Agassi akiri kutumia dawa za nguvu

October 28, 2009

image

Andre Agassi amekiri kupitia tawasifu yake mpya, alidanganya kwa waendesha mchezo wa tennis kuhusu kutumia dawa za kuongeza nguvu ili kukwepa kufungiwa.

Agassi aliyestaafu mwaka 2006, amesema alitumia dawa hiyo mwaka 1997 alipokuwa na msaidizi wake wa zamani ‘Slim’.

Chama cha mchezo wa tennis kwa wachezaji wa kulipwa (ATP) kimesema kinachunguza kukiri huko kwa Agassi.

Katika tawasifu huo uliopatikana na gazeti la Times, Aggasi ameandika "Slim" alimtilia kiasi kidogo cha unga wa dawa hiyo kwenye kahawa.

Na BBC

Advertisements

Kutana na Giuliano Stroe, Baunsa mtoto wa miaka mitano aliyevunja Rekodi ya dunia.

October 28, 2009

juliana

Anaitwa Giuliano Stroe toka Romania, ana miaka mitano tu na tayari ana miraba 6 tumboni mwake (6 pax) na ameshaingia kwenye kitabu cha kumbukumbu cha walivunja rekodi cha Guiness.

akiwa na umri wa kuanza shule Giuliano Stroe aliingia kwenye kitabu cha Guiness mapema mwaka huu baada ya kutembea kwa mikono umbali wa mita 10 akiwa na mpira wenye uzito kati ya miguu yake. Tangu hapo video yake ya dakika 4 imekuwa na hit za ajabu na kuikonga dunia huku kila mtu akitaka kujua kulikoni na kupelekea mtoto huyu kupamba vichwa vya habari mbali mbali duniani. Bonyeza player kupata ushuhuda.


Filandu na Wenge Musica BCBG

October 28, 2009

 

Kuna mdau wangu kwa jina la Baraka ameniomba kuandika Historia ya Wenge Musica tangu ianze mpaka sasa na kila kundi lilipo na wanafanya nini, nakuahidi tu mdau wangu niko nakusanya facts ili nitoke na unachokitaka. Napenda kukujulisha kuwa habari hiyo itatoka wiki ijayo hivyo tega sikio. Kwa leo pata burudani ya kibao Filandu ambacho kiliundwa na Engineer Blaise Bulla wakati hui walipotoka na Albamu ya Pentagone.

Kwa wanaomjua Blaise Bulla wanajua kwa nini aliitwa Engineer, kwa faida ya wadau, Blaise Bulla ndiye alikuwa na kazi ya kupanga mtiririko mzima wa waimbaji katika wimbo kuwa Ataanza nani na nani afuate, na ndiye yeye aliyekuwa na uwezo wa hata kusema ubeti huu ukiimbwa na Werason utapendeza zaidi na wa Werason uimbwe na Dominguez, basi ilimradi kuleta raha na ndio maana alipewa jina la Engineer.


Kroenke akaribia kumiliki club ya Arsenal

October 28, 2009

image

Mkurugenzi wa Arsenal Stan Kroenke  (pichani) amepiga hatua moja zaidi ambapo anaweza kujitolea kununua hisa zote za club hio.

Tajiri huyo wa Kimarekani amenunua hisa kumi zaidi kwa pauni £8,500 kila moja na kupandisha mchango wake katika hisa kufikia asili mia 28.9%.

Hiyo ina maana kwamba Bw. Kroenke ndiye mwenye hisa nyingi zaidi ya wengine, akimshinda tajiri kutoka Uzbekistan Alisher Usmanov, mwenye asili mia 24%. Bw. Kroenke anakaribia kiwango cha juu cha 29.99% ambapo itambidi atangaze nia ya kununua hisa zilizosalia.

Hata hivyo hisa zilizosalia zinashikiliwa na Wakurugenzi wanaozishikilia kwa mkono wa chuma. Bw.Kroenke anayemiliki club ya NBA huko Marekani Denver Nuggets amekua akinunua hisa za club ya Arsenal taratibu mwaka huu akidokoa kila fursa inayojitokeza kutoka kwa wanaotaka kuuza.

Pamoja na Bw.Kroenke, wengine wenye kifua katika kumiliki hisa kubwa ni Bw.Usmanov, Danny Fiszman na Lady Bracewell Smith. Hata hivyo haijaeleweka kama Bw.Kroenke ana nia ya kununua hisa zilizosalia kwa nia ya kuimiliki club nzima ya Arsenal au amenunua hisa hizo kwa ajili ya faida ya uwekezaji wa mda mrefu.


%d bloggers like this: