Ezau wimbo uliomaliza ubishi wa umiliki wa wimbo wa Mulolo na Kin Ebouge

Kwa wafuatiliaji wa Muziki wa Kongo wanajua utata uliokuwepo kati ya umiliki wa nyimbo mbili za Mulolo na Kin ebougee ambazo zilibeba majina ya albamu huku wengine wakimtaja Ngiama Makanda kama mtunzi wa na mmiliki wa nyimbo hizo. Nimeamua kuirudia hii posti kwa ajili ya Stevin/Malewa ambaye mara nyingi hizi nyimbo mbili amekuwa akikataa kuwa sio za JB Mpiana.

JB Mpiana alikuja na wimbo wa Ezzau ambao ulikuwa kwenye albamu ya Anti Terro ambayo kwa kiasi fulani haikutamba hapa nyumbani kwa kutokupata si tu promo bali hata airtime ya kutosha haikupata. Katika wimbo huu JB Mpiana anajifanananisha story yake sawa na story ya  Esau wa kwenye Biblia ambaye alikosa baraka za baba yake ambaye alikuwa kipofu na na alikuwa na manyoya mengi siku Baba aliomba aletewe mwanaye Ezzau ili ampe baraka kwa vile Esau alikuwa hapendwi na mama yake basi mama alimtuma porini na kumpaka manyoya kaka yake ambaye ni Yakobo na Baba alipomshika akajua ni Ezzau na akambariki.

JB Mpiana kwenye wimbo huu anasema histoir eshanjaka te zembo  nanga ya mulolo ebimisa wenge zembo nanga ya kin ebouge ekofirma wenge bolinga bolinga te yango wana akiimaanisha Story haitobadilika wimbo wangu wa Mulolo ndio ulioitoa Wenge, kisha wimbo wangu wa Kin Ebouge ndio ukai komfemu Wenge mtake msitake Stori haitobadilika, na kabla ya hapo JB Mpiana aliwataja mashahidi ambao anasema wanaujua ukweli huku akimtaja Papa Wemba, Presidaa Nyoshi aka Nyoka Longa na Josiki ya Mbukuta kuwa wanaujua ukweli huo.

Hivyo Wimbo huo unamaliza ubishi huo, Maneno yaliyokwenye Wimbo huu ni kama mahubiri ambayo kiukweli kila mtu na muumini anapaswa kuyasikiliza. Kwani anasema kuwa baraka zake zimetoka kwa Mungu ana kusisitiza Binadamu wapendane hakuna sababu ya kuchukiana.

JB anasema ukila pamoja na watu wanakuita ndugu mshkaji lakini siku ya siku unabaki kama Yesu Masia peke yako.

JB anasema Yesu alimfufua Razaro na watu hawakuamini, Mapenzi ni ya Mungu ingawa Mwili unarudi udongoni, mtafanya kila mfanyavyo akisema Mungu yatakuwa. Sichekagi matatizo ya mutu wala kutangaza ubaya kwa sababu nayajua yapo, mlitangaza kwamba nilikuwa Kichaa ili mniharibie kwa watu.

Anaongeza hata leo nikifa mtanikumbuka kwa kitu kimoja yule mwenye deni lake kwangu aseme hapa nimlipe… Kiukweli maneno ya Wimbo huu ni mazito sana. nitamtafuta Papaa Julie we Ston Presidaa Bana Kongolee na Darisalama ili niwaletee wimbo huu mwanzo mwisho.

Anasema ukiwa na pesa wanakuja kwako wanajaa mnakula na kunywa zikiisha nyumba inakuwa kama iko Jangwani hakuna anayekuja, ukiwa unamatatizo na kuumwa hakuna anayekuja kukusalimia au kukusaidia wakisikia umekufa wanakuja na magari ya kifahari na michango wanatoa kukusindikiza kaburini, Kisha anaongeza kuwa yeye si kama Ezzau yeye ni kama Noah aliyeokoa viumbe vya dunia hivyo atawaokoa wote.

Merci Mingi Papaa Julie Weston Ilunga ntakutafuta tumalizie hii kazi.

Advertisements

7 Responses to Ezau wimbo uliomaliza ubishi wa umiliki wa wimbo wa Mulolo na Kin Ebouge

 1. edmas says:

  NAONA UMEISHIWA NA HABARI ZA KUZILETA HUMU HADI UNARUDIA RUDIA MAMBO YA NYUMA. HUYO ALIETAKA HIZO HABARI UNGEMUAMBIA APEKUE KURASA ZILIZOPITA.

  • ayman alzawahiri says:

   ndugu edmas subiri majibu ya jeuri kutoka kwa bloger,utajibiwa kwamba ukafungue blog yako,utaambiwa we fala kafungue blog yako. sikuwahi kujua kama jamaa huyo hapendi changamoto na kukosolewa.he is so unprofessional.anasahau bila wasomaji blog haina maana

   • Pius says:

    Sio Kweli mkuu, Nilipoteza umiliki wa email yangu ambayo nacontrol hii blog na watu takribani 16 (Comments) walijibiwa vibaya, Niliwatumia mail wote kuwaomba Msamaha, Siwezi kumtukana mtu kwa vyovyote. Kwa ambao Email hazikufika, Naomba nichukue nafasi hii Kuwaomba radhi rasmi. Asanteni

    Pius Micky
    Spoti Starehe

 2. Anonymous says:

  Papa cherie mukulu,papa puis bamala tuna kushukuru sana kwa kutupa vitu vitu,history aibadilishi kuna watu pia wana jua story

  vizuri ya wenge pdg mabamba l’infinitif reddy amissy bayilo kanto,tam luk mgoya,deus micky micky wana jua wenge imeanza vipi

 3. Hadj le jbnique says:

  Naungana na blogger kuwataka radhi wote mliopatwa na mkasa wa kujibiwa vibaya,kiukweli na katika hali ya hatutegemei blogger atukane members wa blog yake,ni wazi hilo lilifanywa na wasiolitakia mema barza hili kwa sababu wanazozifahamu,binafsi sikubahatika kuona hayo majibu mabaya otherwise ningechukua hatua ya kumuandikia blogger e mail or even to text him to explain my disapointment cuz mimi naamini zaidi katika challenge-kukosolewa kwani alwayz wanaokukosoa ndio wanaokusaidia zaidi kuliko wanaoku applause kwa kila jambo,mwisho nimalizie kwa kusema,tukubali kutokubaliana kwa kila jambo ili tusonge mbele.melesi mingi.

 4. Anonymous says:

  Huo wimbo ulimalizaje ubishi? Kwa kuwa uliimbwa na Mungu wenu Mpiana, Hivi angekuwa ameimba Werrason na kulia lia kwamba Mulolo ni wimbo wake ubishi ungeisha, Nadhani kwa kupiga kelele wangu wangu kama chura anavyodai maji yote yake inazidi kudhihirisha kuwa Mulolo sio wake, sijasikia mwanamuziki yoyote wa Wenge akimtetea Mpiana, kama ni wake akae kimya! sio kudai wimbo mzuri ni wako kwa kutunga wimbo mbovu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: