Manchester mbende mbende kwa Liverpool

October 25, 2009

Yalala 2-0

image

Matokeo ya leo:

matokeo

 

Msimamo baada ya matokeo ya leo

msim

Advertisements

Sheria Ngowi

October 25, 2009

image

”Sheria Ngowi Designs”

For More Pictures:
Click Here


Mfahamu Ferre Gola

October 25, 2009

image

Anaitwa Ferre Gola lakini jina lake halisi ni Hervé Gola Bataringe, alizaliwa mwaka 1976 huko Lingwala karibu na Kinshasa.

Katika ujana wake Ferre anasemwa kuwa alipenda sana kuimba na alipenda zaidi kuimba nyimbo wa wanamuziki waliotangulia akisemwa kuwa alikuwa mshabiki mkubwa sana wa Wenge Musica ya wakati huo kabla haijavunjika.  Binafsi sikuwa namjua kimuziki lakini nilitambulishwa na rafiki yangu LE Big Producer Maghambo ambaye aliniambia “Ferre Gola, A Man to watch” .

Wenge

Mwaka 1995 akiwa bado kijana mdogo Ferre alijitokeza kwenye onyesho la Wenge wakati huo ikiwa ni Wenge 4×4 na ndipo mwanamuziki Werason alipomuona na kugundua kipaji chake na kumpendekeza kwenye kundi la Wenge, Mwaka 1997 kundi la Wenge Musica BCBG 4×4 lilipanguka rasmi ka kuundwa makundi mawili Wenge BCBG ya JB Mpiana na Wenge Musica Maison Merre ya kwake Werason, Na Ferre alijiunga na Werasson lakini hakutambulika sana mpaka walipotoa albamu na yeye akatoka na wimbo Vita Imana ambao ulitokea kupendwa sana kwenye albamu ya Solola Bien yao WMMM. Pia alitamba tena na wimbo wa que-leu-leu katika albamu yao ya mwaka 2003.

Les Marquis

Mwana 2004 aliamua kuanzisha kundi lao waliloliita Les Marquis de Maison Mère akiwa na wanamuziki wenzie JDT Mulopwe, Bill Clinton Kalonji na huo ukawa mpasuko kwa WMMM, Hapo walifanikiwa kurekodi albamu moja kwa jina la Miracles est une réussite ikiwa na vibao kama ‘100 Kilos’, ‘Amour ya Interêt’, ‘Papitcho Nyanx’, na hii ilikuwa Albam pekee ya kundi hili na kundi kupanguka baada ya kutoelewana baina yao ambapo uongozi mbaya ilitajwa kuwa sababu ya wao kupanguka.

Quartier Latin

Mwaka 2004 Mwanamuziki Koffi Olomide aliamua kumchukua Ferre Gola ili akaungane na Fally Ipupa kwani pia Koffi alipoteza wanamuziki wake wengi ambao alitamba nao kipindi cha nyuma na hapo walitoka na Albam Danger de Mort ambapo Ferre alifanya mambo vilivyo na kuonyesha moto wake. Waliendelea vizuri lakini mwaka 2005 mwishoni malalamiko yalianza na mara ya kwanza alinakiliwa na mtandao wa Digital Congo akisema kuwa Koffi anakiuka mikataba waliotiliana wakati akimchukua na mwaka 2006 Ferre aliondoka kwa Koffi.

Kivyake

Baada ya hapo Ferre Gola aliamua kutoka kivyake kama Solo na alitoka na alikuwa akishirikishwa (featuring) kwenye nyimbo na albamu tofauti kama Doudou Copa (Terre Sacrée), Al Patshino na wengineo na wakati huo akijiandaa kutoka na albamu yake kivyake.

Mwaka 2007 Ferre alitoka na Albamu yake ya kwanza ambayo ilitamba sana katika Jamhuri ya Congo (Kinshasa) huku ikishika chati ya juu kwa muda mrefu. albamu hii ilikuwa na nyimbo kama

comme Biberon, Toucher Jouer, Meilleurs moments, Sans caution, n.k,  Si Congo peke yake kwani Ferre alifanikiwa kupata mikataba ya maonyesho mablai mbali kwa Ufaransa, Holland na Ubelgiji baada ya Albamu hii jambo ambalo lilionyesha kukubalika kwake zaidi.

image

Mwaka 2008 Ferre alitoka na Albamu mpya iliyokuwa katika CD 2 ikiwa na jina la Lubukulukumu. ambayo ilifadhiliwa na Primus, kinywaji kinachopendwa sana Congo. Albamu hiii ilikuwa na remix ya tungo zake kama Vita Imana na nyinginezo ambazo aliwahi kiutamba nazo.

Kwa leo tunaishia hapa usikose wiki ijayo ambapo tutakuletea sehemu ya Pili ya mwanzmuziki huyu hasa tukizungumzia maonyesho yake kwa mwaka 2008 na 2009 na pia albamu yake ambayo iko sokoni ya Qui est derriere toi yaani nani yuko nyuma yako ambayo ni albamu yake mpya.

Fere Gola anatarajia kutumbuiza Dar Es Salaam karibuni


Chelsea 5 – 0 Blackburn Rovers

October 25, 2009

image

Chelsea imefanya mauaji kwa kuitandika bila huruma timu ya Blackburn Rovers kwa mabao 5-0.

Mabao ya Gael Givet (og 20) (lakujifunga), Frank Lampard (48), Michael Essien (52), Frank Lampard (pen 59), Didier Drogba (64) huku moja likiwa la penalti yaliisambaratisha kabisa ngome ya Blackburn.

Mchezo ulikuwa wa upande mmoja huku Chelsea waliwaelemea wenzao na kipindi cha pili kulikuwa kizuri kwao kwani walifanikiwa kufunga mabao 4 ndani ya dakika 15.


Parreira kocha mpya Afrika Kusini

October 25, 2009

image

Kocha Mbrazil aliyewahikushinda kombe la Dunia Carlos Alberto Parreira anarejea kazi yake ya zamani kuinoa Afrika Kusini.

Chama cha mpira wa miguu cha Afrika Kusini kimethibitisha kurejea kwa Parreira katika mkutano uliofanyika Johannesburg.

Parreira anachukua nafasi iliyooachwa wazi kufuatia kuondoka kwa Joel Santana siku ya Jumatatu.

Rais wa chama cha soka cha Afrika Kusini Kirsten Nematandani, amesema haikuwa kazi rahisi kwa kamati kuu kufikia uamuzi huu.

Ameendelea kusema ni jambo la muhimu kwa sababu ya wakati walionao kuhakikisha Parreira anafika mapema na kuendeleza mchakato wa kuinoa timu haraka.


%d bloggers like this: