Eid El Fitr; Ni Karamu ya magoli tuu viwanjani

October 2, 2009

ManU 4-3 Manchester City

image

Chelsea 3-0 Tottenham Hotspur

image

Didie Drogba alimalizia karamu ya magoli 3-0 ya Chelsea dhidi ya Totenham hapo jana, ingawa alipewa guu lililompelekea kutolewa nje ya uwanja kwa machela.

Arsenal wainyambua Wigan

image

Ilididndisha kwa Machester lakini kwa Arsenal imekula bao za kutosha. Pichani ni Spike Lee akionyesha kutabasamu, hii ilikuwa katika mchezo kati ya Arsenal na Wigan ambapo Arsenal ilishinda kwa 4-0.


Baada ya kupata ajali amesauliwa ! hakuna uduma ya matibabu! wadau tumsaidie Mwanamziki huyu!

October 2, 2009

kitambi

Hamisi Kitambi ni mmojawapo wanamziki wakongwe na hadhina waliobakia hapa nchini Tanzania ,bwana Hamisi Kitambi mtunzi wa nyimbo nyingi !mojawapo ya nyimbo zake ni ule wimbo mzuri maarufu kwa jina " Mpenzi wangu !mwenye rangi ya Chungwa" kwa wale wenye kumbukumbu wanajua radha ya utamu wa wimbo huo..

veteran huyu Hamisi Kitambi amefanya kazi na bendi nyingi zikiwamo Tabora jazz,Unyanyembe band,penginepo KIKO KIDS,labda Dar-es-salam Jazz,labda Western Jazz, hadi anapata hajali ya gari alikuwa Juwata (OTTU) Jazz sasa Msondo Ngoma aka Baba ya Mziki, Mwanamziki huyu mkongwe Hamisi Kitambi amepata hajali akiwa katika gari yeye na wanamziki wenzie  Msondo Ngoma walipokuwa safarini Tanga! Mzee Hamisi Kitambi kama anavyoonekana pichani,miguu imevunja na amewekewa vyuma,cha kusikitisha kuwa tangu apate hajali ndio katupwa si ,hana uduma muhimu,mtaji wa masikini ni MIGUU YAKE nayo ndio kama anavyoonekana,Je ! ni haki kwa mwanamziki au mwanadamu aliyechangia kujenga msingi wa fani ya mziki nchini kutupwa kama hivi?

GetAttachment

Basi ata kama hakuna bima ya kulipwa,ata ubinadamu usiwepo?

Tujaribu kumsaidia mzee wetu huyu mwanamziki mkongwe Hamisi Kitambi anapatikana  kwa simu hii Dar 0713576475


%d bloggers like this: