D’banje na Fall in Love

October 3, 2009
Uko kwenye Chart za juu MTV

Walikuja juu kwenye ulimwengu wa Sinema na kuiteka karibia Afrika yote kila nchi ukipita wanapenda na kuangalia sinema za Kinigeria. Sasa wamekuja kivingine na kuiteka Afrika kama si dunia kwa miziki yao.

Leo hii nakuletea video ya wimbo unaitwa Fall in Love toka kwake D’banj aka The KOKO Master akimshirikisha Don Jazzy.

Wimbo huu umeshika kila kona na unapigwa sana hata club, wao wanasema wana angalia soko la nje zaidi, basi kwa mpenzi yeyote wa muziki ataupenda muziki huu iwe kwa kuusikiliza au kwa kuucheza. Wimbo huu fall in love uko kwenye chart za juu za Radio na TElevisheni mbali mbali ikiwemo MTV.

Si maneno tuu hata video ya wimbo huu ni ya hali ya juu ingawa hii iliyoko hapa quality yake si nzuri sana pia Napenda kuusikiliza kutokana na lugha wanayotumia mfano anaposema my sweet portatoo, i wanna make u my wifoo, ur the love of my lifoo, i cant deny oooooo!!

D’banj alikuja Malaysia na kuichanganya vilivyo na huu wimbo ndio ulikuwa umetoka, Weekend hii D’banj atatumbuiza ukumbi wa Club Billicanas. Kwa mujibu wa habari mwanamuziki huyu amehairisha show yake ya Uingereza kwa ajili ya kutaka kuja kufanya mambo jijini Dar. Kazi kwenu watu wa burudani, Burudika na kitu fall in Love na Weekend njema.

Advertisements

Ni Miriam Gerald, Miss Tanzania 2009

October 3, 2009

miss Tanzania

Miriam Gerald – Miss Tanzania 2009

image

image

image

Mashindano ya Miss Tanzania 2009 yalimalizika hapo jana kwa mrembo Miriam Gerald kunyakua taji la Miss Tanzania na Miss Photogenic.

Miriam ambaye kwa mara ya kwanza amevunja mwiko kwa warembo wa Dar Esalaam kuchukua taji hilo la juu kabisa la urembo nchini, ametokea kanda ya Ziwa (Mwanza).

Show ilipambwa vilivyo kwa vijana kutoka Tanzania Tallent House ambao waliwaburudisha watazamaji na kuwakuna vilivyo kwa onyesho maalum la mkongwe marehemu Michael Jackson.

Kwa mengi yaliyojiri gonga hapa. , Picha zote kwa hisani ya Daily News Online na Mzee wa Jiachie.


New African Diva Meje & Tshala Muana – Delestage

October 3, 2009

Maranyingi ukiniuliza napenda nini kwenye nyimbo za kizaire nashindwa kujibu kwani jibu langu huwa napenda “Wimbo”.

Kwangu mimi nikisema Wimbo namaanisha Sauti, Muimbaji, Vyombo, mpangilio wa upigaji vyombo na kila kitu kilichopo kwenye wimbo husika.

Naomba umsikilize Mamaa Tshala Muana akishirikiana na Meje katika wmbo wao wa Delestage, labda wewe unaweza kuniambia umependa nini humu.

Mamaa Sopgia Kessy Upoo?


%d bloggers like this: