Rogers "The Tiger" Mtagwa ndani ya PAY PER VIEW pekee Oktoba

October 7, 2009

Roger Mtagwa

Hali ya uchumi iliulazimisha mwaka huu kuwa na mapambano machache saana ya kulipia (Pay Per View) na katika mwezi huu, kutakuwa na pambano moja tu ambalo katika pambano kuu (main event), anasimama nyota wa ndondi toka Tanzania Rogers "The Tiger" Mtagwa.

Roger Mtagwa 3
Roger mwenye rekodi ya (26-12-2) na anayeshikilia nafasi ya 9 ya ubora wa ndondi kwa uzito wake katika orodha inayotambuliwa na Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) atapambana na Juan Manuel Lopez (49-4-1) wa Caguas, Puerto Rico katika kuwania mkanda wa Lopez katika uzito wa WBO junior featherweight. Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa WaMu Theatre uliopo eneo maarufu la Madison Square Garden jijini New York.
Hii ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa Mtagwa ambaye ameonesha ujasiri na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa ndondi kwa kutwaa ubingwa wa NABF na USBA katika uzito wa Feather na pia kwa kuonekana kuboreka kila ajapo ulingoni kiasi cha kuwafanya wengi kuliona pambano lake la mwaka jana dhidi ya Thomas Villa kama PAMBANO LA MWAKA 2008. Katika pambano hilo lililopiganwa Tucson Arizona, Mtagwa alishinda kwa KO ya raundi ya 10.

Tazama / attach http://www.youtube.com/watch?v=-sPXABfEvW0

Tujiunge kwa pamoja kumshangilia (kwa watakaoweza) na kumuombea Mtanzania mwenzetu anayefanya vema sasa katika ulimwengu wa ndondi aweze kufanikiwa.
Kuwa kwenye pambano pekee la pay per view kwa mwezi huu ni kuonesha thamani yake kwani wapo mabondia wengi wenye majina ambao wameshindwa kuweka mapambano yao kwenye hadhi hiyo.
Kumbuka kuwa nyota kama Yuriorkis Gamboa toka Cuba atapigana katika pambano la utangulizi usiku huo dhidi ya Whyber Garcia katika kuwania umiliki wa mkanda wa WBA "regular" featherweight title unaoshikiliwa na Gamboa kwa sasa. Nyota wengine waliopata kushikilia mikanda ya dunia ambao watapigana kwenye mapambano yasiyo ya kulipia ni pamoja na Jermaine Taylor vs Arthur Abraham watakaochuana Oct 17.

  Tunamtakia Rogers Mtagwa pambano jema

Advertisements

%d bloggers like this: