Akina mama Afrika ya Kusini na soka…..!

October 22, 2009

Huku vugu vugu la kombe la dunia likifukuta kila uchao katika miji ya Africa ya kusini, kundi la akina mama wa makamo wamejikusanya na kuamua kufanya mazoezi kwa kucheza mchezo wa soka, wao wanasema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa ambayo yanaambatana na uzito au uzembe wa kutofanya mazoezi kama Shinikizo la Damu, Kisukari nk.Hii ni changamoto kwa akina mama wa nyumbani na si tu kwa akina mama bali hata siye akina baba yeyoo mazoezi  ni muhimu bana.

Advertisements

Southgate atimuliwa Middlesbrough

October 22, 2009

image

Meneja wa timu ya soka ya Middlesbrough Gareth Southgate ametimuliwa, licha ya kuwa nafasi ya nne ya Championship wakijitahidi kupanda daraja.

Kutimuliwa kwake kumetangazwa mapema siku ya Jumatano, muda mfupi baada ya kuifunga Derby mabao 2-0 nyumbani.

Southgate mwenye umri wa miaka 39 aliteuliwa kufundisha klabu hiyo mwezi wa Juni mwaka 2006, lakini msimu uliopita Middlesbrough ilishushwa daraja kutoka Premier League.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Gibson amesema: "Umekuwa ni uamuzi mgumu niliowahi kuufikia katika soka."

Kitengo cha michezo cha BBC kimebaini Gordon Strachan na Nigel Pearson ni miongoni mwa wanaopewa nafasi ya kuchukuwa nafasi ya Southgateare huko Riverside.

Muda mfupi kabla ya kutimuliwa, Southgate alisema: "Mwenendo wetu ni mzuri. Hatupo mbali na kileleni, lakini hali ingekuwa ngumu zaidi kama tusingeshinda mchezo na Derby.

Na BBC


wanawake 10 wakamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya jumla ya USD 12.5 Milion.

October 22, 2009

image

Wanawake raia wa Iran kumi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Maofisa Usalama na Maofisa wa Forodha wa Indonesia baada ya kukamatwa na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya inayokisiwa kuwa na thamani ya US$12.5 million.

Kwa mujibu wa maofisa wa uwanja wa ndege wa Indonesia wanasema kuwa hiki ni kiasi kikubwa katika historia ya uwanja huo. Jumla ya kilo 26.8 ya unga na Lita 22.8 za madawa mengine yaliyo kwenye hali ya kimiminika yalikamatwa na akina mama hao ambao walikuwa wamevalia Hijab na Baibui Nyeusi ambazo kimsingi huchukuliwa kama ni watu safi.

Kwa mujibu wa sheria za Malaysia, Brunei, Singapore na Indonesia ukikamatwa na kiwango kinachozidi gramu 200 na kukutwa na hatia mahakamani adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa. gonga hapa kwa habari zaidi.


Sweet Eazy is bringing you an evening full of Caribbean flavours:

October 22, 2009

Jhikoman & Afrikabisa live on stage

  • Dar es Salaam’s hottest Ragga, Roots, Reggae & Soca mixes by our Live DJ Crew

  • Jamaican Goat Curry

  • Coconut Rum upon arrival (first 50)

This Saturday, 24 October, from 9pm. See below flyer for details (including dress code).

image


CNN Inside Africa na Hasheem Thabeet

October 22, 2009

Kwa mara nyingine Hasheem Thabeet azidi kugonga vyombo vya kimataifa safari hii ungana na Terry Badoo wa CNN Sports akichambua maisha ya Mwanakikapu huyu kama ilivyoletwa na CNN Inside Africa. Pamoja na mambo mengine Hasheem amezungumzia maisha yake ya kikapu kabla na baada ya kuwa super star pia mama yake mzazi ameongea kidogo.

Bofya player kupata yaliyojiri.


%d bloggers like this: