aje hapa Kin aone ni nani aliye juu kati ya Werra na JB then mtajaza wenyewe lakini huku kuandika tu hakusaidii kitu kwani naona watu wengi wanaandika ni kama vile wana hasira zao wenyewe.

  • mwana paris says:

   kamungu hizo bendi zote zikisharekodi nyimbo lazima zije ulaya sasa basi na walio ulaya wanaweza kukutaka na wewe uje ulaya kwenye hizo maconcert za hizo bendi huku,kumbuka muziki walingala sio wa wana kin peke yao,unapotaka kuchangia changia kwa angle yako sio kuzuia ambao hawako kinshasa wasichangie wanachojua eti mpaka kwanza wafike kin!!! je bercy ipo hapo kin?zenith na olympia zipo hapo?sasa kuna watu tunazisubiri huku wengine canada wengi us etc

 23. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza […]

 24. Mukubwa Shabani says:

  watu wanakuchallenge wewe ulipovuka mpaka na kusema jb kaishiwa,hana nyimbo zaidi ya kufanya matangazo ya bracongo tu!anashindwa mpaka na kabose…lakini mzee watu wakakukumbusha pamoja na hayo matangazo ya bracongo ambayo yanawaingizia chapaa nyingi na kirahisi wanamuziki wa congo kuliko wanapotoa album,jb na bcbg yake wanayo album mpya ambayo imeingia sokoni pamoja na malewa no.2 ya wmmm,album hiyo inaitwa Sayons Serieux,mambo ya “amataka na mpunda” utaifananisha na ile takataka ya ELECTION ya huyo kabose?acha ushabiki kupita kiasi tizama video hiyo hapo chini,kabose anaweza kujaza uwanja namna hiyo?hiyo ni huko huko congo kwako,mi sijui hata ni mji gani lakini nina uhakika ni ndani ya congo ambako jb kaishiwa siku hizi!

  • James Masele says:

   Ndugu zangu tuwe wawazi Jb Mpiana ameitambulisha vizuri Wenge Musica.
   Ametunga ama kuimba peke yale rhumba nyingi tu kama feux de l’amour, omba n.k
   Jb akiwa na wenge original alifanikiwa kupata tuzo nyingi tu na si kwa Wera ambae hakupata tuzo yoyote.
   hivi nambieni wera katunga ama kuimba wimbo gani peke yake? Bila msaada wa vijana?
   Hivyo Jb mpiana ni mwamamuzi kamili. Hana kinyongo na ndio maana huwa anawakumbuka kwenye nyimbo zake hasa wa omba huwataja majina kina Afande, aimelia,tutu na makaba vipi wera anaweza kumtaja ferre?
   Mnakumbuka nyimbo kama masua, education, bana lunda, calvairem solitare, top module nk
   Jamaa yuko juu sana acha aitwe mukulu.
   Yuko juu ya wera hivi wakipigiwa vyombo waimbe na wera bila kushirikisha waimbaji wengine wera ataimba wimbo upi peke yake?

 25. Mukubwa Shabani says:

  Kamungu check na hii hapa

 26. Mwalimu Mkumbe,Muheza,Tanga says:

  kamungu nawewe lete ushahidi kama wenzako acha stori otherwise piga kimya!

 27. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na […]

 28. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na […]

 29. Anonymous says:

  duh nimekubali mkuu maana umenipa story yenyewe kabisa thank man

 30. odran chaula says:

  Nimefurahi saaana kuipata hii blog sita banduka hapa,kuhusu JB kwa upande wangu ni bonge la mwana muziki albam yake mpya ni nzuri sana pia ile Ant Telo pia TH na. Intarnet na Titanic zinanifanya nimuogope sana mimi kwenye gari yangu nina cd za JB tu napenda sana muzic yake ,kwamba kaishiwa sio kweli JB ana toa albam kila wakati lkn Wera hafanyi hivyo anae sema JB kaishiwa ana lake jambo

 31. […] na Werasson kabla hajaamua kutoka kivyake, Kama ulipitwa Aimelia aliondokaje Wenge BCBG gonga hapa. Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne LD_AddCustomAttr("AdOpt", "1"); […]

 32. musakisamba says:

  tuna taka kujua mengi kuhusu ilo kundi kubwa huli mwenguni kwaku himba nyombo mzuri zenye kufuraisha kila mtu ulimwenguni tu ambie mengi tafadhali

 33. […] kuangalia kuanzishwa kwa kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba […]

 34. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza […]

  • Wakuzata says:

   Kwa mtazamo wangu, wachangiaji wengi wamegawanyika kwa JB na Werrason, ila ukweli ni kwamba sisi mashabiki wa WENGE bado tunatamani kundi hilo lirejee upya, japo mie nafahamu tatizo lililoochangia kusambaratika ni JB hata kama watu watachukia na albamu yao ya Pentagone na ziarfa ya Tanzania mwaka 1998 ndiyo kinachoelezwa kisa na mkasa.

 35. ชา tmix says:

  Good day I am so grateful I found your web site,
  I really found you by mistake, while I was searching
  on Aol for something else, Regardless I am here now
  and would just like to say thanks for a incredible post and
  a all round interesting blog (I also love the theme/design), I don’t have
  time to read through it all at the moment but I have book-marked it and also added your RSS feeds,
  so when I have time I will be back to read much more, Please do keep
  up the great b.

 36. starford says:

  Jb mpiana is the best in congo…..sijawaho ona km yeye,,,,,,,kama unabisha shauri yako. Nafunga mjadala

 37. jb ni mwanamziki bora sana ila tukumbuke kila kilicho na mwanzo kinamwisho ndio maana mnamuona jb kaishiwa

 38. Fredy says:

  Kama kuna dhambi ambayo wapenzi wa muziki wa lingala wameifanya hapa duniani basi ni kusema JB MPIANA si lolote kwa WERA, hebu sikiliza ule wimbo wa NO COMMENT SHENGHEN , kautunga yeye na kuimba yeye akisaidiana na wenzake, ni muziki wa viwango vya kimataifa. lakini pia sikiliza wimbo wa PAPITO MBALA, CAVALIE SOLITARE,I LOVE YOU,DOUGLAS ILUMBE, FEUX DE L’AMOUR kwa kweli mpiana ni kama yule tumtarajiaye ambaye hatujui siku wala saa tumpe heshima yake MUKULU.Lakini pia nakubaliana na mchangiaji aliyesema anamkubali sana BLAISE BULA “ENGINEER” hajakosea kwani Blaise kama anavyoitwa Engineer anastahilii ukiangalia umahiri wa sauti yake hakuna anayeweza kumuiga ukisikia nyimbo za wenge za sasa bila sauti ya engineer zinapwaya sana ,lakini pia ile staili ya uchezaji nayo ni ya upekee sana (angalia live ya Parii-Bataclan au Ivory coast, au ile ya London) Pamoja na hayo kumi ni katika utunzi na ufundi wa kuchomeka maneno pale wimbo unapokwenda hewani sikiliza CHOUCHOU DE LONDON, MASAMPU, FILANDU,MASUWA NA LIKALA MOTO…Elly eee!!!..,Alino kizaazaa!!!. Jamaa anajua aisee pengo kubwa kwa Jb.
  Kama tulivyoona sababu kubwa ya kusambaratika kwa wenge ni pesa, basi pesa hizo hizo zinaweza kuwakusanya wenge musica bcbg 4×4 wakafanya shoo moja tu katika sehemu ambayo promota ataona inafaa sjui ni wapi kuna mashabiki wengi wa wenge? labda Dar es salaam??

 39. Mimi nawapongeza sana washabiki wa WENGE MUSICA wenzangu mjadala huu unaonyesha jinsi tulivyohuzunishwa na kusambaratika kwa kundi hili la music wa congo. ama kuhusu werra na JB kuwa nani mkali zaidi mimi naona kama wapo sawa na hawatofautiani sana na kama tofauti ipo basi MPIANA yupo juu kidogo ya werra. sababu ni kwamba werra aliweza kung’aa tu wakati alikuwa na watu mashuhuri kama Domingez na Masela baada ya kuachana nao hakuna albamu aliyotoa ikawika sana lakini mpiana tangu mwanzo alikuwa na wanamuziki ambao hawakuwa na majina sana ndani ya wenge kama Masela na Domingez. Makaba huwezi kumlinganisha na hao wawili. Lakini mpiana alisimama na kugonga ngoma kalikali.

  Hitimisho: Hata wao Mpiana na Werra wanaogopana na ndio maana kwa sasa ni marafiki sana kuliko hata wale waliokuwa nao kwenye bendi zao.

  Ahsante

 40. Mimi nawapongeza sana washabiki wa WENGE MUSICA wenzangu mjadala huu unaonyesha jinsi tulivyohuzunishwa na kusambaratika kwa kundi hili la music wa congo. ama kuhusu werra na JB kuwa nani mkali zaidi mimi naona kama wapo sawa na hawatofautiani sana na kama tofauti ipo basi MPIANA yupo juu kidogo ya werra. sababu ni kwamba werra aliweza kung’aa tu wakati alikuwa na watu mashuhuri kama Domingez na Masela baada ya kuachana nao hakuna albamu aliyotoa ikawika sana lakini mpiana tangu mwanzo alikuwa na wanamuziki ambao hawakuwa na majina sana ndani ya wenge kama Masela na Domingez. Makaba huwezi kumlinganisha na hao wawili. Lakini mpiana alisimama na kugonga ngoma kalikali.

  Hitimisho: Hata wao Mpiana na Werra wanaogopana na ndio maana kwa sasa ni marafiki sana kuliko hata wale waliokuwa nao kwenye bendi zao.

  Ahsante

  • fredy says:

   Yaa! ukweli ni kwamba WENGE MUSICA BCBG 4X4 haipo ,swali la msingi ni je tutarajie kutokea kundi jingine lenye makali kama ya WENGE? Au je tufanye nini sasa mashabiki na manazi wa iliyopkuwa wenge? je tuanzishe wenge club? ambayo tutakuwa tunakutana na kuzipiga zile za wenge pamoja na kubadilishana mastori mbali mbali ya wenge.
   Ushauri wangu ni huo kwanini sisi wana wenge family tusianzishe kitu chetu Fulani ili na wapenzi wengine watuige? naomba maoni yenu mnasemaje wadau?

 41. Nashukuru sana kwa wazo zuri kabisa la kuanzisha WENGE CLUB angalau mashabiki wa wenge tupate mahari pa kukutana na kubadilishana mawazo na kuliwazana baada ya kuwamisi sana wenge musica group.

  Contact: Mimi nipo Tanzania Dar es Salaam
  sehemu ya MBEZI LUIZ
  Karibuni sana.

 42. Anonymous says:

  NDUGU ZANGU KUTOKA CONGO KARIBUNI DAR ES SALAAM, TANZANIA. MKIFIKA KARIBUNI KWANU MTALALA BURE NA TUTAJIKUMBUSHA NYIMBO ZA WENGE

 43. Emanuel Masanja says:

  kuvunjika kwa hili kundi kumepanua zaidi wigo kwa Werra na JB kujulikana kwamba walikuwa na uwezo mkubwa katika gani ya miziki kwani bado hawajachuja.

 44. Anonymous says:

  Asante mzee wangu leo umeweza kunifungua macho na kisa hiki kilichofichika kwa muda mrefu sana, nami ni mwana familia wa jumba kubwa la musica (wenge musica) mzee wangu ina maana hata hule wimbo wa TITANIC wa jb hulikuwa unahusu kuvunjika kwa wenge musica?

 45. NDUGU ZANGU WANAFAMILIA WA WENGE NAOMBA KUULIZA HIVI YULE MSICHANA PEKEE KWENYE ALBAMU YA PENTAGONI YUPO WAPI SASA? NA ANAFANYA NINI? NAPENDA KUJUA MAENDELEO YAKE MAANA ALIKUWA MAHIRI SANA

 46. Anonymous says:

  Hivi hii blogu bado hipo active?,

 47. I want you to thank for your time of this great study!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: