Muambata Kanal Maganga Washington…

October 4, 2009

maganga

Muambata wa kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Washington DC Kanali Emanuel Maganga (Kati) akizungumza na waambata wenzake katika ukumbi wa mikutano katika jengo jipya la Ubalozi wetu huko Washington hivi karibuni. Kanali Maganga ni mshirika mkubwa wa sekta ya habari na mwanamichezo pia.

Picha na Sunday Shomary

Advertisements

Ubaguzi wa rangi kwenye soka-1

October 4, 2009

Nia kamili ya mchezo wowte ni kuburudisha na moja kati ya michezo ambayo imetokea kupendwa na kujinyakulia mashabiki wengi ulimwenguni n mpira wa miguu au soka.

Mchezo huu umetokea kupendwa sana na una mashabiki kote duniani jambo linalopelekea klabu kutoa pesa nyingi kununua wachezaji wenye kiwango cha hali ya juu.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wachezaji wanaokwenda kucheza soka la kulipwa hasa Ulaya ambako kwa kiasi kikubwa soka inalipa kwani hata kwa timu ambazo ziko juu kimpira duniani kama Brazil na Arrgentina ambazo ziko America bado wachezaji wake wakubwa awanacheza bara Ulaya.

Hii imepelekea kwa wachezaji toka Afrika pia kufikiria na kuwa na matarajio ya kucheza soka huko Ulaya lakini kipingamizi kikubwa anachokutana nacho huko ni Ubaguzi wa Rangi. Wengi wa wachezaji wenye asili ya Africa ambao wanakwenda kucheza nchi tofauti na Uingereza basi wanajikuta kwenye wakati mgumu hasa na wakati mwingine kubaguliwa hata na wachezaji wenzao au mashabiki wa klabu zao.

Kwa mujibu wa FIFA ubaguzi umepungua kwa kiasi kikubwa na kuzitaja nchi kama Ujerumani, Italy na Spain kuwa ndio zilikuwa na matatizo makubwa ya ubaguzi mchezoni ukilinganisha na nchi zingine za ulaya ambazo pia matatizo hayo yapo. Kwa nyakati tofauti Spain ilitajwa kuwa ni nchi yenye ubaguzi mkubwa kwa waachezaji wenye asili ya Afrika, Fuatilia mahijiano na baadhi ya wachezaji akiwemo Thiery Henry wanavyoelezea maisha yao kisoka juu ya suala la ubaguzi.


%d bloggers like this: