Werrason akimbiwa na wanamuziki watatu

Mwanamuziki Ngiama Makanda anazidi kupata pigo baada ya kukimbiwa na mwanamuziki wake Fabregas, Miel na Heritier Watanabe. Awali Werrason alikanusha habari hizi akidai kuwa Heritier ni mgonjwa na Miel pamoja na Fabregas wanamuuguza huko ulaya jambo lililopelekea wadadisi kuhoji sana kwani si kawaida wakati WMMM wanasubiriwa kwenye show kubwa ya FIKIN ambayo wanamuziki hawa tegemezi lazima wawepo.

Kwa mujibu wa habari zilizomo kwenye mitandao maarufu wa Digital Congo ni kuwa sasa imebainika Fabregas ameondoka na Heritier pia hii ni kufuatia ugomvi wake na Mwanamuziki mwenzie ajulikanaye kama Tadhe baada ya Heritier kutoa wimbo wake wa Con­fession intime. Tutawaletea habari zaidi lakini kwa sasa habari ndio hiyo.

Advertisements

7 Responses to Werrason akimbiwa na wanamuziki watatu

 1. papa kasapira nakati ya london says:

  hahahahahahhahah!hii ni mara ya tatu katika history ya WMMM kwa wanamuziki kumkimbia Igwee tujiulize kwanini? Wana WMMM muombe mungu kimbangu solo na brigade wasiondoke maana ndio mihimili yenu iliobaki.

 2. Anonymous says:

  kawaida yao hao tatizo mchizi dhulumati kinoma kwenye malipo wakati vijana ndio wanambeba si unajua jamaa hana sauti ya kuimba na hajui kupiga chombo chochote cha muziki ukiacha tuma alizojifunzia mziki,

 3. bcbgque no.2 says:

  nyie waacheni wavurugane sisi tunasonga mbele na mambo ya “mpunda” kama ifuatavyo hapo chini:

 4. mwaikasu,forest, mbeya says:

  Na washabiki wa wmmm mshukuru jb alishasema hatachukua mwanamuziki kutoka Quartier Latin wala maison mere kuepusha ugomvi kwani congo ina vijana wengi wana vipaji lakini hawana kazi hivyo atasaidia vijana wa congo kupata ajira,najua koffi atawachukua kumkoamoa adui yake werrason

 5. werrasonique wa ukweli says:

  na nyie na hiyo mpunda yenu hatunywi maji sasa….album yenyewe mmeaianda miaka mitatu album moja

 6. Anonymous says:

  Kimbangu alishaondoka siku nyingi! hivu mpunda upo? dah sijawahi hata juisikia

 7. Paschal M Canisio says:

  Hapana, taarifa hii si ya kweli. Heritier Watanabe yupo hadi leo, na Miel de Son. Ni kweli Fabbregas aliondoka.
  Lakini kama wote mjuavyo, Werrason ni mtengeneza vipaji: tayari alishaziba pengo. Kwa Werrason hakuna mwimbaji ambaye ni tegemeo zaid yake

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: