Miss Tanzania – Part 1

October 11, 2009

image

Mashindano ya kumtafuta mnyange wa Miss Tanzania yamemalizika wiki iliyopita huku Malkini wa Taji hilo akitokea Mkoa wa Mwanza kwa mara ya Kwanza mkoa wa Dar Es Salaam unatoka patupu!!.

Pamoja na kumalizika kwa mashindano hayo mwaka huu minung’uniko bado ipo huku mashabikii wakisema kuwa masndano yana mbwembwe lakini hakuna mafanikio ambayo tunafikia ambapo mashabiki wamekuwa wakihitaji kuona si mafanikio bali uzito wa mshindi na umuhimu wake kwa jamii hata muda wake ukiisha..

Kuna mambo mengi ya kuyatazama kwenue mashindano hayo mojalikiwa ni ushiriki wa warembo na mafanikio yao ua baadaye kwenye sanaa nzima ya urembo je nini atafanya baada ya muda wake wa uwakilishi wa kundi la warembo kwenye ncho yenye watu zaidi wa Milioni 38 ambapo wanawake na watoto ni zaidi ya silimia 60?.

Je kazi ya Mrembo zaidi ya kwenda kutoa misaada ambayo haangaiki kuitafuta bali makampuni kutoa na kupitishia mikononi mwake tu?. Ni kweli watanzania wanahitaji kujua kesho ya hawa warembo, wengi wa warembo wamejikwamua kutokana na jitihada zao binafsi ama baada ya kuolewa na watu waliofanikiwa au kujihusisha kimapenzi na watu waliofanikiwa.

Si rahisi kulisemea hili kwani jaribu kufikiria warembo wanaoandaliwa na kampuni ya Compass Communication chini ya Maria Sarungi, yeye amekuwa akihangaika hata baada ya mashindano kuwatafutia warembo wake mikataba na kampuni za kueleweka na wengi wanafanya vizuri, Kampuni ya Miss Universe na miaka chini ya mitatu kama sikosei tangu ianze lakini kiukweli tunaona mafanikio waliyofikia.

image

Hivyo basi hapo inaonyesha kuna zaidi ya urembo wa jukwaani kwenye kutafutwa walimbwende.

Hivi karibuni tuliona jitihada za kampuni hiyo kutafuta warembo mashuleni ambapo waandaaji wake wamekuwa wakihangaika kupata mtu wa kuwakilisha na si tu kushiriki kwenye mashindano hayo ya Miss Universe .

Malalamiko yalikuwepo tangu hatua za awali kwani warembo wengi walionyesha kuwa hawana kiwango na hili sio siri siku hizi ukisoma watu wanabadilishana mawazo sana kwenye mitandao ya social networking kama facebook. Mfano kwenye status yake ya leo mrembo ambaye aliwahi kushika nafasi ya juu kwenye mashindano hayo (jina linahifadhiwa) amesema “ kusema ukweli sina la kusema na Miss Tanzania… inakera” baada ya hapo amefuatiwa na wachangiaji zaidi ya 20 ambao kwa pamoja wameonyesha kutofurahia matokeo na si tu matokeo bali mlolongo mzima wa mashindano hayo.

Kwa leo nitaishia hapa lakini usikose sehemu ya pili na ya tatu.

Soma habari kama hii kama ilivyoandikwa na GPL

Advertisements

Wenger avutiwa na wachezaji wake wa Arsenal

October 11, 2009

image

Arsene Wenger anaamini kikosi cha sasa cha Arsenal kinaweza kwenda mbele kadri kinavyotaka baada ya kuonesha kandanda safi walipowalaza Blackburn mabao 6-2.

Wenger ambaye kwa sasa ni meneja aliyefundisha muda mrefu wa timu hiyo, amesema:"Utamaduni wetu ni kwenda mbele na kufunga mabao na umeshuhudia hayo tena".

Ameendelea kusema:"Timu nzima inasonga mbele na tunaweza kufunga mabao kutoka upande wowote ule".

"Kipa anafanya kazi nzuri sana ya kuokoa mabao, lakini tunafunga mabao mazuri. Timu hii ya Arsenal inaweza kusonga mbele kadri itakavyo."

Wenger, anayesherehekea miaka 13 tangu aanze kufundisha Gunners katikati ya wiki, anahisi timu yake inaelekea kupata kitu maalum zaid siku za usoni.


MTV Africa Award bahati haikuwa yetu!!

October 11, 2009

Ingawa AY na Shaa, wasanii waliokuwa wakiiwakilisha Tanzania katika kuwania tuzo za MTV Africa 2009 hawakubahatika kuondoka na tuzo yoyote, lakini wameonesha njia kwa wasanii wengine. AY alikuwa akiwania tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop na Shaa alikuwa akiwania Msanii Bora Chpukizi, ambazo zote zimechukuliwa na MI wa Nigeria…kabla ya shoo kulikuwa na RED CARPET kwa wasanii wote.

AY, SHAA, BAHATI HAIKUWA YAO MTV AWARDS
…AY akihojiwa na mtangazaji wa MTV wakati akipita kwenye Red Carpet
AY, SHAA, BAHATI HAIKUWA YAO MTV AWARDS

Profesa naye akihojiwa Red Carpet.

Habari hii na picha kwa Mujibu wa GPL kupitia kwa Abdallah Mrisho. (Gonga hapa kwa picha zaidi)


BBA, Elizabeth aonyesha msimamo kwa Kevin

October 11, 2009

Mshiriki wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Afrika (BBA) Elizabeth, ambaye amemueleza wazi mshiriki mwenzake Kevin kuwa hadanganyiki!

 

Na Mwananchi

MSHIRIKI wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Afrika jana alimweleza Kevin kutoka Nigeria kuwa hana hisia zozote juu yake na kwamba hawezi kuanzisha uhusiano wowote ndani ya jumba hilo kwani anaye rafiki nje ya jumba hilo.

Kwa mara nyingine Kevin alijitahidi kuwa na ukaribu na Elizabeth na kumtaka walale kitanda kimoja kama ilivyo kwa baadhi ya washiriki wengine. Hata hivyo baada ya kupata jibu hilo toka kwa Elizabeth, Kevin alionyesha kutojali na kuendelea na harakati hizo.

Kevin alikaa karibu naye kwenye kochi, alimshika nywele na kumweleza kuwa anahitaji awe rafiki yake kama anakuwa na hasira pindi anapomwona ni rafiki wa wasichana wengine.

Read the rest of this entry »


Sugu aachia Single ya kwanza toka albamu mpya ya VETO

October 11, 2009

image

Mwanamuziki Joseph Mbilinyi aka Sugu ametoa rasmi single yake ya kwanza kwa umma kwa ajili ya kuitambulisha albamu yake ya VETO. Single hiyo inakwenda kwa jina la Hold On.

Katika wimbo huo kama kawaida Sugu amegusa matukio ya kawaida katika maisha ya kawaida ya mtanzania kuanzia Mdawa ya kulevya, kusimangana, ugonjwa wa ukimwi na mengineyo.

Kwa mujibu wa Sugu alipoongea nami amesema kuwa wimbo huo utaanza kupigwa kwenye fm radio za nyumbani bongo.

Sugu amemshirikisha mwanamuziki anaitwa Andre wa huko huko Marekani, kwa mujibu wa Producer wa Sugu Stiggo anasema kuwa jamaa huyu ambaye anasikika kwenye kiitikio si mwanamuziki ila anajua kuimba (upo hapo?). Kwa waliopata kuisikiliza nyimbo hii kabla ya kutoka wote (pamoja nami) tumeikubali na ama kweli Sugu ameonyesha ukomavu kwenye fani, bila shaka albamu ya VETO itakuwa moja ya gumzo kwenye anga za muziki hasa huu wa kizazi kipya kama mwenyewe alivyotabiria.

Kila la hri mtu mzima.


Msimamo wa mtanange wa Ligi ya Uingereza

October 11, 2009

msimamo


Tina Turner Live in Concert

October 11, 2009

Following the success of the Queen Night, The St George’s Society are proud to announce another big screen concert featuring the inimitable Tina Turner.

Please find attached a poster with details. Closing date for tickets is 14th October.

image


%d bloggers like this: