Werrason na watu wake

Niliwahi kuandika kuhusu Werrason na nafasi yake kwa jamii, Kiukweli Werrason anakubalika sana kwenye miji ya Congo, hii inatokana na kujiweka kwake karibu na jamii hasa watu wa chini, inasema Werrason hupendelea sana kukaa vijiweni na kupiga story zile za mitaani bila kuwatenga watu wake wa Chini na mara nyingi huwa akifurahi huwa anafanya Show za bure bila malipo, hii imemfanya kuwa karibu sana na mashabiki wake tofauti na wanamuziki kama Koffi, Fally, Jb Mpiana na wengineo ambao wanasemwa kunata sana kwenye makundi haya ya jamii.

Huu ni mmoja wapo wa nyimbo ambazo zilikuwa kwenye albamu ya Solola Bien, moja ya kazi za Werrason ambazo nazikubali sanaaaa kwenye albamu za Wenge Musica Maison Merre enzi hizo kikosi kikiwa bado kimetimia watu kama Ferre, Mabiala, Lacoste, Adjani, Baby, Bill, Celeo, Japonais, Kapaya, Dominguez etc, wenyewe waliwaita le barça de la zik congolaise. Barcelona ya Muziki wa Congo.

9 Responses to Werrason na watu wake

  1. clement mkungile says:

    anaurafiki mpaka n sokwe!

  2. edmas says:

    Sio kweli kwamba wimbo huu ulikuwemo kwenye Kibuisa Mpimpa, huu unapatikana ktk albamu ya SOLOLA BIEN, wkt huo Adolphe alikuwa bado kundini, nadhani unamuona Adolphe anavyojichanua hapo.

  3. K'Odero says:

    WERRASON SIKU MOJA ATAKUJA KUWA PRESIDENT DRC, NGOJENI HAPO

  4. mwana congo says:

    Haiwezekani kwa kuwa werra na koffi sio watoto wa congo,labda akagombee urais kwao Rwanda baada ya rais kagame kustaafu na sijui lini hiyo itatokea otherwise atabaki kuwa rais wa bendi yake wmmm

  5. edmas says:

    Mkuu Pius ni kama wiki 2 zimepita ulitoa habari kuwa Ferre Gola alipewa kibali cha kuurudia wimbo MATATA YA MWASI wake Franco. Ulitoa na lyrics yake kilingala.

    Wimbo huu nauhusudu sana lakini sielewi unazungumzia nini. Ingekuwa vizuri kama kuna mdau ambae angeweza kuutafsiri nasi wengine tupate jua

    • Hadj Le Jbnique says:

      kiufupi wimbo huo unazumngumzia matatizo ya mke na mume-kwa kilingala ndio MATATA YA MUASI NA MOBALI,

      Ferre naamini ataweza,unaweza kumtizama hapa alivyojaribu kuupiga wimbo huo live na kuwakuna vilivyo vijana wa zamani waliokuwemo ukumbini humo

  6. At this time it sounds like Drupal is the best blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

  7. Admiring the persistence you put into your blog and in depth information you offer. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Wonderful read! I’ve bookmarked your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

Leave a reply to mwana congo Cancel reply