Langkawi kisiwa cha Starehe..!

October 23, 2009

Ni umbali wa masaa kama 7 kwa gari toka Kuala Lumpur hadi jimbo la Kedah ambapo inabidi kuchukua Boat kwa takribani dakika 45 hivi, ndipo unaingia kisiwa cha Langkawi.

image

Picha ya Ndege mkubwa ambayo inasimama kama alama ya Langkawi.

Mi mjumuiko wa visiwa vidogovidogo takribani 99 na kuna kisiwa kikubwa ndipo raha na starehe zote zipo. Ukiingalia Langkawi unaweza kufananisha na Zanzibar na kama utapata bahati ya kuangalia Picha za Langkawi miaka 15 iliyopita basi inafanana kabisa na Zanzibar ya Leo.

image

Hiki ni kijiji cha Hotel ya Berjaya huko Langkawi.

Kisiwa hiki kilibadilishwa na kufanywa mmoja ya vivutio vya utalii kwa Malaysia baada ya kuonekana kukusanya watalii wengi na miaka ya mwishoni mwa 80 wafanyabiashara walianza kuwekeza kwenye mahoteli ya kitalii na kwa sasa Langkawi ina zaidi ya vyumba 3000 vya mahoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota 3,4 na 5.

image

Sehemu ya Chumba cha hotel ya Four Seasons Resort Langkaw

June 1, 2007 Kisiwa cha Langkawi kilitambuliwa rasmi na UNESCO na kupewa hadhi ya World Geopark status. Kisiwa hiki kinatambulika kwa kuwa na Beach nzuri katika Malaysia na zenye Maji meupe, mfano Pantai Cenang, Pantai Tengah, Burau Bay, Pantai Kok, na Datai Bay.

image

Serikali iliamua kuifanya Langkawi Tax Free Zone na kila kinachouzwa huko hakilipiwi kodi katika jitihada zake za kuvuta watalii wengi zaidi na mpaka sasa Langkawi inaongoza kwa kukusanya watalii wengi zaidi. Wakati Tanzania tunafurahia kupokea watalii Milion 1.7, Nchi ya Malaysia ilipokea watalii Million 22 kwa mwaka jana pekee.  Binafsi sioni sababu ya upungufu huu mkubwa ila kwa Malaysia ukilinganisha na sehemu yeyote kwa Mashariki ya mbali (Far East Asia) bei ya Hotel iko chini mnoo kwani Hotel ya nyota tano zinaanzia Dola 50 hadi Dola 150 na hizi zina hadhi ya kimataifa.

image

Langkawi kam ainavyoonekana toka ndani ya Cable Car.

Watalii wengi wanapenda Tour Packages ambazo zikiandaliwa vizuri huwa zinaondoa usumbufu wa hali ya juu ambao mtalii angeupata kama angeamua kupanga mwenyewe. Mfano kero ya kutafuta Hotel, usafiri, chakula na utaratibu mzima ambapo Malaysia iko mbele sana na imepiga hatua kwenye suala zima la uuzaji wa Package za utalii.

IMG_0042

Langkawi ni pazuri kwa safari ya kifamilia au mkienda kundi la marafiki.

Advertisements

Chelsea yataka marufuku isimamishwe

October 23, 2009

image

Mahakama ya usuluhishi wa michezo(Cas), imethibitisha Chelsea inataka FIFA isimamishe marufuku iliyoweka ya usajili wa wachezaji hadi rufaa yao itakaposikilizwa.

Klabu hiyo imepigwa marufuku na FIFA kusajili wachezaji wapya hadi mwaka 2011 baada ya kuonekana wamekiuka mkataba wa kumsajili Gael Kakuta kutoka klabu ya Lens 2007.

"Uamuzi wa maombi hayo ya Chelsea huenda ukatolewa mwanzoni mwa mwezi wa Novemba". Iwapo Cas itakubaliana na maombi ya Chelsea, timu hiyo itaweza kusajili itakapofika mwezi wa January.

Chini ya taratibu za adhabu za FIFA, Kakuta ni lazima alipe fidia ya euro 780,000 sawa na paundi 710,000.


Arsene Wenger atimiza miaka 60

October 23, 2009

image

Ni ajabu kuona kwamba Arsene Wenger ameweza kudumu kwa mda huo licha ya miaka minne ya ukame bila kushinda kombe lolote lakini kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier anawauliza wakosoaji wanaohoji uwezo wa Wenger, kua mbona Real Madrid wanampigia magoti ikiwa hali ni hio.

Wenger anayesherehekea siku ya kuzaliwa alhamisi tarehe 22 oktoba anaonekana kama mtu aliyebadili nadharia kwamba ushindi wa kombe siyo kigezo pekee cha ufanisi. Mabadiliko na kujenga msingi wa michezo ya kusisimua na mapato ya kujitosheleza kwa club pia ni mchango mkubwa wa ufanisi na maendeleo ya club. Hivyo wadadisi wanasema Wenger amejijengea ajira ya kudumu kwa uwezo wake wa mpango madhubuti.

Kocha aliyeiongoza club ya Auxerre wakati Wenger akiichzea club hio, Guy Roux anamfahamu Wenger tangu mwaka 1969 akiwa mwenye umri wa miaka 20 anamtaja kama mkufunzi bora kuliko wengine barani Ulaya.

Read the rest of this entry »


%d bloggers like this: