SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – III

 

image

Pichani ni JB Mpiana akiwa na ma stage show wake wakiwa katika moja ya show za Wenge BCBG

Baada ya majuzi kuona jinsi akina Tshai Ngenge, Acolpa Alba, Rio na wengineo walivyoingia Wenge BCBG sasa tunaendelea na jinsi Wanamuziki wengine walivyoingia na kutoka BCBG.

Makala Hii ni muendelezo wa Sehemu ya Kwanza ambayo tuliona vile Wenge Musica BCBG ilivyo vunjika, na Sehemu ya Pili ttukaona Jinsi Wenge BCBG ilivyoundwa na sasa tuko Sehemu ya Tatu.

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA. Sasa Endelea…

Wakiwa katika maandalizi ya safari hiyo ya Paris, bahati mbaya Blaize Bulla akapata viral infection kwa muda mrefu, hivyo akashindwa kuungana na wenzake kwenda safari hiyo. Lakini anadai alipokuwa kwenye hali hiyo JB na Makaba walimtosa, hawakumjali sana yeye wala afya yake badala yake wao wakawa focused kwenye mafanikio ya concerts hizo hasa ikizingatiwa hizo ni kumbi kubwa na zenye heshima ya pekee na wao ndio wamepata nafasi ya kwanza kutumbuiza huko kabla ya mahasimu wao MAISON MERE, hivyo walipania kufunika, kutokana na hatua hiyo Blaize Bula inasemekana alihuzunika sana,kuapa kuamua kuitosa BCBG rasmi akiwa kitandani na bendi ikiwa ulaya.Lakini inaonekana ni wazi Blaize Bula alikua akimlenga zaidi Jb Mpiana kwani ndio anaeishi Kinshasa ambako yeye alilazwa. Kwani kama tulivyoona huko nyuma makaba wakati huo alikua tayari ameshahamia ulaya akiungana na wenge pale inapokua na show za huko na wakati wa kurekodi album na alikua akifanya hivyo toka enzi za wenge original ikiwa katika siku zake za mwisho mwisho hivyo basi hata this time BCBG walikutana nae hukohuko. Hilo la Blaize Bulla likabaki Kinshasa.

image

Pichani ni Werason, JB Mpiana na Blaise Bulla wakitumbuiza mwishoni mwa miaka ya 80 huko Congo

 

Bendi ikasafiri bila Blaize Bula mpaka Paris.Lakini wakiwa katika maandalizi kuelekea siku ambayo watapiga zenith ambako ndio walipangiwa kupiga kwanza kabla ya olympia,ulizuko mgogoro kati ya JB na Makaba,mgogoro ambao chanzo chake kilikua ni makaba kutokubaliana kabisa uamuzi uliochukukuliwa na bendi huko Kinshasa ku-recruit wanamuziki wapya ambao makaba aliona kama hawakuwa na uwezo wa kutosha kuwa wanamuziki wa wenge BCBG  mpya,hapa tukumbuke kwamba katika mtiririko wa vyeo walivyopeana makaba alikua ndio artistic director hivyo hakuwakubali wasanii wapya yani Jules Kibens, Rio, Chai Ngenge na Genta.

Mgogoro huo ulidumu mpaka siku ya show yenyewe ndani ya zenith  dakika chache kabla ya kupanda stejini kuanza show kulitokea majibizano ya maneno baina ya marafiki hao yaliyopelekea mpaka JB Mpiana kulia machozi baada ya Alain Makaba kutumia maneno makali sana yaliyofanana na matusi dhidi yake, JB aliumia sana moyoni kwani kazi ya ku recruit aliifanya Blaize Bula, Jb akasusa kupanda jukwaani hali iliyopelekea showa rasmi ichelewe kuanza huku kina Alain mpela na Aimelia wakiwa wanaendelea kuimba nyimbo za utangulizi stejini, ikabidi mkewe Jb, mama Amida Shatur pamoja na rafiki yake JB waliekuwa pamoja maisha ya utotoni JDL ambae wakati huo alikua ni mpiga keyboard wa Wenge El Paris waingilie kati kumsihi JB apande stejini kwani wapenzi hawatawaelewa kabisa hasa ikizingatiwa Blaize Bula nae hayupo (JDL kwa sasa yuko na bcbg kama muimbaji).

Sehemu ya Show ya Zenith ilivyokuwa

Baadae Jb akakubali na kupanda stejini akiwa amevaa crown ya mfalme kichwani na koti refu lenye rangi ya dhahabu akisindikizwa na Tutu Kaludji ukumbi mzima ukizizima kwa kushangilia na moja kwa moja akashika mic na kuanza kuimba wimbo wake COURAGE kwa hisia kali na masikitiko makubwa, huku akiwataja wakongwe Papa Wemba, Pepe Kalle, Adui yake wakati huo Koffi Olomide (japo alipomtaja watu walizomea) huku akisema kwamba yeye ni mdogo kwa hao wote, unaweza kutazama hapo chini jinsi alivyokua akiimba kwa hisia kali wimbo huo siku hiyo,ambapo baada ya huu akaamba mulolo, Parie Bouge (Kin e Bouger) na n.k. mnaweza kuitafuta video hii kamili kwa ambao hamjaiona, mimi huwa hainichoshi kuitazama, ni nzuri sana,imeandikwa JB Mpiana & WENGE bcbg Zenith 1999!
vIDEO:

Wenge alikomelea kwenye kutunga zaidi na vijana walipewa nafasi vijana zaidi, Wimbo huu unaitwa Serge Palmi ukiwa ni utunzi wa kinaja Burkina Faso Mboka Liya aka Burkifaso Kasongo mmoja wa vijana wakongwe kwenye BCBG.

Katika show hii kwa upande wa makaba nae alisusa kabisa kupiga solo, akakaa back stage, mpaka mwishoni kabisa alipobembelezwa sana na wadau wa bcbg ndio akapanda stejini akapiga solo kwenye wimbo omba ambao hupendwa sana na wamama wa congo, tena hakua yule makaba tunaemjua, mcheshi, mchangamfu na mbwembwe nyingi stejini,bali alikua amenuna, mwenye hasira akipiga solo lake huku akiwa amewapa mgongo mashabiki!!mimi mwenyewe nilipoiona hii video enzi hizo 2000 kabla ya kujua kilichotokea nilimshangaa sana makaba kwa style ile ya upigaji gitaa huku amewapa mgongo mashabiki, niliona kama ilikua ni dharau!tafuta video ya live concert hii bora kabisa uangalie vituko hivyo vya prince makaba.

Baada ya show hiyo JB akaamua kuachana na Makaba kwenye show ya Olympia ambayo ndio ilifuata siku chache baadae.Show ambayo ilikuja kuwa voted kama BEST CONGOLESE CONCERT OF THE CENTURY., Baada ya mafanikio ya concert hiyo JB na BCBG kiujumla walikubaliana kumvua rasmi Makaba cheo cha artistic director kwa kumdhalilisha rais wa bendi JB Mpiana, ndipo makaba akakasirika na kuamua kuachana kabisa na kitu kinachoitwa wenge pamoja na kushawishiwa mara kadhaa na werrason ajiunge maison merre.Hii hapa chini ni video ya showa ya OLYMPIA.
VIDEO:

Pata Kitu Process Mambika, Hii ni sehemu ya show ya Olympia–1999 wakati unameza mate.

Baada ya hapo JB na vijana wake mwishoni mwa 1999 wakaingia studio huko huko paris na kufyatua single ya YA PAS MATCH, hawakukaa sana tena mwanzoni mwa mwaka 2000 wakaja na single nyingine iliyokuja kuwika sana PAPITO MBALA REMIX ambao ni wimbo uliokuwa umetungwa na “Teja” ZULEMA Kijana mcongoman lakini akiwa ametumia muda wake mwingi huku Brazzavile akiimbia bendi moja huko mpaka JPS PRODUCTION waliomkuta akizurura Paris na kuamua kumleta Kinshasa ajiunge  maison merre japo werra alimkubali tatizo la  kutumia madawa likamkosesha kazi. Japo alifanya kazi hiyo ya PAPITO REMIX na BCBG kipindi hicho Zulema hakua mwanamuziki wa bcbg, walikutana tu paris na kwa kuwa Kibens waliwahi kufanya kazi pamoja huko Brazaville ndio akamtambulisha kwa Jb wakawa wanafanya mazoezi pamoja nae sasa kwa kuwa ana kipaji cha kutunga ndio katika muda mfupi akatunga hiyo single, kabla bcbg hawajaamua wawe nae ndio JPS wakampeleka kwa Werra japo kwa sasa yuko na BCBG, Jb anamkubali sana sema tatizo lake ndio huo uteja.

Baada ya kuachia single hizo mbili,ndio sasa wakaanza maandalizi ya album ya T.H.bila Blaize Bula wala Makaba,lakini wanafanya mixing ya hiyo album huko paris baada ya kuwa wamesharekodi sauti na vyombo yaani kila mtu kaimba na kupiga sehemu yake kwenye album nzima na imesharekodiwa,ghafla Aimeli Lyase nae akatangaza kujiondoa kundini huko huko Paris na kuamua kuungana na mkewe na mwanae wanaoishi huko Paris akipanga kutoa album yake binafsi ya CONSTAT,nae Burkinafaso ambae Jb sasa ndio ilikua roho yake baada ya kuachana na makaba,akanyakuliwa na wapinzani wao Wenge Maison Merre akiahidiwa kupewa gari na dola 10,000 na wafadhili wa Werrason,mbaya zaidi Burkinafaso hakuondoka peke yake,aliondoka na mpiga gita kiraka wa bass na Rythm Patient Kusangila ambae yeye alikasirishwa na kitendo cha kufanywa mpiga gita namba 2 nyuma ya ACCOMPA ALBA(solo)na Sunda Bass(Bass).

image

Shabiki Nambari One wa BCBG Zadio Kongolo (ZK) akifurahia kumtunza Mpiana

Kuondoka kwa wanamuziki hawa watatu kwa mpigo tena bendi ikiwa studio kulimchanganya sana JB hasa kuondoka kwa Burkinafaso na Aimelia ambao tayari walikua wameshaingiza sauti zao wanasubiri kufanya mixing tu then album iingie sokoni,kukawa hakuna jinsi ikabidi releasing ya T.H. ichelewe kwa sababu walilazimika kurudi tena studio ili kuondoa vocals za Aimelia na sehemu ambazo Burkina faso alipiga solo, japo hawakuweza kufuta mikono ya Burkinafaso kabisa kama walivyofanya kwa sauti ya Aimelia ambayo haisikiki kabisa kwenye TH,Ndio ukiisikiliza T.H. upande wa solo gitaa utaona inafanana sana na TERRAIN EZA MINE ya MAISON MERRE ni kwa sababu zote mbili ni mikono ya Burkinafaso japo FICARE MWAMBA alijaribu kuondoa ondoa athari za burkinafaso lakini wapi.. ikashindikana.

Kwa kuwa burkinafaso mapigo yake aliyopiga kwenye T.H. akaenda nayo vilevile kwenye TERRAIN EZA MINE nadhani alifanya vile makusudi si unajua mambo ya upinzani tena hadi kile kibwagizo cha Souverain premier.. souverain premier binadaaaaaaaaaaam souverain premier jb mpianaaaaaaaa tutu calugi alikibadilisha tu jina tu kwenye T.H., Lakini ukweli ilikua ni cha burkinafaso ndio maana akahama nacho na kina Bill Clinton wakakiimba Burkinafasooo burkinafasoooooo……..Hali iliyopelekea Bill Clinton kwenye ile concert ya WMMM Bercy awapige kijembe BCBG kwa mafumbo,kuna sehemu anasema “BURKINAFASO MOPAYA SOKI ALONGWE AKENDAKA NA NYONSO ATA RIDEAU YA PAMBA (MTU  AKIJA KWAKO AKITAKA KUONDOKA ANAENDA NA KILA KITU ALIKUJA NACHO).

image

Genta Machine akiwa na mdau, huyu ndio ameziba Pengo la Tutuu Kaludji na kuwa Atalaku nambari One wa BCBG

Lakini yote kwa yote mwisho wa siku T.H. ikawa released, JDL yule rafiki wa JB toka maisha ya utoto akajiunga bcbg kama muimbaji si mpiga keyboard tena kama kule Wenge el Paris, baadae rafiki mwingine wa JB toka maisha ya utoto BIKU LEBRUN nae akajiunga akitokea UK ENGLAND, TH ikapata mafanikio makubwa sokoni, ikiwapatia BCBG Kazi nyingi kwa maana ya concerts ulaya, america na hata africa, baadae kijana mdogo sana mpiga solo akijulikana kama Patou Solo akajiunga na bendi kuongeza nguvu lakini hakuwa full time musicien wa wenge bcbg kwa sababu kipindi hicho alikua mwanafunzi akifanya degree yake ya mambo ya sheria na pia akifanya degree ya sound engineering mpaka 2003, pia kipindi hicho hicho wakajiunga Richard  Mukena rafiki mwingine wa jb waliekulia nae sehemu moja,Bogus Bompema na mpiga gitaa anaetumia mkono wa kushoto Pathy Moleso.

Wakarekodi album ya INTERNET ambayo ikawapatia contract ya kusafiri kwenda ulaya kufanya concert ndani ya BERCY,Wakapania sana kwenda kuivunja record iliyokuwa imekwishawekwa na Koffi pamoja Werrason hapo bercy kwa kujaza watu wengi sana.

image

Wanamuziki wa Wenge BCBG wakishambulia jukwaa, Hii ilikuwa show ya Olympia

Watu walijaa lakini si sana kama ilivyokuwa kwa Koffi na Werrason walipopiga hapo siku za nyuma na hii ilitokana na kwamba concert hii ya bcbg hapo Bercy ilifanyika ndani ya siku 11 baada ya ile milipuko ya september 11 marekani, hivyo kwa wageni wengi waishio ulaya na marekani kipindi hicho kilikua kigumu sana kwao kwani askari walikua wakivamia kila penye mkusanyiko wa wageni na kuharass watu na kama mnavyojua tena waafrika wengi huwa tunaishi bila makaratasi kwenye nchi hizi sasa watu wengi wakaogopa kujitokeza kwenye hiyo concert kwa kuhofia mkono wa sheria za uhamiaji, lakini show ilikua nzuri sana chini ya BADIVE.
Hiyo ndio ilikua miaka mitatu ya mwanzo ya uhai wa BCBG.

Stay tuned kwa miaka mitatu ya mwanzo wa uhai wa MAISON MERE,

 • Walianza vipi ku recruit vijana,
 • nani alikua wa kwanza kujiunga baada werra, adolphe na masela? Bill clinton alipatakanaje?
 • Je Wajua kuwa Fally Ipupa aliwahi kufanya Inter View WMMM?

Tutajua hapa hapa Spoti na Starehe, Shukrani za kipekee kwa Papaa Henry Kasapira nakati ya londone, Juma Mukubwa Muzee ya Air Port, Le Big Prodyuza Maghambo tuko pamoja, Papaa Julie We Ston weeee Ndenge nini papaa?, Papaa Hadji Le Becebegeeque Nambari wan!! Uko Juu Papaaa, Mamaa Tabou Fatou ya Tanzanie weeeee Kitokoooooo, Papaa Farid Wa Muscat, Mamaa Perovee, Mukubwa Shabani, Papaa Mwalimu wa Muheza Waambaze Mgoshi?,  Sadik Titanike weeee, Alain Kamangu Merci Mingi papaa, Mamaa Fatuma Mtanga tuko Pamoja Meree, Samson wa Delila karibu sana, Mke Mimi nakati ya Ujiji Chighoma, Ubeleji na wachangiaji na Wasomaji wote tuko pamoja na Asante kwa support yenu

Merci Mingi, Till then….

18 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – III

 1. Mukubwa Shabani says:

  kazi nzuri sana kaka kwa mara nyingine,haya mambo hatukuyajua kabisa kumbe maisha ya bcbg hayakuwa rahisi hivyo….ndio maana jb hataki kushirikiana na hawa jamaa zake kiasi cha kususia show ya wenge re-union iliyoandaliwa na zain,pia tutu kaludji nae hakuhudhuria lakini,tunausuburi upande wa maison mere kwa shauku kubwa

 2. Mamaa President says:

  Merci mingi bana spotistarehe na kati ya tanzanie

 3. Anonymous says:

  Tuko pamoja!lete vitu.

 4. Anonymous says:

  naisubiri kwa hamu maison mere nijue ilivyoundwa,waliwapata wapi vijana wa kazi katika muda mfupi kuweza kuisimamisha bendi na kumtingisha mpiana na genge lake na badae koffi kabla ya kuiteka congo nzima.

 5. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  Hivi jb,makaba, werrason na blaizee bula wakiionanaga video hii hapa chini huwa hawajisikii uchungu?hebu watazameni walivyokua bado wandugu,ilikua bien sana,namuona ekokota alikua mtoto kabisa hapo,sijui hata alikua anachezea nini mkononi

 6. mkigoma,kariakoo says:

  Ndenge nini papa mukulu wa bakulu,tunakupenda sana kwa kazi nzuri,dada mkemimi hapo juu merci mingi mamaa kwa hiyo video ya hapo old days hapo juu,kumbe walianzia kupiga mitaani mpaka kuwa masuper star africa muzima!

 7. Haji Drogba says:

  wimbo pentagone ulitungwa na nani eti?maana kuna ubishi hapa maskani kwetu,wengine wanasema werrason na wengine wanasema na wa jb mpiana,tunaomba ufanunuzi kwa anayejua.

  asante

 8. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo […]

 9. Anonymous says:

  Pentagone ni Generique iliyotungwa na ROBERTO EKOKOTA “Le Grand Chibuta”

 10. papa kasapira nakati ya london says:

  I used to respect Didi Kinuani but not now kwa kitendo chake cha kumshawishi Tutu kalugji(R Kelly) the number one kuondoka Wenge BCBG ni kutaka tu kuona band yetu kama itakufa ila thanx to Genta Machine BCBG still rules the world wishing Tutu Kalugji all the best na band yake mpya ila soon he will regret kuiacha BCBG. Merci

  • Hadj Le Jbnique says:

   Pamoja na DIKIN kuchangia kweli kuondoka kwa Tutu Caludji hasa kwa upande wa pesa za kujitegemea,lakini chanzo kikuu ni kutoelewana kwake na Mpiga drums mtiifu kwa jb ambae amekua kama mdogo wake,huyu drammer boy ni Seguin Mignon,yeye pia ndio chanzo cha Burkinafaso pia kuondoka hapo bcbg,inasemekana ukigombana na seguin maisha ya bcbg yanakua magumu…tutakuja na stori yake kamili uko mbele huyu bwana seguin mignon,tujue yeye ni nani ndani ya bcbg

   • papa kasapira nakati ya london says:

    thanx Hadj Le Jbnique naomba tena msaada wako kujua nini hasa kilikua chanzo cha ugomvi kati ya fally ipupa na the king of the new generation ferre gola kipindi wote wapo katika bnd ya Le Gramo Pao Mokonzi Koffi Olomide , ua mwana blog yoyote anayejua chanzo cha ugomvi huo merci.

 11. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza […]

 12. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza […]

 13. […] kivyake, Kama ulipitwa Aimelia aliondokaje Wenge BCBG gonga hapa. Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne LD_AddCustomAttr("AdOpt", "1"); LD_AddCustomAttr("Origin", "other"); […]

 14. […] Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza […]

 15. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo […]

 16. I believe this is an informative publish and it really is knowledgeable and extremely valuable. I’d like to thank you to the efforts you’ve got created in writing this post.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: