RWANDA KUPATA WAWAKILI WA MISS EAST AFRICA 2009 JUMAMOSI!!

October 29, 2009
 

Hawa ni baadhi ya warembo wa Rwanda watakaowania kushiriki Miss East Africa 2009.

Warembo watakaoiwakilisha Nchi ya Rwanda katika mashindano ya kimataifa ya MISS EAST AFRICA 2009 watapatikana wiki hii katika mashindano yanayosubiliwa kwa hamu kubwa Nchini humo.
Mashindano hayo ya Rwanda yanaayoandaliwa na kampuni ya Rwanda Events Limited ya Nchini humo yatafanyika siku ya Jumamosi wiki hii jijini Kigali.
Washindi wawili wa mashindano hayo wataiwakilisha Nchi ya Rwanda katika fainali za mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yatakayofanyika tarehe 18 Desemba, 2009 jijini Dar es salaam, Tanzania.
Wawakilishi wa Rwanda katika mashindano ya Miss East Africa mwaka jana yaliyofanyika Bujumbura, Burundi walikuwa ni Kaneza Brigitte na Idmulisa Dominique from RWANDA

Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha warembo 28 kutoka Nchi 14 ambazo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi. Zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Madagascar, Seychelles, Mauritius, Comoros, na Re union,Mashindano ya Kimataifa ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.

Wakati huohuo droo ya kila mwezi ya bahati nasibu ya Miss East Africa imefanyika jana na washindi kutangazwa. Washindi hao wa droo ndogondogo za kila mwezi wamejishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shillingi million mbili ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, simu za mkononi, ticketi za VIP za kuangalia fainali ya mashindano ya Miss East Africa, n.k.

Zawadi kubwa katika bahati nasibu hiyo inayoendelea Nchi nzima ni Gari aina ya Range Rover Sport, kutoka CMC Automobile Ltd. Ili kushiriki bahati nasibu hiyo unatakiwa kununua ticketi kutoka kwa wauzaji wa Magazeti Nchini, au kutuma SMS ya neno “SHINDA” kwenda namba 15567 kwa kutumia simu ya mkononi.


Penang Marathon 09

October 29, 2009

penang

Siku zimeisha!, Nimeambiwa wakenya wamechangamkia mbio hizi ambazo zinakatiza kwenye daraja refu kuliko yete ulimwenguni likiwa na Kilomter zipatazo 15 ndani ya bahari likiunganisha Penisula Malaysia na kisiwa cha Penang. Natumai watanzania hamjachelewa kwa habari na kujiandikisha gonga hapa. Tafadhali zingatia kumaliza hatua zote 7 katika kujiandikisha.


Shikito kupamba shoo ya Ferre Gola Dar

October 29, 2009

 

Kombo ‘Shikito’

MWIMBAJI nyota chipukizi wa Kongo Makinu Kombo ‘Shikito’ anatarajiwa kuongozana na mkali wa bolingo kutoka nchini humo, Ferre Gola Batangire, akiwa miongoni mwa wanamuziki 17 watakaokuja nchini kwa mwaliko wa New Habari(2006)Ltd.

“Katika orodha ya wanamuziki 17 ambao Ferre ametutumia majina yake, yupo pia Shikito lakini mtoto mwingine aitwaye Ilunga hatakuja kwenye msafara huu,” alisema.Aziza Aliwataja wanamuziki wengine wanaokuja na Ferre kuwa ni pamoja naFreddy Makola Linakasi, Nikodeni Kanday Ngoy, Olenga Makiese, ClizoKalonda Lopeta, Sungu Mbobolo, De Gaule Matima Makitela, Guy NgolaMawesele na Awulu Wala Tshipanga Wale.

Wengine ni Ngwanzu Bavuidibio Gaza, DebosSunguesabena wa Kayembe, Mabiala Mobele, Mchele Mkelele Kitongo naChristian Solo Kabongo Muyambi.Wengine ni Vicky Moleka Leta, Patricia Isako Apakati, Renate KungaMuwangu, Nancy Mbemba-Lohuma.

Shikito ni kijana mdogo ambae amejichukulia umaarufu mkubwa sana ndani nanje ya Kongo kwa kuwa mwimbaji mahiri mwenye umri mdogo zaidi katika anga ya muziki wa dansi afrika.

Habari kwa niaba ya Michuzi


%d bloggers like this: